Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar

    Report Post
    Page 3 of 18 FirstFirst 1234513 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 354
    1. #1
      Morani75's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st March 2007
      Location : Duniani
      Posts : 662
      Rep Power : 761
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar

      Wana JamiiForums wenzangu...

      Hii habari ninayoiweka ni kutoka kwenye gazeti la Guardian, 09/07/2007. Kwa kweli UCLAS wamekuja na mpango mzuri. Lakini kwa wale ambao wapo kwenye vyombo kama ERB, UDSM, DIT na vyuo vingine kwa pamoja na serikali na sekta binafsi ikiwemo Polisi, Ujenzi, TANROADS, Conslutants, SUMATRA, MUWADA etc wachangie mawazo. Wenzetu wa UCLAS kama mpo jumuisheni wadau wengine ili mpango wenu uwe maridhawa na utoe suluhu ya tatizo hili la usafiri.

      Wazee wa vyuo vikuu, jamani wanafunzi wakati wanafanya projects kwa nini wasipewe mwamsho wa kuweza chunguza na kutoa mapendekezo yao kuhusu suala hili...tayari UCLAS wameshatupa "skeleton" what we need now ni "flesh and blood". Congrats UCLAS but don't hide the info to yourself, share and improve it to cater for the need......

      The article is as below:

      UCLAS: Here is the major solution for Dar congestion

      2007-07-09 09:49:32
      By Pascal Shao



      The University College of Lands and Architectural Studies (UCLAS) has come with a cost effective and permanent solution on road traffic jams in Dar es Salaam.

      UCLAS Assistant Research Fellow, Hussein Rajab, told The Guardian that should the government take into account the said solution, traffic congestion in the city of Dar es Salaam would become history.

      He said: ``Most traffic congestions arise at the junctions. The only answer to traffic jams is to improve the intersections where vehicles converge. Improvement here means construction of either flyovers (overpass) or underpass lanes.

      ``Overpass or underpass is a permanent solution as vehicles will not meet at the junctions as the situation appears at the moment,`` he said.

      He said the lanes would facilitate movement of vehicles heading to final destinations without meeting at the junctions (where there are traffic lights).

      Rajab said the solution would be suitable for small vehicles rather than daladalas due to stoppages and heavy vehicles, as 80 percent of traffic to city centre is made up of small vehicles.

      He said that overpasses could be applicable at the junctions of Mwenge, Morocco, Ubungo, Tabata, Shekilango to mention a few, while the underpasses could be built at the slopes of Kawe Road, St Peter road junction etc.

      ``Construction of an overpass or underpass is a one time investment,`` he said.

      Rajab said expansion or adding more roads would not reduce traffic jams but would instead facilitate vehicles to meet at the junctions.

      He said that traveling on congested roads resulted in increased fuel consumption.

      He mentioned effects of traffic congestion as time wastage, environmental pollution, tear and wear and stress. He further mentioned other effects as difficulties in case of emergencies, noise as motorists try to divert to other quiet areas such as hospitals and schools.

      Dar es Salaam has been experiencing traffic jams, which normally occur during peak hours in the mornings and evenings, as most traffic is heading to and from the city centre due to most offices being located there.

      SOURCE: Guardian

      Hali ilivyo kwa Dar as at March, 2010:


      Ali Hassan Mwinyi road


      Morogoro road near Magomeni Mapipa


      Old Bagamoyo road near Shopper's plaza


    2. Miaka 50

    3. #41
      MwanaHaki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2006
      Posts : 1,413
      Rep Power : 1003
      Likes Received
      156
      Likes Given
      91

      Default Re: Tatizo la Msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam

      Wakuu wote mliochangia,

      Minawashukuru sana kwa mawazo yenu, maoni na ushauri wenu. Hakika mawazo mliyonayo yanatosha kunidhihirishia kwamba (a) Watanzania tuna kila sababu ya kuwa mojawapo ya nchi tajiri kuliko zote hapa duniani, (b) kwamba Watanzania tuna uwezo mkubwa wa kutatua matatizo yetu kutokana na kuwa na upeo mkubwa wa kugundua nini chanzo cha matatizo yetu, na (c) popote pale ambapo Watanzania tutahitajika kutoa mawazo yetu, kwa kuleta maendeleo ya kasi na ya jumla kwa nchi yetu, uwezo huo tunao, na tunaweza kuufanyia kazi bila pupa wala papara.

      Mmenithibitishia kwamba, ufumbuzi uko kwenye mipango na utekelezaji. Mimi nilitoa chachu, kwamba fly-overs ni mojawapo ya solutions, sio solution pekee, na ninyi mkachambua zaidi. Nawapongezeni sana kwa hilo.

      Kimsingi, Dar es Salaam haipaswi kuwa na msongamano wa magari wa aina yoyote. Lakini kutokana na wahusika wa mipangomiji (hawa ndio main culprits) kuvuruga Dar City Masterplan ya 1967, sasa tunajikuta mahali ambapo kila unapoangalia, watu wamefanya ujenzi wa kudumu kando kando ya barabara, tena kwenye eneo la hifadhi ya barabara. Upanuzi wa Barabara ya Morogoro wala haukuwatoa watu barabarani, walibomolewa, lakini wamebakia kwenye eneo la hifadhi! According to Hon. Magufuli, eneo la hifadhi la barabara kuu (highway) ni mita 400 tokea kati kati ya barabara, kwa pande zote 2. Nenda Morogoro Road ukapime, kama hukuzikuta nyumba na majengo kadhaa yakiwa kwenye reserve area.

      Kama hao (samahani kama kuna watu ambao nitakuwa nimewakwaza kwa hili...) mambumbumbu ambao wamekataa ushauri, wangekubali kuanza kutekeleza mfumo wa business clusters, kusingekuwa na tatizo la vertical growth ya CBD... Business Clusters zingejengwa kila mahala, na mkazi wa - mathalan Mbagala - asingelazimika kupanda basi hadi Tegeta, kwenda ofisini kwake, kwani hapo hapo alipo kungekuwa na ofisi ambayo angeweza kufanyia kazi.

      Serikali - na sijui kuna ugumu gani wa kutekeleza jambo rahisi kama hili - mpaka leo inawalazimisha watu waende Wizara ya Ardhi kulipa kodi ya ardhi, wakati wanaweza kuweka Ward and District Lands Offices, ili watu walipie kodi hizo huko wanapoishi. Mtu anaishi Yombo, Buza, Tandika, au hata Kimanzichana (achilia mbali Kinyerezi, Pugu Kajiungeni, au segerea), analazimika kupanda basi, au kuendesha gari yake, hadi Kivukoni, Wizara ya Ardhi, akalipe kodi ya kiwanja chake! Mbona tayari Wizara ya Ardhi imetengeneza lands database, ambayo inawawezesha kujua nani amelipa kodi ya ardhi na nani hajalipa? Wamefanya aircraft survey na kujua ni viwanja vipi (wame cross-check na GIS data) vimejengwa, vipi havijajengwa. Wamefika mbali, lakini kwenye utekelezaji hapo ndio tatizo.

      Wasiseme kwamba hakuna ICT infrastructure inayowawezesha kuwa na online au hata offline data transfer, kwani hicho ni kichekesho. Kama Kimanzichana wanaweza kupata Internet access kupitia TTCL Mobile au Broadband, sembuse ofisi ndogo ya Lands, ya Kata?

      Nadhani hapa nimeeleweka. Suala ni utekelezaji. Secondary roads zinaweza kukarabatiwa ili kuwawezesha watu kutumia secondary roads badala ya primary roads. Na hizi secondary roads zipo nyingi tu, kwenye hali mbaya. Ipo hiyo ya kupitia Kijitonyama hadi kuungana na ya Mwananyamala (Kwa Kopa, Komakoma hadi Mwinyijuma), na kwa bahari nzuri, secondary road inayotoka Sayansi hadi Tandale kwa Ali Maua, Uzuri, Uwanja wa Fisi, Magomeni Makanya hadi Magomeni Mapipa inapitika vizuri tu... ni ya lami! Hii inaokoa sana msongamano.

      Lakini nasisitiza, bado fly overs ni muhimu ili kuondoa kabisa kuwa na haja ya traffic lights. Tukifanikiwa kwa hili tutakuwa tumepiga hatua kubwa, na utakuwa mwanzo wa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!

      Ndio, Maisha Bora yanawezekana... tutayaleta sisi, sio JK wala mtu mwingine yeyote.

      Suala la financing? Wapo watu ambao wana nia njema OUTSIDE of Tanzania, ambao tunaweza kuwatafuta, na tukaingia ubia nao. Hili linawezekana. Daraja la Kigamboni linatafutiwa mwekezaji... kuna yeyote mwenye ideas?

      ./Mwana wa Haki
      Speaking Openly, without fear!

    4. #42
      Bin Maryam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd October 2007
      Posts : 698
      Rep Power : 731
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Tatizo la Msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam

      Quote By MwanaHaki
      Wadau,

      Ndugu zangu wa JF ambao mnaishi kwenye Jiji la Dar es Salaam mnalifahamu vema tatizo (ambalo sasa ni janga halisi) la msongamano wa magari barabarani. Tatizo hili limejidhihirisha wazi zaidi hususan kwenye siku za muda mfupi uliopita, wakati wa msimu wa mvua ndefu (masika) ambao uliungana na msimu wa mvua fupi (vuli) kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya kidunia (Global Climatic Change).

      Mojawapo ya mapendekezo ya iliyokuwa Kamati ya Uchambuzi juu ya Tatizo la Msongamano wa Magari, iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, lilikuwa ujenzi wa barabara zinazopita juu ya ardhi, maarufu kwa jina la fly-overs.

      Lengo kuu la fly-overs ni kuwezesha magari kupita juu ya barabara moja kwa moja kwenye kila sehemu ya makutano, hivyo kuondoa haja ya kusubiri magari yanayoruhusiwa kupita (kwa zamu) na taa za kuongoza magari (traffic lights). Kwa mfano, iwapo kungekuwa na fly-over kwenye makutano ya Barabara ya Ali H. Mwinyi na Barabara ya Kawawa (Morocco), magari yaendayo Kinondoni kutokea Msasani yangepita moja kwa moja, na yale yaendayo Msasani kutoke Kinondoni nayo pia yangepita moja kwa moja, huku yale yaendayo Jijini kutokea Mwenge, Mbezi Beach, na Tegeta (na sehemu nyinginezo) yangepita moja kwa moja, na yale yatokeayo Jijini kwenda Mwenge, Mbezi Beach, Tegeta, na sehemu nyinginezo, vile vile yangepita moja kwa moja.

      Kwenye fly-over hiyo, iwapo gari ingetaka kwenda Msasani kutokea Mwenge, kungekuwa na sehemu (mstari) maalum ya kuliwezesha gari hilo kuingia pole pole kwa kutumia utaratibu wa kisheria unaojulikana kama "yielding". Utaratibu huo ungetumika pia kwa wale ambao wangetaka kwenda Kinondoni kutokea Mwenge, hivyo kuwezesha magari kutembea kwa kasi zaidi bila kusimama, na hivyo kufanikiwa kuondoa kabisa tatizo la msongamano wa magari.

      Watanzania wasingelazimika kuamka saa 9 alfajiri (kwa wale wanaoishi Mbezi Beach, Tegeta, Bunju, Boko, n.k.) ili waweze kuondoka nyumbani kwao saa 10 alfajiri ili kuwahi ofisini saa 1 au 1.30 asubuhi, tayari kwa kazi, kwa wale ambao wana ajira kwenye Serikali Kuu, kwani, badala ya kutumia muda wa saa 3 au 4 barabarani, wangeweza kutumia muda wa saa 1 au 2 tu!

      Ujenzi wa fly-over si kitu cha ajabu wa kitu kigeni. Ujenzi huu unatumika sana nchi za ulaya, na umeondoa na kupunguza kabisa tatizo la msongamano wa magari kwenye nchi nyingi. Tukumbuke pia kwamba, tunapotumia muda mwingi kwenye msongamano wa magari, sio tu kwamba hasara kubwa inatokea kutokana na (a) matumizi makubwa ya mafuta ya petroli, na (b) upotevu mkubwa wa muda ambao ungetumika katika shughuli za uzalishaji, bali pia (c) sisi wenyewe tunaathirika kiafya kutokana na kuvuta hewa iliyochanganyika na moshi wa magari ambao huwa na sumu na kemikali zenye madhara kwa afya zetu. Niliwahi kujikuta kwenye msongamano wa magari nikitokea Mbezi-Luguruni, nikiwa Ubungo-Kibo. Sehemu ambayo, kwa kawaida, kufika kwenye makutano ya Barabara ya Morogoro na Barabara ya Sam Nujoma huchukua muda wa dakika 2 au 3, nililazimika (pamoja na watu wengine kadhaa) kutumia muda wa saa 2! Nilikuwa ninatokea Mbezi-Luguruni kurudi nyumbani Mbezi Beach. Nilipofika nyumbani nilishindwa kabisa kuona, nikalazimika kuosha macho yangu kwa maji, lakini sikupata nafuu, nikaenda kulala. Siku hiyo ilikuwa Jumamosi, nilifika Ubungo-Kibo saa 12.30 jioni, ilipofika saa 1.30 usiku ndio nilifanikiwa kuvuka makutano ya Barabara hizo, hatimaye kufika nyumbani saa 3.30 usiku! Nilikuwa nimealikwa kwenye sherehe ya harusi ya jamaa wa familia; sikuweza tena kwenda kutokana na kuumwa macho. Nimdai nani?

      Swali langu, baada ya kutoa hoja, ni, je, Watanzania wenzangu mliopo nje ya nchi mnaonaje kama mtachukua jukumu la kuongea na makampuni ya ujenzi wa barabara ili yaweze kuja Tanzania na kuingia ubia na, ama (a) Serikali Kuu au (b) Watanzania wenye uwezo wa kushirikiana nao ili kuweza kujenga hizi fly-over na kuondoa kabisa hili tatizo? Serikali Kuu tayari imekwishaweka mkakati wa ujenzi unaojulikana kama Build-Operate-and-Transfer (BOT), ambao unamwezesha mjenzi kukopa pesa kwa minajili ya kurejeshewa alichowekeza kwa njia ya kutoza kodi za moja kwa moja au "indirect taxation". Ninaamini kwamba Watanzania waliopo nchini(hususan Dar es Salaam) hawatapinga nyongeza ya kodi kwenye mafuta ya petroli kuwarejeshea wajenzi wa fly-over kile walichowekeza, ili mradi fly-over zinajengwa na tatizo la msongamano linaondolewa kama si kupunguzwa kwa kiwango kikubwa.

      Naomba kuwasilisha hoja.

      ./Mwana wa Haki
      Wadau:

      Msongamano wa magari una factors nyingi. Moja wapo ni mlipuko wa ongezeko la watu katika miji wakati miundo mbinu imebaki hile hile ya enzi ya Sir Richard Turnbull.

      Na tatizo la mlipuko wa ongezeko la watu limesababisha matatizo mengi pia kama mifereji ya maji machafu, ugavi wa umeme, maji safi, mashule na mambo mengine.

      Tukirudi kwenye mada. Ujenzi wa Fly-over unasaidia lakini ujenzi huo utakapomalizika bado inawezekana kama usisaidie kuondoa tatizo hilo kama vile ndugu Lowassa na wengine wanavyofikiria. Kuna wasomi hapa walisoma mambo ya simulation, queue theory na vitu vingine. Mathematically hawa watu wanaweza kutuambia kwa kutumia utafiti wa kisayansi je ujenzi wa fly-over unaweza kusaidia kwa kiwango gani.

      Ubora wa mtiririko wa kitu kwa kupitia njia fulani (uwe mtiririko wa matumizi ya simu, matumizi ya maji, matumizi ya barabara, matumizi ya network za computer) unategemea weakest link. Mfano wa weakest link ni barabara nzuri ambayo ina kipande kilicho kibovu. Kama hicho kipande kibovu kitachelewesha magari kwa zaidi ya saa nzima basi uzuri wa barabara nzima hautakuwepo.

      Barabara za DSM zina weakest links nyingi sana. Ukijenga fly-over utakuwa umepunguza moja ya hizo. Lakini vilevile magari mengi mabovu yanatembelea na kuharibika katikati ya barabara mara kwa mara. Vile vile madereva hawafuati sheria za usalama barabarani.

      Vilevile usambazaji wa huduma na bidhaa muhimu umejazana sehemu moja hivyo kusababisha watu kusafiri kutafuta vitu ambavyo wangevipata katika sehemu wanazaoishi. Kwanini soko la samaki liwe feri na sio karibu na vitongoji.

      Kama nilivyosema hapo juu. Msongamano umesababishwa zaidi na mlipuko wa ongezeko la watu. Mwanzo ulisababisha matatizo ya maji na mpaka leo tumeshindwa kutatua na sioni ufumbuzi wa karibu wa kutatua matatizo ya msongamano wa magari kama watu pamoja na serikali hawatabadilika na kuanza kuishi kwa kutumia kanuni za miji.

      Na kuhusu kutumia wataalamu wa nje kujenga Fly-over. Wakati umefika watanzania kujifunza kufanya mambo kwa kutumia resource zao. Asilimia 20 inakwenda kwenye ujenzi wa vitu na asilimia 80 inakwenda katika maintanance na uendeshaji. Hivyo kutumia wataalamu kutoka nje na wewe kushindwa kuendesha au kufanyia maintance inakupa ufumbuzi wa muda mfupi na ni ULEVI.
      Believing in God costs you nothing if you're wrong, and wins you everything if you're right.

    5. #43
      Morani75's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st March 2007
      Location : Duniani
      Posts : 662
      Rep Power : 761
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Exclamation

      Quote By MwanaHaki
      Wakuu wote mliochangia,

      Minawashukuru sana kwa mawazo yenu......

      Mmenithibitishia kwamba, ufumbuzi uko kwenye mipango na utekelezaji.......

      Kimsingi, Dar es Salaam haipaswi kuwa na msongamano wa magari wa aina yoyote. Lakini kutokana na wahusika wa mipangomiji (hawa ndio main culprits) kuvuruga Dar City Masterplan ya 1967.......

      Suala la financing? Wapo watu ambao wana nia njema OUTSIDE of Tanzania, ambao tunaweza kuwatafuta, na tukaingia ubia nao. Hili linawezekana. Daraja la Kigamboni linatafutiwa mwekezaji... kuna yeyote mwenye ideas?

      ./Mwana wa Haki
      MwanaHaki, hapo naona mkuu umeweka mambo bayana.... Lakini naomba pia niweke my 2 cents kwenye zile "bold & red" kama ifuatavyo:
      1. Utekelezaji na planning ndipo haswa tunapochemsha... Leo nimesoma kwenye Daily News kuwa eti TANROADS Singida wameweza kutumia less than 50% of approved budget?? Kwa kweli kwa sisi tunaofahamu Tanzania na mikoa yake na barabara zake je kweli huyu Manager amekosa kutafuta barabara za kutumia pesa hizi?? - Angalia attached artcle kule chini

      2. Dar Master Plan ya 1967, c'mon ina maana that is all we have?? Tumeshaliongelea hili sana tu na naona umweuwekea what is the masterplan we are following, 1967..... Mungu atubariki!!

      3. i. Hili la Financing naona niseme reference ya 2 instances.... Kwanza ni kwenye article ileile ya Daily News kuwa Singida TANROADS could not spend 50% of approved budget.... Pili ni kwenye swala zima la ripoti ya CAG bungeni kuhusu Budget excesses zinaendaga wapi manake haziko documented kama zimerudishwa Hazina or what?? Wakuu hili nipo tayari kuanzisha mjadala sababu liliachwa open na hakuna ajuaye manake kama TANROADS Singida pekee wanarudisha 50% of More than 3Bn, je mikoa yote Tanzania ikifanya hivyo (ni kitu cha kawaida sana kushindwa kutumia pesa) manake ni zaidi ya 48Bn, je hizi zinaendaga wapi? Hii ni TANROADS tu hujaweka sehemu nyingine lukuki!!

      3. ii. Hili la Daraja la Kigamboni naona umekuwa mchezo wa kuigiza sasa manake hatuoni mbele wala nyuma (with some of wanaJamvi saying watatuletea data za mchawi)... Sasa Mkuu unasema tatizo ni Investor, mbona tulishaambiwa huku jamvini kuwa nadhani ni Holand walikuwa tayari kulipia part of the costs, sasa hili tena????

      Namba kuwakilisha wakuu....

      Daily News la jana ni hili:

      Agency spent over 1.8/- on regional roads

      ABBY NKUNGU in Singida
      Daily News; Thursday,
      May 01, 2008


      THE Tanzania National Roads Agency (TANROADS) in Singida region spent over 1.8bn/- for the maintenance of its various roads in the region between July 2007 and March 31, this year.

      Presenting the Implementation performance report of the financial year 2007/2008 before the Regional Roads Board meeting here, TANROADS Regional Manager, Mr Yusitaki Kingolle said the amount so far spent was only
      49.8 per cent out of the approved budget of 3.7b/-.

      According to Mr Kingolle, the work carried out during the period included routine and periodic maintenance, spots improvements, construction and installation of bridges on various trunk and regional roads.

      Giving the breakdown, he said that over 299.4m/- was spent on repairing trunk roads, 443.6m/- on rehabilitating regional roads, over 536.6m/- on improving the spots and more than 394.2m/- ended up on periodic maintenance as well as 170m/- on bridges.

      He named the trunk roads as the Singida - Itigi, Rungwa - Itigi - Mkiwa, Singida - Manyara region border and Mbeya border - Rungwa Singida. Those repaired for the last nine months as he cited are Ilongero- Mtinko-Nduguti, Kidarafa-Nkungi, Njuki-Ilongero-Ngamu, Sabasaba-Sepuka, Kinyamsindo- Kititimo and Ikungi-Londoni-Kilimatinde. Others in the list included Manyoni-Heka-Ikasi, Heka-Sasilo-Iluma, Sekenke-Shelui, Misigiri-Kiomboi, Kizaga-Sepuka-Mlandala and Ulemo-Gumanga-Sibiti.

    6. #44
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,744
      Rep Power : 1162
      Likes Received
      251
      Likes Given
      2511

      Default

      Sasa huyu Waziri tena Dr na ndio anaongoza Wizara ya Miundo mbinu, lakini haelewi kuwa tatizo la msongamano wa Magari dar unaongezwa na wanasiasa kuchukua nafasi ya wataalamu, kwa kutoa maamuzi ya kuwekeza kila kitu katikati ya Mji au kariakoo, unategemea nini.

      Mwal hakuwa Mjinga alipo amua Serekali ihamie Dodoma, angalau Shughuli za serekali zingekuwa Dom, na wafanyabiashara wakawa Dar. Ok sasa ya Dom inaonekana ni ndoto au itachukua Muda.

      Solution ni kuacha kuongeza Maofisi katikati ya Mji, wakati bara bara ni zilizile na uwezekano wakuzipanua hakuna, parking hakuna.

      So Stop Development ya Majengo Makubwa Kariakoo na Katikati ya Mji wakati uwezo wa kuongeza miundo mbinu hakuna, hata hilo Jengo la UV-CCM, litaongeza hilo tatizo la misongamano, unless it is meant kwa wenzetu wadosi walio kosa makazi katikati ya mji.


      Msongamano wa magari wamsumbua Waziri wa Miundombinu

      Na Kizitto Noya

      WAZIRI wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa, amewataka wahandisi kubuni mbinu mbadala ili kupunguza kero ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

      Akifungua mkutano wa sita wa wahandisi uliofanyika Dar es Salaam juzi jioni, Dk Kawambwa alisema, msongamano huo wa magari unahatarisha maisha ya watu na kuathiri uchumi wa taifa kwa kuwa watu wanapoteza muda mwingi barabarani kuliko kazini.

      “Fikiria mkandarasi anapokaa kwenye msongamano wa magari anapoteza saa moja ambayo angekuwa kazini angeingiza Sh5,000,” alisema.

      Alisema mbali ya hilo, msongamano wa magari jijini Dar es Salaam unahatarisha maisha ya watu kwa kuwachelewesha madaktari bingwa kufika kazini pamoja na kuathiri sekta zingine zinazochangia uchumi wa taifa.

      Katika hatua nyingine, Kawambwa amewapiga marufuku makandarasi kuingia mikataba ya kazi bila kuwashirikisha wahandisi katika kazi husika ili kudumisha ubora wa kazi zao.

      Alisema juzi katika mkutano huo kuwa, kitendo cha makandarasi kutumia majina hewa ya makampuni ya wahandisi au kufanya kazi bila kuwashirikisha wahandisi ni hatari kwa usalama wao na ubora wa kazi.

      Awali, akisoma risala ya bodi, Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Steven Mlote, alielezea masikitiko yake kwa baadhi ya makandarasi kufanya kazi bila kuwashirikisha wahandisi.

      Alisema, kitendo hicho ndicho kinachosababisha kuporomoka kwa majengo na kufanya kazi zisizokuwa na ubora na hata kuhatarisha maisha ya watu.

    7. #45
      Mkimbizi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd August 2008
      Location : Hard disk
      Posts : 222
      Rep Power : 596
      Likes Received
      30
      Likes Given
      36

      Default Re: Msongamano wa magari wamsumbua Waziri wa Miundombinu

      Naona wanajaribu kuhamisha ofisi mbali mbali(long term plan). Mlimani city, millenium towerz etc. TOWN YA BAADAE NI KNYAMA, SINZA NA KWA KAKOBE PALE. lol

    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      Kiroroma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th February 2009
      Location : Lady Brand, RSA
      Posts : 300
      Rep Power : 584
      Likes Received
      35
      Likes Given
      21

      Angry UBUNGO JUNCTION hili nalo limekaaje?

      Nimetumia barabara ya Morogoro takriban wiki sasa ,Nimebaini kuwa Junction ya Ubungo ni chanzo kikubwa cha foleni ndefu katika eneo hilo.Pamoja na stendi ya mabasi yaendayo bara limekuwa ni tatizo kubwa sana.

      Askari wa Usalama barabarani wanajitahidi sana lakini bado ngoma ni nzito.Hivi hakuna suluhisho la kudumu mahali hapa?Wenzetu wanaweka flyovers sisi tunashindwa nini hasa?Pesa zipo,watalaam wapo,kinachogomba ni nini hasa.

      Wadau hebu tuishauri serikali na TANROAD.
      "Thinking is the hardest work there is,
      which is probably the reason so few engage in it.”

    10. #47
      Albedo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Posts : 4,978
      Rep Power : 1573
      Likes Received
      1076
      Likes Given
      555

      Default Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Wakuu wana bodi, mimi ni mmoja kati ya watu ambao wamekuwa wakikerwa sana na Foleni za Magari katika jiji la Dar Es Salaam! Kwa muda mrefu zimekuwepo zikichukuliwa hatua kadhaa katika kupambana na tatizo hili ambalo linamkera karibu kila mtu aishiye jijini hapa! Nikiwa ni mmoja ya wale wanaojarbu kwenda Mbali zaidi ya Kukerwa nimekuwa nikijaribu kufikiria njia ambayo yaweza kuwa nzuri na isiwe na cost kubwa ( Njia ambazo sitazizungumzia ni Fly Over Bridge ambazo wadau wengi wameshazizungumzia tayari).

      Kuna Maswali najiuliza ambayo kama yatajibiwa basi yaweza kuwa ni moja ya njia ya kupunguza msongamano usio wa lazima wa magari:

      1: Kwani ni Lazima mtu akitoka Kimara kwenda Tegeta lazima apitie Morogoro road + Sam Nujoma + Alli Hassan Mwinyi? Na kinyume chake?

      2: Kwani ni Lazima Mtu akitoka Kimara kwenda Ukonga lazima apite Morogoro road + Mandela + Nyerere Road? Na kinyume chake?

      Kwani Serikali isifikirie Kujega Major Road ( Mfano wa Sam Nujoma + Mandela road maeneo ya Kimara ambayo itatokea Segerea, ukonga na Upande mwingine Mbezi na tegeta ili ku off load Ubungo junction?


      "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM


    11. #48
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 4,033
      Rep Power : 1416
      Likes Received
      609
      Likes Given
      44

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Mkuu barabara zetu zinajengwa kutokana na matakwa ya kisiasa zaidi kuliko ya kiuchumi. Kama ingekuwa zinajengwa kwa matakwa ya kiuchumi na kuhakikisha hakuna msogamano, siku nyingi hilo tatizo lingekuwa limeondolewa. By the way, kujenga flyover ubungo hakuepukiki, serikali kwa sasa haioni kama hiyo ni priority kwa sababu sasa hivi inabidi wajilinde kwanza na kesi za EPA, Richmond, Kiwira etc etc

    12. #49
      Ufunuo wa Yohana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th October 2007
      Posts : 327
      Rep Power : 658
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Quote By Bongolander
      Mkuu barabara zetu zinajengwa kutokana na matakwa ya kisiasa zaidi kuliko ya kiuchumi. Kama ingekuwa zinajengwa kwa matakwa ya kiuchumi na kuhakikisha hakuna msogamano, siku nyingi hilo tatizo lingekuwa limeondolewa. By the way, kujenga flyover ubungo hakuepukiki, serikali kwa sasa haioni kama hiyo ni priority kwa sababu sasa hivi inabidi wajilinde kwanza na kesi za EPA, Richmond, Kiwira etc etc
      Flyover ubungo si lazima sana kwa sasa ,, maana unaweza jenga flyover wakatipembeni tu barabara ya mtaani in ya vumbi na madimbwi ya kufa mtu. Kuna barabara ya vumbi kutoka Hill park UDSM hadi Kimara baruti inamadibwi si mchezo lakini ni fupi sana hata robo ya project ya flyover haiishi na wakati huo huo utakuwa umesaidia wakazi wa huko.
      Yohana alikuwa ktk roho, akasikia sauti kuu nyuma yake. Naye Yohana aliyoonyeshwa yanadhihirisha Yesu anakaribia. Mwenye masikio na alisikie Neno Roho ayaambia makanisa.

    13. #50
      Cynic's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th January 2009
      Location : Around
      Posts : 2,151
      Rep Power : 967
      Likes Received
      317
      Likes Given
      185

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Juzi juzi hapa nilisoma Kawambwa amezindua mradi wa barabara Dar ili kumaliza tatizo la foleni. Hebu soma Mwananchi Communications Ltd. Sasa sijui ni geresha tu .... kuelekea 2010!
      '... Knowledge is good, but wisdom is even better ...'

    14. SMU
      #51
      SMU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th February 2008
      Location : Mavurunza
      Posts : 4,531
      Rep Power : 3810
      Likes Received
      1311
      Likes Given
      1916

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Tatizo la foleni ni zaidi ya barabara!

      Barabara hazitatosha endapo hakuna jitihada za makusudi kuzuia ongozeko la magari lisilo la lazima katika jiji letu. Jaribu kufikiria ni magari mangapi tuna import na yanaingia barabarani hapa Dar kwa mwaka. Kasi hii ya magari ni kubwa kuliko kasi ya uboreshaji wa barabara zetu.

      Fikiria watu wa familia moja (mtu na mkewe) lakini kila mmoja anakwenda na gari lake kazini! Magari ya kawaida ya binafsi mengi yana uwezo wa kubeba watu watano (5 seaters) lakini ukitizama magari haya nyakati za asubuhi na jioni you hardly see two people in a single car!. Hili ni tatizo la si tu attitude yetu sisi wananchi lakini pia linachangiwa na uduni wa public transport. Kama mnafanya kazi sehemu moja, kuna ubaya gani wa kuchangia usafiri (kwa zamu)?

      Kwa maoni yangu, kama usafiri wa public (daladala or the like) ungeboreshwa, wengi wetu tusingekuwa na haja ya kuja na magari ofisini/kazini na hili lingepunguza foleni kwa kiasi kikubwa. Mradi wa mabasi ya kasi ilikuwa ni idea nzuri lakini sioni kama tupo serious kuutekeleza.

      Kuna mabo menginge ya town planning na distribution ya huduma za kijamii ambayo tumeshakosea na itachukuwa muda mrefu kurekebisha.

      Kwa kuanzia tunaweza;
      - Kuondoa vipanya kama sehemu ya public transport
      - Kuwekwe standard ya mabasi ambayo itakuwa enforced (gari safi, viti safi, konda safi, dereva safi nk nk)
      - Kuboresha miundombinu ya stendi za daladala
      - Kuweka utaratibu wa kuboard kwenye hizi daladala (Kenya wenzetu wanapanga foleni and it works!). Kwa utaratibu uliopo sasa public transport haivutii (angalia pale posta jioni! wale wa mbagala! Mwenge! - huwezi kutamani kupanda daladala kama una pesa ya kununua gari!)
      - Kwa nyakati za asubuhi na jioni, kuwepo na specified lane kwa ajili ya daladala tu. Hii itafanya public transport kuwa convenient zaidi kwa watu zaidi ya private transport.

      Mambo haya yakienda pamoja na uboreshaji wa barabara zilizopo naamini tutafika.

    15. #52
      Ntambaswala's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th December 2008
      Posts : 244
      Rep Power : 581
      Likes Received
      51
      Likes Given
      11

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Nchi yetu ina matatizo kila sekta- afya, barabara, elimu, ujenzi nk. Inahitaji kiongozi ambaye ataweka vipau mbele katika kupunguza au kumaliza hayo yote. Lakini kiongiozi anayejaribu kuguisa kila sehemu hawezi kufanikiwa kwa vile resources ziko kidogo???.

      Mfano JK angewza kusema kipau mbele chake kwa miak 2 ni kuimarisha miundo mbinu ya barabara Dar- mfano kujengwa kiwango cha lami hizo barabara za pembeni. Mfano katika ujenzi wa majengo mjini kule wangesema hakuna kujenga jengo lisilo na parking za juu basi wachahche wangejenga majengo yenye maana kuliko hizi sasa mtu akiwa na 180milioni anawaza kujenga ghorofa kariakoo hakuna maegesho, hakuna nafasi kati ya jengo hadii jengo, hakuna mitaro ni fujo tupu. Tujaribu kiuiga mji wa maputo mbona majengo yao japo maya ni machache lakini yana viwango kuliko ya kwetu

      Wakandarasi wa barabara ni hivyo kabisa viwango ni vya chini sana... sijui itakuwaje hadi mtu unapata ghadhabu

    16. #53
      Mpita Njia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 6,697
      Rep Power : 3254
      Likes Received
      979
      Likes Given
      753

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Quote By Ndege ya Uchumi
      1: Kwani ni Lazima mtu akitoka Kimara kwenda Tegeta lazima apitie Morogoro road + Sam Nujoma
      + Alli Hassan Mwinyi? Na kinyume chake?

      2: Kwani ni Lazima Mtu akitoka Kimara kwenda Ukonga lazima apite Morogoro road + Mandela + Nyerere Road? Na kinyume chake?
      Zipo barabara mbadala lakini nadhani watu wengi hawazitambui. Kwa mfano, kutoka Mbezi beach (Tangi Bovu) kuna barabara nzuri tu inatokea kule Mbezi ya Kimara, lakini hakuna watu wengi wanaoitumia. Zamani ilikuwa mbaya kidogo lakini imekarabatiwa na sasa ipo bomba lakini wengi hawaitumii
      I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.

    17. #54
      Mr II's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th February 2009
      Posts : 30
      Rep Power : 528
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Hongera kwa kukumbusha tatizo hilo sugu. Najaribu fikiria hali itakuwaje baada ya miaka 10 au 20 ijayo. tatizo kubwa nchi hii inaongozwa na viongozi wengi wasio wabunifu. tatizo la Ubungo lilisha zungumziwa hata Bungeni.Na ikashauriwa ijengwe flyover. lakini waziri akasema pesa hakuna. kwa maoni yangu huko ni kukosa uwezo wa kufikiri. ukitaka kujenga nyumba na ukasema pesa huna sasa hutakuja ujenge milele. wewe panga kufanya, halafu panga na namna ya kutafuta pesa. na zitapatikana tu.

      Kuhusu public transport, nadhani tunaendesha mambo kisiasa mno, huo mradi wa mabasi utanza lini?. kila wakati tunaambiwa mwakani!!. Hali ya kugombania mabasi pale Posa, inaiaibisha nchi na jiji la Dar. tembea nchi nyingi utaona kuna utaratibu wa kupanda mabasi, first in first out. Hiyo inahitaji viongozi wajiji waweke utaratibu, wasimamie mwanzoni, watu wakishakuwa wastaarabu hutahitaji kusimamia tena. hata hilo tunahitaji mzungu au mwekezaji aje atuanzishie??.

      Angalia matatizo mengi utagundua tunakosa viongozi wabunifu wa kuanzisha, labda JK akiwambia viongozi wa jiji ndipo watakapo fanya.Vinginevyo wataendelea kukaa ofisini na kuendesha vikao vya kupatia posho tu.

    18. #55
      Mr II's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th February 2009
      Posts : 30
      Rep Power : 528
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Ni kweli resource tunazo kidogo. lakini hata hizo kidogo tunatumiaje. Kama hatuna pesa za kujenga parking, angalau tungekuwa na maeneo yaliyo pangwa kwa lengo hilo. lakini hao viongozi wa jiji inaonekana, wanachojua ni kuuza maeneo yote tu hata open space ambazo tungeweza kuzitumia kwa lengo hilo. tatizo kama la watu kugombania mabasi halihitaji resource nyingi sana. Hilo jiji wanaweza anza hata kesho wakitaka. mji wa Dar hauna mpangilio kabisa. Mimi najiuliza hivi watu huwa wanafanya ziara nchi za watu kutembea au kwa mafunzo.huwa tunajifunza nini?, hatuoni aibu?. Nadhani tunahitaji kuwaamusha hao wahusika bado wamelala.

    19. #56
      Mujuni2's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th June 2008
      Posts : 141
      Rep Power : 586
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Hayo yote mliochangia yalishafanyiwa planning na ujenzi siku nyingi enzi za Magufuli kwa mfano ile barabara inayotoka Tangi Bovu through Goba to Mbezi mwisho ilikuwa iwe kiwango cha lami, then ikifika Mbezi mwisho inakatiza kufuata njia ya ng'ombe (Karibu na mbezi kwa Msuguri) mpaka Vingunguti, so mtu wa Bagamoyo au Mbezi Beach na Tegeta hana haja kupita Mwenge kwenda Airport.

      Tatizo letu ni change of regimes kila regime inakuja na priorities zake, so hakuna longterm plans,labda regime hii priority ni siasa na kiinimacho cha kukomesha ufisadi, kwahiyo wandugu pole msahau kupungua kwa foleni.

      Namuunga mkono anayesema flyover sio suluhisho kwa taarifa tu,Dar hakuna magari mengi kama watu wanavyofikiri, immediate solution ni kukarabati feeder roads ziwe passable.

    20. #57
      Albedo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Posts : 4,978
      Rep Power : 1573
      Likes Received
      1076
      Likes Given
      555

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Quote By Mpita Njia
      Zipo barabara mbadala lakini nadhani watu wengi hawazitambui. Kwa mfano, kutoka Mbezi beach (Tangi Bovu) kuna barabara nzuri tu inatokea kule Mbezi ya Kimara, lakini hakuna watu wengi wanaoitumia. Zamani ilikuwa mbaya kidogo lakini imekarabatiwa na sasa ipo bomba lakini wengi hawaitumii
      Kaka Barabara Mbadala au feeder road zipo lakini haziko katika Kiwango kizuri cha kushawishi watu wapitishe mikoko yao, Nakubaliana na Mchangiaji mmoja aliyesema kwamba dar hakuna Magqri Mengi ya kutisha tatizo letu ni Poor Reasoning, Viongozi wetu kila siku wako Ulaya wanashindwa Kuja na Ubunifu ambao utasaidia kuondoa hili tatizo, angalia miji kama Munich. London na mingine mingi tu ambayo viongozi wetu huwa hawaishi kwenda huko lakini hamna kitu. Why shouldn’t copy their system na kumodify in a way itakayo suit Mazingira yetu.

      Always a complex problem can be solved by a simple solution, Kinachotakiwa hapa ni Serikali pamoja na Manispaa Husika

      1: Kuboresha Feeder Road kwa kiwango cha Lami

      2: Kuboresha public transport ( hili inabidi tuliongelee kwa kina), ifikie mahala hata ma DG waende kazini na Public transport, Muda Fulani nilishangazwa na Project Meneja Kampuni moja yenye kuheshimika hapo London, jamaa alikuwa anapanda Baiskeli yake Mpaka kwenye stesheni ya trein anaipaki then anachukua Train kwenda kazini, nikasema whats so diference between that manager in a developed country with our Leaders. Public transport ikiwa decent watu wengi watakimbilia huko.
      "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM


    21. #58
      Mpita Njia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 6,697
      Rep Power : 3254
      Likes Received
      979
      Likes Given
      753

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      Quote By Ndege ya Uchumi
      Kaka Barabara Mbadala au feeder road zipo lakini haziko katika Kiwango kizuri cha kushawishi watu wapitishe mikoko yao,
      Ni kweli nyingi hazipo katika hali nzuri na zinahitaji kuboreshwa kama ilivyoboreshwa hiyo niliyoitolea mfano ya Tangi Bovu-Mbezi
      I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.

    22. #59
      Mwikimbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2008
      Posts : 1,543
      Rep Power : 948
      Likes Received
      346
      Likes Given
      128

      Default Re: Ubungo kitovu cha foleni, nini kifanyike?

      nilisoma kwenye magazeti kuhusu mradi wa mabasi yaendayo kasi wakitangaza kutafuta makandarai zaidi ya miezi sita iliyopita, sijui bado hawajampata mkandarasi au ndo wanavutana kuhusu 10%, katika tanzania yetu, mtu anaweza kufanya mradi usitekelezeke kama hana uhakika wa kupewa rushwa, nina mifano mingi tu ya pesa zilizotolewa na world bank na japan kwa ajili ya ukarabati wa ofisi za the then regiona engineers, hazikutumika baada ya watekelezaji kushindwa kupata mwanya wa rushwa kwa ajili ya masharti magumu ta taasisi hizi

      kuna mradi wa dar ring road, kimara baruti hadi university of dsm(hill park), mbezi mwisho hadi airport , mbezi mwisho hadi tangi bovu, utagharimu 20bn only huu naona mchakacho wake unaendelea vema.

      kuna mzalendo mmoja, manager wa tanroads aitwae james nyabakari, huyu walim-dump huko rukwa kwa miaka 14, juzi tu ndo akabahatika kuja dsm, huyu mtu ni mbunifu sana, ndo engine ya hiyo mradi hapo juu.

      huyu pia ameipitia mradi wa nelson mandela express way unaojengwa na spencon, malitauro jv, nasikia amepunguza baadhi ya vitu kama taa za barabarani etc, ili aokoe pesa kidogo ajenge angalau fly over pale ubungo na tazara, NINA UHAKIKA HATADUMU HAPO TANROADS KWA KUWA HUWA HANA BEI HANUNULIKI NA WANASIASA, WANAOPENDA AKAE PALE HALAFU AWAPELEKEE PESA JIONI NYUMBANI.

    23. #60
      Shadow's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th May 2008
      Posts : 2,003
      Rep Power : 962
      Likes Received
      147
      Likes Given
      102

      Default Njia Tatu Dar: Kupunguza foleni au Kumtoa Kafara mwananchi?

      Nimekuwa nikiangalia hili suala la njia tatu hapo Dar Es Salaam. Serikali yetu imeshindwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kuboresha miundo mbinu ya jiji letu.

      Inabidi tufanye perfomance appraisal ya hizo njia tatu na kujua kama hizo barabara kuanzishiwa njia tatu kumeleta faida au hasara? kama vifo na uaribifu wa mali ndo umezidi lazima tupige kelele serkali isitishe zoezi hilo la njia tatu.

      My take:

      Kuna haja ya TANROADS kuanza kupimwa kwa kuangalia kwamba kwa nini ajali zinatokea eneo fulani kila mara.Je, ni ubovu wa barabara? Ndiyo, Madereva wanachangia lakini pia TANROADS nao wanachangia na wanawajibika kuakikisha kuwa bara bara ziko katika kiwango cha kisasa na usalama. Tizama bara bara ya Morogoro, imepitwa na wakati na si ya kuwa na njia moja. tunatakiwa tubadilike na kuanzisha barabara kubwa na za kisasa.

      Pili, wizara ya mambo ya ndani ituambie lini itatuondolea trafiki 'vichomi'? Lini tutawekewa kamera kwenye maungio? kudhibiti madereva wakorofi?

    Page 3 of 18 FirstFirst 1234513 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    Similar Topics

    1. Replies: 89
      Last Post: 11th April 2013, 16:57
    2. IBM (Tanzania) kupunguza msongamano wa magari katika Barabara za DSM!
      By Baba_Enock in forum Business & Economic Forum
      Replies: 31
      Last Post: 22nd March 2012, 12:19
    3. Replies: 1
      Last Post: 30th June 2011, 12:35
    4. Replies: 4
      Last Post: 15th June 2011, 18:40
    5. Replies: 47
      Last Post: 21st April 2009, 16:11

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...