GADDAFI NA SIASA ZA MASHARIKI YA KATI
Wiki hii mapambano dhidi ya wanajeshi wanaomuunga mkono hayati Ghaddafi yamefikia ukingoni. Ni baada ya mapambano makali katika mji wa Sirte alikozaliwa Gaddafi.
Mapambano ya kuukomboa mji wa Sirte yalikuwa makali sana na yaliwagharimu wapinzani kwa kiasi kikubwa. Majerhi walikuwa wengi na hakika kasi ya mapambano ilikuwa ni ya kinyonga. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Gaddafi alikuwa anacheza karata yake ya mwisho. Alifahamu wazi kuwa hatima yake ilikuwa imefika ukingoni lakini kama alivyowahi kusema, yeye ni mwanamapinduzi na atafia katika nchi aliyoipenda.
Mtoto wake Saif al Isama( kwa maana ya upanga wa uislam) akiwa katika mahojiano na waandishi wa vyombo vya magharibi alisema kuwa yeye, baba yake na wenzake walikuwa na plan (3). A. To fight and die in Libya B.To fight and die in Libya c;To fight and die in Libya akimaanisha hakukuwa na jingine isipokuwa kufia Libya.
Wiki chache zilizopita ulionekana msafara ukielekea nchi ya Algeria ambayo Gaddafi alikuwa na uswahiba nayo. Hata pale majeshi ya NATO yalipobaini hilo bado hayakuweza kuushambulia. Ilisemekana kuwa Gaddafi alikuwa anakimbia, lakini baadaye ikabainika ni mmoja wa watoto wake.
Inaweza kuwa NATO walitaka Gaddafi aondoke ili mapambano yaishe au kuogopa kauli yao ya kuwa Gaddafi sio 'target'.
Ni msafara ulioonekana Alhamisi ndio ulioshambuliwa na majeshi ya NATO na kumlazimisha Gaddafi kutoka na kukimbilia ndani ya calvet katika jitihada za kujiokoa. Hapo ndipo alipokutana na wapiganaji na akapata kipigo na kupakizwa katika gari la wazi ili apelekwe katika ambulance iliyokuwa mita 500 tu. Haijulikani nini kilitokea na hatima ya Gaddafi ikawa ni mauti.
Mtoto wake aliyekuwa mshauri wa mambo ya ulinzi pia ameonekana katika video akiwa amechoka na chupa ya maji huku akivuta sigara yake. Naye pia haijulikani nini kimetokea ameuawa.
Gaddafi na mwanawe wamewekwa chumba cha baridi na sio kuhifadhi maiti huku mamia wakimshuhudia.
Ikumbukwe kuwa siku ya Jumanne, state secretary bibi Hilal Clinton alikuwa na ziara Tripol. Haijulikani ni ujumbe gani alikwenda kujadiliana na NTC.
Tunapoweka katika mizani na yale ya ushambulizi wa msafara wa Gaddafi tofauti na ule uliokuwa unaelekea Algeria kuna kila shaka Marekani na washirika walijua nini kinatokea Libya hasa kuhusiana na Gaddafi.
Umoja wa mataifa na jumuiya zinazotetea haki za binadamu zimetoa rai ya uchunguzi wa mazingira ya kifo cha Gaddafi.
Inawezekana kabisa kulikuwa na ujumbe mahususi kuwa akikamatwa amalizwe ' take him out of the scene' kama ilivyokuwa kwa Osama.
Hii itapunguza popularity yake na influency kwa waliobaki na uaminifu. Hata hivyo ni mapema mno kujua nini hasa kilitokea ila tunajua kwa uhakika kuwa Gaddafi na mwanawe wameuawa.
Mustakabali wa Libya bado ni tete kwasababu kumeanza minong'ono inayoashiri hamkani kutokuwa sawa. Wapo wanaosema mji mkuu uhamishiwe Benghazi kwasababu ni chimbuko la mapinduzi.
Wapo wanaoona ni dhalili kwa jinsi Rais wao alivyodhalilika mbele ya dunia. Na wapo wanaoungalia ukabila kwa jicho la husda.
Tofauti na Iraq wao wameamua kuwatumia askari na makundi mbali mbali yaliyokuwa chini ya Gaddafi. Hili linaweza kusaidia kuondoa misuguano isiyo ya lazima ingawa si lazima liwe ni suluhisho.
Viongozi wengi wameonyesha kunyong'onyea hasa wa nchi za Africa ambao hakika si kutokana na mashambulio ya NATO bali wanaililia nafsi zao. Wanajua wazi kuwa ipo siku wanaweza kulala sakafuni uchi kama Gaddafi. Wanajua haya ukizingatia kuwa maovu yao mengine ni makubwa kuliko ya Gaddafi. Wanahofu kuwa endapo jeshi la nguvu limeshindwa na nguvu ya umma basi hakuna aliye salama. Kwahiyo ukimya wao si kwa sababu ya masilahi ya nchio zao bali kuzililia nafsi zao.
Mabadiliko yanayotokea katika nchi za kiarabu yanaonekana kutishia nchi nyingi ikiwemo Israel. Waziri mkuu Benjamin Netanyahu anaonekana kuwa mgumu kutafuta suluhu na Wapalestina. Hii ilipelekea Obama kuwataka Waisrael warudi katika meza ya majadiliano katika hotuba yake ambayo alisema ' The time for miltary edge is over, diplomacy is to be complimented by military edge' yaani muda wa nguvu za kijeshi umekwisha, majadiliano yasaidiwe na nguvu za kijeshi.
Jambo baya zaidi ni kuwa nchi za jumuiya ya ulaya na washirika wa mzozo wa Palestine (Quartate) wanaonekana kuchoshwa na dil dal za Israel katika majiadiliano. Ni kwasbabu hizo hata msukumo wa Palestine kutaka kuwa mwananchama wa UN unamsukumo wa aina fulani.
Mabadilishano ya mateka wa kivita kati ya Israel na Palesti katika uwiano wa 1:1000 unaashiria hofu kubwa na umezua mjadala ndani ya Israel.
Wakati hayo yakiendelea Misri imejikita kuwapatanisha Fatah na Hamas kitu ambacho Israel isngependa kitokee.
Ni Misiri hiyo hiyo imefungua mpaka wa Rafah ili misaada iende Gaza kitu kisichokuwa cha kawaida katika utawala wa Mubarak.
Hali ya kisiasa mashariki ya kati ni ya wasi wasi na hakika Mwisrael anaonekana kuwa na hofu zaidi hadi kuondoa masharti ya mazungumzo na kuwataka Waisrael warejee mezani. Israel inapoteza nguvu ya uungwaji mkono kutokana na siasa zake za kiburi zisizozingatia matakwa ya kimataifa. Dola a ulaya inaonekana kuimarika zaidi na kupunguza ushawishi wa marekani, shirika mkubwa Israel.
Swali ni kuwa je kuna anayejifunza kutokana na mageuzi ya mashariki ya kati? (spring revolution)
Nguruvi
Follow Us Here