Zakumi
Kwenye sanyansi hakuna mitizamo mbalimbali na tofauti kuhusiana na definitions za dhana mbalimbali. Kwa mfano kanuni ni moja inayo define Anatomy, Electron, Quantum physics, Biology na Tunaposema Kilometer, Voltmeter, wavelength hakuna maoni tofauti au
... ile hali ya kusema kama mimi ninaovyoona... !!
Umesema Viongozi wa Tanzania walipokea Kwa kishindo maazimio hayo. Niseme hivi kama hao viongozi walikuwa 100 kuna uwezekano kulikuwa na namna 100 tofauti walivyoyaona na kuyatafsiri. Hakuna Kanuni yoyote inayoweza kudhihirisha UNIFICATION ya Maazimio hayo kwa kuwa swala la maendeleo ni kila mtu kulichukulia kama anavyotaka na anavyoona (Niko tayrai kurekebishwa) kwani haliongozwi na kanuni yeyote ambayo inaweza kuwa universal.
Nani aniambie Kama Taifa Ni Nini Definition yetu ya Maendeleo ni nini? Na namna ya kuyafikia!!! Wachiliambali Taifa, Kama kila familia kuna definition Moja ya Mendeleo ni nini na namna ya kuyafikia? Tufike chini kabisa Kwa mtu mmoja mmoja hapa ndio kabisa .. mwengine anaamini maendeleo ni kukimbizana na albino na kumkata mkono, mwingine kumuibia muajiri wake, mwingine misison town, mwingine anaamini azmio la arusha , mwingine azimio la zainzbar nk
Nikiangalia EMT, AshaDII, Mkandara , Azimio Jipya, ZaKumi nk kila mtu anasema kivyake vyake kuhusu maendeleo ni nini na namana ya kuyafikia ... Na jambo hili ni hivyo hivyo kwa kila waziri, mbunge na kila Rais wa kila awamu!! Sifikiri kuwa hivi ni sahihi. Kuna kazi ya msingi kabisa ya kufanya kabla ya kwenda mbali kuanza kutekeleza swala zima la umasikini na maendeleo ya mwandamu.
Kwa mfano chukulia viongozi wote wanafuata Mtizamo wako Zakumi wa "Result oriented Business"
- eradicating extreme poverty and hunger,
Kiongozi mmoja kwa kuwa anataka kupata ubunge anaweza kuhujumu miradi mbalimbali ilikupta hela za ziada na kuwanunulia wananchi wa kijiji chake chakula na kuwagawia kwa malengo ya kupata kura. lakini atasimamia kuwa anatekeleza azimio la UN. That is immoral sio mkweli kwani moyoni anajua kabisa anacholenga. lakini ataonekana kuwa ni champion wa maendeleao nk. Kiongozi mwingine atatumia njia zake za kibinafsi kwa malengo yake na kuoyesha kafikia Matokeo na kusema ametekeleza azimo la UN lakini Moyoni ananjua kuwa ni Muongo tu! Lakini ataonekana kuwa kaleta maendeao na kafikia malengo... hivi maendeleo hata yakiletwa chini ya Uwongo uwongo, udanganyifu na ukosefu wa nidhamu bado yanaitwa maendeleo? Sikubaliani na jambo hili!! Nakubaliana kwanza hali ya ukamilifu na ukomavu wa ubinadamu kuwa NGUVU pekee inayosukuma matokeo yatakayoitwa maendeleo.
- achieving universal primary education,
Kuna haja ya kwenda kwa undani juu ya shule za kata ..kuonyesha mitizamo tofauti juu ya kila kiongozi na kinachotokea pale? Na sisitiza Kwa kuwa We can not universally define What is development kwa hiyo hatuwezi kupima maendeleo. Kila mtu atakuja na vigezo vyake na maono yake. Mpaka hapo tutakapo weza kukubaliana na what define what is development na kwa hoja yangu kama HUMAN FACTORS kukua na kukomaa kwa haki za binadamu, thamani za ubinadamu hakujumuishwi nk sidhani kama tutaweza kuwa tunajadili kitu kimoja kwenye hoja ya umasikini na maendeleo ya mwanadamu. Bila kwanza Haki na ubinaadamu wenyewe kuchukuliwa kuwa ndio NGUVU ya kusukuma na kujenga Maendeleo na Kufuta umasikini Mimi sikubaliani na hicho kinachotwa maendeleo.
- promoting gender equality and empowering women
Pia siamini kabisa kuwa wote tuna maanisha kitu kimoja hapa. Kwanza kwa waafrika hata hao wanaosemekana kuwa wameedelea sidhani kama wana kanuni inayosimamia jambo hili na kama kanuni hiyo inakubalika kwa wote. Hapa kwetu Tanzania Watu wa musoma na watu wa pwani wote hawawezi kuwa pamoja kwa issue kama hii wachilia makabila mengine. Kwa kukosa defining unifying principle ya jambo kama hili tutakesha hapa kulitafutia majibu kwani kila mtu ana mtizamo wake.
Sidhani kama hata nina haja ya kuendelea kuchambua hayo maazimio mengine au hata definitions nyingine.
Maazimio yote hayo nigefurahi kama nigeweza kufahamishwa vigezo vya kuyafikia na kama vigezo hivyo vimejumuisha maendeleo na ustawi wa MAADILI, UBUNADAMU, KUHESHIMIANA na hali zote za Ustawi wa binadamu.
Unafahamu nini?
Maazimio yote hayo yanawez akufikiwa huku Maadili, haki za binadamu, heshima nk vikiwa vinakandamizwa na kudidimia lakini bado yataitwa maaendeleo na kufuta Umasikini. Sikubaliani kabisa na Mtizamo huu!!!
Follow Us Here