JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

  Report Post
  Page 1 of 9 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 174
  1. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Katika mijadala mingi inaonyesha, inaonyesha kuwa watanzania wengi wanakubaliana kuwa chanzo cha matatizo ya nchi yetu ni uongozi. Wengine wanasema kuwa ni nchi inaongozwa bila dira. Wengine wanasema kuwa viongozi ni mafisadi. Na wengine wanasema kuwa viongozi sio wacha Mungu.

   Swali langu je tukipata kiongozi mwenye sifa zote hapo juu tutaweza kuondokana na matatizo? Jibu ni 50/50. Tanzania inaweza kupata kiongozi mwenye sifa zote watanzania wanazoziotea ndoto na bado nchi ikaboronga. Sifa zinazotajwa na watanzania wengi sio sifa za kuondoa umasikini na kuboresha maisha ya watanzania wengi. Nasema hivyo kwa sababu kuondoa umasikini na kuboresha maisha kwa nchi masikini kama Tanzania ni Result Oriented Business.

   Nikikutana na maadui zangu wanaopenda siasa za Ujamaa, siku zote wananitolea mifano ya mafanikio ya China. Tofauti kubwa kati ya China na Tanzania ni kuwa wa-China are result oriented and Tanzanians aren't. Miaka kama saba iliyopita China na India walikuwa wanashindana kwenye ujenzi wa reli za kasi kwenda kwenye viwanja vya ndege vilivyopo kwenye wilaya za viwanda (Industrial Districts). Katika kipindi cha chini ya miaka mitatu waChina walimaliza ujenzi. Sijuhi wahindi wamefikia wapi. Ujenzi wa viwanja na Olimpiki na uendeshaji wa michezo hiyo nchini China na Ujenzi wa viwanja vya michezo kwa ajili ya jumuia za madola nchini India ni vitu viwili tofauti.

   Kwa kutumia mifano hii, inaonyesha safari ya China na Tanzania ni tofauti japokuwa nchi hizi mbili ziliwahi kufuata siasa zinazofanana.

   Kuwa mpenda matokeo katika kazi sio siasa. Hivyo kama utajiingiza kwenye mdahalo huu, ningependa mambo ya siasa yakae pembeni. Na jaribu kuelezea uzoefu wako wa kazi au taaluma yako hili tunaweza kubadilisha utamaduni wetu na kuwa watu wa kufanya kazi zenye kuleta matokeo.

   Tunaendelea................... ..........................
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

  2. Gaijin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2007
   Posts : 11,898
   Rep Power : 25013
   Likes Received
   5104
   Likes Given
   2566

   Default

   Watanzania tuna tabia ya mazowea na kuona muhali. Na tabia hizo zinakwamisha maendeleo

   Nchi inatoa tenda kwa mkandarasi, tunajengewa daraja au barabara iliyo chini ya viwango au yenye dosari ndogo ndogo kadhaa, lakini tunaona muhali kumlazimisha mkandarasi kurekebisha kwanza.

   Tabia hiyo imeanzia chini kwa raia mmoja mmoja, kamwe hatujazowea kudai marekebisho au kukataa huduma isiyofikia viwango. Si migahawani, madukani, wala maofisini

   Hakuna maendeleo kama hatutaweka nadhari kwenye details. Mambo madogo madogo huzaa makubwa

  3. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania Is a Result Oriented Business -

   Quote By Gaijin View Post

   Gaijin,

   Haya matatizo yanatokea sehemu mbalimbali. Hili kupunguza matatizo kama haya wenzetu wanazo quality assurance methodologies. Na Tanzania inapoteza sehemu kubwa ya mapato yake katika masuala ya quality. Mtu anakwenda kukodisha ndege itakayotumika kibiashara na shirika la ndege anachukua ndege ambazo hazina quality yoyote.

   Vilevile suala hili lipo kwenye mikataba ya kisheria. Ni lazima tujenge utamaduni wa kuweka mikataba mizuri ya kisheria. Na lazima tufuatilie mikataba hiyo. Kwa mfano, serikali ilipotoa tenda kwa Richmond, basi pale Richmond iliposhindwa kutimiza wajibu wake, ilitakiwa Richmond ianze kuilipa serikali kwa kuchelewesha mkataba. Lakini inavyooneka Richmond ni mshindi.

   Ni Result Oriented individuals wanaoweza kufuatilia quality assuarance na mikataba ya kisheria.
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

  4. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 16,573
   Rep Power : 124739545
   Likes Received
   8258
   Likes Given
   8156

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania Is a Result Oriented Business -

   Zakumi,
   Mkuu wangu mbona majibu unayo.. Ikiwa tumepoteza DIRA, hiyo result oriented itatoka wapi?.. au ndio ulitaka kusema hivyo.
   Exploration of reality

  5. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania Is a Result Oriented Business -

   Quote By Mkandara View Post
   Zakumi,
   Mkuu wangu mbona majibu unayo.. Ikiwa tumepoteza DIRA, hiyo result oriented itatoka wapi?.. au ndio ulitaka kusema hivyo.
   Matatizo ya kutokuwa na matokeo au kifikia matokeo yanaanza na mapungufu ya dira. Ukipanga dira ambayo haiwezekani na haieleweki, ni wazi kuwa watendaji watapoteza dira hiyo.

   Hivyo inawezekana kupotea kwa dira yetu imetokana na dira yenyewe kutokuwa realistic. Hivyo hili watanzania waweze kufanikiwa ni lazima wajue kupanga vitu vinavyowezekana. Na hili ni moja ya matatizo letu.
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

  6. jmushi1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2007
   Posts : 16,111
   Rep Power : 32245502
   Likes Received
   5418
   Likes Given
   6437

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By Gaijin View Post
   Tabia hiyo imeanzia chini kwa raia mmoja mmoja, kamwe hatujazowea kudai marekebisho au kukataa huduma isiyofikia viwango. Si migahawani, madukani, wala maofisini
   Watasema wewe si mpole, sifa kuu ya utanzania.

   Ukiuliza haki yako bongo utaitwa mkorofi.

   Hata humu ndani same thing, watu wanataka uwe mpole.

   Nilipotembelea bongo nilikasirika karibia kila ofisi ya huduma niliyotembelea, na kama humjui mtu pahali ndo mbaya zaidi, labda uwe na pesa ya kuhonga, hayo ni maisha ya kawaida ya mbongo.
   "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

  7. AshaDii's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 16th April 2011
   Location : Changeable
   Posts : 16,196
   Rep Power : 33249117
   Likes Received
   17614
   Likes Given
   18766

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Zakumi nionavo mimi ni kuwa kuna tatizo kubwa sana katika jamii ya wananchi wa Tanzania; achilia mbali matatizo ya uongozi. Wananchi tumekua na kasumba ya kuamini kua Maendeleo ya nchi hii yetu changa yataletwa na Uongozi wa Inchi, kwamba raisi akiwa na qualities zote za Uzalendo baaas!

   Tunasahau kua Yule kiongozi ana delegate tu, tukisahau kua kila mwananchi ana nafasi yake katika kutaka boresha maisha na maendeleo ya inchini kwake, tukisahau kua ni mwananchi wa kawaida kabisa anae changia kuporomoka na kurudi nyuma kwa maendeleo ya wananchi.

   Ma Boss wa taasisi mbali mbali za serkali, Wakubwa wa Mali za Umma, na Viongozi hadi wa chini kwa kiwango kikubwa wanafanya kazi chini ya maadili….

   Kila mmoja ni mbinafsi, Kila mmoja hana uzalendo na wala hana Uchungu na mali ile ambayo anasimamia…. Kukomboka kwa inchi.

   Na the Irony ni kua hao hao wanachi wanaofanya kazi kinyume cha maadili na kujilimbikizia pesa ambazo sio zao wanazipata kwa Magendo wapo so MAD at leaders such as akina BWM na EL.

   Mwalimu katika hotuba yake (Ilikua Mbeya if not mistaken) alim quote Marehemu Rais wa Marekani J. F. Kennedy…. “Usiulize Inchi yako itakufanyia nini, Jiulize wewe Utaifanyia nini Inchi yako”. (This quote is applicable to the issue umewakilisha hapa)
   “Never get angry. Never make a threat. Reason with people.”
   - Mario Puzo (The God Father)

  8. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By jmushi1 View Post
   Watasema wewe si mpole, sifa kuu ya utanzania.

   Ukiuliza haki yako bongo utaitwa mkorofi.

   Hata humu ndani same thing, watu wanataka uwe mpole.

   Nilipotembelea bongo nilikasirika karibia kila ofisi ya huduma niliyotembelea, na kama humjui mtu pahali ndo mbaya zaidi, labda uwe na pesa ya kuhonga, hayo ni maisha ya kawaida ya mbongo.
   JMushi,

   Wakati serikali imetwaa mashamba ya mkonge kutoka kwa watu binafsi, ilifuata utaratibu wa manamba ambao mtu alikuwa analipwa kutokana na performance yake kazi.

   Na badala yake watu wakawa wanalipwa kutokana na masaa ya kazi. Matokeo yake hata wale wafanya kazi mahodari wakawa wavivu.

   Na sasa hivi watanzania wengi wamezoea kufanya kazi kwa masaa manane na kurudi nyumbani. Labda tuanze kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa perfomance.
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

  9. Gaijin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2007
   Posts : 11,898
   Rep Power : 25013
   Likes Received
   5104
   Likes Given
   2566

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Hatuwezi kuondokana na umaskini kama hatujui kujieleza. Kama hatujui kujieleza hatuwezi kupata tunachotaka. Hili linaanzia kwenye mtu mmoja mmoja na hatimae serikalini.

   Angalia hapa JamiiForums panapoitwa Home of Great Thinkers kwa mfano, watu hatujui kujieleza na kinachoshangaza zaidi si kuwa mtu hawezi kujieleza tu, lakini hata kuandika Kiswahili hajui na haoni tabu kuwa hajui. Lakini mtu huyo huyo anaona aibu akichapia neno la Kiingereza

   Tumeona mifano mingi ya viongozi au wanajamii wakihojiwa kwa Kiswahili na kudumbukiza maneno ya Kiingereza na bila ya aibu kumuomba mtangazaji awa tafsirie kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili lakini hawa hawa hawawezi kamwe kuomba watafsiriwe neno la Kiswahili kwenda kwenye Kiingreza wanapohojiwa kwa Kiingereza.
   Maendeleo hayaji bila ya kujikomboa ki-fikra na hajaji bila ya sisi kuweza kuwasiliana vizuri na kuweza kujieleza

  10. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Uchambuzi wa dira.

   Kwa watanzania wengi walioishi kipindi cha uongozi wa JKN, wana kiu kikubwa cha kuwa na dira. Kwa maoni yangu binafsi, suala la dira ni lazima liangaliwe kiundani. Kwani dira zina matatizo yake.

   Moja ya matatizo ya dira ni u-fanatic. Nchi inaweza kuanzisha dira na kuamini kuwa mpinzani wa dira ni adui wa nchi. Na matokeo yake nchi ikawa inapoteza rasimali nyingi kuilinda dira kuliko kuboresha maisha ya wananchi.

   Kwa mfano,tulipokuwa na Ujamaa, kila mtu aliyekosoa Ujamaa alionekana kama adui. Na kuilinda nadharia hiyo kukawa na vyuo vya itikadi ya chama karibu kila mkoa. Na vilevile mafunzo ya kijeshi yakaendelezwa kila kona, mgambo, JKT, JWTZ, Police, Magereza, Usalama wa taifa n.k.

   Mpaka sasa nchi kama North Korea au Iran zinaendeleza kung'ang'ania dira na kutumia sehemu kubwa ya mapato ya nchi kuilinda itikadi na sio kuboresha maisha ya wananchi.

   Nchi inaweza kuendelea bila kuwa na dira yoyote hili iwapo serikali itakuwa na sera za kutatua na kuelezea matatizo ya wananchi. Na hili hizo sera ziwe na mafanikio ni lazima ziwe na sifa zake. Kwanza ziwe zinatumika katika kipindi cha muda fulani. Pili ziwe zinategemea rasilimali za nchi. Tatu ziwe zinaweza kufanyika. Nne zishilikishe kwa namna fulani wananchi.
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

  11. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By AshaDii View Post
   Zakumi nionavo mimi ni kuwa kuna tatizo kubwa sana katika jamii ya wananchi wa Tanzania; achilia mbali matatizo ya uongozi. Wananchi tumekua na kasumba ya kuamini kua Maendeleo ya nchi hii yetu changa yataletwa na Uongozi wa Inchi, kwamba raisi akiwa na qualities zote za Uzalendo baaas!

   Tunasahau kua Yule kiongozi ana delegate tu, tukisahau kua kila mwananchi ana nafasi yake katika kutaka boresha maisha na maendeleo ya inchini kwake, tukisahau kua ni mwananchi wa kawaida kabisa anae changia kuporomoka na kurudi nyuma kwa maendeleo ya wananchi.

   Ma Boss wa taasisi mbali mbali za serkali, Wakubwa wa Mali za Umma, na Viongozi hadi wa chini kwa kiwango kikubwa wanafanya kazi chini ya maadili….

   Kila mmoja ni mbinafsi, Kila mmoja hana uzalendo na wala hana Uchungu na mali ile ambayo anasimamia…. Kukomboka kwa inchi.

   Na the Irony ni kua hao hao wanachi wanaofanya kazi kinyume cha maadili na kujilimbikizia pesa ambazo sio zao wanazipata kwa Magendo wapo so MAD at leaders such as akina BWM na EL.

   Mwalimu katika hotuba yake (Ilikua Mbeya if not mistaken) alim quote Marehemu Rais wa Marekani J. F. Kennedy…. “Usiulize Inchi yako itakufanyia nini, Jiulize wewe Utaifanyia nini Inchi yako”. (This quote is applicable to the issue umewakilisha hapa)
   AshaDii,

   Unalosema lina ukweli mkubwa sana. Lakini miaka ya 70 watanzania walifanya vitu vingi bila kutegemea sana serikali. Walijenga mashule ya msingi kwa nguvu za wananchi. Kwa sisi tulio kaa Mwanza, kiwanja cha Kirumba na sekondari za wakulima ni ushahidi wa kutosha.

   Tatizo linalokuja ni kuwa, viongozi wa Tanzania hawajuhi ku-manage expectations za kazi za kujitolea. Na hii imekatisha tamaa sana. Unapowajengesha watu shule, wanategemea watoto wao wafanye vizuri. Waendelee na masomo au kupata ujuzi wa kuwasaidia.

   Kuna nchi zimeanza kutoa MBA za jinsi ya kuendesha mashirika ya kujitolea (NGO) Nadhani umefika kwa viongozi wa Tanzania nao kuanza kujifunza kuwa hili watu waendelee kujitolea na kutoitegemea sana serikali kuna vitu muhimu vya kuangalia.
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

  12. AshaDii's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 16th April 2011
   Location : Changeable
   Posts : 16,196
   Rep Power : 33249117
   Likes Received
   17614
   Likes Given
   18766

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Na hapa ndio hapo unapoona kua kazi ipo! Kila mwananchi anaona lile ambalo yeye anajua na kutambua ama kusimamia ndio Msingi na guideline ya wote kufuata.

   Kwamba sababu haamini kuwa Kiongozi wake kuonesha kua ni true Leader lazima awe na traits Fulani tu ila zikiwa nje ya hapo ni batili; hata kama huyo kiongozi ni mzuri na afanya kazi yake vizuri... Unabaki washangaa hivi kabla ya kulalama umeangalia content? Umeangalia kazi zake? Au sababu tu ni Kiongozi na ni wa kundi Fulani baaas that is enough kumjudge kua yeye ni magamba; basi yeye ni fisadi.

   Siku zinavozidi kuenda ndio tanavozidi jichanganya na dunia katika mambo mbali mbali…. Na kutumika kwa lugha ngeni is un avoidable Period! For instance…. Kimsingi hapa as a Home of Great thinkers yenye members mbali mbali toka walo verified members, Politicians, Scholars, wanaharakati na the like…. ni mahala ambapo kama Forum kubwa hapa inchini ikiwa na watu wa kila aina na hasa wasomi; things like alternative use of the Language is unavoidable…..

   Kwamba it should be the basis of defining one’s capability and capacity of thinking and output towards the nation and its people? Labda kwa mtafsiri ndio aweza onekana tatizo….. Uzuri ni depending on one’s perspective. Na sababu kila mmoja hutaka perspective yake ndio ionekane bora bila kuangalia walo mzunguka iko vipi…. Inakuwa mashindano hivo in one way or another kila mmoja kucheza nafasi ya kusimamisha shughuli kuweza songa mbele ambayo yaweza kua maslahi ya taifa; Kiasi kwamba makundi yote mawili yasipokua makini at the end of the day wote ni boguses....
   “Never get angry. Never make a threat. Reason with people.”
   - Mario Puzo (The God Father)

  13. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By Gaijin View Post
   Hatuwezi kuondokana na umaskini kama hatujui kujieleza. Kama hatujui kujieleza hatuwezi kupata tunachotaka. Hili linaanzia kwenye mtu mmoja mmoja na hatimae serikalini.

   Angalia hapa JamiiForums panapoitwa Home of Great Thinkers kwa mfano, watu hatujui kujieleza na kinachoshangaza zaidi si kuwa mtu hawezi kujieleza tu, lakini hata kuandika Kiswahili hajui na haoni tabu kuwa hajui. Lakini mtu huyo huyo anaona aibu akichapia neno la Kiingereza

   Tumeona mifano mingi ya viongozi au wanajamii wakihojiwa kwa Kiswahili na kudumbukiza maneno ya Kiingereza na bila ya aibu kumuomba mtangazaji awa tafsirie kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili lakini hawa hawa hawawezi kamwe kuomba watafsiriwe neno la Kiswahili kwenda kwenye Kiingreza wanapohojiwa kwa Kiingereza.

   Maendeleo hayaji bila ya kujikomboa ki-fikra na hajaji bila ya sisi kuweza kuwasiliana vizuri na kuweza kujieleza
   Gaijin,

   Kwa kuongezea tu. Kuna kasumba zimeanza kwa miaka mingi. Nilipokuwa mwanafunzi Tanzania, tuliamini kuwa kuna watu wenye necha (nature) ambao wao watapata A bila hata kusoma.

   Kwenye mashule niliyopitia nikiwa Ulaya na Marekani nawaona wale wenye vipaji vya kuzaliwa ndio wanaotumia muda mwingi kuboresha fani zao. Nadhani umefika wakati tuache sifa za kuwa na akili za kuzaliwa na tuanze kutumia muda kujiendeleza.

   Tukiondoa hii kasumba na kujaribu kuboresha vipaji vyetu vya lugha na mambo mengine tunaweza kufanya mabadiliko.
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?

  14. Gaijin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2007
   Posts : 11,898
   Rep Power : 25013
   Likes Received
   5104
   Likes Given
   2566

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By AshaDii View Post

   Siku zinavozidi kuenda ndio tanavozidi jichanganya na dunia katika mambo mbali mbali…. Na kutumika kwa lugha ngeni is un avoidable Period! For instance…. Kimsingi hapa as a Home of Great thinkers yenye members mbali mbali toka walo verified members, Politicians, Scholars, wanaharakati na the like…. ni mahala ambapo kama Forum kubwa hapa inchini ikiwa na watu wa kila aina na hasa wasomi; things like alternative use of the Language is unavoidable….....
   Hapa tunarudi kule kule kwenye sisi Watanzania kukosa umakini kwenye vitu vidogo vidogo na hivyo kushindwa kwenye mambo makubwa yanayoundwa na madogo.

   Hakuna tatizo kwa watu kutumia lugha mbadala wakati wa kujieleza, au hata kuchanganya lugha kwa kuazima maneno ya lugha ya kigeni wakati wa kuzungumza Kiswahili. Kinachogomba hapa ni ile watu hususan Great Thinkers au ‘wasomi’ kutoweza kuandika Kiswahili cha msingi tu lakini kuweza kuandika lugha ya kigeni, na kuona hilo ni jambo la kawaida.

   Tuchukulie sentensi hii moja kwa mfano. Bila ya kusahihishana kanuni za uandishi tunaona kuwa kuna tatizo la uelewa wa lugha ya Kiswahili

   Tunasahau kua Yule kiongozi ana delegate tu, tukisahau kua kila mwananchi ana nafasi yake katika kutaka boresha maisha na maendeleo ya inchini kwake, tukisahau kua ni mwananchi wa kawaida kabisa anae changia kuporomoka na kurudi nyuma kwa maendeleo ya wananchi.
   Suala la wananchi hususan ‘wasomi’ kushindwa kuandika Kiswahili si suala dogo, na linaturudisha kwenye mtaala wa elimu yetu na ile tabia Zakumi aloitaja ya kujilemaza kwa kusingizia necha [nature]; ati kwa vile wewe ni Mtanzania basi unajua Kiswahili na hutakiwi kujifunza zaidi. Tupo radhi kujua kuyaandika maneno mazito ya lugha ya kigeni lakini hatujui kuandika maneno yanayotumika kila siku katika lugha ya Kiswahili

   China (yenye herufi zipatazo 10,000 ambapo takriban 4,000 hutumika kwenye matumizi ya kawaida) baada ya kuona kuna wastani wa makosa 46 kwa kila nakala ya gazeti inayochapwa, ilihitimisha kuwa kuna tatizo katika mfumo wa elimu.

   Sawa, tutasema hapa Jamiiforums hakuna mhariri wa kurekebisha makosa ya waandishi, lakini nadhani hapa hasa ndipo panapoweza kutupa mwanga wa kiasi gani wananchi ikiwa ni pamoja na kundi la wasomi, wanaelewa Kiswahili.

   Tunatabia ya kuridhika mno na tulivyo, tukipatacho, na tuhudumiwavyo. Na hii si sifa ya wataka maendeleo
   Last edited by Gaijin; 31st March 2012 at 09:46.

  15. jmushi1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2007
   Posts : 16,111
   Rep Power : 32245502
   Likes Received
   5418
   Likes Given
   6437

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By Zakumi View Post
   JMushi,

   Wakati serikali imetwaa mashamba ya mkonge kutoka kwa watu binafsi, ilifuata utaratibu wa manamba ambao mtu alikuwa analipwa kutokana na performance yake kazi.

   Na badala yake watu wakawa wanalipwa kutokana na masaa ya kazi. Matokeo yake hata wale wafanya kazi mahodari wakawa wavivu.

   Na sasa hivi watanzania wengi wamezoea kufanya kazi kwa masaa manane na kurudi nyumbani. Labda tuanze kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa perfomance.
   Ndo maana kuna bonuses base on performances etc

   Hiyo ya manamba ilikuwa ya kiuonevu zaidi.Ndo maana wenzetu wameweka minimum pay.Pamoja na incentives ambazo ni based on performance.
   "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

  16. AshaDii's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 16th April 2011
   Location : Changeable
   Posts : 16,196
   Rep Power : 33249117
   Likes Received
   17614
   Likes Given
   18766

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By Gaijin View Post
   Hapa tunarudi kule kule kwenye sisi Watanzania kukosa umakini kwenye vitu vidogo vidogo na hivyo kushindwa kwenye mambo makubwa yanayoundwa na madogo.
   In other words una maana kua Viongozi na Watanzania walo wengi wanashindwa kuwajibika ama kua wazalendo sababu ya kuelewa vizuri lugha ya Kiswahili? Gaijin are you serious?

   Quote By Gaijin View Post
   Hakuna tatizo kwa watu kutumia lugha mbadala wakati wa kujieleza, au hata kuchanganya lugha kwa kuazima maneno ya lugha ya kigeni wakati wa kuzungumza Kiswahili. Kinachogomba hapa ni ile watu hususan Great Thinkers au ‘wasomi’ kutoweza kuandika Kiswahili cha msingi tu lakini kuweza kuandika lugha ya kigeni, na kuona hilo ni jambo la kawaida.
   Well nakubaliana na wewe kua ndio wapo wasomi ambao hawawezi kuandika Kiswahili cha msingi na kuweza kuandika lugha ya kigeni; thou bado sijaona kama ndio ipo responsible kwa wao kushindwa fanya kazi zao kwa umakini. Kwamba wasomi/viongozi wanashindwa kusoma maneno mazito ya Kiswahili ni tatizo moja wapo; kwamba huo ujumbe unakua so disoriented kiasi kwamba the person in question inamfanya ashindwe kua capable? Kumbuka kua kuna maneno ambayo ni ya lugha za kigeni lakini majority ya hao hao Watanzania wanajua maana ya maneno yalo mengi ambayo huchanganyiwa na ukilitumia watakuelewa tu. Nitolee mfano mdogo hapa chini ni wazi hata wewe ambae wapenda ujitahidi sana kuandika katika lugha moja kuna wakati wajikuta umechanganya na lugha ngeni. Kama solution nikuliandika hilo neno lisomeke Kiswahili hali ni lugha ngeni swala lipo pale pale.

   Quote By Gaijin View Post
   Suala la wananchi hususan ‘wasomi’ kushindwa kuandika Kiswahili si suala dogo, na linaturudisha kwenye mtaala wa elimu yetu na ile tabia Zakumi aloitaja ya kujilemaza kwa kusingizia necha [nature]; ati kwa vile wewe ni Mtanzania basi unajua Kiswahili na hutakiwi kujifunza zaidi. Tupo radhi kujua kuyaandika maneno mazito ya lugha ya kigeni lakini hatujui kuandika maneno yanayotumika kila siku katika lugha ya Kiswahili
   Quote By Gaijin View Post
   Tunatabia ya kuridhika mno na tulivyo, tukipatacho, na tuhudumiwavyo. Na hii si sifa ya wataka maendeleo
   The above quotation una support my first post... Kwamba tulowengi kutegemea kufanyiwa kila kitu tukitegemea maendeleo... Which is quiet cumbersome.....
   “Never get angry. Never make a threat. Reason with people.”
   - Mario Puzo (The God Father)

  17. Gaijin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2007
   Posts : 11,898
   Rep Power : 25013
   Likes Received
   5104
   Likes Given
   2566

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By AshaDii View Post
   In other words una maana kua Viongozi na Watanzania walo wengi wanashindwa kuwajibika ama kua wazalendo sababu ya kuelewa vizuri lugha ya Kiswahili? Gaijin are you serious?

   Nisome vizuri na unielewe, hakuna hata sehemu moja niliyosema kuwa viongozi wanashindwa kuwa wazalendo au kuwajibika kwa sababu hawaelewi lugha ya Kiswahili. Sijui hata umefikiaje hitimisho hilo kutoka kwenye maandiko yangu.

   Well nakubaliana na wewe kua ndio wapo wasomi ambao hawawezi kuandika Kiswahili cha msingi na kuweza kuandika lugha ya kigeni; thou bado sijaona kama ndio ipo responsible kwa wao kushindwa fanya kazi zao kwa umakini.
   Sijui hili la kudhani Gaijin anasema mtu kutokuelewa Kiswahili sanifu kunamfanya ashindwe kufanya kazi yake kwa umakini linatokea wapi. Mada husika hapa ni namna ya kuondoa umaskini na kuleta maendeleo Tanzania na sio uzalendo au hata viongozi.

   Mimi nimeamua kuangalia tatizo kwenye ngazi ya chini. Kuwa Watanzania [sijazungumzia viongozi pekee] tuna tatizo la kutokujua kujieleza na hilo ni moja ya vinavyotukwamisha kupata maendeleo, kwa sababu usipojua kujieleza huwezi kupatiwa huduma stahiki unayoihitaji. Pia usipojua kujieleza huwezi kuwapatia wengine huduma stahiki na badala yake unaweza hata kuwapotosha na kupelekea kuibuka kwa matatizo mengine

   Kwa mujibu wa sensa ya taifa ya mwaka 2007, asilimia 22.3 tu ya wakazi wa Dar es Salaam [asilimia 9.7 kwa Tanzania nzima] ndio wanaoweza kuelewa lugha zote mbili za Kiswahili na Kiingereza [na hapa hatujui wanaelewa kwa kiwango gani]

   Wataalamu na wasomi wetu wanaposhindwa kujieleza kwa kutumia Kiswahili, inamaanisha kuwa wanashindwa kuwahudumia wananchi wanaowategemea.

   Na kama watu wanafika kuwa "wasomi" lakini hawawezi kuandika Kiswahili cha msingi tu, basi kuna tatizo kubwa kwenye mitaala yetu pamoja na fikira zetu, kwani mbali na mitaala hakuna sababu ya "msomi" kushindwa kujieleza kwa Kiswahili sanifu.

   Nitolee mfano mdogo hapa chini ni wazi hata wewe ambae wapenda ujitahidi sana kuandika katika lugha moja kuna wakati wajikuta umechanganya na lugha ngeni. Kama solution nikuliandika hilo neno lisomeke Kiswahili hali ni lugha ngeni swala lipo pale pale.
   Kwanza tuelewane kuwa sijakataza mtu kuazima maneno ya kigeni na kuyatumia anapojieleza kwa Kiswahili. Niliandika wazi kuwa jambo hilo haligombi

   Pili tuelewane pia kuwa mimi Gaijin si kipimo cha chochote kwenye jamvi hili, wala si wewe wala mwengine mwenye kujua kuwa Gaijin anajitahidi sana kuandika kwa lugha moja tu. Huwezi kujua kama anajitahidi tu seuze anajitahidi sana. Huwezi kujua chochote kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa jitihada wakati Gaijin anapoandika hapa jamvini

   Mbali ya hayo, mfano ulioutumia wa kumkosoa Gaijin si sahihi kwa sababu yeye alieleza kuwa ananukuu maneno ya Zakumi   Mjadala huu pia umedhihirisha jambo jengine ambalo linatufanya Watanzania tuendelee kuwa maskini. Watanzania hatutaki kujirekebisha hata pale tunapokuwa wazi tumekosea na kukosolewa.

   Tukitaka maendeleo kama taifa lazima tujenge jamii ambayo ipo tayari kukubali makosa na kujirekebisha ili tusonge mbele.
   Last edited by Gaijin; 31st March 2012 at 12:52.

  18. AshaDii's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 16th April 2011
   Location : Changeable
   Posts : 16,196
   Rep Power : 33249117
   Likes Received
   17614
   Likes Given
   18766

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By Gaijin View Post
   Nisome vizuri na unielewe, hakuna hata sehemu moja niliyosema kuwa viongozi wanashindwa kuwa wazalendo au kuwajibika kwa sababu hawaelewi lugha ya Kiswahili. Sijui hata umefikiaje hitimisho hilo kutoka kwenye maandiko yangu.
   Naona nawe umeona hilo... (kwamba mjadala wahusu nini); Gaijin what I post I mean, hivo nakua nimekusoama na nimekuelewa..... BTW nipo discussion na wewe hivo naku address as Gaijin in that sense…. Nimekusoma kuhusu kurekebisha maandishi. Well naelewa kua (kua ni kuwa); tumetofautiana tabia katika uandishi unapokua unaandika when discussing na unapoandika Kazi ambayo inatakiwa ni Print na iende mahala. The way I write hapa katika forums discussions is more influenced as a result of the fact kua when I type hapa, I am speakin to myself... hivo mara nyingi saana ukitaka kunisaidia kutaka rekbisha niandikavo then kweli kabisa hutokosa makosa kwangu (makosa ambayo hata mimi nikiamua kupitia upya, nitayatambua nikitaka uandishi fanisi). Hata hivo sikukatishi tamaa; Ukifanya hio campaign hapa JF yaweza tusaidia sana maana kuna wengine hupost hapa as if they are sending a text message…. Hua inaboa (but yet again ukute it is the same with you na unandishi ulo below standards wa Kiswahili).

   Quote By Gaijin View Post
   Sijui hili la kudhani Gaijin anasema mtu kutokuelewa Kiswahili sanifu kunamfanya ashindwe kufanya kazi yake kwa umakini linatokea wapi. Mada husika hapa ni namna ya kuondoa umaskini na kuleta maendeleo Tanzania na sio uzalendo au hata viongozi.
   Hapo sasa na mimi ndipo niikua nimekushangaa na kushindwa kukuelewa…. Kua utumiaji wa Lugha ngeni na topic ya Zakumu wapi na wapi? Kwamba ndio mfano uliokua perfect kuelezea jinsi mambo madogo madogo yaweza fanya makubwa yashindwe kufanyika? Hence tumefika huku…. You can scrap the matter; or go on with it in case hujapata hufafanuzi vema.

   Quote By Gaijin View Post
   Mimi nimeamua kuangalia tatizo kwenye ngazi ya chini. Kuwa Watanzania [sijazungumzia viongozi pekee] tuna tatizo la kutokujua kujieleza na hilo ni moja ya vinavyotukwamisha kupata maendeleo, kwa sababu usipojua kujieleza huwezi kupatiwa huduma stahiki unayoihitaji. Pia usipojua kujieleza huwezi kuwapatia wengine huduma stahiki na badala yake unaweza hata kuwapotosha na kupelekea kuibuka kwa matatizo mengine.
   Hapa tupo pamoja.... Naomba nisome na mimi unielewe pia (hasa my first post in the thread); Nakubali tatizo sio viongozi pekee... tatito lipo hata kwa wananchi pia....

   Quote By Gaijin View Post
   Wataalamu na wasomi wetu wanaposhindwa kujieleza kwa kutumia Kiswahili, inamaanisha kuwa wanashindwa kuwahudumia wananchi wanaowategemea.
   Hivi unaweza nipa mfano wa Kiongozi ambae anashindwa kufanya kazi yake kwa Ufanisi sababu tu hawezi kujieleza kwa Kiswahili? Alafu BTW hivi tuna Kiongozi wa ngazi ya juu (hata ya kati) ambae hajui kutumia Kiswahili to the extent wananchi wasimuelewe?

   Quote By Gaijin View Post
   Pili tuelewane pia kuwa mimi Gaijin si kipimo cha chochote kwenye jamvi hili, wala si wewe wala mwengine mwenye kujua kuwa Gaijin anajitahidi sana kuandika kwa lugha moja tu. Huwezi kujua kama anajitahidi tu seuze anajitahidi sana. Huwezi kujua chochote kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa jitihada wakati Gaijin anapoandika hapa jamvini
   Ofcourse Gaijin wewe sio kipimo cha vitu vyote… Na hakuna alo kipimo cha vitu vyoote mbona yaweza kua kero ikiwa hivo. Ndio maana nikagusia kila mmoja ana beliefs zake… Na kila mmoja hutaka beliefs zake ziuze ama kuonekana za maana kulizo za wengine. Kana kwamba yeye aweza kua rite all the time na hawezi kosea….. Swala ambalo linachangia sana kurudisha taifa nyuma hasa inapokua Ki/Viongozi wana outlook hio…. Kuhusu jitihada za Gaijin nje ya jamvi I am not interested.... Hayanihusu, lakin as my fellow member na hapa we are discussing I would be reall stupid kuchukulia everything on the surface bila kujaibu kukuelewa. Kama hivi nime point out, I maybe wrong tokana na mtazamo wako... napata jibu. In the future najua what to avoid tukijaaliwa kukutana tena....

   Quote By Gaijin View Post
   Mbali ya hayo, mfano ulioutumia wa kumkosoa Gaijin si sahihi kwa sababu yeye alieleza kuwa ananukuu maneno ya Zakumi .
   Hapa basi Gaijin inabidi ajifunze quotations... pale hukumnukuu Zakumi, ila ulizungumzia alilo comment… else kama hujui taratibu za kunukuu zipo vipi then nitakuelewa. Ungekua umetumia hizo taratibu amini ningejua hauna haja ya kukusahihisha maana umenukuu tu.

   Quote By Gaijin View Post
   Tukitaka maendeleo kama taifa lazima tujenge jamii ambayo ipo tayari kukubali makosa na kujirekebisha ili tusonge mbele.
   Thanks Gaijin.... Haya maneno yako yanaungana na Signature yangu…. “The Critiques are our friends, they tell us our Faults” hivo pamoja saana.
   “Never get angry. Never make a threat. Reason with people.”
   - Mario Puzo (The God Father)

  19. Gaijin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2007
   Posts : 11,898
   Rep Power : 25013
   Likes Received
   5104
   Likes Given
   2566

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By AshaDii View Post
   Gaijin what I post I mean, hivo nakua nimekusoama na nimekuelewa.....

   Hapo sasa na mimi ndipo niikua nimekushangaa na kushindwa kukuelewa….
   Matatizo yale yale ya Mtanzania. Hueleweki! Umenisoma na kunielewa au umeshindwa kunielewa?!

   Gaijin
   Pili tuelewane pia kuwa mimi Gaijin si kipimo cha chochote kwenye jamvi hili, wala si wewe wala mwengine mwenye kujua kuwa Gaijin anajitahidi sana kuandika kwa lugha moja tu. Huwezi kujua kama anajitahidi tu seuze anajitahidi sana. Huwezi kujua chochote kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa jitihada wakati Gaijin anapoandika hapa jamvini
   Ashadii
   Ofcourse Gaijin wewe sio kipimo cha vitu vyote… Na hakuna alo kipimo cha vitu vyoote mbona yaweza kua kero ikiwa hivo.

   Kuhusu jitihada za Gaijin nje ya jamvi I am not interested....
   Ama hukunisoma na kuelewa au hujui tofauti baina ya "vitu vyote" na "chochote"

   Hakuna anaezungumzia jitihada za Gaijin nje ya jamvi. Kwa ufupi nilichokieleza ni kwamba huwezi kujua kama Gaijin anachukua jitihada sana au kidogo, au haweki jitihada hata chembe anapoandika kwa kutumia lugha moja.
   Hakuna mwanachama humu Jamiiforums anaeweza kujua jitihada ya mwanachama mwengine wakati wa kuandika hapa jamvini. Tuache kuwatolea hukumu na mahitimisho wanachama tusiowajua.

   Hivi unaweza nipa mfano wa Kiongozi ambae anashindwa kufanya kazi yake kwa Ufanisi sababu tu hawezi kujieleza kwa Kiswahili?
   Sijui kwako wewe kiongozi ni nani, lakini kwangu daktari, mwalimu, bwana/bibi shamba, fundi mchundo wote hao ni sehemu ya viongozi kwenye jamii

   Daktari asipoweza kujieleza kwa lugha ambayo mgonjwa anaweza kumuelewa inaweza kupelekea kupotea kwa maisha. Mwananchi anapokwenda kuhudumiwa serikalini lakini akakutana na wahudumu wasioweza kumueleza akaelewa kirahisi na kwa kutumia muda mfupi, kuna athiri idadi ya watu wanaoweza kuhudumiwa kwa siku na pia matokeo ya huduma hiyo kwa mwananchi.

  20. AshaDii's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 16th April 2011
   Location : Changeable
   Posts : 16,196
   Rep Power : 33249117
   Likes Received
   17614
   Likes Given
   18766

   Default Re: Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

   Quote By Gaijin View Post
   Matatizo yale yale ya Mtanzania. Hueleweki! Umenisoma na kunielewa au umeshindwa kunielewa?!.
   No Gaijin... Haya ni matatizo ya watu ambao hawajui type ya figure of speeches... Kiasi kwamba kila anapokuta statement; for instance swali anadhani ni lazima ajibu; kumbe saa ingene alouliza aliuliza out of rhetorism.... Ujanja ni kuelewa the meaning behind. Ni swala la kua sharp in grasping. Language haiwi na literally meaning kila mara.

   Quote By Gaijin View Post
   Ashadii Ama hukunisoma na kuelewa au hujui tofauti baina ya "vitu vyote" na "chochote"
   Nimekuelewa Gaijin I just meant EXACTLY that. Kua huwezi kua kipimo cha "vitu vyote"; Hapo nilikua na maana waweza kua kipimo cha vitu vingine baadhi (hapa hapa Jamvini); Nikisema chochote that would be absuard... Kwamba huna lolote la kuweza kua kipimo? iwe below or above standards? Like I said it would be absurd.... You are one of the Members with "some" brilliant inputs and point of views ambazo zaweza kua vipimo in other matters whether you like it or not!

   Quote By Gaijin View Post
   Hakuna anaezungumzia jitihada za Gaijin nje ya jamvi. Kwa ufupi nilichokieleza ni kwamba huwezi kujua kama Gaijin anachukua jitihada sana au kidogo, au haweki jitihada hata chembe anapoandika kwa kutumia lugha moja. Hakuna mwanachama humu Jamiiforums anaeweza kujua jitihada ya mwanachama mwengine wakati wa kuandika hapa jamvini. Tuache kuwatolea hukumu na mahitimisho wanachama tusiowajua.
   Oh' Gaijin jamani... you are hurting my feelings... I feel like I know you kiduchu (najua it is of no importanced kwako and I don't care); Back to the matter I don't judge assuming that the person behind the avatar yupo hivo... NO! Ila I judge kua the avatar of the person posting the post in question yupo hivo. Ndio maana kuna maneno hapa jamvini kama "Wachakachuzi" "Wanasiasa" "Doctor" "Vulgar" - Unapotumia maneno kama hayo haraka kuna majina ya members huja kichwani. Kwa mfano tukitaja jf Doctor haraka jina litakuja la Member mwenye ID ya Riwa ama Mzizimkavu.... Hio jitihada za kila member ziwe chini, kati ama juu.... Hua zaonekana na hizo ndizo zatumika kumjudge hapa jamvini. Kama you don't do it - it is Ok. But others we do.....

   Quote By Gaijin View Post
   Sijui kwako wewe kiongozi ni nani, lakini kwangu daktari, mwalimu, bwana/bibi shamba, fundi mchundo wote hao ni sehemu ya viongozi kwenye jamii.
   Na ndio maana kuna sehem nimekujibu kua viongozi wa ngazi mbali mbali.... Hii nime copy katika post yangu ya Kwanza. Hivo utakuta tupo pamoja. Just read between the lines...
   Tunasahau kua Yule kiongozi ana delegate tu, tukisahau kua kila mwananchi ana nafasi yake katika kutaka boresha maisha na maendeleo ya inchini kwake, tukisahau kua ni mwananchi wa kawaida kabisa anae changia kuporomoka na kurudi nyuma kwa maendeleo ya wananchi. Ma Boss wa taasisi mbali mbali za serkali, Wakubwa wa Mali za Umma, na Viongozi hadi wa chini kwa kiwango kikubwa wanafanya kazi chini ya maadili….

   Quote By Gaijin View Post
   Daktari asipoweza kujieleza kwa lugha ambayo mgonjwa anaweza kumuelewa inaweza kupelekea kupotea kwa maisha.
   Kwa hio bila mgonjwa kumuelewa doctor basi Doctor atapo run matibabu yatagoma? Alafu honestly speaking.... Kuna terms za kidoctor ambazo zimetoka katika lugha za wageni hata hao wenye lugha hawaelewi maana yake; nakubali kua Lugha yaweza pelekea damage katika certain issues, ila huu mfano wako wa Doctor ulotoa hapa haujitoshelezi.
   “Never get angry. Never make a threat. Reason with people.”
   - Mario Puzo (The God Father)

  Page 1 of 9 123 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...