Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Vigogo 4,700 hawajataja mali zao

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Vigogo 4,700 hawajataja mali zao





      Rabia Bakari na Rose Itono

      ZAIDI ya viongozi wa kisiasa na wa umma 4,700 hawajeresha fomu zinazotaja mali zao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ghivyo kuwa katika hatihati ya
      kuchukuliwa hatua za kisheria.

      Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Kamishna Mkuu wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Kaganda alisema jumla ya viongozi wa siasa waliotumiwa fomu hizo ni 4,346 ambao kati ya hao ni 1,446 ndio waliorejesha huku 3,047 bado wakiwa hajawarejesha fomu hizo.

      Aidha kwa upande wa viongozi wa umma, waliotumiwa fomu hizo ni 4,064 ambao kati ya hao 2,324 wamerejesha na 1,741 wakiwa bado wanadaiwa fomu hizo.

      Alisema idadi kubwa ni ya wanasiasa ambao hawajarejesha fomu inasababishwa na madiwani ambao taratibu za uteuzi na uundwaji wa mabaraza ya halmashauri kutokamilika.

      "Hadi kufikia Desemba 31, mwaka jana, jumla ya madiwani 2,844 sawa na asilimia 73.37 hawarejesha fomu.

      Taratibu za kuwafikia zinaendelea kufanyika ili kila muhusika aweze kuwajibika kutekeleza sheria," aliongeza.

      Ukiondoa madiwani, viongozi waandamizi wa siasa 56 sawa na asilimia 11.9 hawakurejesha fomu kwa wakati.

      Jaji Kaganda alisema kwa upande wa viongozi wa umma, idadi kubwa ya mahakimu wa mahakama za mwanzo na wilaya ambao wanakadiriwa kufikia 1,631 sawa na asilimia 40.13 hawakurejesha fomu kwa wakati kutoka na hali ya kijiografia na ugumu wa mawasiliano.

      Kwa mujibu wa sheria za maadili ya viongozi wa umma, namba 13 ya mwaka 1995, inawataka viongozi kuwasili silisha tamko lao ndani ya siku 30 baada ya uteuzi, kila mwisho wa mwaka na baada ya kuacha wadhifa.

      "Sheria inamtaka kiongozi yeyote wa umma kutoa tamko rasmi kuhusu mali na madeni yake, mke au mume na watoto walio chini ya miaka 18 ambao hawajaoa wala kuolewa," alifafanua Jaji Kaganda.

      Akitaja hatua zitakazochukuliwa kwa wale wasiowasilisha fomu hizo kwa wakati, Jaji Kaganda alisema Sekretarieti ya maadili itawahoji wahusika kwanini wasichukuliwe hatua zaidi kwa mujibu wa sheria, na kama maelezo hayatoridhisha, viongozi husika wataitwa mbele ya Baraza la Maadili ambalo litawasikiliza na kutoa mapendekezo kwa kamishna wa maadili juu ya hatua zinazofaa kuchukuliwa.

      "Taarifa ya baraza itawasilishwa kwa mheshimiwa rais na nakala kwa Spika wa bunge kwa hatua mbalimba za kiutumishi na kiutawala, pia tutasimamia kwa nguvu utekelezaji wa sheria kwa viongozi kuhakikisha kuwa Mamlaka za Nidhamu za Viongozi husika zinawajibika ipasavyo kutekeleza mapendekezo ya Sekretarieti dhidi ya viongozi wasiotekeleza misingi ya maadili,"alisema.

      Aliongeza kuwa, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi imejidhatiti kutoa elimu ya mara kwa mara kwa viongozi wa Umma ili kuongeza mwitikio wa urejeshaji wa fomu za Tamko.

      "Viongozi wa Umma wanahitaji kupewa elimu mara kwa mara kuhusu sheria ya Maadili ya uongozi ili wafahamu wajibu wao wa kuzingatia kanuni za maadili",alisema Jaji Kaganda.

      Aliongeza kusisitiza kuwa, mkazo utatiliwa katika kutoa elimu ya maadili kwa viongozi waliochaguliwa au kuteuliwa kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Vigogo 4,700 hawajataja mali zao


      Akitaja hatua zitakazochukuliwa kwa wale wasiowasilisha fomu hizo kwa wakati, Jaji Kaganda alisema Sekretarieti ya maadili itawahoji wahusika kwanini wasichukuliwe hatua zaidi kwa mujibu wa sheria, na kama maelezo hayatoridhisha, viongozi husika wataitwa mbele ya Baraza la Maadili ambalo litawasikiliza na kutoa mapendekezo kwa kamishna wa maadili juu ya hatua zinazofaa kuchukuliwa.

      "Taarifa ya baraza itawasilishwa kwa mheshimiwa rais na nakala kwa Spika wa bunge kwa hatua mbalimba za kiutumishi na kiutawala, pia tutasimamia kwa nguvu utekelezaji wa sheria kwa viongozi kuhakikisha kuwa Mamlaka za Nidhamu za Viongozi husika zinawajibika ipasavyo kutekeleza mapendekezo ya Sekretarieti dhidi ya viongozi wasiotekeleza misingi ya maadili,"alisema.
      Hizi ni danganya toto...................kinacho takiwa ni kuwafikisha mahakamani wote na hapo ndipo utaona kila kiongozi anajirudi......lakini hatua za kiutawala kwa makosa haya ya jinai.............give us a huge break......................... ........because we fully deserve it.........
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    4. Miaka 50

    Similar Topics

    1. Replies: 0
      Last Post: 24th June 2011, 10:21
    2. Vigogo 23 ‘kortini’ kwa kutotangaza mali zao
      By Rutashubanyuma in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
      Replies: 14
      Last Post: 16th April 2011, 08:39
    3. Vigogo 4,700 hawajataja mali zao
      By kilimasera in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 4
      Last Post: 5th January 2011, 08:57
    4. Replies: 6
      Last Post: 4th December 2010, 08:01
    5. Serikali ni mali ya watu, na watu ni mali ya Mungu
      By MPadmire in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 1
      Last Post: 30th August 2009, 12:58

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...