Kenya Waamua Kuwa Na Ccm Yao - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Habari na Hoja mchanganyiko


Habari na Hoja mchanganyiko Una jambo umeliona kutoka chanzo chochote cha habari? Usisite, liweke hapa uwahabarishe wenzako. Hoja binafsi pia ziwekwe hapa.


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 20th December 2006, 10:24 PM   #1
Kenya Waamua Kuwa Na Ccm Yao
Ole Ole is offline 20th December 2006, 10:24 PM

Quote:
Ukiishangaa CCM ya Tanzania utaiona CCM ya Kenya

Mwandishi Wetu



KENYA inajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu Desemba, 2007.


Hadi sasa kuna vyama zaidi ya 63 vilivyosajiliwa na vimeshapata tiketi ya kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.


Hivi sasa kuna wimbi zito la mageuzi ndani ya vyama mbalimbali vya siasa nchini Kenya. Kila chama kimekumbwa na migogoro ya uongozi. Kwa kifupi joto la uchaguzi Kenya liko juu sana.


Kwa wanasiasa kuhama na kujiunga na vyama vingine pamoja na kuanzishwa kwa vyama vipya, ni jambo la kawaida kabisa nchini Kenya kwa sasa.


Moja ya vyama vilivyoundwa hivi karibuni ni Chama Cha Mwananchi (CCM).


Kama jina lake linavyoonyesha, CCM ya Kenya inafanana sana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Tanzania.


Kimeamua kujiita CCM kwa madai kuwa kimevutiwa na CCM ya Tanzania na kinatamani kuwa kama CCM ya Tanzania.


Chama hicho kimeanzishwa na Naibu Waziri wa Habari na Utangazaji nchini Kenya, Koigi Wamwere.


Ameanzisha chama hicho cha CCM kinachotumia kaulimbiu ya Mwanzo Mpya, Watu Wapya na Kenya Mpya.


Ufupisho wa chama hicho cha CCM ya Kenya pamoja na kaulimbiu yake, vinashabihiana sana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini hapa, ambacho mbali ya kuwa na ufupisho wa CCM, pia kinajinadi kwa kaulimbiu ya Nguvu Mpya, Ari Mpya na Kasi Mpya.


CCM ya Kenya imeanzishwa Septemba mwaka huu, na tayari imepata usajili wa kudumu, hivyo kupata tiketi ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Kenya.


Itikadi ya CCM ya Kenya inasema kuwa taa ya CCM ni Ujamaa na Demokrasia, wakati CCM ya Tanzania ilikuwa na itikadi ya Ujamaa na Kujitemegea.


Katika kuonyesha kuwa CCM ya Kenya inataka kuiiga CCM ya Tanzania, tayari CCM ya Kenya imepata nakala ya Ilani na Katiba ya CCM ili baadhi ya vipengele viweze kuingizwa kwenye Ilani na Katiba ya CCM ya Kenya.


Katibu Mkuu wa chama hicho, Sammy Mwaniki, katika mazungumzo yake na Tanzania Daima kwa njia ya simu, anasema wameamua kuiga CCM ya Tanzania baada ya kufurahishwa na jinsi chama hicho kinavyoongoza nchi.


“Ni kweli chama chetu kina mambo mengi mazuri tuliyoiga kutoka CCM ya Tanzania. Na tunafikiria kuomba mashirikiano ya kindugu na chama hicho,” alisema Mwaniki.


Alikiri kuwa chama chake kinatumia baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye Ilani na Katiba ya CCM ya Tanzania na kuiingiza kwenye Ilani na Katiba ya CCM ya Kenya. “Yote hayo tumefanya kwa nia nzuri tu ya kutaka kukiimarisha chama chetu kiwe imara na sifa kama CCM ya Tanzania,” alisema Mwaniki.


Mwenyekiti wa chama hicho Wamwere, kwa sasa ni Naibu Waziri wa Habari na Utangazaji wa serikali ya Rais Mwai Kibaki (NARC), ambaye ameamua kuanzisha chama hicho ili kishiriki uchaguzi mkuu ujao baada ya kuona NARC imepoteza mwelekeo na haina uwezo wa kushinda tena uchaguzi ujao.


Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Subukia – Nakuru, aliwahi kuishi nchini, eneo la Ilala, Bungoni, mwaka 1978 hadi 1979.

Ilani

Ilani ya Chama Cha Mwananchi (CCM), kwanza, inaamini katika uhuru, haki, usawa na uaminifu.


Ilani hiyo inasema CCM ni chama cha wananchi walioonewa na kunyanyaswa, si mabwanyenye wanyonyaji, CCM ni chama cha Wakenya wote, si cha kabila au makabila fulani.


Pia inasema CCM si shamba la wanyama, wanachama wake wote ni sawa.


CCM ni ngome ya kondoo na wala nyasi wote. Haitawaalika masimba, mafisi na mambweha zizini, mafisadi, wezi, madikteta, watesi na wasaliti wa wananchi wote ni marufuku chamani.

Kaulimbiu na itikadi

Kaulimbiu ya chama hicho inashabihiana sana na CCM, kwani inasema Mwanzo Mpya, Watu Wapya na Kenya Mpya, wakati CCM ya Tanzania inasema Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya.


Kwa upande wa itikadi, inasema Taa ya CCM ni Ujamaa na Demokrasia wakati CCM ya Tanzania inatamba na itikadi iliyokuwapo wakati ule ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ya Ujamaa na Kujitegemea.

MALENGO YA CCM-Kenya

CCM inasema itatawala kwa mujibu wa sheria, haki na kanuni za demokrasia. Lengo la CCM hiyo ni kuwapa wananchi wenye umri mdogo, wazalendo, nafasi ya kupata uongozi wa nchi.


CCM inasema daima, itapinga udikteta na itapigania katiba mpya itakayofuta mizizi ya uimla na kusimamia masilahi na haki za Wakenya wote wakati serikali yake itatetea haki zote za binadamu.


Inatamba kuwa itarejesha maridhiano miongoni mwa Wakenya kwa kuunda Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano kuchunguza madhambi yote waliyofanyiana Wakenya na kuomba wasameheane, kwani ndoto ya CCM ni kuifanya Kenya iwe nchi iliyoendelea kiuchumi.


Chama hicho kinajigamba kuwa kitakuza uchumi unaomilikiwa na Wakenya, si wageni,


kitazingatia maendeleo ya wasio nacho, ya kufuta umaskini, maradhi, njaa na upofu wa kiakili, si maendeleo ya walio nacho, viongozi na matajiri.


Malengo mengine yaliyoainishwa na CCM hiyo ni kupigania ugavi wa mali ya nchi unaolenga kumtimizia kila mwananchi mahitaji yake ya lazima, chakula, nyumba, nguo, elimu, matibabu na usafiri.


Pia imelenga kutoa bila malipo elimu ya msingi, upili, vyuo vikuu, vyuo vya ufundi na taasisi za utafiti kama msingi wa maendeleo yanayotegemea teknolojia, itawaomba Wakenya waliong`ambo warudi nyumbani wasaidie kujenga nchi upya bila kupoteza uraia mwingine, itamaliza wizi wa mali za umma na serikali kwa kuwafunga wote watakaopatikana na ufisadi.


Pia ina lengo la kuwashitaki mafisadi warudishe pesa walizopora na kuweka nje, na kuishitaki katika Mahakama ya Dunia, Serikali ya Uingereza iilipe Kenya, Mau Mau na mashujaa wengine wa uhuru hasara iliyowapata wakati wa vita ya uhuru, itakuza maendeleo katika sehemu zote za nchi.


Chini ya CCM, walio nyuma na walio mbele watakuwa sawa.


Pia itahakikisha uchumi unatolea wasio na kazi, ajira na wafanyakazi mishahara bora na haki zao, italinda masilahi ya wafanyabiashara wadogo kama vile wachuuzi, wapiga viatu rangi, bodaboda, jua kali na kina mama wa sokoni, itahakikisha wakulima hawapunjwi jasho lao, itahakikisha mashamba makubwa zaidi yanapunguzwa na yale yasiyolimwa yanatwaliwa ili yapewe maskuota na wakazi wa miji ya mabanda.


CCM itahakikisha waathirika wa vita ya kikabila wanapewa mashamba na makao, itarudisha, kuhifadhi na kupanua misitu na kustawisha utalii kwa kujenga barabara za lami, mbuga za wanyama, itaunganisha nchi kwa misingi ya uzalendo na utaifa, itaharamisha ukabila na ubaguzi wake, itagawa kazi, rasilimali na wizara kwa mujibu wa sifa, haki na uhitaji, badala ya ukabila, ukoo, familia na urafiki.


Pia serikali ya CCM itahakikisha popote waishipo Wakenya watakuwa sawa na wasioishi katika makazi yao ya jadi hawatabaguliwa tena na serikali kuu, serikali za mitaa au kundi lolote la kisiasa, badala ya majimbo, CCM itatetea Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa nchi na serikali moja ya Afrika Mashariki, itapiga marufuku ubaguzi wote wa kijinsia, CCM itakataa ubaguzi wote wa kidini.


Pia inasema itatetea maadili ya uandishi yatakayofanya vyombo vya habari viwe vyombo vya watu, uzalendo, endelevu, sahihi na maadui wa ukabila na ufisadi na lugha ya Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya CCM, na itajenga uhusiano wa kiamani na kirafiki na nchi zote za Afrika na dunia, ambazo hazina ugomvi na Kenya.


Mwenyekiti wa chama hicho, Koigi Wamwere, alizaliwa mwaka 1950, Nakuru-Subukia. Katibu Mkuu wa chama hicho ni Sammy Mwaniki.


Alianza siasa mwaka 1974, baada ya kurejea kutoka masomoni Marekani, Chuo Kikuuu cha Coe.


Katika harakati za kisiasa, Wamwere, Raila Odinga, Ngungi Wathiong’o, na Mwalimu Maniganki Kamau, waliwahi kukamatwa kwa kosa la kuandaa mapinduzi ya serikali ya Moi mwaka 1982, na walikuwa katika Gereza la Kamiti kati ya mwaka 1982 na 1984.


Akiwa bado anakabiliwa na kesi hiyo, mwaka 1985 alitoroka na kwenda uhamishoni Norway. Alirejea nchini mwaka 1990, na kugombea ubunge katika Jimbo la Nakuru North kwa tiketi ya Kanu.


Baada ya kuwa mbunge wa Kanu, mwaka 1994 aliondolewa kwenye nafasi hiyo kwa sababu ya kupinga watu wachache kumiliki ardhi, na kuamua kurejea nchini Norway.


Mwaka 1996, alirejea Kenya na kuanzisha Chama cha KPF kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mwaka 1997.


Aligombea urais kwa tiketi ya KPF, ambapo alishika nafasi ya nne.


Mwaka 1998-2000 alirejea tena Norway na baadaye alikwenda Marekani kwa shughuli za kibiashara. Aliamua kurejea tena Kenya mwaka 2001 na kujiunga na NARC ili kushiriki katika uchaguzi mwaka 2002.


Mwaka 2002-2006, amekuwa mbunge kwa tiketi ya NARC, Jimbo la Subukia – Nakuru, hadi leo ndiye Naibu Waziri wa Habari na Utangazaji wa serikali ya Kibaki.


Septemba mwaka huu, aliamua kuanzisha Chama cha Mwananchi, na atakuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Pengine wameona tunafaidi bure bure tu?

 
Ole's Avatar
Ole
JF Senior Expert Member
Points: 280,360, Level: 100 Points: 280,360, Level: 100 Points: 280,360, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
Join Date: Sat Dec 2006
Posts: 950
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Views: 800
Reply With Quote
  #2  
Old 20th December 2006, 11:50 PM
Game Theory's Avatar
Game Theory Game Theory is offline
Game Theory has no status.
JF Premium Member
Points: 6,834,698, Level: 100 Points: 6,834,698, Level: 100 Points: 6,834,698, Level: 100
Activity: 13% Activity: 13% Activity: 13%
 
Join Date: Tue Sep 2006
Posts: 7,285
Thanks: 60
Thanked 425 Times in 178 Posts
Rep Power: 19
Game Theory is an unknown quantity at this point
Default

mabepari wa Kenya sidhani kama wanaweza kukopi iani ya CCM ya TZ si unajua sie bado wajamaa kiaina ?
Reply With Quote
  #3  
Old 22nd December 2006, 08:36 AM
Jafar's Avatar
Jafar Jafar is offline
Jafar a believer in creativity
JF Senior Expert Member
Points: 250,471, Level: 100 Points: 250,471, Level: 100 Points: 250,471, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Fri Nov 2006
Posts: 512
Thanks: 1
Thanked 15 Times in 9 Posts
Rep Power: 25
Jafar will become famous soon enoughJafar will become famous soon enoughJafar will become famous soon enoughJafar will become famous soon enoughJafar will become famous soon enoughJafar will become famous soon enoughJafar will become famous soon enoughJafar will become famous soon enough
Default

Hawa jamaa naona wanajiandaa katika jumuiya ya Afrika Mashariki ya kisiasa. Labda huko mbele wamesikia kuwa vyama vya siasa itabidi viwe na wanachama Kenya, Uganda na Tanzania ili kutambulika kama ni chama cha EAC. Ikifikia hapo (kama ni kweli) basi wataungana na wajanja CCM-Bongo.
Reply With Quote
  #4  
Old 25th January 2007, 05:21 PM
omarilyas omarilyas is online now
omarilyas has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 255,450, Level: 100 Points: 255,450, Level: 100 Points: 255,450, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Wed Jan 2007
Location: Morogoro
Posts: 1,613
Thanks: 31
Thanked 109 Times in 57 Posts
Rep Power: 27
omarilyas will become famous soon enoughomarilyas will become famous soon enoughomarilyas will become famous soon enoughomarilyas will become famous soon enoughomarilyas will become famous soon enoughomarilyas will become famous soon enoughomarilyas will become famous soon enoughomarilyas will become famous soon enough
Send a message via MSN to omarilyas
Default

Maskini Koigi,

anongelea CCM ipi. Ya Mwalimu ama ya Baada ya mwalimu?

Lakini napenda kumpongeza kwani ameanza kuonyesha njia wengine wafuate. Wakati umefika kwa vyama vya siasa Afrika Mashariki kuanza mikakati inayolenga kuunganisha vyama.

Wengine wafuate sio kwa majina lakini kwa kujaribu kusabahisha dira, sera, mikakati na malengo yao.

Hongera Koigi lakini pia nakuonea huruma.

Tanzanianjema
Reply With Quote
  #5  
Old 25th January 2007, 07:46 PM
Mkandara Mkandara is online now
Mkandara Aviator
JF Premium Member
Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Thu Mar 2006
Location: T dot
Posts: 7,289
Thanks: 463
Thanked 742 Times in 325 Posts
Rep Power: 80
Mkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the rough
Default

Makubwa haya jamani1

CCM TZ ni rolemodel!
__________________
Exploration of reality
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
ccm, kenya, kuwa, waamua, yao


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Kashfa ya Richmond: The FACTS FairPlayer Celebrities Forum 1354 12th March 2010 01:37 PM
Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia! Mzee Mwanakijiji Jukwaa la Siasa 348 16th January 2010 09:30 AM
Tambwe Hiza anaishabikia CCM iliyopoteza mwelekeo MwanaCCM Habari na Hoja mchanganyiko 1 4th December 2009 10:39 AM
CCM na mbinu chafu za kushinda uchaguzi MwanaCCM Habari na Hoja mchanganyiko 0 7th March 2007 10:11 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 05:13 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com