Chuma ulete yazua songombingo Dar, Wakimbiza pesa benki kwa hofu - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Habari na Hoja mchanganyiko


Habari na Hoja mchanganyiko Una jambo umeliona kutoka chanzo chochote cha habari? Usisite, liweke hapa uwahabarishe wenzako. Hoja binafsi pia ziwekwe hapa.


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 5th August 2008, 03:12 PM   #1
Chuma ulete yazua songombingo Dar, Wakimbiza pesa benki kwa hofu
mwanaizaya mwanaizaya is offline 5th August 2008, 03:12 PM

Chuma ulete yazua songombingo Dar, Wakimbiza pesa benki kwa hofu

*Wakimbiza pesa benki kwa hofu

Na Adam Hussein

MZOZO mkubwa huenda ukazuka kati ya baadhi ya wenye nyumba na wapangaji katika maeneo mbalimbali wilayani Temeke huku wapangaji wakidai kuwa wenye nyumba wanaingia mifukoni mwao kwa kutumua juju na kuchomoa pesa zao kimiujiza kwa mtindo unaojulikana zaidi kama chuma ulete.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya wapangaji katika maeneo ya Kigamboni, Mtoni na Yombo wamekuwa kwenye mzozo mkubwa na wenye nyumba kwa imani kuwa wanaibiwa pesa zao kimiuijiza na kuwaacha kwenye lindi la umaskini.

Baba mmoja anayeishi Kigamboni aliyeomba jina lake lisitajwe kwa hodu ya kutimuliwa kwenye nyumba amedai, anashangazwa na mzee mwenye nyumba ambaye amekuwa akifukiza madawa fulani ndani ya nyumba na kusababisha baadhi yao kuhama kwa kuhofia pesa zao zisichukuliwe.

"Kila anapofukiza dawa hizo, utakuta mpangaji yoyote akiingia na pesa na kuziweka nyumbani, zinapotea katika mazingira ya kutatanisha au matumizi yasiyojulikana na kujikuta pesa inakwisha haraka," amelalamika na kuongeza: " "Lakini asipofukiza dawa utakuta pesa inatulia na unaweza kufanya mambo ya maana."

Akadai kuwa baba huyo ana wake wawili hana kazi na familia inakula na inalala na si kwamba ana watoto wakubwa wanaomsaidia kwani yeye anashinda amekaa akicheza bao katika vijiwe vya eneo hilo na muda wa chakula ukifika anakula na kulala.

Hofu hiyo ya kupoteza pesa kwa njia hiyo sasa imewafanya wakazi wengi wa jiji kukimbilia benki mara tu wanapopokea mishahara au malipo yoyote kutokana na biashara zao wakidai kwamba wanazinusuru na wenye nyumba wajanja.

Mama mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina la Apronia amesema: "Ilibidi niende kwa mganga ili atambue nini kinachofanya nishindwe kufanya maendeleo wakati nina uwezo wa kuingiza pesa za kutosha ambazo zinaweza kunipa maendeleo makubwa. Mganga alinishauri nihame nyumba na nikaanza kupata maendeleo."

Hamza Jumanne anayeishi katika Nyumba za Tazara Temeke anashangazwa na matumizi ya pesa siku hizi. "Tuko watu watano kwenye familia ila nikipata shilingi elfu hamsini Ijumaa nikifika Jumatatu ninakuwa sina kitu. Sio bure, naona tunachezewa," amedai.

Mkazi wa Kurasini, Joseph Mlawa amekana akisema kwamba chuma ulete ni imani za watu ambao hawajui kwamba kutokana na mfumuko wa bei pesa inatumika nyingi kununulia vitu vichache.

"Hapa hakuna mchawi. Ni kupanda tu kwa hali ya maisha kwa sababu kama mwaka jana ulitumia sh 10,000 kununua vitu vitano, leo utatumia pesa hiyo kununua vitu viwili vitatu tu. Kama ni chuma ulete inaletwa na hali ya uchumi na wala siyo wenye nyumba," amesema Mlawa.

Amesema kuwa wanaoamini kwamba kuna chuma ulete wanashindwa kwenda na wakati na kufuatilia vizuri mabadiliko ya bei za vitu, mapato na matumizi yao nyumbani na nje ya nyumba.

"Kila siku tunaambiwa shilingi inashuka thamani maana yake ni kwamba unatumia pesa nyingi kununua vitu vichache tu. Hebu angalia kwa sasa nauli zinapanda, vinywaji vinapanda, mboga zinapanda, dawa zinapanda na hata hao waganga wanaotuambia kuna chuma ulete wamepandisha dau. Nasema chuma ulete ipo kwenye hali halisi ya maisha lakini siyo wenye nyumba," amesisitiza.

Imani kwamba kuna chuma ulete inazidi kuota mizizi hasa jijini Dar es Salaam ambapo matumizi ya pesa ni makubwa huku baadhi wakiamini kwamba wanachomolewa pesa kwa kutumia madawa na wengine wakiamini kwamba kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma ndiko kunasababisha hali hiyo.

mwanaizaya
Senior Member
Points: 132,282, Level: 100 Points: 132,282, Level: 100 Points: 132,282, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
Join Date: Sat Apr 2008
Posts: 135
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Views: 197
Reply With Quote
  #2  
Old 5th August 2008, 03:37 PM
Faith Faith is offline
Faith has no status.
Member
Points: 90,559, Level: 100 Points: 90,559, Level: 100 Points: 90,559, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Wed Jul 2008
Posts: 47
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
Faith will become famous soon enoughFaith will become famous soon enoughFaith will become famous soon enoughFaith will become famous soon enoughFaith will become famous soon enoughFaith will become famous soon enoughFaith will become famous soon enoughFaith will become famous soon enough
Default Re: Chuma ulete yazua songombingo Dar, Wakimbiza pesa benki kwa hofu

du! hii kali hizi imani balaa lkn nashukuru zimesaidia kwani atlast watu wanakimbiza pesa zao bank mahali ambapo ni salama zaidi
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
benki, chuma, dar, hofu, pesa, songombingo, ulete, wakimbiza, yazua


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Kazi ya kuubomoa upinzani ndiyo imeanza ama inatekelezwa? Mugishagwe Jukwaa la Siasa 12 2nd February 2010 10:21 AM
Majambazi Arusha: Mabomu, Bunduki, Risasi, Bastola - Hii ni Kashfa JWTZ Hasara Jukwaa la Siasa 225 11th December 2009 03:53 PM
Sera Ya Vijana; 'inaeleweka?' John Mnyika Habari na Hoja mchanganyiko 6 10th August 2008 09:54 AM
When the Pressure Group Called ...before the hurricane.... Taasisi Jukwaa la Siasa 11 13th April 2008 10:50 PM
The Confession of Nazir Karamagi Zitto Jukwaa la Siasa 40 4th March 2008 10:10 AM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 04:11 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com