Your point stimulates kitu kingine. Sote tunajua umuhimu wa diaspora remittance - fedha ambazo kwa mfano, watanzania walio nje wanatumia ndugu zao. Kwanini sisi tupo nyuma ya nchi nyingi sana Za Afrika? Kenya, Uganda, wametupita sana katika hili. Wakenya, Waganda, waliopo Canada huko kwako Mkandara, waliopo UK, USA, etc, kila mwaka wanatuma jumla ya dollar zaidi ya billioni moja; Sisi Tanzania hata nusu ya hizo hatutumi nyumbani. Na takwimu za WorldBank zinaonyesha kwamba, idadi ya fedha hizi kuja bara la afrika ni kubwa kuliko idadi ya Foreign Aid. Fedha hizi za waafrika waliopo nje wanaotumia ndugu zao, wingi wake umepitwa na Foreign Direct Investment Pekee, then second ndio hizi fedha, na third ni Foreign Aid. Na hizi ni jumla ya fedha watu wanazotuma western union n.k.
Kwanini sisi watanzania tupo nyuma katika hili? hatupendi ndugu zetu nyumbani wafanikiwe? tuna roho mbaya? Kwanini waganda, wakenya wanatupita katika hili? Wataalam wanasema kwamba impact ya fedha hizi ni kubwa kuliko ile ya Foreign Aid kwani unlike foreign aid ambayo ina matatizo mengi kama masharti ya WorldBank jinsi gani ya kuzitumia, ubadhirifu na ufisadi wa viongzi wetu n.k, diaspora remittances - fedha zinazotumwa na watanzania waliopo mfano wa Ulaya, Marekani kuja Tanzania zinaenda moja kwa moja kwa mlengwa na nyingi husaidia familia zao in terms of ada za shule, matibabu, lakini pia zinanunua viwanja, baiskeli, zinajenga nyumba n.k.
Hata hapa kwetu Tanzania, ni kabila moja tu ndio lenye tabia ya kujali kwao - nao ni wachaga. Hawa kwao kuna maendeleo kutokana na utamaduni wao wa kutuma fedha makwao, kuanzisha miradi makwao, kujenga n.k. Lakini wanyakyusa, wahehe, wanyamwezi, wahaya, wabondei, wasukuma, wakurya, wangoni, n.k, wengi wao hawafanyi hivyo. Ina maana makabila mengine hawana uwezo wa fedha kama wachaga? Au wana roho mbaya au ni hawana moyo wa kizalendo kwa ndugu zao huko mikoani? Makabila mengi, kipimo cha mafanikio yao ni matumizi Dar-es-salaam.
Follow Us Here