Wakuu nimechunguza siku moja baada ya bunge kupitisha bajeti ya wizara ya nishati na madini mgao wa umeme umerejea katika makali yake.kwa wale walioko arusha mnaweza kuelezea jinsi mgao wa umeme ulivyokuwa kuanzia jana (jumapili)
Wakuu nimechunguza siku moja baada ya bunge kupitisha bajeti ya wizara ya nishati na madini mgao wa umeme umerejea katika makali yake.kwa wale walioko arusha mnaweza kuelezea jinsi mgao wa umeme ulivyokuwa kuanzia jana (jumapili)
Morogoro leo kumekuwa na Mgao kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa mbili na nusu usiku. Nakubaliana kuwa mgao umeongezeka baada hiyo bajeti.
Jana umeme ulirudi saa mbili na nusu usiku na kukatika saa tano kamili.kwa ufupi umeme ulipatikana kwa masaa mawili na nusu in 24 horas.nimeanza kuhesabu masaa ambayo umeme hautakuwepo kwa leo(kuanzia saa 6 usiku)
kweli ngeleja mtoto wa mjini!
Heri yenu waunaukata kwa ratiba inayojulilama huku kwetu ROMBO unakatwa na kurudishwa bila mpangilio kana kwamba unatusababishia hasara kubwa ya kuunguliwa na vitu je nikwamba wanakomoa majimbo yanayongozwa na CHADEMA?
Pole sana Jackbauer,
Jifunze kutumia ubongo wako vizuri kutafuta njia mbadala za kupata umeme badala ya kutegemea umeme wa Tanesco!
Sisi wa line ya magogoni ndogo hatuelewi mgao ni kitu gani.
Niko Temeke tayari hamna nishati kuanzia saa kumi na moja unusu alfajiri
Kijitonyama umekatika saa 8 za usiku mpaka muda huu haujarudi bado
Serkali inatufanya wananchi wake kuwa sisi ni 'wajinga ndio waliwao'
grrrrrr! aaaaaaghhh! sijui nitukane tusi gani ambalo halina ban!!!!huku kwetu umeme ulikatika juzi jumapili saa kumi na moja asubuhi umerudishwa usiku wa leo nadhani saa saba au nane kwani nilikuwa macho hadi saa sita, nimeamka nakuta kuna umeme ile nachomeka tu kalaptop kangu kwenye charger wamechukua megawati zao!amaaa kweli tanzania bila umeme inawezekana, big up ngeleja
MBUZI WA NINI UNAPOKWENDA MIKUMI KUWINDA
Follow Us Here