Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

    Report Post
    Page 5 of 5 FirstFirst ... 345
    Results 81 to 89 of 89
    1. #1
      Mohammed Dewji's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 30th November 2009
      Posts : 3
      Rep Power : 0
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Mambo mengi yamesemwa kuhusu tatizo la umeme nchini Tanzania, mimi nitaanza kwa kugusia mambo machache yanayoonyesha matatizo ya umeme yalivyokuwa makubwa ndani ya bara letu la Afrika:

      • Hatujawekeza ipasavyo kwa miaka 15 hadi 20 katika kitengo cha uzalishaji na usambazaji wa umeme, hayo maneno yalitamkwa na Lawrence Musaba, Meneja wa Southern African Power pool, muungano na mtandao wa nchi kumi na mbili kusini mwa Sahara.
      • Kuanzia Nigeria, Ghana mpaka Luanda hela nyingi inatumika kuzalisha umeme kwa majenereta hali inayofanya uchumi wa nchi nyingi za Afrika kupungua ukuaji kwa asilimia mbili – ripoti ya Benki ya dunia.
      • Ukiitoa nchi ya Afrika Kusini kwenye mambo hayo, nchi zote zilizobaki za kusini mwa jangwa la Sahara lenye watu milioni 700, linapata umeme sawa na wananchi wa Poland ambao ni milioni 38 tu.
      • Eskom, kampuni ya umeme ya Afrika Kusini mwaka 1998 iliambiwa mwaka 2007 itaanza kupata tatizo la mgao wa umeme nchini iwapo isipopanga jinsi ya kuongeza uzalishaji wa nishati, lakini kutokana na matatizo ya fedha na mipango kampuni haikufanyia kazi yale mapendekezo ya wataalamu kwenye ripoti ya mwaka 1998, na kuanzia mwaka 2006 Afrika Kusini imeanza kupata misuko suko ya mgao wa umeme pia.
      • Nigeria, nchi yenye watu wengi kuliko wote Afrika na yenye utajiri wa mafuta ina vituo 79 vya kuzalisha umeme lakini ni vituo 19 vinavyofanya kazi na hivyo kusababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni moja kwa mwaka kiuchumi.

      Ukienda kuangalia hapo juu ni mifano michache ya matatizo ya umeme barani Afrika, lakini ninachoweza kusema tatizo kubwa linatokana na ukosefu wa mipango. Nishati ya umeme inapatikana kwa njianyingi, kuna umeme wa nguvu za maji, nguvu za jua, kwa njia ya nguvu za upepo, umeme wa majenereta, na njia nyingine nyingi ambazo wataalamu wanaweza wakatuambia zinatufaa.

      Lakini hili tatizo linaweza likakaa milele kwa nchi zetu za Afrika iwapo hatutaamka kwa kuangalia tatizo hili kama la miaka hamsini ijayo. Sisi tunazinduka pale umeme unapoanza kuwa wa mgao jijini Dar Es Salaam, je tunajiuliza vipi kule Kigoma mjini ambao wanapata adha ya mgao huo miaka nenda rudi.

      Mimi ninafikiria tatizo la umeme nchini linaweza likapatiwa ufumbuzi iwapo tukiamua sasa kuwa nchi inabidi iangalie matumizi ya nishati ya umeme itakavyoongezeka miaka ijayo hivyo tujiandae kuongeza Megawati nyingi kwa ajili ya miaka ijayo na pia kuboresha usambazaji.

      Unaweza ukachagua kampuni isiyokuwa sahihi kwenye mchakato mzima iwapo maamuzi yako yanakuwa yale ya haraka na yaliyofanyika kutokana na matatizo yanayowakabili watu wako kwa muda huo. Lakini iwapo ukiwa na muda wa kutosha ninaamini tunaweza tukaamua vizuri kwa ajili ya kusuluhisha matatizo ya umeme yanayotukabili.

      Kitu kingine ambacho wataalam mbalimbali walioulizwa (consultantancy experts) jinsi ya kulitatua tatizo hilo walikuja na njia moja kuu.

      Wakasema kuwa ili nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ziweze kujinasua kwenye tatizo hilo inabidi zijenge vituo viwili au vitatu vikubwa vya kuzalishia umeme kwa pamoja, kuliko kila mtu kuanza kutengeneza kituo chake ambacho kitakuwa kidogo na gharama yake ya uzalishaji inaweza ikawa kubwa kuliko ile ya vituo vikubwa.

      Maoni yangu ili Tanzania iweze kuondokana na tatizo hili la umeme inabidi viongozi wahusika wakae chini watafakari nini kifanyike ili sehemu nyingine za Tanzania umeme ufike wa kutosha kwa miaka mingi ijayo, tusiwe na fikra za kufikisha Megawati kadhaa kwa ajili ya sasa hivi, tuwe tunajiuliza vipi hapo baadaye tutafanyaje?

      Hivyo tatizo la umeme la leo nchini Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika linatokea kwa sababu hatuoni mbele, kama mfano wa Eskom ya Afrika Kusini ambao kama wangeweza kupanga vizuri basi leo mgao wa umeme kwao usingetokea, vivyo hivyo TANESCO inabidi waje na mipango thabiti ya kutupa umeme wa kutosha kwa miaka mingi ijayo.

      Nashukuru kwa kusoma makala haya, ninajua kuna mengi sijagusia lakini mimi ninapendelea kuongelea jambo kwa kutoyarudia yaliyosemwa badala yake napenda kuongeza vitu vipya kwenye mjadala ili tuweze kujadiliana kwa kina.

      MO


    2. #81
      Bin Maryam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd October 2007
      Posts : 698
      Rep Power : 735
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Darwin View Post
      Tazama ramani utaona nchi nzuri
      Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka
      Nchi hio mashughuli huitwa Tanzania.


      Tumesikia mara kibao bwawa limekauka maji nakwahio haliwezi kuzalisha umeme unaotosha.

      Kuna baadhi ya mito mikubwa Tanzania.

      Kama serikali haiwezi kutengeneza mabwawa mengine kutokana na uhaba wa pesa, [Ooops nimesahau pesa za EPA.]

      Kwanini serikali isitoe mwito kwa kila mtanzania kwenda kujenga dam kwa mikono?

      Watu 33 Mn kwa sensa ya 2002 tushindwe kujenga dam kwa mikono yetu linaloweza kuzalisha umeme wakututosha na pengine wakuuza kwa nchi za jirani?
      Mzee hapa una-bore. Haya masuala ya kutazama Ramani yalitumika miaka hile ya zamani wakati tunatafuta identity ya utaifa.

      Miaka ya sasa ni lazima tuachane na fantasy na kuangalia reality. Ujenzi wa dam una negative impacts kwa ecosystem.
      Believing in God costs you nothing if you're wrong, and wins you everything if you're right.

    3. #82
      Gelange Vidunda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th August 2008
      Posts : 306
      Rep Power : 614
      Likes Received
      20
      Likes Given
      37

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By August View Post
      .........................Pili Mo wewe ukiwa kama mbunge wa Singida, na kwa kuwa serikali kwa hivi sasa wamejikita zaidi katika kuwekeza kwenye Miradi midogo midogo ya MW 100 nk
      je umefanya nini kushauri wadau binafsi kama wewe, au halmashauri ya Mji wa kauza Shares ilikupata mtaji wa kufungua katanesco kadogo hapo Singida, na mkiona Mtaji unao hitajika ni mkubwa, basi mnaweza omba mitaji toka nje ya Singida, na kutoka kwenye institution zingine kama world bank, na watu wa moja moja hapa Bongo na Nje?
      Ili mradi shares ziwe zinauzwa pale DSE
      Mkoa wa Tanga kupitia kampuni iitwayo Katani Limited wameweza kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya mmea wa katani. Inachukua mabaki yote ya mmea wa katani, mabaki ya kiwandani etc ili kuzalisha umeme na end product yake inatoa mbolea murua kabisa. Umeme huo, according to one Mr. Shamte unaweza kuzalisha umeme wa kutosha kuelectrify Tanga nzima and Kilimanjaro regions - the problem is wanaambiwa wauingize kwenye grid ya taifa!

      Kuna mtu hapo juu kasema maybe microplant ndogondogo ni jawabu lakini problem itakuwa na monopoly ya TANESCO kwani lazima kumuuzi yeye.

      BTW, Mo, Shamte told me wana mpango wa kwenda Singida kwani kule kuna masalio ya mashamba ya katani ambayo yamekuwa neglected miaka mingi kwa hiyo lengo ni kwenda kung'oa yale makatani (na kupanda mingine) na kuyatumia kuzalisha umeme. Maybe get in touch with him on that.
      "Ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora"
      Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa.

    4. #83
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Bin Maryam View Post
      Mzee hapa una-bore. Haya masuala ya kutazama Ramani yalitumika miaka hile ya zamani wakati tunatafuta identity ya utaifa.

      Miaka ya sasa ni lazima tuachane na fantasy na kuangalia reality. Ujenzi wa dam una negative impacts kwa ecosystem.
      Mkuu, haiwezekani hii kuwa ni lugha ya biashara maanake hawa wanasayansi wetu wa siku hizi biashara ndio hujenga Uchumi wa nchi zao. China, Canada, Norway, Brazil, Venezuela, ndizo zinaongoza kwa matumizi ya Hydro lakini sijasikia matatizo hayo na wanaendelea ujenzi wa Hydro ktk nchi zao..Na wanatisha kiuchumi na maendeleo..

      Kweli nakubali inawezekana sana ujenzi wa Hydro kubwa sana kuelta madhara lakini kwetu sisi na hizi za chini ya MW1000 kweli zinaweza kuwa na madhara hayo! labda nipeni mfano maanake Hydro nyingi zimejengwa miaka zaidfi ya 50 iliyopita, tungesikia...
      Last edited by Mkandara; 3rd December 2009 at 18:06.
      Exploration of reality

    5. #84
      Darwin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2008
      Posts : 906
      Rep Power : 748
      Likes Received
      39
      Likes Given
      4

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Bin Maryam View Post
      Mzee hapa una-bore. Haya masuala ya kutazama Ramani yalitumika miaka hile ya zamani wakati tunatafuta identity ya utaifa.
      Kumbe kusifia chako kuna muda?
      I,m a nationalist forever
      St. Shaughn 5 : 31 "If I bear witness of myself, my witness is not true" Jesus says about himself

    6. #85
      Semilong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th March 2009
      Posts : 1,614
      Rep Power : 1255
      Likes Received
      92
      Likes Given
      112

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      hii article yako yote umeitoa NY times halafu umeitafsiri, sio kitu kibaya lakini unge wa acknoledge. usiposema source watu tunaona ni plagiarism.
      link hii hapa
      Quote By Mohammed Dewji View Post


      Hatujawekeza ipasavyo kwa miaka 15 hadi 20 katika kitengo cha uzalishaji na usambazaji wa umeme, hayo maneno yalitamkwa na Lawrence Musaba, Meneja wa Southern African Power pool, muungano na mtandao wa nchi kumi na mbili kusini mwa Sahara.
      Ukiitoa nchi ya Afrika Kusini kwenye mambo hayo, nchi zote zilizobaki za kusini mwa jangwa la Sahara lenye watu milioni 700, linapata umeme sawa na wananchi wa Poland ambao ni milioni 38 tu.

      http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html
      hii ndio article ya kiingereza ambayo umetafsiri kwa kiswahili. maneno haya yafananishe na hapo juu

      “We’ve had no significant capital injection into generation and transmission, from either the private or public sectors, for 15, maybe 20 years,” said Lawrence Musaba, the manager of the Southern African Power Pool, a 12-nation consortium of electricity utilities at the continent’s tip.

      The gravity of this year’s shortage is all the more apparent considering how little electricity sub-Saharan Africa has to begin with. Excluding South Africa, whose economy and power consumption dwarf other nations’, the region’s remaining 700 million citizens have access to roughly as much electricity as do the 38 million citizens of Poland.


      http://www.nytimes.com/2007/07/29/wo...a/29power.html
      hii article inanikumbusha uk 2007 nikiwa nimekaa na watu kutoka kenya, uganda, nigeria, ghana, ivory cost na cameroon tukawa tunajidili jinsi waandishi wa habari jinsi wanavyoiandika vibaya africa na effect zake kwenye tourism na kuzuia investment flows. niliposoma hii ya kwako kwa kiswahili nikajua tu utakuwa umeitafsiri, nikatumia kama nusu saa kuitafuta mpaka nikaipata.

      mo ukisoma hizi habari au research paper yeyote lazima uingalie kwa makini
      na uitafakari. "the region’s remaining 700 million citizens have access to roughly as much electricity as do the 38 million citizens of Poland".
      huu ni uongo wa hali ya juu ambao unaandikwa na waandishi wa habari wa nje juu ya africa, kina chosikitisha na wewe ume copy na ku paste na kuja kutulisha hapa JF. huyu mwandishi ni watu ambao wanakuja mara moja tu africa na kuondoka na hawajui hali ya africa na kazi yao ni kuandika negative about africa.

      ukiangalia TZ peke yake tukasema dar na mwaza kuna umeme, kwa ajili sio kila mtu ana umeme katika mikoa hii miwili kwa hiyo tuseme mikoa mingine yote ya tz haina umeme (arusha, mbeya, kilimanjaro, tanga na kwingineko kote hamna umeme). watu wa dar + mwanza ni 8mil, kwa hiyo ni watu mil 8 out of 40m wana access to electricity which is 20% of all tanzanians.
      nimetembea kenya sehemu mbali mbali, na kenya watu wengi wana umeme zaidi ya tanzania.
      jamaa zangu wa nigeria, ghana, ivory cost, cameroon na uganda walinitolea mifano hiyo hiyo na wakanihakikishia kuwa more than 20% of their pop has access to electriicty. ukijumlisha 20% ya inchi zote utaona inapita 38mil by miles.
      hata UN estimate ni 12% which is 84mil.

      tuachane na data turudi kwenye mada

      tatizo kubwa ambalo linaikabili sekta ya umeme africa ni uongozi/corruption. nchi za africa zina viongozi ambao wanafikiria matumbo yao tu na si kutatua matatizo ya watu waliowapigia kura.
      mfano ethiopia wanajenga bwawa kubwa sana la umeme (huu ni mpango wa long term) lakini shutuma ndio zile zile kwamba ni hela nyingi imeliwa na hela pia haitoshi.
      http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/7937480.stm
      tukienda nigeria obasanjo na wenzake wametafuna karibuni $2bn ambazo zilikuwa zitumike kwenye umeme.

      tukirudi dar rashid ametuambia tusiponunua mitambo ya rafiki yako dowans tutakaa kwenye giza, hii ni dhairi kabisa watu hawataki kufanya mipango ambayo haifaidishi matumbo yao.

      karibu JF
      Mkandara and MziziMkavu like this.
      You can not keep 40m people quite forever....
      one year one month one day they will wake up..........


    7. #86
      Darwin's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2008
      Posts : 906
      Rep Power : 748
      Likes Received
      39
      Likes Given
      4

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mlalahoi View Post
      Generally,kuna wanasiasa wanaoguswa kwa dhati na matatizo yanayoikabili nchi yetu lakini kinachowakwaza ni unity yao na CCM.Nadhani tunahitaji sana wazalendo wanaoweza kujitoa mhanga kwa manufaa ya nchi,na hiyo ni pamoja na kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya kuendeleza itikadi za siasa.If you try that,Mheshimiwa Dewji,I'll be the first to shout aloud "MOHAMMED DEWJI FOR PRESIDENT OF TANZANIA

      Wacha kumponza mwenzako.

      Na akigombea u-president hata kama ni kwa kutumia CCM ataangushwa vibaya.

      Mheshimiwa aendelee kuwa mbunge wa jimbo lake kwani juhudi zake tunaziona. Na najua kwa vyovyote vile atachaguliwa tena kwenye jimbo lake kwa juhudi zake.

      Labda ategemee nafasi ya kuteuliwa kuwa waziri fulani kupitia CCM lakini Urais utamponza.

      Hii ni kwamba:
      Japokuwa Mo ni mtanzania mwenye asili ya Asia na moyo wake ni wa kiafrika lakini mambo kama ya EPA ndiyo yatakayomponza.

      Wako wanasiasa ambao wataitumia hio nafasi ya kumshambulia kutokana na watanzania wenzake wenye asili ya Asia walivyofanya Radar, EPA etc
      St. Shaughn 5 : 31 "If I bear witness of myself, my witness is not true" Jesus says about himself

    8. #87
      Fundi Mchundo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2007
      Posts : 4,351
      Rep Power : 2682
      Likes Received
      194
      Likes Given
      137

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mkandara View Post
      Mkuu, haiwezekani hii kuwa ni lugha ya biashara maanake hawa wanasayansi wetu wa siku hizi biashara ndio hujenga Uchumi wa nchi zao. China, Canada, Norway, Brazil, Venezuela, ndizo zinaongoza kwa matumizi ya Hydro lakini sijasikia matatizo hayo na wanaendelea ujenzi wa Hydro ktk nchi zao..Na wanatisha kiuchumi na maendeleo..

      Kweli nakubali inawezekana sana ujenzi wa Hydro kubwa sana kuelta madhara lakini kwetu sisi na hizi za chini ya MW1000 kweli zinaweza kuwa na madhara hayo! labda nipeni mfano maanake Hydro nyingi zimejengwa miaka zaidfi ya 50 iliyopita, tungesikia...
      Mkuu Mkandara,

      Tuambie ni mara ipi mipya ya Hydro inajengwa katika nchi hizo? Three gorges wa China ni disaster. Aswan ni disaster. Sidhani kama Venezuela na Brazil wana miradi mikubwa mipya ya Hydro. Canada sijui. Norway nao sidhani kama wanampango. Lakini hata hivyo ukiangalia mazingira ya Norway ni tofauti na sisi, wao wanamajabali na fjords ambazo waliweza kutumia bila madhara makubwa. Hawana kitu kujaa tope, kwa mfano. Hivi karibuni nadhani ni India ndiyo walikuwa na mradi mkubwa ambao na wenyewe umekumbwa na matatizo.

      Amandla......
      Mkandara likes this.
      Fundi Utumbo

    9. #88
      Neiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2012
      Location : My Profile
      Posts : 619
      Rep Power : 6936
      Likes Received
      460
      Likes Given
      553

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Naona nishukuru Makutano Show kwa kufanya hii Link kuweza kuiona... Hii topic iko valid bado to date. Maswala kama haya Mkuu Invisible nashauri kama ingewezekana mngeweka utaratibu wa kumfuatilia mhusika kama mna contact hasa kama ni verified kama mh. Dewji. A great (very valid) discussion but bado inaelea...
      "Sometimes its Ok not to be Ok"

    10. #89
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Fundi Mchundo View Post
      Mkuu Mkandara,

      Tuambie ni mara ipi mipya ya Hydro inajengwa katika nchi hizo? Three gorges wa China ni disaster. Aswan ni disaster. Sidhani kama Venezuela na Brazil wana miradi mikubwa mipya ya Hydro. Canada sijui. Norway nao sidhani kama wanampango. Lakini hata hivyo ukiangalia mazingira ya Norway ni tofauti na sisi, wao wanamajabali na fjords ambazo waliweza kutumia bila madhara makubwa. Hawana kitu kujaa tope, kwa mfano. Hivi karibuni nadhani ni India ndiyo walikuwa na mradi mkubwa ambao na wenyewe umekumbwa na matatizo.

      Amandla......
      Wee fanya ku- google utaziona kibao...
      Wakati mwingine tufikirie sana hizi hypes za West wanapopiga vita kitu hutokana na kwamba wao hawauzi kitu. Matumizi ya mafuta yanatumaliza walati wao wenyewe wanatumia Nuclear, tukitengeneza sisi wanasema tunataka kutengeneza vichwa vya mabomu na hatari. Kuna kitu hatari kama global warming mbona wote wanatetea kwamba hakuna kitu hicho..
      Exploration of reality

    Page 5 of 5 FirstFirst ... 345

    Similar Topics

    1. Replies: 121
      Last Post: 24th May 2013, 04:10
    2. Nyumba ya kukodi Dar kwa muda mfupi
      By Sokwe Mjanja in forum Matangazo madogo
      Replies: 3
      Last Post: 30th August 2011, 10:59
    3. Replies: 9
      Last Post: 4th March 2011, 11:42
    4. Natafura rent ya muda mfupi
      By Kwame Nkrumah in forum Matangazo madogo
      Replies: 9
      Last Post: 26th August 2010, 17:31

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...