Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mengi alia na mafisadi; na yeye achunguzwe!

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 41
    1. #1
      Pdidy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 12,283
      Rep Power : 3442
      Likes Received
      1322
      Likes Given
      855

      Default Mengi alia na mafisadi; na yeye achunguzwe!

      Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano


      *Abainisha hana ndoto za kuwa mwanasiasa

      Na Mwandishi Wetu


      MWENYEKITI Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi, amesema limejitokeza kundi la mafisadi waongo na vibaraka uchwara, wanaomvumishia kuwa anajijengea umaarufu wa kisiasa, tayari kwa kugombea uongozi wa kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao.

      Bw. Mengi amesema kundi hilo la watu waovu, wanataka kuharibu uhusiano wake na viongozi wa kisiasa nchini.

      "Nia yao ni kuhakikisha kuwa ushupavu na uadilifu wa wale wote wanaomuunga mkono Mhe. Rais katika vita dhidi ya ufisadi, wanadhoofishwa na wakati huo huo mizizi ya ufisadi, inajichimbia zaidi na mafisadi wanajijenga zaidi na kuimarika," alisema Bw.Mengi kupitia katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

      Alisema mafisadi hao wanadiriki hata kusema kuwa vyombo vya habari anavyovimiliki na vinavyopiga vita ufisadi, ni adui wa nchi na vinataka isitawalike.

      "Sasa tujiulize, adui wa nchi ni yupi, ni yule anayetetea na kulinda mali za nchi yetu au ni yule anayezipora. Je anayetaka nchi yetu isitawalike ni yule anayepora mali ya umma na yule anayepiga vita uporaji wa mali ya umma ?" Alihoji Bw. Mengi.

      Aliwaomba wananchi wenye nia njema na nchi yao, wawapuuze mafisadi na waongo, badala yake waongeze nguvu katika vita dhidi ya ufisadi.

      Alisema binafsi ameridhika na biashara zake na kwamba anaunga mkono kauli ya Rais kuhusu umuhimu wa kutengenisha shughuli za kibiashara na uongozi wa kisiasa.

      "Vile vile naomba ndugu zangu Watanzania waone kwamba heka heka hizi za mafisadi na waongo, zina nia mbaya na ni fitina zenye nia ya kujenga chuki na kuvuruga nchi," alisisitiza ,Bw. Mengi kupitia katika taarifa yake ya kurasa mbili.

      Aliwashauri wale aliowaita kuwa ni mafisadi, kuacha fitina za kueneza chuki baada ya kupora mali za umma na kwamba wasitumie nguvu za ufisadi wao kupora amani ya nchi.

      "Nawashauri warudishe mali za umma walizopora, waombe ushauri wa viongozi wao wa kiroho, watubu uovu wao na waombe msamaha," alisema.

      Alisema litakuwa jambo la kushangaza kuzungumza juu ya kumsamehe yeyote yule wakati mamilioni ya ya fedha yaliyoporwa yamehifadhiwa katika mabenki ndani na nje ya Tanzania wakati wananchi wanakosa fedha za kununulia dawa.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Kevo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2008
      Location : Around the World
      Posts : 1,348
      Rep Power : 827
      Likes Received
      16
      Likes Given
      14

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Mengi knows once he goes against CCM he is finished.They will bring him down in an instant therefore he knows its best for him if he keeps his political life away from business life.
      'I could have annihilated all the Jews in the World,but I left some of them so you will know why I was killing them'-Adolf Hitler;Mien Kampf

    4. #3
      ByaseL's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 1,772
      Rep Power : 941
      Likes Received
      89
      Likes Given
      11

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      I agree with Bwana Mengi. Some of the people behind the EPA rip off are just big time conmen masqarading as businessmen. In Mengi these so called "succesful " businesmen have found their match. They are "mafisadi" and unpatriotic and will remain so in the hearts and minds of Tanzanians. They have their bodies in Tanzania but their souls in India (or Iran) and keep their money in Europe. Shame and curse be upon them.

    5. #4
      Njowepo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Location : Santiago
      Posts : 7,606
      Rep Power : 22057
      Likes Received
      997
      Likes Given
      784

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Wengi wanajua ndiko aelekeako hasa haya mambo ya kijipublicise kwa kila afanyanyacho kwa jamii
      WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

    6. #5
      Kevo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2008
      Location : Around the World
      Posts : 1,348
      Rep Power : 827
      Likes Received
      16
      Likes Given
      14

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Quote By Njowepo
      Wengi wanajua ndiko aelekeako hasa haya mambo ya kijipublicise kwa kila afanyanyacho kwa jamii
      Hell yeah!A Small thing and its all over the news with so much pomposity!
      'I could have annihilated all the Jews in the World,but I left some of them so you will know why I was killing them'-Adolf Hitler;Mien Kampf

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Songambele's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2007
      Posts : 746
      Rep Power : 741
      Likes Received
      74
      Likes Given
      189

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Mbona kila anayepambana anasema anawajua mafisadi hawataji? Mafisadi noma kila mtu anasemea pembeni na mafisadi wanatisha. Tunajaza thread hapa uwezi ona jina la fisadi, isijekuwa tunajitisha wenyewe? Hata mkuu wa kaya anawaogopa.

      Sasa Mengi nae analalamika! Mengi apunguze kulalamika, si nayeye alichota NBC au wakati huo ufisadi ilikuwa bado. Ifikie wakati mafisadi tuwajue tuchukue hatua wenyewe.

    9. #7
      Mwikimbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2008
      Posts : 1,543
      Rep Power : 948
      Likes Received
      346
      Likes Given
      128

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      unakukumbusha article ya mwanakijiji leo mtanzania daima, imenikumbusha ule wimbo tukiwa wadogo

      watoto wangu eh, mimi baba yenu eh
      sina nguvu tena eh
      kupambana na simba eh

      tulikuwa tunaimba tunazunguka kwenye mabalamwezi kijijini kwetu kusiko na umeme, watoto hatukuwa na mipaka, kama mnavyofungia watoto wa mjini kwenye mageti, hata kama mnawafungia kwenye mageti, msisahau kuwaimbisha kama alivyoandika mwanakijiji leo

      watanzania wangu eh, mimi rais wenu eh
      sina nguvu tena eh, kupambana na m afisadi eh
      lowasa kanizidi eh, kaungana nao eh
      nikipambana nao eh, nitawapata wapi eh
      pesa za kampeni eh,

      watoto wangu eh, mimi baba yenu eh

    10. #8
      Mshiiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2008
      Location : Sillicon Valley - USA
      Posts : 1,351
      Rep Power : 1233
      Likes Received
      58
      Likes Given
      17

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Mafisadi wanajulikana kwanza na familia zao, ndugu zao, marafiki zao, vimada wao, mafiasadi wenzao, ofisi zao, wafanyakazi wao, jirani zao, bank zao, hospitali zao, hoteli zao, clubs zao, soko lao, maduka yao; JE serikali hapa haijui bado? Wasitu***** akili zetu bwana!
      “You will not be punished for your anger; you will be punished by your anger.”

    11. #9
      Koba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2007
      Location : Pasadena California
      Posts : 4,006
      Rep Power : 1409
      Likes Received
      177
      Likes Given
      103

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      ...bora ya Mengi ambaye practically kutokana na biashara zake amesaidia familia nyingi sana through ajira na analipa kodi na kutuletea services nyingi tuu,impact ya Mengi ni kwa maelfu for the better....akifilisika msifikiri he'll go down by himself ni wengi watahangaika sana,i respect mengi kwa anayofanya ingawaje naona mmeanza kumponda eti its all publicity,waulizeni ambao watoto wao wanakula na kwenda shule kwa ajira za mengi ndio mtaelewa,hope tungekuwa na Mengi wengine maelfu tungeendelea sana...heshima mbele kwa watu kama kina Mengi sio wanasiasa uchwara wa CCM ambao ni kulinda maslahi yao tuu na matumbo yao!
      "Freedom is incomplete if it is exercised in poverty."-Harry Schwaz

    12. #10
      Mwana wa Mungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th August 2008
      Posts : 989
      Rep Power : 746
      Likes Received
      16
      Likes Given
      6

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Ni uhusiano gani anaoongelea hapa? uhusiano na nani, kwani wanafanya biashara pamoja?, anyway, sitaki kuingilia sana hili, lakini nafikiri anajitetea yeye mwenyewe/he is defending his interests, labda kashindwa kupigana nao chini kwa chini akaona bora apige kelele. nimeona leo katoa press release kwenye gazeti la Dairy News, ameongea hivyohivyo.

    13. #11
      Mshiiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2008
      Location : Sillicon Valley - USA
      Posts : 1,351
      Rep Power : 1233
      Likes Received
      58
      Likes Given
      17

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      If you can not beat them join them
      “You will not be punished for your anger; you will be punished by your anger.”

    14. #12
      WildCard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 6,453
      Rep Power : 1979
      Likes Received
      1797
      Likes Given
      59

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Mengi ni "mtaalam" wa kutafuta HURUMA kwa WaTZ. Na anajua muda na namna ya kuwasilisha "malalamiko" yake! Awataje wanaomuandama ili tulie nao kwa niaba yake?

    15. #13
      Fidel80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 19,049
      Rep Power : 9497
      Likes Received
      3170
      Likes Given
      1231

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Mimi naona Mengi anajitafutia umaarufu kinamna aseme nani kasema anataka yeye agombee urais??
      si amtaje na wapi wameeneza uvumi huo?
      Chombo gani kilicho tumika?
      Huyu anatafuta umaarufu tu hakuna kitu.
      **^^+..Ukiuza Utumbo usiogope nzi..+^^**
      Chuda Raha
      Email: [email protected]

    16. #14
      Kevo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2008
      Location : Around the World
      Posts : 1,348
      Rep Power : 827
      Likes Received
      16
      Likes Given
      14

      Default Re: Mengi alia na mafisadi,adai wanataka kumharibia uhusiano

      Quote By fidel80
      Mimi naona Mengi anajitafutia umaarufu kinamna aseme nani kasema anataka yeye agombee urais??
      si amtaje na wapi wameeneza uvumi huo?
      Chombo gani kilicho tumika?
      Huyu anatafuta umaarufu tu hakuna kitu.
      Yaani wewe na Wildcard ndio mmepalenga vizuri sana!Mengi thinks simply coz he is good when it comes to charity and seems like it is one of his favorite pasttimes kwamba he is a saint in the eyes of the Tanzanians and when he has a small problem we should all carry it on our shoulders.Guess he is mistaken.Ugomvi wake na manji ulipelekea hadi kuundwa kwa kamati za viongozi wa dini kuutatua ulikuwa exaggerated.masuala yake na Masilingi ambayo yalimfanya Mkapa arejee nchini kuja kuwapatanisha vilevile yalikuwa exggerated.Sasa he wants to create a molell out of anthill then wote tuingie kuomba yaishe!
      JK alipokuwa anamtambulisha Mengi Marekani kipindi fulani kabla ya mkutano wa Sullivan alisema he is everything in TZ nadhani its gonna be proved!
      'I could have annihilated all the Jews in the World,but I left some of them so you will know why I was killing them'-Adolf Hitler;Mien Kampf

    17. #15
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,586
      Rep Power : 1516
      Likes Received
      64
      Likes Given
      54

      Default Mengi naye achunguzwe na asitegemee huruma za wananchi!

      Wakuu heshima mbele,

      Baada ya juzi kupitia taarifa kwa vyombo vya habari amabyo ilitolewa na mmoja wawafanyabiahara maarufu,Bwana Mengi kuhusu watuhumiwa wa ufisadi kwamba wanaeneza fitna dhidi yake, na badala yake kurejesha mapesa ya umma waliyoiba.

      Ukiangalia kwa Undani,kuhusu kauli hii ni kuwa inawezekana kabisa Mengi anawafahamu wanoeneza fitina juu yake,kwanini hakuwataja watu hao.Mhe . Mengi amekuwa akitaka huruma toka kwa watanzania bila yeye kuguswa huku ni mmoja wao ambao wamesababisha sisi tuwe hapa.


      Naomba ninukuu moja ya maneno ya mengi ni kuwa "Nawaomba ndugu zangu Watanzania waone kwamba hekaheka hizi za mafisadi na waongo zina nia mbaya na ni fitna zenye nia ya kujenga chuki na kuvuruga amani,”.Hii inaonesha ni jinsi ganiMengi anawafahamu hao ambao wanataka kuvuruga amani ya nchi na kwanini asiwapeleke katika Vyombo vya kisheria ili waadhibiwe.Naomba Ahojiwe na watu wa usalama na aeleze umma ni kina nani ambao wanataka kuhatarisha amani ya nchi yetu.

      Mengi ameenda mbali zaidi,kwamab wanaharibu mahusiano yake na rais wa nchi,hapa mie nimeshindwa kuelewa faida yake ni ipi kama akiwa karibu na viongozi wa juu wa nchi..Inasaidia nini?Kama ana mpango wa kuwasaidia watanzania siyo lazima kuwa karibu na Rais wa nchi.

      Kimsingi nimekereka na taarifa hii,haina manufaa kwa sisi watanzania zaidi ya kuchochea vurugu na kuharibu mwelekeo wa Hotuba aliyoitoa Mhe. Rais Wiki iliyopita.rais aliweza kuziba kelele za muungano na akaongelea mambo muhimu ya nchi yetu hasa suala la mipango iliyopo ya chuo kikuu cha DODOMA.

      Watu wanatumia siasa kupata sympath,kama wana gomvi wao wa kibiashara siye hautuhusu.


      Kwa hili Mengi ameteleza,na kamwe asipende kutegemea huruma za wananchi,kama anawaju mafisadi na awataje kwa majina ns iyo kuzungumza kwa uhalisia.
      As long as I am leader, Our position is not going to change from that of our forefathers. I do not want the responsibility for selling the rights of our children yet unborn

    18. #16
      mutua12's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th August 2008
      Posts : 39
      Rep Power : 556
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Yes I have said..Mengi naye Achunguzwe na asitegemee Huruma Za wananchi!

      Kwa hili Mengi ameteleza,na kamwe asipende kutegemea huruma za wananchi,kama anawaju mafisadi na awataje kwa majina ns iyo kuzungumza kwa uhalisia.[/SIZE][/QUOTE]

      yamekuwa hayo, kila mtu anazake

    19. #17
      MwanajamiiOne's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 24th July 2008
      Location : On My Seat
      Posts : 9,306
      Rep Power : 13761
      Likes Received
      5150
      Likes Given
      4535

      Default Re: Yes I have said..Mengi naye Achunguzwe na asitegemee Huruma Za wananchi!

      Kumbe sikuwa peke yangu......!

      Au angalau angetujulisha hayo waliyomfanyia hata aseme wanataka kuvuruga amani then we (Tanzanians) ndo tujaji kama ni mbinu za kuvuruga amani au ni personal issues zao yeye na wao. Kuna kilichofichika hapa

      Sijui pengine amekisema sikukisikia. mimi huwaga nabadilisha chanel mara awekwapo huyu maana akianza kuhutubia basi wimbo unaanza chanel 5 na kuisha bado akiongea..... anabore sometimes.!
      LOVE is a flower, and YOU,its only seed
      Mjukuu Mtiifu, 2012.

    20. #18
      Msongoru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2008
      Location : Japan
      Posts : 305
      Rep Power : 628
      Likes Received
      14
      Likes Given
      37

      Default Re: Yes I have said..Mengi naye Achunguzwe na asitegemee Huruma Za wananchi!

      Kwa kweli... Huyu mzee anaheshimika lakini amekuwa na tabia fulani ya kutuweka Watanzania upande wake kila akizungumzia matatizo yake na wafanyabiashara wenzake!!! Nakumbuka hata wakati wamepelekana mahakamani na Manji alipohojiwa alikuwa anajiunganisha na Watz kana kwamba tunajua bifu lao. Nimemfuatila kwa muda mrefu ni mtu anayetafuta public sympath siku zote.

      Itabidi naye achunguzwe, mbona kodi alizokwepa watu wanaelewa na hawasemi? au tuanike uozo wake hapa Jf? Nadhani hajawa msafi kiasi cha kujiunganisha na watanzania kana kwamba tuna vita moja na yeye!

      Sio kweli hata kidogo!!!! Na wewe kwa maana moja au nyingine ni.....

    21. #19
      wajinga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th June 2008
      Posts : 152
      Rep Power : 587
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Yes I have said..Mengi naye Achunguzwe na asitegemee Huruma Za wananchi!

      mengi sio fisadi magazeti yake yanaandika habari za ufisadi, kwani nyie hamwajui mafisadi mbona sasa tunakuwa kama hatuwajui. walishatajwa na wakatishia kwenda mahakamani labda wameficha ukweli sasa lakini hakun mtanzania mwenye akili timamu asiyewajua mafisadi hapa.ni kama vile kusema hakuna ukimwi tanzania na hakuna mmoja wetu ambae hajakumbwa na janga la ukimwi. linganisha ukimwi na ufisadi.

    22. #20
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1174
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Yes I have said..Mengi naye Achunguzwe na asitegemee Huruma Za wananchi!

      Mengi anashangaza sana kila anapozidiana kete na wenzie yeye hukimbilia kwa wananchi kuomba sympathy. Ch akushangaza hapa imemwaga hilo press realease lake tata na kuweka mafumbo chungu nzima sjui anatagemea nani ategue hicho kitendandawili. Kwanini asiwataje hao watu anaishia kumwaga mafumbo?

      Ni usanii kwa kwenda mbele........
      Mkulima kala Mbegu......

    Page 1 of 3 123 LastLast

    Similar Topics

    1. Mukama alia: Tutawaondoa tu mafisadi, hatuogopi
      By SILENT ACtOR in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 49
      Last Post: 28th June 2011, 10:12
    2. Kikwete: Waziri yeye, katibu mkuu yeye, injinia yeye
      By maandamano in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 8
      Last Post: 12th May 2011, 19:28
    3. Spika Sitta alia na mafisadi wa bara la Afrika
      By BAK in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 3
      Last Post: 8th May 2009, 09:40
    4. Makamba amwinda Mengi, yeye awataja mafisadi rasmi!
      By BAK in forum Jamii Intelligence
      Replies: 486
      Last Post: 4th May 2009, 09:12
    5. Tetesi: Mafisadi wanatumia fedha za wizi kujisafisha- Mengi
      By mmaroroi in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 7th January 2009, 17:13

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...