Black Mafya wateka mtoto Dar - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Habari na Hoja mchanganyiko


Habari na Hoja mchanganyiko Una jambo umeliona kutoka chanzo chochote cha habari? Usisite, liweke hapa uwahabarishe wenzako. Hoja binafsi pia ziwekwe hapa.


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 18th July 2008, 06:59 AM   #1
Black Mafya wateka mtoto Dar
Bubu Msemaovyo Bubu Msemaovyo is offline 18th July 2008, 06:59 AM

Ukisoma taarifa hizi utadhani unaangalia filamu fulani ya kutisha, lakini ukizinduka na kuona kumbe huoni picha bali unasoma ndipo unapata mawazo mapya kwamba huenda uko sehemu nyingine na siyo hapa Tanzania tunapopaita "Kisiwa cha Amani" ili uweze kukubaliana nami soma hapa.

Click image for larger version

Name:	Mtoto atekwa Dar.jpg
Views:	63
Size:	24.6 KB
ID:	1823

*Watoa masharti ya kupewa sh. milioni 10
*Baba mtu ajitosa msituni usiku kuwapelekea

Na Mwandishi Wetu

KUNDI la majambazi linalojiita Black Mafya, limemteka mtoto Fardosa Mohamed Othuman (2), mwenye asili ya kisomali mkazi wa Mtoni Saba Saba, Dar es Salaam.

Tukio la kutekwa kwa mtoto huyo ambalo lilitokea juzi saa 3 asubuhi karibu na baa ya Ikweta Grill.

Akizungumzia tukio hilo Dar es Salaam jana, mama mzazi wa mtoto huyo, Bibi Anab Ahmed, alidai kuwa mtoto wake alitekwa saa tatu asubuhi, huku watekaji wakiacha masharti makali kwa familia yake.

Alidai kuwa masharti yaliyoachwa na watekaji hao ni kwamba hawatakiwi kutoa taarifa sehemu yoyote wala kituo chochote cha Polisi na wakibainika kufanya hivyo, mtoto waliyemteka atauawa.

"Ni tukio la kusikitisha katika familia yetu, kwani baada ya mtoto kuchukuliwa na watu hao, wakatuachia masharti makali yakiwamo ya kututaka tufiche siri kwa kutosema kwa mtu yeyote kupitia barua ambayo walikuwa wameleta saa chache kabla ya kumteka mtoto wangu," alidai Bibi Ahmed.

Aliongeza kuwa masharti mengine yalikuwa ni kupewa sh. milioni 10 ili mtoto huyon aachwe akiwa salama.

Alidai siku ya tukio kabla ya mtoto wake kutekwa kuna mtu alipeleka barua nyumbani kwao akidai kuwa ni ya mumewe.

Wakati huo nyumbani kulikuwa na watoto huyo na wengine na wafanyakazi wa ndani wawili, hivyo walichukua ile barua na kuiweka ndani ili baba yao atakaporudi wampe.

Baada ya muda mfupi kupita, mtoto huyo ambaye alikuwa ndani ya eneo la uzio wa nyumba yao, aligundulika kutoweka.

"Muda wote mtoto alikuwa akicheza ndani na wala hakutoka nje ya lango la nyumba yetu, lakini cha kushangaza baada ya yule mtu kuleta barua, alipoondoka mtoto hatukumwona ndipo tulipomtafuta bila mafanikio.

"Hata hivyo, tuliamua kupiga simu kwa baba yake kumpa taarifa za kupotea kwa mtoto na kumweleza kuwa kabla ya mtoto kutekwa, kuna barua yako imeletwa na watu ambao ndio watakuwa wamemchukua," alidai Bibi Ahmed kwa masikitiko makubwa.

Baada ya taarifa hiyo, baba wa mtoto, aliwaruhusu waisome barua hiyo, kwani yeye hakuahidiana na mtu kupeleka barua nyumbani, na walipoisoma ile barua, ndipo ilipoonesha wazi kuwa mtoto ametekwa na majambazi hao.

Alidai kuwa ndani ya barua hiyo kulikuwa na vitisho kwa wazazi kwamba vizipotekelezwa mtoto wao atakuwa hatarini.

Aliendelea kudai kwamba ilipofika saa 7 mchana, watu hao walipiga simu kwa baba na kusisitiza kuwa watamwachia iwapo atatimiza masharti yao kabla ya saa 24 kupita.

"Ilituchukua muda kuamini kama mtoto wetu yuko hai au la kwa sababu kila tulipotafakari tulishindwa kuelewa, lakini tulichofanya ni kumwomba Mungu mtoto wetu tumkute salama," alidai Bibi Ahmed.

Aliongeza kuwa majambazi hao walitoa taarifa kwamba wangepiga simu tena saa 11 jioni kujua wapi wanaweza kukutana na baba wa mtoto, ili wapewe fedha walizohitaji ili wamwachie mtoto huyo.

Hata hivyo kuanzia saa 7.30 mchana simu waliyokuwa wakitumia majambazi hao ilizimwa na kuwashwa saa 12 jioni na kupiga simu kwa baba wa mtoto wakitaka wakutane maeneo ya Mbagala katika vichaka.

Alidai kuwa baba wa mtoto alikubali amri hiyo na kuchukua sh. milioni 3.5 baada ya kukosa sh.milioni 10 waliyokuwa wakiihitaji majambazi hao.

"Ukweli hatukuwa na kiasi hicho cha fedha, hivyo tulichukua sh. milioni 3.5 na baba wa mtoto kwenda walikopanga kukutana. Baada ya kufika ikiwa ni saa 3 usiku, alifuata maagizo ya kuweka fedha hizo chini.

"Walizichukua fedha hizo na kumwachia mtoto na kurudi naye wakafika nyumbani saa nne usiku wa kuamkia leo (jana)," alisisitiza Bibi Ahmed.

Alidai mtoto huyo alikuwa amechoka na aliporudi nyumbani na inawezekana ni kutokana na kukosa kula kwa muda wote aliokuwa mateka.

Alieleza kuwa walifuatilia Polisi Chang'ombe jana asubuhi, ili kujua kama majambazi waliokuwa wamemteka mtoto wao wanafahamika lakini wakaambiwa bado uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika.

Kwa upande mwingine, walisema ulinzi uliopo katika eneo hilo ni mdogo na hivyo ni vigumu wao kutambua nani adui na nani mwema.

"Tunaishi kwa hofu na mashaka makubwa hivi sasa, maana hatujui nini kitafuata baada ya tukio hili, ukiangalia na masharti tuliyokuwa tumepewa na watu hao," alisema dada wa mtoto aliyetekwa, Bi Saad Mohamed.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Bw. Emmanuel Kandihabi alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo, na kusema uchunguzi unaendelea ili kuwakamata waliohusika na utekaji huo.

Wakati huo huo, wakati waandishi wawili wa gazeti dada la Dar Leo, Bi Stella Aaron na mpiga picha Charles Lucas wakifuatilia tukio hilo nyumbani kwa mateka, waliwekwa chini ya ulinzi na polisi wa Chang'ombe wakidaiwa kuingia nyumbani kwa mtu bila idhini.

Kamanda Kandihabi alipouliuzwa kuhusiana na hatua hiyo, alisema alitoa amri ya kukamatwa kwa wanahabari hao ili kuwahoji na kujiridhisha kama hawakuwa wamevamia nyumba ya mtu baada ya baba wa mtoto kuwatilia shaka.

"Tumewakamata ili kuona kama hawa waandishi walivamia au la, kwani tukio lenyewe ni la ndani...lingekuwa la hadharani tusingehangaika nao, lakini mtu yuko ndani nyumbani kwake akifanya mambo yake, unaingiaje huku amefunga milango?," alihoji Kamanda huyo na kusema aliwasiliana na baba wa mtoto ambaye alionesha wasiwasi wa watu kuingia nyumbani hapo.


http://www.majira.co.tz/kurasa.php?s...bariNamba=7339

__________________
"If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart." Nelson Mandela

 
Bubu Msemaovyo's Avatar
Bubu Msemaovyo
JF Senior Expert Member
Points: 352,922, Level: 100 Points: 352,922, Level: 100 Points: 352,922, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
Join Date: Wed May 2007
Location: All around the World
Posts: 895
Thanks: 0
Thanked 3 Times in 3 Posts
Views: 461
Reply With Quote
  #2  
Old 18th July 2008, 09:08 AM
Bill Bill is offline
Bill says: Kukumbatia ufisadi pia ni ufisadi
JF Senior Expert Member
Points: 196,857, Level: 100 Points: 196,857, Level: 100 Points: 196,857, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Fri Oct 2007
Posts: 631
Thanks: 32
Thanked 30 Times in 19 Posts
Rep Power: 24
Bill will become famous soon enoughBill will become famous soon enoughBill will become famous soon enoughBill will become famous soon enoughBill will become famous soon enoughBill will become famous soon enoughBill will become famous soon enoughBill will become famous soon enough
Default Re: Black Mafya wateka mtoto Dar

Du kizungumkuti, Dar tumefikia hatua hiyo.
Reply With Quote
  #3  
Old 18th July 2008, 09:28 AM
Kidatu Kidatu is offline
Kidatu has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 196,229, Level: 100 Points: 196,229, Level: 100 Points: 196,229, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Wed Jun 2008
Posts: 615
Thanks: 55
Thanked 17 Times in 13 Posts
Rep Power: 63
Kidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the roughKidatu is a jewel in the rough
Default Re: Black Mafya wateka mtoto Dar

Poleni sana wazazi na ndugu wa mtoto huyo.

Utekaji kama huo zingefanyiwa familia za mafisadi ili zirudishe mapesa yetu na mali zetu zote.
Reply With Quote
  #4  
Old 18th July 2008, 10:23 AM
Single D's Avatar
Single D Single D is offline
Single D has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 95,552, Level: 100 Points: 95,552, Level: 100 Points: 95,552, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Feb 2007
Location: Duniani
Posts: 439
Thanks: 2
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 24
Single D will become famous soon enoughSingle D will become famous soon enoughSingle D will become famous soon enoughSingle D will become famous soon enoughSingle D will become famous soon enoughSingle D will become famous soon enoughSingle D will become famous soon enoughSingle D will become famous soon enough
Default Re: Black Mafya wateka mtoto Dar

Duh,hiyo kali sana.pesa inatafutwa kwa nguvu
Hawa walijua kabisa wangeweza kupata chochote pale na nadhani wanamfahamu mhusika kwa karibu na nyendo zake zilikuwa zikufuatiliwa,Mwenye njaa hawezi kwenda hospitalini kutafuta chakula bali ataenda hotelini.

Tukio kama hili liliwahi tokea jijini Dar,pale MAGOMENI h/girl kutokomea na mtoto Dodoma na wazazi wakawa wanapigiwa simu tu na kupewa masharti,wahusika walitegewa mtego wakakamatwa na polisi.
__________________
'Without unity, there is no future for Africa' J.K.Nyerere,1997,Accra Ghana.
Reply With Quote
  #5  
Old 18th July 2008, 11:27 AM
Shapu's Avatar
Shapu Shapu is offline
Shapu a Citizen of the World
JF Senior Expert Member
Points: 151,439, Level: 100 Points: 151,439, Level: 100 Points: 151,439, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Thu Jan 2008
Location: Citizen of the World
Posts: 766
Thanks: 211
Thanked 67 Times in 49 Posts
Rep Power: 24
Shapu will become famous soon enoughShapu will become famous soon enoughShapu will become famous soon enoughShapu will become famous soon enoughShapu will become famous soon enoughShapu will become famous soon enoughShapu will become famous soon enoughShapu will become famous soon enough
Default Re: Black Mafya wateka mtoto Dar

Mhhh. Hii ni habari motomoto kwa Kamand Kova. Hii styl ni mpya sasa bongo.
__________________
"If silence is golden,speech is platinum.It dispels ignorance,ventilates grievances,stimulates curiosity and lessens the fundamental loneliness of the soul."
Reply With Quote
  #6  
Old 18th July 2008, 01:03 PM
Nemesis Nemesis is offline
Nemesis has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 312,655, Level: 100 Points: 312,655, Level: 100 Points: 312,655, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Wed Feb 2008
Posts: 2,051
Thanks: 84
Thanked 185 Times in 93 Posts
Rep Power: 67
Nemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the roughNemesis is a jewel in the rough
Default Re: Black Mafya wateka mtoto Dar

wakiteka mtoto wa masikini asie na hata laki 1 (100,000) itakuwaje? umh au mambo ya kuzulumiana! i can't believe.

Na hao waandishi wa habari walioingia huku milango imefungwa ilikuwaje?
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
black, dar, mafya, mtoto, wateka


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Majambazi Arusha: Mabomu, Bunduki, Risasi, Bastola - Hii ni Kashfa JWTZ Hasara Jukwaa la Siasa 225 11th December 2009 03:53 PM
Mapambano ya Polisi na MajambaziArusha Yapamba moto! Pinokyo Jukwaa la Siasa 34 10th May 2008 01:07 AM
Why and How the African Child is Miseducated in the Western Educational System Mtoto wa Mkulima Jukwaa la Elimu (Education Forum) 1 16th November 2007 10:06 PM
Karibu Dar Es Salaam Shy Habari na Hoja mchanganyiko 1 20th August 2007 06:41 AM
Black Economic Empowerment (BEE), A good move to Copy in Tanzania? FairPlayer Business & Economic Forum 4 25th August 2006 02:25 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 08:45 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com