Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Bosi wa bodi ya kahawa anaendesha shirika la umma kama shirika lake binafsi

    Report Post
    Results 1 to 3 of 3
    1. #1
      JICHOBODI's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 27th February 2011
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Bosi wa bodi ya kahawa anaendesha shirika la umma kama shirika lake binafsi

      Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania Mheshimiwa Adolfu Kumburu anaendesha Shirika la Umma kama shirika lake binafsi ili kutekeleza ajenda zinazomnufaisha yeye binafsi.

      Mheshimiwa Kumburu baada ya kuajiriwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa alifumua muundo wa Bodi na kuunda muundo mpya. Muundo wake huo mpya hata kabla haujaidhinishwa na Serikali akaanza kuutumia kuengua wafanyakazi aliodhania watakuwa kikwazo katika kutekeleza maslahi yake binafsi kwa kuwahamisha na au kufuta vyeo vyao.
      Pale alipoona hawezi kutumia mabadiliko ya muundo akawafukuza kwa kuwabambikiza makosa.

      Baada ya hapo akaanza kuajiri wafanyakazi wapya anaofikiri atawatumia kutekeleza maslahi yake. Ajira zake hizo mpya hazijali mahitaji halisi ya Bodi kwani mahitaji halisi yanaweza kujulikana pale tu serikali itakapokuwa imeidhinisha muundo mpya wa Bodi ya Kahawa.

      Mkurugezi Mkuu huyu ameingia ubia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambazo anazunguka nazo Ulaya na Balozi za Ulaya Magharibi(EU) kuomba pesa kusaidia maendeleo ya kahawa ambapo pesa zinazotolewa kwa NGOs hizo zinawanufaisha wao binafsi.

      Mheshimiwa Adolfu Kumburu ameingiza Bodi ya kahawa katika malumbano na viongozi wa Mkoa ya Kigoma na Wilaya ya Tarime kwa kuandika waraka zinazolinda maslahi ya makampuni yanayogharamia safari zake za Marekani.
      Matokeo yake wakulima wamefikia hatua ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari (TBC-1) kumlalamikia.

      Bila ya kujali makubaliano yaliyofanywa baina ya serikali na wawekezaji kuwaruhusu waanzishe vinu vya kukoboa kahawa ilikuboresha kahawa ya Tanzania amefuta leseni ya kununua kahawa mbivu (Cherry buying license ) ili kulinda maslahi ya Kilicafe ambayo alishiriki kuiunda wakati akiwa Technoserve isipate ushindani. Hii ni kuwahujumu wakulima kwani ushindani ngazi ya mkulima unaongeza kipato cha mkulima na ndiyo sera ya serikali. (Kuna wasiwasi kama hapokei mishahara miwili kwa kuendelea kulipwa pia na Technoserve)

      Ameshindwa kumwajili afisa utumishi ili aendeshe shirika kama mali yake binafsi kwa kuhita wajumbe wa menejimenti wa kila kikao kwa kutegemea ajenda. Anaalika wajumbe wale tu anaoona hawatahoji ajenda zake za siri.

      Wakati mwingine maamuzi ya vikao vya wakuu wa Idara anayageuza kuwa maamuzi ya menejimenti.

      Ameunda kamati ya nidhamu ambapo yeye akiwa ndie mtuhumu kwenye kikao cha nidhamu anageuka kuwa Mwenyekiti. Wakati akiwa Mwenyekiti anachofanya ni kuhakikisha anahalalisha tuhuma zake. Baadae anageuka kuwa ndiye mtoa adhabu. Kwenye vikao hivi hashirikishi hata chama cha wafanyakazi.

      Matokeo ya yote haya Mheshimiwa Aldolfu anaendesha shirika la umma bila ya kujali sheria, kanuni na taratibu za kuendesha mashirika ya umma. Wafanyakazi amewafanya kuwa mali yake binafsi ambapo haki za msingi anazitoa kama zawadi.

      Kwa muda mfupi aliokaa Bodi ya Kahawa, amejilimbikizia mali inayotokana na mahusiano na hizo NGOs pamoja na posho anazojilipa kwa kukaa muda mwingi akiwa safari. Hata hizo siku chache anazokuwa ofisini anazitumia kwa vikao ambavyo navyo anajilipa posho.

      Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa wamemuandikia barua ya wazi Waziri wa Kilimo kumuomba aingilie kati kulinda maslahi ya Taifa ili shirika la umma lisigeuzwe mali ya mtu binafsi.


    2. #2
      HakiMoja's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 9th June 2011
      Posts : 9
      Rep Power : 407
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Bosi wa bodi ya kahawa anaendesha shirika la umma kama shirika lake binafsi

      Mh waziri wa Kilimo mbona hushughulikii swala hili la bodi ya Kahawa? Au nako kuna kuchakachua? Mkurugenzi Mkuu bado anatunyanyasa na kutuhamisha bila kuzingatia haki ya watumishi. Tunakosa pakuegemea jamani. Nae awajibishwe.

    3. #3
      matengo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st June 2011
      Posts : 24
      Rep Power : 412
      Likes Received
      1
      Likes Given
      2

      Default Re: Bosi wa bodi ya kahawa anaendesha shirika la umma kama shirika lake binafsi

      Katika kutapatapa tunasikia aliwaleta waganga wa kwao ofisini kujizindika asingolewe. Pia anatumia pesa za umma kuwahonga wakubwa ili wapeleke taarifa zisizo sahihi kwa Waziri. Je TAKUKURU mko wapi.

    Similar Topics

    1. Replies: 135
      Last Post: 1st January 2012, 02:13
    2. Zanzibar Kuanzisha Shirika Lake la Ndege
      By X-PASTER in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 0
      Last Post: 11th July 2011, 21:34
    3. Siamini TBC1 kama ni Shirika la umma lenye Kutenda haki
      By jnuswe in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 1
      Last Post: 11th May 2011, 15:52
    4. Tbc ni shirika la ccm au la umma?
      By matongo manawa in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 14
      Last Post: 13th April 2011, 15:38
    5. Hivi EWURA ni shirika la umma ama la binafsi!
      By asha ngedere in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 4
      Last Post: 6th November 2009, 09:48

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...