Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mfuko wa bima ya afya ni kero kwa wafanyakazi

    Report Post
    Results 1 to 3 of 3
    1. #1
      Tikerra's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2008
      Location : Morogoro
      Posts : 1,588
      Rep Power : 864
      Likes Received
      100
      Likes Given
      3

      Default Mfuko wa bima ya afya ni kero kwa wafanyakazi

      Mfuko wa Bima ya afya uliingizwa kinyemela.Wala wafanyakazi hatukuhojiwa kama tunapenda au laa.Kwa hiyo mishahara yetu ilikatwa bila ridhaa yetu.Kitendo hiki kisheria si halali,na nadiriki kusema kwamba serikali ilikiuka haki za msingi za wafanyakazi wake.Kana kwamba hilo halitoshi,bado mfuko huo umeendelea kuwa kero kubwa kwa wafanyakazi.Mpaka leo wafanyakazi wengi hawana vitambulisho na vituo viko mbali mno na wafanyakazi,kiasi kwamba wengi hatupati huduma hiyo muhimu.Jambo la kushangaza ni kwamba uongozi wa mfuko huo hauonyeshi jitihada zozote za dhati za kupeleka huduma hiyo karibu na wanachama wake.Hata pale unapojikongoja na kufika kwenye kituo chote chote kinachotoa huduma hizo, huduma kwa ujumla ni mbovo sana.Hata zile huduma ambazo mfuko unasema unatoa kama vile miwani ya macho,matibabu ya Typhoid nk.vituo vingi hata kama vina uwezo wa kutoa huduma hiyo vinasema havitoi.Mimi binafsi nimeanza kukatwa huduma ya afya zaidi ya miaka mitano iliyopita,kwa kiwango cha Sh.20,000 kwa mwezi,lakini nimeshawahi kupata huduma hiyo mara tatu tu.Jamani kama sio uonevu huo na wizi wa hela zetu ni nini.Malengo ya huduma hiyo sio mabaya,lakini utekelezaji wake ni mbaya mno.Naomba serikali ichukue hatua za dhati za kusimamia uboreshwaji wa huduma zinazotolewa na mfuko huo.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Nansawa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 126
      Rep Power : 569
      Likes Received
      15
      Likes Given
      0

      Default Re: Mfuko wa bima ya afya ni kero kwa wafanyakazi

      kwa kweli mfuko unaboa! na kweli ni MFUKO!! maana tunatunisha tu mifuko na matumbo ya wakurugenzi wake. Wanachojua ni kukopeshana marangerover tu! Kwanza kuna ufisadi uliwahi ripotiwa hapa kutoka NHIF. mNAJUA ULIISHIA WAPI? ULIZIMWA KWA GHARAMA KUBWA BADALA YA KUTULETEA HUDUMA WANAFUNGA SAFARI NJE YA JIJI ETI KUMSAFISHA HUYO MKURUGENZI MKUUJamani msicheze na pesa za sie wagonjwa tusiopata dawa nyie mnatanua . Jirekebisheni kabla hatujaaamua sie wanachama hatununuliwi! HUMBA WATCH OUT

    4. #3
      Ng'azagala's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 7th June 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 992
      Rep Power : 757
      Likes Received
      79
      Likes Given
      301

      Default Re: Mfuko wa bima ya afya ni kero kwa wafanyakazi

      naomba mwenye ile taarifa ya kusitishwa mkataba kati ya marie stopes na NHIF nimesikia somewhere kwenye radio sijajua ni gazeti gani.
      hawa marie stopes wamelalamikia sana ufisadi wa hawa NHIF mpaka wameshindana nao

    5. RukaaJuu Final

    Similar Topics

    1. Kero ya kilimanjaro hospital na bima
      By wakumbuli in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 22nd September 2011, 18:36
    2. Maombi kwa mfuko wa bima ya afya(NHIF)
      By kipindupindu in forum JF Doctor
      Replies: 1
      Last Post: 27th May 2011, 16:55
    3. Bima ya Afya kwa babu!
      By Safety last in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 1
      Last Post: 23rd May 2011, 17:29
    4. Mkurugenzi mkuu mfuko wa taifa wa bima ya afya ni mnyanyasaji na muonevu
      By mkereketwakamil in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 4
      Last Post: 25th September 2010, 10:40
    5. Mfuko wa taifa wa bima ya afya
      By mkereketwakamil in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 27th August 2010, 14:43

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...