Quote:
Originally Posted by Dar Es Salaam
Nakupa pole kwa hilo, na mara nyingine uwe makini sana na hawa jamaa wa ma-showroom, binafsi nam-recommend jamaa mmoja wa Kariakoo anaitwa Abdul, mara nyingi hujitangaza katika Advertising Dar. Huyu anakuagizia gari kutoka Japan na anakupa data zote kabla hajaileta na gharama zake ni nafuu kweli. Utampata katika 0754-484384. Mwambie Dar. ndie aliempigia debe.
|
Hakuna haja ya kumtumia mtu kuagiza gari Japan, kuna makampuni yayoeleweka Dar ambayo unayapa katika mtandao na kumalizana nayo. Kampuni nyingi za kijapan zina wawakilishi Dar, we waone hao hao unaagiza mwenyewe kwenye mtandao bila commission wala mission town. Usimuamini mbongo yoyote kukuagizia gari, Utamaduni wetu umebadilika sana kila kitu mtu anaona deal.
Mimi niliagiza gari Japan mwenyewe kupitia kwenye mtandao wa AUTOREC tena nikiwa nje ya Tanzania na gari lilifika likiwa salama na nililipeleka jamaa wakalicheki lipo safi na mpaka leo lipo quality.
Nilitumia wiki kulitoa bandarini na siku tatu registration. Tusipende mkato ndugu zangu. Show room nyingi Bongo ni kanyaboya, watu wanaendesha magari yao bongo yakipata mzinga wanayatengeza na kurudisha showroom.
Yaani mimi mentali yangu ni kwamba mbongo don't trust hata kidogo tumekuwa kunguru kinoma kila mtu anataka kuwa tajiri kwa shortcut. Mpaka tutakapokuja kujua kuwa Biashara ni uhusiano, kwamba ukiniuzia kizuri leo na kesho nitakuja tena au kumleta mtu ndiyo tutakapokuwa na sustainable businesses.
Vinginevyo hizi showroom zote zitakufa kifo cha kawaida kwa kuji-demarket na ujanja wao wa kupata leo hawaangalii future.