Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

    Report Post
    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 89
    1. #1
      Mohammed Dewji's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 30th November 2009
      Posts : 3
      Rep Power : 0
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Mambo mengi yamesemwa kuhusu tatizo la umeme nchini Tanzania, mimi nitaanza kwa kugusia mambo machache yanayoonyesha matatizo ya umeme yalivyokuwa makubwa ndani ya bara letu la Afrika:

      • Hatujawekeza ipasavyo kwa miaka 15 hadi 20 katika kitengo cha uzalishaji na usambazaji wa umeme, hayo maneno yalitamkwa na Lawrence Musaba, Meneja wa Southern African Power pool, muungano na mtandao wa nchi kumi na mbili kusini mwa Sahara.
      • Kuanzia Nigeria, Ghana mpaka Luanda hela nyingi inatumika kuzalisha umeme kwa majenereta hali inayofanya uchumi wa nchi nyingi za Afrika kupungua ukuaji kwa asilimia mbili – ripoti ya Benki ya dunia.
      • Ukiitoa nchi ya Afrika Kusini kwenye mambo hayo, nchi zote zilizobaki za kusini mwa jangwa la Sahara lenye watu milioni 700, linapata umeme sawa na wananchi wa Poland ambao ni milioni 38 tu.
      • Eskom, kampuni ya umeme ya Afrika Kusini mwaka 1998 iliambiwa mwaka 2007 itaanza kupata tatizo la mgao wa umeme nchini iwapo isipopanga jinsi ya kuongeza uzalishaji wa nishati, lakini kutokana na matatizo ya fedha na mipango kampuni haikufanyia kazi yale mapendekezo ya wataalamu kwenye ripoti ya mwaka 1998, na kuanzia mwaka 2006 Afrika Kusini imeanza kupata misuko suko ya mgao wa umeme pia.
      • Nigeria, nchi yenye watu wengi kuliko wote Afrika na yenye utajiri wa mafuta ina vituo 79 vya kuzalisha umeme lakini ni vituo 19 vinavyofanya kazi na hivyo kusababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni moja kwa mwaka kiuchumi.

      Ukienda kuangalia hapo juu ni mifano michache ya matatizo ya umeme barani Afrika, lakini ninachoweza kusema tatizo kubwa linatokana na ukosefu wa mipango. Nishati ya umeme inapatikana kwa njianyingi, kuna umeme wa nguvu za maji, nguvu za jua, kwa njia ya nguvu za upepo, umeme wa majenereta, na njia nyingine nyingi ambazo wataalamu wanaweza wakatuambia zinatufaa.

      Lakini hili tatizo linaweza likakaa milele kwa nchi zetu za Afrika iwapo hatutaamka kwa kuangalia tatizo hili kama la miaka hamsini ijayo. Sisi tunazinduka pale umeme unapoanza kuwa wa mgao jijini Dar Es Salaam, je tunajiuliza vipi kule Kigoma mjini ambao wanapata adha ya mgao huo miaka nenda rudi.

      Mimi ninafikiria tatizo la umeme nchini linaweza likapatiwa ufumbuzi iwapo tukiamua sasa kuwa nchi inabidi iangalie matumizi ya nishati ya umeme itakavyoongezeka miaka ijayo hivyo tujiandae kuongeza Megawati nyingi kwa ajili ya miaka ijayo na pia kuboresha usambazaji.

      Unaweza ukachagua kampuni isiyokuwa sahihi kwenye mchakato mzima iwapo maamuzi yako yanakuwa yale ya haraka na yaliyofanyika kutokana na matatizo yanayowakabili watu wako kwa muda huo. Lakini iwapo ukiwa na muda wa kutosha ninaamini tunaweza tukaamua vizuri kwa ajili ya kusuluhisha matatizo ya umeme yanayotukabili.

      Kitu kingine ambacho wataalam mbalimbali walioulizwa (consultantancy experts) jinsi ya kulitatua tatizo hilo walikuja na njia moja kuu.

      Wakasema kuwa ili nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ziweze kujinasua kwenye tatizo hilo inabidi zijenge vituo viwili au vitatu vikubwa vya kuzalishia umeme kwa pamoja, kuliko kila mtu kuanza kutengeneza kituo chake ambacho kitakuwa kidogo na gharama yake ya uzalishaji inaweza ikawa kubwa kuliko ile ya vituo vikubwa.

      Maoni yangu ili Tanzania iweze kuondokana na tatizo hili la umeme inabidi viongozi wahusika wakae chini watafakari nini kifanyike ili sehemu nyingine za Tanzania umeme ufike wa kutosha kwa miaka mingi ijayo, tusiwe na fikra za kufikisha Megawati kadhaa kwa ajili ya sasa hivi, tuwe tunajiuliza vipi hapo baadaye tutafanyaje?

      Hivyo tatizo la umeme la leo nchini Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika linatokea kwa sababu hatuoni mbele, kama mfano wa Eskom ya Afrika Kusini ambao kama wangeweza kupanga vizuri basi leo mgao wa umeme kwao usingetokea, vivyo hivyo TANESCO inabidi waje na mipango thabiti ya kutupa umeme wa kutosha kwa miaka mingi ijayo.

      Nashukuru kwa kusoma makala haya, ninajua kuna mengi sijagusia lakini mimi ninapendelea kuongelea jambo kwa kutoyarudia yaliyosemwa badala yake napenda kuongeza vitu vipya kwenye mjadala ili tuweze kujadiliana kwa kina.

      MO

    2. #21
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,215
      Rep Power : 12282
      Likes Received
      6065
      Likes Given
      6932

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mag3 View Post
      Hata hivyo nina kaswali kadogo tu kwa Mheshimiwa - kwa nini aliutafuta ubunge kwa tiketi ya CCM. Nauliza hivi kwa sababu hii post yake yaonyesha wazi kuwa kwa hili la umeme haridhiki na sera zinazotekelezwa na chama chake.

      Matatizo ya umeme nchini ni zao la hizo sera na ilani ya uchaguzi za chama tawala na amepiga kura mara ngapi kupinga miswada inayowakilishwa bungeni na serikali. Katika uchaguzi ujao kama atasimama tena kugombea ubunge, je ana mkakati gani kuwa haya mapendekezo yake yatapewa kipaumbele kama chama chake kinashinda ?
      Je ni haki kulalamika kuwa miradi kama hii inahitaji hela nyingi wakati rasilimali za taifa zinatapanywa kama vile hazina mwenyewe.

      Karibu Mh. Mohamed Dewji, Mbunge wa Singida.
      Sidhani kama sera fulani ikikukwaza kwenye chama chako lazima ukimbilie chama kingine, na sidhani Mo amekuja kulalamika kwenye JF. Na at least ame-dare ku-talk openly sijui huko chamani watamuambiaje maana kuna watu hawataki kusikia chochote kuhusu mapungufu yao

      Amefanya la maana kuleta hoja kama Mo kutokana na his faith kwamba JF kuna great thinker na sio sinkers

      Sometime japo kwa sekunde tujaribu kuweka constructive idea halafu tuone kama ataleta impact yoyote...
      ....Time is the wisest counselor !!!

    3. #22
      Magezi's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 26th October 2008
      Posts : 2,668
      Rep Power : 0
      Likes Received
      34
      Likes Given
      54

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Kibunango View Post
      Sasa wewe hujui hapa kuna kitu kinaitwa profile? click kwenye jina la mtoa mada na utakutana na profile yake. Pili ameweka blog yake chini ya bandiko, fuata hiyo link ili kumjua. Tatu unaweza kumpm na Nne unaweza kumfuta huko Singida(M) kuhakikisha kama ndie ama sie.

      ...Na hii ina maana gani?
      Samahani sana mkuu wangu naona kangara ya ughaibuni imenizidia

    4. #23
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,752
      Rep Power : 1168
      Likes Received
      253
      Likes Given
      2541

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      suala la umeme na maendeleo mengine, naona iko haja ya mikoa, wabunge na wananchi kwa ujumla kuchukua hatua zifaazo badala ya kuiachia serikali ya ccm, aidha wabunge kuwa mobilise watu wao ili wajifanyie kitu cha maana, na hata kwa barabara, ni kuzikaba halamashauri ili mikoa inayo pakana waweze kujiunganisha kwa barabara zilizo bora, kwani ustawi wa maendeleo yao yatatokana na juhudi zao. na kuimarisha miundo mbinu, na nishati

    5. #24
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,816
      Rep Power : 13657
      Likes Received
      938
      Likes Given
      345

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mag3 View Post
      .....kwa nini aliutafuta ubunge kwa tiketi ya CCM. Nauliza hivi kwa sababu hii post yake yaonyesha wazi kuwa kwa hili la umeme haridhiki na sera zinazotekelezwa na chama chake. ....

      Kimsingi kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake popote pale, cha muhimu asivunje sheria wala kukanyaga haki za wenzake katika kutoa mawazo yao. Kuwa katika CCM hakumnyimi Mo haki yake ya kutoa mawazo yake nje ya chama. Katiba ya nchi inamruhusu!
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    6. #25
      Kimey's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th March 2009
      Location : Counter ya Juu!
      Posts : 4,093
      Rep Power : 1340
      Likes Received
      763
      Likes Given
      673

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Currently Active Users Viewing This Thread: 12 (5 members and 7 guests) Kimey, Burn, Magezi, Mohammed Dewji
      Muheshimiwa nakuona unaichungulia thread kuna hoja nyingi zimetolewa tunaomba ufafanuzi!
      I may be walking slowly, But I never walk backwards! and Whenever I walk backwards, Its for a long jump!!

    7. #26
      Mohammed Dewji's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 30th November 2009
      Posts : 3
      Rep Power : 0
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Ninashukuru kwa comments wadau.......ni post yangu ya kwanza lakini ninataka wadau wajue kuwa tatizo la umeme limeshamiri mpaka katika nchi kama Nigeria wakati wamejaliwa utajiri wa mafuta......tukiyaacha hayo I believe constructive discussion should be encouraged...

      WanaSingida nimeshirikiana nao katika kuliendeleza jimbo letu kwa kiasi kikubwa miaka minne iliyopita.....sasa ninaamini vijana wa nchi hii tusaidiane kujenga taifa.....and that's my motto KUHAMASISHA VIJANA KUJENGA TAIFA LETU

      Mungu Ibariki Tanzania

    8. #27
      Nduka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2008
      Posts : 5,803
      Rep Power : 13851
      Likes Received
      432
      Likes Given
      571

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mohammed Dewji View Post
      WanaSingida nimeshirikiana nao katika kuliendeleza jimbo letu kwa kiasi kikubwa miaka minne iliyopita.....sasa ninaamini vijana wa nchi hii tusaidiane kujenga taifa.....and that's my motto KUHAMASISHA VIJANA KUJENGA TAIFA LETU

      Mungu Ibariki Tanzania
      Tafadhari tupe mifano hai ya mambo mliyoshirkiana katika hili la umeme, je ni miradi mingapi ya umeme wa upepo imeanzishwa na kumilikiwa na wanasingida? ni maeneo gani haswa mmefanikiwa na yepi hamkufanikiwa ili na sisi wa jimbo la tabora mjini tujifunze?

      Mungu ibariki Tanzani..Amina
      I am super bad

    9. #28
      Yegomasika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2009
      Location : Mwanza
      Posts : 1,916
      Rep Power : 905
      Likes Received
      447
      Likes Given
      308

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Hivi Maximum demand wakati wa peak hours, 20:00-23:00 kwa sasa ni megawatt ngapi kwa nchi nzima?. Nina maana kwa mikoa yote ambayo imeunganishwa na grid ya taifa?. Nadhani jamaa zangu wa pale National Grid Center watatusaidia kutupa jibu.
      Happiness Begins With Facing Life With A Smile And A Wink.

    10. #29
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,622
      Rep Power : 46738
      Likes Received
      16720
      Likes Given
      8561

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Wabunge ndio hupitisha mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu ya serikali na ni wao huitengenea fedha. Na pale ambapo hakuna sheria ya kusababisha jambo fulani kufanyika wabunge wana uwezo (kama kundi -chama, au kama mtu mmoja mmoja) kuleta mswada wa sheria wa kusababisha jambo hilo kutendeka au kutotendeka.

      Suala la tatizo la nishati siyo geni kwa TAnzania na kwa eneo letu la Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa upande wetu Tanzania tatizo hili ni dalili tu ya tatizo lenyewe tulilonalo ambalo ni mipango mibovu ya wanasiasa wetu. Tanzania haina sababu hata chembe ya kuwa upungufu wa nishati ya umeme.

      Leo hii kuweza kuyarejesha mabwawa yetu yote ya kuzalishia umeme kwenye full capacity inakadiriwa kutumia karibu dola bilioni 2! Lakini tukifanya hivyo zaidi tutakachopata ni kama Megawatts 1000 hivi (kama sikosei). Lakini wakati huo huo tukitamua kujenga bwawa moja kubwa la Stielger's Gorge itatugharimu karibu dola bilioni 2 vile vile lakini tunaweza kupata Megawatts zaidi 2900!

      Wanasiasa wetu hawajui wachague nini! suluhisho lao ni kuingiza majenereta ya umeme na kutoa tenda zaidi ya majenereta. Wako tayari shilingi milioni nyingi kila siku na ukiwauliza hadi leo (kuanzia 1995) serikali imetumia kiasi gani katika kulipia mafuta na IPPs, jibu lake litawafanya muinamishe kichwa kwa aibu!

      Sasa, Mhe. Dewji,

      a. una mpango gani wa kuleta mswada Bungeni wa kusababisha ujenzi wa Stielger's gorge au kutengea fedha mradi huo mkubwa ilii hatimaye tuondokane na tatizo la umeme?

      b. Una msimamo gani kuhusu kampuni ya Dowans ambayo iliingia nchini kitapeli na hadi leo tunahangaika na majenereta yao. Je, kwa maoni yako serikali itaifishe mitambo hiyo na kuwachukulia hatua wahusika wote?

      c. Unafikiri Kamati yenu Teule ya Bunge ilifanya kazi yake vizuri katika suala la Richmond na hivyo kazi yake iheshimiwe na wabunge wote au unaamini ilikuwa imewaonea watu mbalimbali?
      MziziMkavu likes this.
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    11. #30
      Fundi Mchundo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2007
      Posts : 4,351
      Rep Power : 2682
      Likes Received
      194
      Likes Given
      137

      Mzee Mwanakijiji.

      Mradi huo wa Stiegler Gorge ni bomu. Gharama yake kimazingira itazidi faida ya huo umeme. Athari yake kwenye Ruaha basin na Rufiji delta ni kubwa mno. Kibaya kingine ni kuwekeza kwenye source moja kubwa ambapo kama ikija pata matatizo tutaumbuka.

      Matatizo yetu kwenye vyanzo vya sasa si kukesekana kwa mvua tu bali ni uchakavu wa mitambo na hali mbaya ya distribution system. Mimi ningewashauri hao wakubwa waachane na mawazo ya kwamba kuna jawabu rahisi. Tuboreshe usambazaji wa umeme na kuhakikisha kuwa ni kiasi kidogo tu kinachopotea njiani kuelekea kwa mtumiaji.

      Tuangalia vyanzo vidogo vidogo. Ukiangalia mahityaji yetu ya umeme kwenye miji mingi ni madogo na si ya kutisha. Tuangalia solution zinazoendana na sehemu hizo. K.m. Singida wawekeze kwenye upepo na jua, sehemu za milima kwenye maporomoko madogo nako wanaweza kujenga vi micro power station (maporomoko ya mita moja yanaweza kuzalisha umeme wa kutosha kijiji), sehemu zenye wafugaji waangalie bio-gas, sehemu zenye wakazi wengi, taka taka zao zitumike kuzalisha umeme, kodi kwenye vifaa vya kuzalisha umeme endelevu (sio jenereta) ipunguzwe ili wananchi waweze kuzalisha umeme kwenye majumba yao na kwenye maofis, wenye viwanda kama vya sukari wahamasishwe kuzalisha umeme kutokana na masalio ya miwa, vile vile wenye viwanda vinginei n.k.

      Vyote hivi vikiunganishwa, hili tatizo tutalitatua kwa kiasi kikubwa na zaidi ya yote kuweka umeme karibu na wananchi wa kawaida ambao sehemu kubwa hadi leo wanaosikia kwenye redio zao za betri!

      Tuachane na hii miradi mikubwa ambayo sana sana inawafaidisha wachache sana.

      Amandla........
      Fundi Utumbo

    12. #31
      Mdondoaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2009
      Posts : 4,731
      Rep Power : 1490
      Likes Received
      808
      Likes Given
      343

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Mo,

      Ni maoni mazuri na sio kusema Dr Idriss hafai au anafaa. Kwa kuongezea ni kwamba Tanzania tusifikirie one energy source tunaweza kufocus katika Nuclear Energy. Sababu kuu ni tatu kwanza hii energy ni renewable energy therefore inaweza kuwa environmental friendly. Pili Tanzania ina reserve kubwa ya uranium madini ambayo ni haba duniani na malighafi kuu katika uzalishaji wa umeme. Tatu, maji or hydro-electical na windpower energy ni seasonal hivyo basi panaweza kutokea shortage ya umeme kipindi fulani but Nuclear energy inatwanga throughout the year.

      Disadvantage zake ni kwamba ni expensive na sometimes can be dangerous kwasababu technologia yake huweza kubadilishwa kuwa silaha but to me those are trivial issues. Kuhusu gharama tunaweza kuspread costs tukashirikiana na wenzetu uganda na Kenya (even though kenya wenzetu wameshatenga budget ya hiyo kitu). But tunaweza kushirikiana na wenzetu. Pia tunaweza kuomba funding from world bank tukawalipa kidogo kidogo kwani tukishaanza kuzalisha umeme tunaweza kuuza nchi za jirani tukapa pesa za kulipa deni na shirika likajiendesha kibiashara. Kuhusu silaha nadhani Atomic Agency ya Professor Mohammed Elbaradei. Hii inasimamia na hivyo basi watatoa misimamo yao. Tuna mtaalamu mkali anayetambuliwa duniani Dr Shein (Vice president wa Tanzania tumtumie kwa faida ya Tanzania).

    13. #32
      Fundi Mchundo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2007
      Posts : 4,351
      Rep Power : 2682
      Likes Received
      194
      Likes Given
      137

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Ni maoni mazuri kusema Dr Idriss hafai au anafaa.
      Hawezi kuepuka responsibility hata umtetee vipi. It was under his watch hali ya sasa ndiyo imetokea. Obama analaumiwa kuhusu kukesekana kwa kazi marekani ingawa wote wanajua matatizo yalianza na George W. Yeye ndiye yuko kwenye madaraka na hawezi kukwepa responsibilty. Ndivyo ilivyo kwa Idriss. Hawezi kuepuka kwa kuwasingizia waliomtangulia au wanasiasa. Yeye angeona yote haya kama ni obstacle basi angeachia ngazi.

      Hapana, Mkuu. Dr. Rashidi hafai kuendelea na uongozi wa Tanesco. Awapishe wengine wajaribu. Sababu nyingine ziko hapa http://allafrica.com/stories/200907280404.html

      Amandla.....
      Fundi Utumbo

    14. #33
      Mdondoaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2009
      Posts : 4,731
      Rep Power : 1490
      Likes Received
      808
      Likes Given
      343

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Fundi Mchundo View Post
      Hawezi kuepuka responsibility hata umtetee vipi. It was under his watch hali ya sasa ndiyo imetokea. Obama analaumiwa kuhusu kukesekana kwa kazi marekani ingawa wote wanajua matatizo yalianza na George W. Yeye ndiye yuko kwenye madaraka na hawezi kukwepa responsibilty. Ndivyo ilivyo kwa Idriss. Hawezi kuepuka kwa kuwasingizia waliomtangulia au wanasiasa. Yeye angeona yote haya kama ni obstacle basi angeachia ngazi.

      Hapana, Mkuu. Dr. Rashidi hafai kuendelea na uongozi wa Tanesco. Awapishe wengine wajaribu. Sababu nyingine ziko hapa http://allafrica.com/stories/200907280404.html

      Amandla.....
      Mie nina swali moja tu kwako na link uliyotupa kuhusu matengenezo ya nyumba. Je makisio ya shirika yanasemaje? Kama Board iliyapitisha, basi Idrissa hata mumseme vp kama yamo ndai ya budget tatizo lipo wapi mkuu??? na Mohammed Dewji kazungumzia opinion yake kuhusu umeme inahusiana vp na Dr Idrissa hiyo hoja ipeleke kwenye Thread ya Dr. Idrissa mie nimeitoa kama rhetoric statement ya kwamba tuzungumze cha maana kuhusu Tanesco kwani hapa JF na hakika hata Rais akipata muda huwa anaisoma aone maoni ya wananchi sasa tuzungumze constructive criticism na sio destructive ili nchi iendelee na sio kurudi nyuma

    15. Tom is offline
      Tom
      #34
      Tom's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2007
      Posts : 504
      Rep Power : 719
      Likes Received
      17
      Likes Given
      30

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mkandara View Post
      Tumewekesha nguvu za Umeme ktk Hdro power miaka 30 iliyopita na nguvu zake zinatuwezesha kila kata nchini kupata umeme.. Swala kubwa ni UKARABATI, utamaduni ambao sisi MIAFRIKA hatuna..

      Inashangaza na kusikitisha sana naposoma makala ikisema tuna Hdropower yenye uwezo wa kuzalisha Mw 4,700 lakini ni only asilimia 12 ya uwezo huo ndio inatumiwa..

      Na ukirudi ktk matumizi tunaambia only asilimia 12 ya wananchi ndio wanapata Umeme kitu ambacho kinanipa imani kwamba kama Mw zote 4,700 za hdropower zikifanya kazi tutakuwa na uwezo wa kuwapa wananchi kwa asilimia 100..Hapo bado hatujahesabu nguvu nyinginezo..

      Ni uzembe mtupu unatumika kwetu sijui hizo nchi nyinginezo lakini binafsi sioni sababu nje ya kutokuwa na VIONGOZI BORA..
      Hili nimewahi kulizungumzia hata wakati tunauza viwanda vyetu...Matatizo yalikuwa tulishindwa kuzalisha kulingana na kiwango cha viwanda vyenyewe, haya soko lilikuwepo iweje tunauza viwanda wakati tatizo sii viwanda ila ni uongozi mbaya wa viwanda hivyo?..

      Haya sii ndio ya mwanamme kumtalakia mke kwa sababu hapati mtoto hali ukweli ni kwamba bwana ndiye mwenye matatizo ya uzazi?..
      Inawezekana design ilikuwa hiyo MW 4,700 kama unavyosema lakini baada ya matumizi ya miaka mingi hicho kiasi hupungua tokana na kupungua kwa kina cha maji baada ya ukame ama mkusanyiko wa matope chini ya bwawa. Tope huletwa na mto. Kuondoa matope ni ghali sawa na kujenga hydro nyingine ama zaidi.

      Kama turbines zipo zenye uwezo zaidi (yaani zina mizunguko zaidi kwa kiasi kilekile cha maji), basi dawa ni kubadilisha. Lakini kuna uwezekano zilizopo TZ ni zile bora hivyo jibu ni kuendelea kujenga hydro zingine. Kama hatuna sehemu za kujenga hydro moja kubwa basi inabidi tuangalie sana uzalishaji kwa solar ama thermal power. Nuclear ni jibu zuri lakini je tunaiweza? Nchi nyingi, hata China walianza kwa kujengewa nuclear power, nasi tunaweza fanya hivyo.

      Lakini je CCM inaweza SIMAMIA maana badala ya nafuu itakuwa ghali na hapo ndio naungana nawe kua HATUNA UONGOZI BORA kutuletea mbadala wa vihydro.

    16. #35
      Jahom's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 26th August 2008
      Posts : 221
      Rep Power : 596
      Likes Received
      15
      Likes Given
      4

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Kwa nini Afrika tu? They are still with us. Kumbuka wale jamaa waliotaka kuhujumu mitambo ya Msumbiji akiwemo mjerumani nadhani ili wapate dili la biashara za majenereta. Wafanyabiashara nanyi mmo kwa kutengeneza matatizo!! Hata tatizo letu ni artficial, kuna watu wanafanya biashara zao, na ndivyo zilivyo nchi nyingine za Afrika.

    17. #36
      Fundi Mchundo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2007
      Posts : 4,351
      Rep Power : 2682
      Likes Received
      194
      Likes Given
      137

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mdondoaji View Post
      Mie nina swali moja tu kwako na link uliyotupa kuhusu matengenezo ya nyumba. Je makisio ya shirika yanasemaje? Kama Board iliyapitisha, basi Idrissa hata mumseme vp kama yamo ndai ya budget tatizo lipo wapi mkuu??? na Mohammed Dewji kazungumzia opinion yake kuhusu umeme inahusiana vp na Dr Idrissa hiyo hoja ipeleke kwenye Thread ya Dr. Idrissa mie nimeitoa kama rhetoric statement ya kwamba tuzungumze cha maana kuhusu Tanesco kwani hapa JF na hakika hata Rais akipata muda huwa anaisoma aone maoni ya wananchi sasa tuzungumze constructive criticism na sio destructive ili nchi iendelee na sio kurudi nyuma
      Mkuu, wewe ndiye uliyemuingiza Idriss humu. Hamna cha rhetoric whatever. Usitake kukwepa responsibility kama anavyotaka kufanya huyo unayemtetea.

      Tatizo sio kuwa matengenezo yalikuwemo kwenye bajeti au la. Tatizo ni item kama ya maua ya plastiki iliingiaje kwenye hiyo bajeti. Tatizo ni kuwa katika wakati huu mgumu, kiongozi makini anaweza kupeleka maombi kama hayo kwa bodi yake? Kupitishwa na bodi si hoja. Bodi zetu mara nyingi zinategemea fadhila za menejimenti au unadhani vibahasha vinatoka wizarani au bungeni?

      Wakati mwingine tunahitaji kubomoa kabla ya kujenga. Hapa hakuna anayemchukia Dr. Idriss kama mtu bali tuna kila haki ya kupinga kuwa anastahili kuendelea kama ilivyo kwako kumtetea kuwa anafaa.

      Amandla.......
      Fundi Utumbo

    18. #37
      Kaniki1974's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2008
      Posts : 357
      Rep Power : 609
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Pengine TANESCO wamewahi kuwa na mpango kabambe kama huo. Hebu watwambie kama wamehi kuwa nayo ili tujue ni kwa kiasi gani siasa zetu chafu na mipango mibovu imekwamisha juhudi za wataalamu! Tatizo kubwa ni uongozi usio na uwezo, nia, dira wala uzalendo!
      'The rich of the future are those who are rich in mind'. Winston Churchill

    19. #38
      Chapakazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2009
      Location : Kathmandu
      Posts : 2,910
      Rep Power : 1100
      Likes Received
      256
      Likes Given
      272

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      Wabunge ndio hupitisha mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu ya serikali na ni wao huitengenea fedha. Na pale ambapo hakuna sheria ya kusababisha jambo fulani kufanyika wabunge wana uwezo (kama kundi -chama, au kama mtu mmoja mmoja) kuleta mswada wa sheria wa kusababisha jambo hilo kutendeka au kutotendeka.

      Suala la tatizo la nishati siyo geni kwa TAnzania na kwa eneo letu la Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa upande wetu Tanzania tatizo hili ni dalili tu ya tatizo lenyewe tulilonalo ambalo ni mipango mibovu ya wanasiasa wetu. Tanzania haina sababu hata chembe ya kuwa upungufu wa nishati ya umeme.

      Leo hii kuweza kuyarejesha mabwawa yetu yote ya kuzalishia umeme kwenye full capacity inakadiriwa kutumia karibu dola bilioni 2! Lakini tukifanya hivyo zaidi tutakachopata ni kama Megawatts 1000 hivi (kama sikosei). Lakini wakati huo huo tukitamua kujenga bwawa moja kubwa la Stielger's Gorge itatugharimu karibu dola bilioni 2 vile vile lakini tunaweza kupata Megawatts zaidi 2900!

      Wanasiasa wetu hawajui wachague nini! suluhisho lao ni kuingiza majenereta ya umeme na kutoa tenda zaidi ya majenereta. Wako tayari shilingi milioni nyingi kila siku na ukiwauliza hadi leo (kuanzia 1995) serikali imetumia kiasi gani katika kulipia mafuta na IPPs, jibu lake litawafanya muinamishe kichwa kwa aibu!

      Sasa, Mhe. Dewji,

      a. una mpango gani wa kuleta mswada Bungeni wa kusababisha ujenzi wa Stielger's gorge au kutengea fedha mradi huo mkubwa ilii hatimaye tuondokane na tatizo la umeme?

      b. Una msimamo gani kuhusu kampuni ya Dowans ambayo iliingia nchini kitapeli na hadi leo tunahangaika na majenereta yao. Je, kwa maoni yako serikali itaifishe mitambo hiyo na kuwachukulia hatua wahusika wote?

      c. Unafikiri Kamati yenu Teule ya Bunge ilifanya kazi yake vizuri katika suala la Richmond na hivyo kazi yake iheshimiwe na wabunge wote au unaamini ilikuwa imewaonea watu mbalimbali?
      d. Na wewe mtoa mada una mpango gani wa kusababisha ujenzi wa Stielger's gorge kwa kusudi la kusaidia tuondokane na tatizo la umeme?
      Change begins with YOU

    20. #39
      Cynic's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th January 2009
      Location : Around
      Posts : 2,172
      Rep Power : 975
      Likes Received
      318
      Likes Given
      187

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post

      Leo hii kuweza kuyarejesha mabwawa yetu yote ya kuzalishia umeme kwenye full capacity inakadiriwa kutumia karibu dola bilioni 2! Lakini tukifanya hivyo zaidi tutakachopata ni kama Megawatts 1000 hivi (kama sikosei). Lakini wakati huo huo tukitamua kujenga bwawa moja kubwa la Stielger's Gorge itatugharimu karibu dola bilioni 2 vile vile lakini tunaweza kupata Megawatts zaidi 2900!
      Nadhani tatizo ni kukosa utashi. TRA wanakusanya close to US$ 2 billion kwa mwaka. Kama kungekuwa na utashi hata kwa makusanyo yetu ya ndani tungeweza kukamilisha miradi kama hii kwa miaka 5-10.

    21. #40
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,622
      Rep Power : 46738
      Likes Received
      16720
      Likes Given
      8561

      Default Re: Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

      Quote By Mtoto View Post
      d. Na wewe mtoa mada una mpango gani wa kusababisha ujenzi wa Stielger's gorge kwa kusudi la kusaidia tuondokane na tatizo la umeme?
      mpango wao ndio huo!
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 121
      Last Post: 24th May 2013, 04:10
    2. Nyumba ya kukodi Dar kwa muda mfupi
      By Sokwe Mjanja in forum Matangazo madogo
      Replies: 3
      Last Post: 30th August 2011, 10:59
    3. Replies: 9
      Last Post: 4th March 2011, 11:42
    4. Natafura rent ya muda mfupi
      By Kwame Nkrumah in forum Matangazo madogo
      Replies: 9
      Last Post: 26th August 2010, 17:31

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...