Habari na Hoja mchanganyikoUna jambo umeliona kutoka chanzo chochote cha habari? Usisite, liweke hapa uwahabarishe wenzako. Hoja binafsi pia ziwekwe hapa.
Date::11/19/2008
Waziri asihi vyombo vya habari kuachana na habari za EPA, migomo ya walimu
Festo Polea na Kuruthum Ahmed
Mwananchi
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwamtumu Mahiza amevitaka vyombo vya habari nchini kuachana na habari zinazohusu sakata la wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje, (EPA) pamoja na masuala ya migomo ya walimu kwa madai kuwa masuala hayo tayari yametafutiwa ufumbuzi.
Badala yake alivitaka vyombo hivyo kuelekeza nguvu hizo katika habari nyingine ikiwa ni pamoja na kufichua na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanafunzi.
Waziri Mahiza alisema hayo jana wakati akizindua kampeni ya “Jifunze bila woga” iliyofadhiliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Plan-Tanzania yenye lengo la kupinga ukatili wa kijinsia mashuleni.
Mahiza alisema anachukizwa kuana masuala ya EPA na migomo ya walimu ikishikiliwa bango kila kukicha wakati tayari malalamiko hayo yamefika mwisho kwa sababu walimu wameanza kulipwa na watuhumiwa wa EPA wameshafikishwa Mahakamani.
“Sasa tubadilishe CD, kila wakati EPA na migomo ya walimu, waandishi wa habari na vyombo vya dola tubadilike, mimi nikiona mnalivalia njuga kwa kufichua masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, kuwafichua waharibifu wa wanafunzi, kisha wakakamatwa nitafurahi sana,” alisema Waziri Mahiza
Mahiza alitumia nafasi hiyo kulaani walimu wote wanaoharibu watoto kijinsia kwa kutumia udhaifu wa wanafunzi wa kike na kiume kwa kuwarubuni kwa kuwapa vitu vinavyowashawishi kama Simu na magari.
Alisema masuala ya ukatili wa kijinsia yanaongezeka licha ya kukemewa mara kwa mara.
Aliwataka viongozi wa dini mbalimbali nchini kuandaa makongamano yenye lengo la kuombea laana walimu na watu wengine wanaorubuni wanafunzi bila kujali maisha yao ya baadae.
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwamtumu Mahiza amevitaka vyombo vya habari nchini kuachana na habari zinazohusu sakata la wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje, (EPA) pamoja na masuala ya migomo ya walimu kwa madai kuwa masuala hayo tayari yametafutiwa ufumbuzi
Mahiza alisema anachukizwa kuana masuala ya EPA na migomo ya walimu ikishikiliwa bango kila kukicha wakati tayari malalamiko hayo yamefika mwisho kwa sababu walimu wameanza kulipwa na watuhumiwa wa EPA wameshafikishwa Mahakamani.
Tafadhali mpelekeeni ujumbe huu
Tutaacha kuzungumzia EPA pale kesi itakapo isha kwani tuna experience tuliyoipata Richmond alipojiuzulu Lowasa tulimaliza na nyie mkatulia sinahabari imefikia wapi hope JK atatuambia mwisho wa mwaka kama atakuwa nchini
na walimu mpaka alipwe mwalimu wa mwisho kwa sababu tumeyaona ya wazee wa East Africa.
ya migomo ya chuo mpaka rais azungumze suala la vyuo vingi kufungwa kwa pamoja sio la kulivyalia suti na kwenda LIBYA km hakuna kitu ni swala la kuahirisha safari na kutuma ujumbe kuna emegency imetokea nchini kwangu sitaweza kuhudhuria kikao anyways ndo vijana wa siku hizi wazee wamelala mlangoni kwakwe yeye anapita na ving'ora kama ni takataka tu poor me...
Mama Bakari Mahiza,nafikiri umekalia kuti la kuanguka,CD unazozisikia ni ule mlio wa kuti kuanza kumeguka na kuanguka.Waandishi wa habari ambao ni kioo cha jamii ndio wanatujulisha juu ya kuti bovu linalotaka kuanguka.Isije ikawa ajabu kuti hilo litakapomeguka kabisaa! maana CD yake tumeshaicheza.Kumeguka kimya kimya wataumia wengi zaidi maana wanao umia na huo wimbo wa EPA, Richmond n.k. wanajua nyimbo hizo walizitunga vipi.Endelea kucheza mama ,na kama wewe hazikuhusu basi kaa chini na wenyewe wenye CD hizo wataendelea kunengua, kama waandishi wetu na vyombo vya habari wanavyo koleza vibwagizo!!!!!
Kuna mwalimu wangu alinifundisha kuwa 'Unless we put meaning into it, a word has no meaning'. Akafafanua kidogo kuwa maana ya neno hutokana na jamii sio mtu fulani mfano waweza kuwa mwanaume kijinsia lakini jamii fulani inayotambua mwanaume aliepita jando isikutambuwe kuwa mwanaume.
Hivyo basi jamii yawatanzania ndio inayojua ni kwa kiasi gani suara la EPA and ndugu zake limeshughurikiwa sio Mahiza? Hivyo awaachie wanahabali jamii ikiridhika automatically suala la EPA, etc litakuwa historia, hivyo namsihi awaache wadili nao. Kwani tatizo nini eti Mh, au na wewe upo nini?
Suala la unyanyasaji kijinsia jamani wana JF tuliangalie kwa mapana kidogo. Sijafanya research lakini nimefanya observation kama mwanajamii. Kwa observation yangu unyanyasaji halisi nauona kwa vijana wa kiume kuliko wa kike. mtakubaliana na mimi vijana wa kike wengi wanajitegesha kwa tamaa zao na kukosa maadili. na swala hili hata baadhi ya mama zao wanachangia sana. Mimi naona hata uile sheria ya kumwadhibu mwanaume kwa kosa la kupeana mimba na msichana wa shule haiko sawa kwa sababu inawanyanyasa vijana wa viume kijinsia. Mi naona waadhibiwe wote sawa kabisa hii ndio suruhisho la kukomesha mimba mashuleni. Wasichana wengi wanao shika mimba mashuleni ni wale ambao CV zao hazijatulia katika masuala ya mahusiano. Na mara nyingi unakuta ni wasichana wa kuanzia kidato cha 2 - 4. Sasa jamani wana JF katika ulimwengu huu wa Dotcom. Msichana huyu wa Form 2 - 4 kwanini akubali kushika mimba na yeye ni mwanafunzi. Mbona wenzao kwenye nchi zilizoendelea wanakuwa na boyfriends na wanafanya mchezo mbaya kuanzia primary na hawashiki mimba???
Huyo wazili si mlaumu ndio uwezo wake wa kufikilia.
Ukiona ivyo kwenye ilo zengwe anaguswa indirectly.
Tumelizwa billioni 133 unasema tubadili CD,hana ata haya
__________________
Europe has 2take concrete steps to ensure its banks are less of a safe haven for looted African funds?
Mh!! mama Mahiza mbona utakuwa na kazi kusimamia CD ipi ichezwe na ipi isichezwe!!
Labda ujaribu kunzia kwenye hizo circle zenu muache ufisadi na viini macho, ndipo CD itabadilishwa.