Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

    Report Post
    Results 1 to 14 of 14
    1. #1
      kyemo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 62
      Rep Power : 444
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Hivi karibuni kumekuwa na matangazo mbalimbali yakitoka kwenye mabango na Television lakini hayabebi uhalisia kutokana na muonekano wa washiriki wa matangazo hayo

      Mfano:

      kama umebahatika kupita maeneo ya sinza Afrika sana karibu kabisa na kona baa(corner bar/Ambianze night club)
      kuna bango moja kubwa lenye Tangazo la mtoto wa mwenzio ni wako,linalohamasisha watu wazima kuacha kuwatongoza watoto wa shule

      Tatizo ni kwamba huyo mtoto wa shule mwenyewe hana uhalisia wa kuwa mtoto wa shule,yani kuanzia mavazi hadi muenekano wake hauendani kabisa na kinachotangazwa kwenye bango hilo

      Mfano wa pili:

      Kama ni muangaliaji mzuri wa Television kuna matangazo mawili moja likimuonesha mwanafunzi akitumia simu darasani wakati mwalimu akifundisha na la pili likimuonesha muhusika huyohuyo aliyekatazwa kutumia simu shuleni akiwa amerudishwa nyumbani kwa kosa la kukutwa na simu shuleni

      Tatizo pia linakuja muhusiaka habebi muonekano wa kiuanafunzi,yani zaidi ya mwanafunzi

      Kama umeshawahi kuona hayo matangazo niliyoyasema hapo juu,unadhani ni kweli hayo matangazo yanabeba maudhui au maana halisi ya matangazo hayo,sababu wahusika wenyewe hawabebi ujumbe kwa muonekano wao

      Ni mawazo tu naomba mawazo yako tafadhari labda mimi nimekuwa rigid sana.........


    2. #2
      Avatar's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2011
      Posts : 557
      Rep Power : 542
      Likes Received
      54
      Likes Given
      12

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Ndo wanafunzi wa kisasa walivyo!...

    3. #3
      'The Choosen''s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Location : Humuhumu
      Posts : 427
      Rep Power : 519
      Likes Received
      58
      Likes Given
      18

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      msiyazingatie matangazo ya kipuuzi namna hiyo............endeleeni na mambo yenu kama kawa.mambo yamebadilika,kila mtu atajiambia mwenyewe tu
      Siasa ni hoja na si vinginevyo

    4. #4
      kyemo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 62
      Rep Power : 444
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Quote By Avatar
      Ndo wanafunzi wa kisasa walivyo!...
      Ina maana wanafunzi wa kisasa ndio kama wale wanaotumika kwenye matangazo?????
      kama ndio hivyo basi matangazo hayo yamechelewa

    5. #5
      kyemo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 62
      Rep Power : 444
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Quote By 'The Choosen'
      msiyazingatie matangazo ya kipuuzi namna hiyo............endeleeni na mambo yenu kama kawa.mambo yamebadilika,kila mtu atajiambia mwenyewe tu
      Matangazo sio ya kipuuzi mzee.........yana ujumbe mzuri sana, tatizo lipo kwa wanaobeba ujumbe kuufikisha kwenye jamii(wahusika) hawaonekani kujaa kwenye maudhui!!!!
      hata mimi leo nikikwambia piga picha kama mwanamuziki upo kwenye jukwaa unaimba wimbo wa furaha lakini wewe ukauvaa uhusika kama upo shambani unalima haitaleta maana mzee.......


    6. #6
      NEGLIGIBLE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2011
      Location : TANZANIA
      Posts : 277
      Rep Power : 479
      Likes Received
      50
      Likes Given
      120

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Umesomea marketing?

    7. #7
      chetuntu's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 10th January 2011
      Location : Paediatrique ward
      Posts : 956
      Rep Power : 619
      Likes Received
      100
      Likes Given
      90

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Umeshawaona wanafunzi wa siku hizi ,wanja,lipbam, wave, hereni , pouwda nk. Wanafunzi wa sasa ndio hao hawana uhalisia wa kiuwanafunzi hasa wa mijini.

    8. #8
      kyemo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 62
      Rep Power : 444
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Quote By NEGLIGIBLE
      Umesomea marketing?
      Sidhani km kusomea Marketing kuna uhusiano wowote na haya matangazo, Cause haya matangazo hayatangazi products or service zozote bali yanaelimisha maadili au kuweka madadili sawa katika jamii mzee

    9. #9
      kyemo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 62
      Rep Power : 444
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Quote By chetuntu
      Umeshawaona wanafunzi wa siku hizi ,wanja,lipbam, wave, hereni , pouwda nk. Wanafunzi wa sasa ndio hao hawana uhalisia wa kiuwanafunzi hasa wa mijini.
      kaama ndio wanafunzi wa siku hizi ndivyo walivyo, basi hakuna shaka lakini km sio......... they are totally wrong!!!!!!!!!!!!

    10. #10
      Bumela's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd September 2009
      Posts : 128
      Rep Power : 520
      Likes Received
      8
      Likes Given
      45

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Quote By kyemo
      kaama ndio wanafunzi wa siku hizi ndivyo walivyo, basi hakuna shaka lakini km sio......... they are totally wrong!!!!!!!!!!!!

      Ndugu ya hawa hawajaelewa somo na ndio maana wanakujibu hivyo lkn sisi tulioelewa tumekupata.Hao wanatafuta hela ziende kwao tu maana wanaona wakiwatumia wabeba ujumbe halisi watazikosa hizo hela kwa hiyo wanafanya bora liende.Uko sahihi kabisa mi ndio maana hatakuwaangalia nimeacha ujumbe tofauti na wahusika tofauti.Ni sawa na mtu anaigiza stori ya kijijini lakini anaonekana Kariakoo sokoni, maneno ya kijijini muonekano wa mjini.Nadhani pana haja ya kuwafikishia ujumbe wahusika.

    11. #11
      kyemo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 62
      Rep Power : 444
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Quote By Bumela
      Ndugu ya hawa hawajaelewa somo na ndio maana wanakujibu hivyo lkn sisi tulioelewa tumekupata.Hao wanatafuta hela ziende kwao tu maana wanaona wakiwatumia wabeba ujumbe halisi watazikosa hizo hela kwa hiyo wanafanya bora liende.Uko sahihi kabisa mi ndio maana hatakuwaangalia nimeacha ujumbe tofauti na wahusika tofauti.Ni sawa na mtu anaigiza stori ya kijijini lakini anaonekana Kariakoo sokoni, maneno ya kijijini muonekano wa mjini.Nadhani pana haja ya kuwafikishia ujumbe wahusika.
      Sahihi kabisa,yani umenipata vizuri sana na nimeupenda zaidi mfano wako

    12. Kbd
      #12
      Kbd's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th October 2009
      Posts : 942
      Rep Power : 681
      Likes Received
      294
      Likes Given
      139

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Ni kweli hata mimi nimeshawahi kujiuliza kuhusu hilo tangazo la mtoto wa mwenzio ni wako; yaani huyo mdada ni kama changu fulani tu ni dizaini za wadada (kwa muonekano) wanaotafuta mashuga dadi halafu ati anakataa.
      Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu.....Zab 23:6

    13. #13
      Mwendabure's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2011
      Posts : 1,047
      Rep Power : 628
      Likes Received
      180
      Likes Given
      41

      Default Re: Washiriki wa matangazo na uhalisia wake

      Naona kuna kila dalili za kupeana ulaji linapokuja suala la uteuzi wa wahusika ktk tangazo husika. Na si matangazo tu, hadi ktk filamu zetu mambo haya ndo yamepitiliza. Ubabaishaji unaua sekta nyingi nchini. Sitaki kuamini kuwa tumelaaniwa sisi...loooh!!

    14. #14
      Mutambukamalogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th January 2011
      Posts : 401
      Rep Power : 505
      Likes Received
      58
      Likes Given
      3

      Default

      [QUOTE=kyemo;1766249]Sidhani km kusomea Marketing kuna uhusiano wowote na haya matangazo, Cause haya matangazo hayatangazi products or service zozote bali yanaelimisha maadili au kuweka madadili sawa katika jamii mzee[/QUOTE. Mkubwa modern marketing ina cover kila angle. Bidhaa,huduma mbalimbali hata zitolewazo na taasisi za kijamii na taasisi za kidini zote zipo covered na marketing. Haujasikia tangazo la Rwakatare radio clouds au haujaona tangazo la kuwahimiza watu wajifunike net. Yote yanalenga final objective ya marketing.

    Similar Topics

    1. Maana na uhalisia wa Degree ya heshima
      By OSOKONI in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 0
      Last Post: 22nd October 2011, 08:56
    2. Bajaji za Wajawazito, Uhalisia na Vipaumbele vya Taifa
      By Gurudumu in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 0
      Last Post: 10th March 2011, 10:52
    3. MAJINA NA UHALISIA(Without Prejudice)
      By mayenga in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 10
      Last Post: 11th January 2011, 14:30
    4. Najitambulisha kwa uhalisia
      By Mathias Byabato in forum Utambulisho (Member Intro Forum)
      Replies: 28
      Last Post: 28th November 2010, 17:14

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...