JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

  Report Post
  Page 1 of 2 12 LastLast
  Results 1 to 20 of 26
  1. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,068
   Rep Power : 372936423
   Likes Received
   7646
   Likes Given
   4407

   Default Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Gonga hapa kupata matokeo ya Kidao cha Nne - 2010
   au
   Hapa


   • SHULE ZA SERIKALI ZAGARAGAZWA TENA, SEMINARI JUU

   na Betty Kangonga
   JUMLA ya watahiniwa 177,021 waliofanya mtihani wa taifa wa Kidato cha Nne Oktoba mwaka jana wamefaulu huku wasichana wanane wakishika nafasi kumi bora kitaifa.

   Kwa mujibu wa matokeo hayo, kiwango cha ufaulu kimeporomoka kwa asilimia 22.11 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka juzi.

   Shule za binafsi hususan seminari zimeendelea kung’ara wakati zile za umma zikifanya vibaya na kushika nafasi za mwisho.

   Katika matokeo hayo, wanafunzi wanne wamefutiwa matokeo kutokana na kuandika lugha ya matusi katika mitihani ya masomo ya Biolojia, Historia, Kemia na Jiografia.

   Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Joyce Ndalichako, alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo ni zile zilizokuwa na watahiniwa kuanzia 40 na zaidi, ambazo ni Uru Seminari (Kilimanjaro), Marian Wasichana (Pwani), St Francis (Mbeya) na Canossa (Dar es Salaam).

   Nyingine ni Msolwa (Morogoro), Feza Wavulana (Dar es Salaam), St Mary Goreti (Kilimanjaro), Abbey (Mtwara), St Joseph’s Iterambogo (Kigoma) na Barbro - Johnson (Dar es Salaam).

   Aliwataja wanafunzi walioshika nafasi kumi bora kitaifa kuwa ni Lucylight Mallya, Maria –Dorin Shayo wa Shule ya Wasichana ya Marian, Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson, Diana Matabwa na Neema Kafwimi wa Shule ya Wasichana ya St Francis.

   Wengine ni Beatrice Issara wa St Mary Goreti, Johnston Dedani wa Ilboru, Samwel Emmanuel wa Moshi Technical, Bertha Sanga wa Marian na Bernadetha Kalluvya wa St Francis.

   Hata hivyo, pamoja na wasichana kung’ara katika nafasi kumi za kwanza kitaifa, bado wavulana wameendelea kufaulu kwa wingi.

   “Wasichana waliofaulu ni 69,996 sawa na asilimia 43.47 na wavulana ni 107,025 sawa na asilimia 56.28,” alibainisha Ndalichako.

   Alizitaja shule kumi za mwisho kitaifa zilizokuwa na watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni Changaa, Kolo, Kikore, Hurui, Thawi, (Dodoma), Pande Darajani (Tanga), Igawa (Morogoro), Makata (Lindi), Mbuyuni na Naputa (Mtwara).

   Ndalichako alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo zipo katika kundi la watahiniwa chini ya 40 ni pamoja na Don Bosco (Iringa), Feza wasichana (Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro) na Queen of Apostle Ushirombo (Shinyanga).

   Nyingine ni Sengerema Seminari (Mwanza), Sanu Seminari (Manyara), Bethelsabs Wasichana (Iringa), St Joseph –Kilocha Seminari (Iringa), Dungunyi Seminari (Singida) na Mafinga Seminari (Iringa).

   “Pia zipo shule za mwisho ambazo zimefanya vibaya zilizokuwa na watahiniwa chini ya 40 kati ya hizo ni Sanje ya mkoani (Morogoro), Daluni (Tanga), Kinangali (Singida), Mtanga (Lindi), Pande (Lindi), Imalampaka (Tabora), Chongoleani (Tanga), Mwamanenge (Shinyanga), Mipingo (Lindi) na Kaoze (Rukwa)”, alisema.

   Jumla ya watahiniwa 311 na watahiniwa wawili wa kujitegemea wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

   “Baraza pia limefuta usajili wa kituo cha watahiniwa wa kujitegemea P1189 cha Biafra kutokana na kukiuka taratibu za uendeshaji mitihani…maana kituo hicho kilikuwa na watahiniwa wengi kuliko uwezo wake, jambo lililosababisha usumbufu,” alisema.

   Pia baraza hilo limetangaza kusitisha matokeo ya wanafunzi 1,448 ambao walifanya mitihani bila ya kulipa ada ya mtihani, ambapo watatakiwa kulipa na faini katika kipindi cha miaka miwili ili waweze kupewa matokeo hayo.

   “Wanafunzi wawili wamefanya mtihani kwa sifa zinazofanana, hivyo tumesitisha matokeo yao hadi wakuu wa shule hizo watakapowasilisha nyaraka kuthibitisha uhalali,” alieleza.

   Ndalichako alisema watahiniwa 35 wa Shule ya Sekondari Bara wamefutiwa matokeo na kuondolewa katika usajili baada ya kutumia majina ya watahiniwa ambao walichaguliwa kujiunga na shule hiyo lakini hawakwenda kuripoti.

   Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2010 walikuwa 458,114 wakiwamo wasichana 216,084 sawa na asilimia 47.17 na wavulana 242,030 sawa na asilimia 52.83, ikilinganishwa na mwaka 2009 ambao walikuwa 351,152, hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa watahiniwa 106,962.

   “Watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 441,426 sawa na asilimia 96.36 na watahiniwa 16,688 hawakufanya mtihani sawa na asilimia 3.64 ya waliosajiliwa,” alifafanua.
   source: Tanzania Daima
   CCM NI CHAMA CHA MAJANGILI, WABAKAJI, MAFISADI, WATEKAJI, KUUA NA KUNGOA MENO BILA GANZI...


  2. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,068
   Rep Power : 372936423
   Likes Received
   7646
   Likes Given
   4407

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   watu wameshaanza kuzimia teh teh
   CCM NI CHAMA CHA MAJANGILI, WABAKAJI, MAFISADI, WATEKAJI, KUUA NA KUNGOA MENO BILA GANZI...

  3. nziriye's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd January 2011
   Posts : 886
   Rep Power : 730
   Likes Received
   93
   Likes Given
   102

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   hey crashwise are u serious kuwa tokeo limetoka au wataka kutia watu presha,halafu mbna matokeo yamechelewa and no body seems to care,are we serious kweli ama ?

  4. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,068
   Rep Power : 372936423
   Likes Received
   7646
   Likes Given
   4407

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By nziriye View Post
   hey crashwise are u serious kuwa tokeo limetoka au wataka kutia watu presha,halafu mbna matokeo yamechelewa and no body seems to care,are we serious kweli ama ?
   angalia hiyo link hapo juu....wamechelewesha labda walikuwa wanachakachua ................
   CCM NI CHAMA CHA MAJANGILI, WABAKAJI, MAFISADI, WATEKAJI, KUUA NA KUNGOA MENO BILA GANZI...

  5. JoJiPoJi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th August 2009
   Location : Mars
   Posts : 1,762
   Rep Power : 1384
   Likes Received
   358
   Likes Given
   121

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Watu wamechoka, wanafanya siasa tu sasa.
   Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli


  6. Kachanchabuseta's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th March 2010
   Posts : 7,303
   Rep Power : 2051
   Likes Received
   633
   Likes Given
   1457

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010


  7. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,068
   Rep Power : 372936423
   Likes Received
   7646
   Likes Given
   4407

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By jojipoji View Post
   watu wamechoka, wanafanya siasa tu sasa.
   wako busy na dowans na kujipanga kupanguya hoja z wapinzani.....
   CCM NI CHAMA CHA MAJANGILI, WABAKAJI, MAFISADI, WATEKAJI, KUUA NA KUNGOA MENO BILA GANZI...

  8. Lyangalo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th September 2009
   Location : Kintinku-Dodoma
   Posts : 660
   Rep Power : 772
   Likes Received
   119
   Likes Given
   36

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Jamani hali ni mbaya sana matokeo ya shule za kata kama ilivyotarajiwa. Je sasa hii ndo itakuwa turning point ya wanavijiji huko vijijini kuwahusudu CCM? Je serikali itatoa tamko gani? Hapa ndo tunaona umuhimu wa kutenganisha siasa na maswala yanayohitaji taruma.

   WANANCHI AMKENI SASA DOWANS + MATOKEO VYATOSHA KUWAWEKA BALABALANI MPAKA KIELEWEKE!
   A MAN'S BEST OR WORST CHOICE IN LIFE IS HIS WIFE

  9. #9
   Lweye's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 15th April 2010
   Posts : 108
   Rep Power : 615
   Likes Received
   53
   Likes Given
   25

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By nziriye View Post
   hey crashwise are u serious kuwa tokeo limetoka au wataka kutia watu presha,halafu mbna matokeo yamechelewa and no body seems to care,are we serious kweli ama ?

   Mkuu hapo kweye red. Kwani yalitakiwa yatoke lini. Manake mtihani wamemaliza Oktoba mwishoni. Mie nadhani tuwapongeze NECTA this time wamewahi ukizingatia idadi ya shule za kata zilizoongezeka
   owakachwa

  10. Ndachuwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th March 2006
   Location : ARUSHA
   Posts : 3,750
   Rep Power : 1562
   Likes Received
   933
   Likes Given
   693

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Mkuu ungeboresha hoja yako kwa kuweka mkutasari wa Best and last ten performers hapa tungefuatilia vizuri
   "Effective leadership is not about making speeches or being liked; leadership is defined by results not attributes" Peter Drucker

  11. Albedo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Posts : 5,582
   Rep Power : 54733566
   Likes Received
   1391
   Likes Given
   623

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By vincent augustino View Post
   mkuu ungeboresha hoja yako kwa kuweka mkutasari wa best and last ten performers hapa tungefuatilia vizuri
   1: Uru seminary
   2: Marian girls
   3: St. Francis
   "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM


  12. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,068
   Rep Power : 372936423
   Likes Received
   7646
   Likes Given
   4407

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By Vincent Augustino View Post
   Mkuu ungeboresha hoja yako kwa kuweka mkutasari wa Best and last ten performers hapa tungefuatilia vizuri
   Ningependa sana kufanya hivyo lakini inahitaji muda na neti iko slow sana kama vipi nisaidie...
   CCM NI CHAMA CHA MAJANGILI, WABAKAJI, MAFISADI, WATEKAJI, KUUA NA KUNGOA MENO BILA GANZI...

  13. Gsana's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th August 2010
   Location : Africa
   Posts : 3,843
   Rep Power : 438650
   Likes Received
   814
   Likes Given
   628

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Shule zenye majina ya rais wa Tanzania na viongozi wastaafu zimehaibisha majina yao. Nakusudia kupeleka pingamizi Wizarani majina yabadilishwe ili tuendelee kuyaenzi majina yao ktk njia nyingine mfano viwanja vya ndege,vya mpira,magari n.k Mfano:1. J.K.kikwete div.one 0,div.two 4,div3 2 div4 ni 29 na FLD 52. Na shule ya Jakaya Kikwete div1 0,div2 ni 1,div3 ni 5 ,div4 48 na FLD 76. Pia ana mkapa FLD 107. Aidha mwanaJF mwenzetu Mwanalugali kama ID yake ilivo imefeli vibaya div.1&2 ni 0,div3 1 na div4 30, FLD 107,naye atafute ID nyingine kukwepa aibu. Kwa ujumla nawapongeza wote Tanzania waliohitimu elimu iyo,ambayo mpaka leo serikali imesema ni Elimu ya lazima yani itakuwa compulsory/primary Education. Hongera.

  14. Albedo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Posts : 5,582
   Rep Power : 54733566
   Likes Received
   1391
   Likes Given
   623

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Duh, nangojea Statistics za NECTA ila hali ni Mbaya sana,
   "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM


  15. Albedo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Posts : 5,582
   Rep Power : 54733566
   Likes Received
   1391
   Likes Given
   623

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Shule za Dini Zimeendelea Kutesa kama Kawaida sijui kama kuna Shule ya Serikali kwenye top ten
   "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM


  16. Safari_ni_Safari's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2007
   Location : Kibaruani
   Posts : 17,812
   Rep Power : 3277026
   Likes Received
   9582
   Likes Given
   3670

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By Albedo View Post
   Shule za Dini Zimeendelea Kutesa kama Kawaida sijui kama kuna Shule ya Serikali kwenye top ten
   Dini ipi mkuu.....maana tuna mbili kuu
   "If you can't RESPECT EXISTENCE then you must EXPECT RESISTANCE!"

  17. Albedo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Posts : 5,582
   Rep Power : 54733566
   Likes Received
   1391
   Likes Given
   623

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By Safari_ni_Safari View Post
   Dini ipi mkuu.....maana tuna mbili kuu
   Aaah, Nkuu Itakuwa Ugomvi bana ngoja niache mpaka Magazeti yaseme
   "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM


  18. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,068
   Rep Power : 372936423
   Likes Received
   7646
   Likes Given
   4407

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By Albedo View Post
   Shule za Dini Zimeendelea Kutesa kama Kawaida sijui kama kuna Shule ya Serikali kwenye top ten
   kuna shule inaitwa bondeni ni shule ya ndugu zetu waislam daah yaani hii shule kila mwaka wao balaa....
   CCM NI CHAMA CHA MAJANGILI, WABAKAJI, MAFISADI, WATEKAJI, KUUA NA KUNGOA MENO BILA GANZI...

  19. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,068
   Rep Power : 372936423
   Likes Received
   7646
   Likes Given
   4407

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By Safari_ni_Safari View Post
   Dini ipi mkuu.....maana tuna mbili kuu
   zile zinazo unga upade wa ufisadi hoi...
   CCM NI CHAMA CHA MAJANGILI, WABAKAJI, MAFISADI, WATEKAJI, KUUA NA KUNGOA MENO BILA GANZI...

  20. Albedo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Posts : 5,582
   Rep Power : 54733566
   Likes Received
   1391
   Likes Given
   623

   Default Re: Matokeo ya kidato cha nne hewani - 2010

   Quote By Crashwise View Post
   kuna shule inaitwa bondeni ni shule ya ndunguze waislam daah yaani hii shule kila mwaka wao balaa....
   Kaka Nilikuwa sijui kumbe kuna Seminary zinafanya Vibaya hivi

   http://www.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/s1842.htm
   "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM  Page 1 of 2 12 LastLast

  Similar Topics

  1. Matokeo ya kidato cha nne 2010 yatangazwa
   By palalisote in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 6
   Last Post: 5th June 2013, 19:58
  2. Angalia hapa matokeo kidato cha nne 2010 - tanzania
   By Kisendi in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 12
   Last Post: 11th January 2012, 13:51
  3. Matokeo ya Kidato cha Nne 2010 Kujirudia Tena Mwaka Huu wa 2011
   By SolarPower in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 5
   Last Post: 23rd October 2011, 19:24
  4. Maoni yangu matokeo kidato cha nne 2010
   By Ngalikivembu in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 1
   Last Post: 1st February 2011, 03:35
  5. Matokeo ya kidato cha sita 2010 hadharani
   By Albedo in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 3
   Last Post: 2nd May 2010, 20:53

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...