Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?

    Report Post
    Page 4 of 4 FirstFirst ... 234
    Results 61 to 73 of 73
    1. BAK
      #1
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,537
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8278
      Likes Given
      8280

      Default Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?

      Mkapa ajuta

      • Ahuzunishwa wageni kuhodhi uchumi

      na Mwandishi Wetu | Tanzania Daima~Sauti ya Watu

      RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, amesema anajutia kitendo chake cha kuliingiza taifa katika ubinafsishaji wa rasilimali bila ya kujiandaa kikamilifu na mabadiliko hayo.

      Mkapa alitoa majuto hayo katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) uliofanyika Zanzibar wiki iliyopita katika Hoteli ya Zamani Kempinski na kuhudhuriwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.

      Mbali ya Mbeki, viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale - Mwiru.

      Mmoja ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ambaye alizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa sharti la kutokutajwa jina lake, alisema Mkapa alikiri kuwa sera ya ubinafsishaji haijamsaidia kwa kiwango kilichotarajiwa Mtanzania na badala yake wamegeuka wageni katika rasilimali zao.

      Chanzo hicho kilidokeza kuwa Mkapa alibainisha kuwa kukubali kwake sera hiyo kulikuwa na lengo zuri la kuwafanya Watanzania waondokane na lindi la umaskini kupitia uwekezaji utakaofanywa katika rasilimali zao.

      “Alituambia sera ya ubinafsishaji inamuumiza mno, kwani alipoikubali hakutarajia kama ingeweza kuwafanya wageni wawe na sauti katika rasilimali za taifa kuliko wazawa kama ilivyo sasa,” kilisema chanzo hicho.

      Chanzo hicho kilibainisha kuwa Mkapa alifikia hatua ya kudai kuwa kama angepata nafasi ya kuwa kiongozi tena wa taifa hili angerekebisha sera ya ubinafsishaji haraka ili walau Watanzania waanze kufaidi rasilimali za nchi yao, badala ya kuwa mashuhuda wa wageni wanaoendelea kuneemeka na rasilimali za nchi.

      Alisema tatizo kubwa lililopo katika nchi za Afrika ni kutumia baadhi ya mambo wanayotakiwa kuyafanya na wafadhili au mifuko ya fedha, bila kuyafanyia tathmini ya kina ili kujua kama hayataleta madhara katika siku za usoni.

      “Mkapa alionyesha kujutia uamuzi alioufanya kwenye uwekezaji na aliweka wazi kuwa kama angeruhusiwa kurudi katika nafasi hiyo, basi jambo la kwanza kulirekebisha ni ubinafsishaji,” kilisema chanzo hicho.

      Mkapa katika utawala wake alibinafsisha mashirika mengi ya umma, ikiwemo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa bei ya chini, kitendo ambacho kilizua malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, pia alibinafsisha Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na mengine mengi, kiasi cha kuzua malalamiko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

      Aidha, katika utawala wake pia alilalamikiwa kwa kuwapendelea wawekezaji wa kigeni kuliko wazalendo, hasa katika sekta ya madini na kuingia mikataba mibovu ambayo hadi sasa imekuwa mzigo mkubwa kwa taifa, sambamba na wawekezaji hao kupata misamaha ya kodi kwa kigezo cha kuwavutia.

      Kuingia mikataba mibovu huku ndiko kulikomfanya Rais Jakaya Kikwete kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini na kutoa ushauri wa namna bora ya kushughulikia sekta hiyo.

      Majuto hayo ya Mkapa yanakuja huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge na wananchi wakitaka afutiwe kinga yake ili aweze kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yake akiwa ikulu.

      Katika utawala wake, Mkapa anadaiwa kutumia madaraka yake kuanzisha miradi mbalimbali inayomhusu, ama kwa kupitia familia yake au ndugu zake, ukiwemo ule wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao hivi karibuni wamiliki wake wametajwa hadharani kwa mara ya kwanza.

      Chagizo la kutaka kutolewa kinga limezidi kupata kasi baada ya waliokuwa mawaziri wake, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja, kufikishwa mahakamani kwa kosa la kulisababishia taifa hasara ya sh bilioni 11 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya M/S Stewart.

      Kinga ya Mkapa inaweza kuondolewa kama Bunge litapiga kura ya kutaka kutengua kinga hiyo, lakini ni lazima hoja hiyo iungwe mkono na theluthi mbili ya wabunge wote.
      Last edited by Silencer; 25th January 2009 at 06:53.
      nick mgongolwa likes this.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    2. Study Abroad

    3. #61
      Keil's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd July 2007
      Posts : 2,381
      Rep Power : 1089
      Likes Received
      756
      Likes Given
      292

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By Jasusi
      Kiwanda cha bia TBL na kiwanda cha sigara havijawahi kuendeshwa kwa hasara. Actually hata kuna wakati Mwalimu alisema kuwa serikali ilikuwa inategemea zaidi kiwanda cha bia kwa fedha za matumizi yake. Tatizo la kiwanda cha bia lilikuwa ni management na si hasara. Bia ilikuwa haiivi na supply ilikuwa haikidhi demand. Actually walichofanya Makaburu baada ya akina Mwinyi kuwauzia ni wali flood soko la bia Tanzania na bia zao Castle, na hapo ndipo walipopata fedha za kukarabati mitambo ya TBL. Kaburu hakuweka hata senti tano ya Afrika kusini katika TBL wakati wa ubinafsishaji. Hii inaonyesha jinsi soko la bia Tanzania lilivyokuwa kubwa. Hata kama kilitoa kodi ya bilioni moja wakati huo. hakikuendeshwa kwa hasara na kilisaidia kuendeshea matumizi ya serikali na faida ilikuwa inaingizwa serikalini. Eniwei, umeshakumbatia uwekezaji na ubinafsishaji sitaki kukuondoa huko. Lakini ukweli hubaki pale pale.
      Hilo ndio lilikuwa tatizo la mashirika mengi ya umma. Management, Bodi, na serikali kuingilia maamuzi ya bodi/management.

      Mifano mizuri bado tunayo, TANESCO. Walipokuwa wanakuja NetGroup Solution, Management, Board na TUICO walipinga kwa nguvu zote mpaka wakamsomesha Waziri wa Nishati na Madini zama hizo Maokola Majogo na akawaelewa na kukubaliana na TANESCO kwamba NetGroup wasije. Mkapa alipoona home-boy wake Maokola Majogo ame-side na TANESCO, Majogo alitupwa ofisi ya Makamu wa Rais (Kuondoa Umasikini) akaletwa mwingine ili kuja kukamilisha deal. Kilichoendelea wote tunajua, na hata Richmond nayo hivyo hivyo, ni serikali kuilingilia kila kitu.

      TPA na wao hawakuachwa, kuna siku DG wa TPA nimesahau jina lake, alimwambia Mkapa wakiwa Mtwara, kwamba kama yeye (DG wa TPA) angepewa mamlaka ambayo wanapewa wageni ya kufanya maamuzi bila kuingiliwa, ana uhakika TPA ingekuwa mbali. Tatizo la mashirika mengi ya umma, kila unachofanya lazima kipate approval kutoka wizarani, na huko wizarani wanaangalia kwanza maslahi. Hilo ndilo lililikuwa kikwazo kwa mashirika mengi sana. Utahangaa GM au DG yule yule aliyekuwa anaongoza shirika kwa hasara, once likibinafsishwa kampuni inaanza kutengeneza faida, hakuna cha kuongeza mtaji wala nini, na si ajabu hata teknolojia ni ile ile.
      W. J. Malecela and engmtolera like this.

    4. #62
      W. J. Malecela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th March 2009
      Posts : 4,511
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2029
      Likes Given
      1819

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By Jasusi
      Kiwanda cha bia TBL na kiwanda cha sigara havijawahi kuendeshwa kwa hasara. Actually hata kuna wakati Mwalimu alisema kuwa serikali ilikuwa inategemea zaidi kiwanda cha bia kwa fedha za matumizi yake. Tatizo la kiwanda cha bia lilikuwa ni management na si hasara. Bia ilikuwa haiivi na supply ilikuwa haikidhi demand. Actually walichofanya Makaburu baada ya akina Mwinyi kuwauzia ni wali flood soko la bia Tanzania na bia zao Castle, na hapo ndipo walipopata fedha za kukarabati mitambo ya TBL. Kaburu hakuweka hata senti tano ya Afrika kusini katika TBL wakati wa ubinafsishaji. Hii inaonyesha jinsi soko la bia Tanzania lilivyokuwa kubwa. Hata kama kilitoa kodi ya bilioni moja wakati huo. hakikuendeshwa kwa hasara na kilisaidia kuendeshea matumizi ya serikali na faida ilikuwa inaingizwa serikalini. Eniwei, umeshakumbatia uwekezaji na ubinafsishaji sitaki kukuondoa huko. Lakini ukweli hubaki pale pale.
      - Thank you great thinker!

      William.

    5. #63
      kimondo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Posts : 100
      Rep Power : 454
      Likes Received
      7
      Likes Given
      3

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Prof. Shivji aliwahi kupewa u RDD (Regional Development Director) katika Mkoa wa Rukwa enzi za Mwalimu, akachemka.

    6. #64
      engmtolera's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2010
      Posts : 3,605
      Rep Power : 1330
      Likes Received
      779
      Likes Given
      655

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By W. J. Malecela
      - Then tukubaliane kwamba sera ya kuuza mashirika na viwanda ilikuwa sawa kimsingi, sasa waetekelezaji nini kosa la Mkapa kwa hoja yako mkuu? Je tulitegemea Rais wa Jamhuri aache kazi zake wka taifa akasimamie ubinafsishaji?

      - I mean ninakubaliana na wewe kwamba kuna makosa makubwa yaliyotokea kwenye the process, lakini still the outcome bado no progressive sio kama the process isingfanyika!

      William.
      unauza njia kuu za uchumi then unategema nchi kupaa kiuchumi?

      ktk dunia hii sijawahi ona nchi iliyoendelea kwa kuuza viwanda vyake,haipo mahali popote pale,yaani serikali inauza mashirika ya umma na viwanda vyake ili ijikite ktk ukusanyaji kodi na hata ktk ukusanyaji kodi bado unampa mwekezaji miaka mitano ya majaribio na kumlipiza TSH 250/H kt ardhi then unategemea utatoka ktk umasikini,haiwezekani hata siku moja
      Elisha Ray likes this.
      "The person who says it cannot be done should not interrupt the person doing it."

    7. #65
      Mimibaba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2009
      Posts : 3,148
      Rep Power : 1527
      Likes Received
      754
      Likes Given
      590

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Bahati mbaya si rahisi sasa kumdanganya mtwana anaeguswa na athari za maamuzi ya kipuuzi na hasa anapojua haki zake.

      1. Mwinyi was a disaster

      2. Mkapa was a calamity

      3. JK is both a disaster, a calamity and a liability

      4. CCM is the devil himself engineering all the above

      My uncle Willy you are a right product of the above
      Last edited by Mimibaba; 26th April 2012 at 15:20.
      zumbemkuu and Elisha Ray like this.
      Ukweli utakuweka huru daima

    8. Miaka 50

    9. #66
      W. J. Malecela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th March 2009
      Posts : 4,511
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2029
      Likes Given
      1819

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By engmtolera
      unauza njia kuu za uchumi then unategema nchi kupaa kiuchumi?

      ktk dunia hii sijawahi ona nchi iliyoendelea kwa kuuza viwanda vyake,haipo mahali popote pale,yaani serikali inauza mashirika ya umma na viwanda vyake ili ijikite ktk ukusanyaji kodi na hata ktk ukusanyaji kodi bado unampa mwekezaji miaka mitano ya majaribio na kumlipiza TSH 250/H kt ardhi then unategemea utatoka ktk umasikini,haiwezekani hata siku moja
      - Katika dunia hii sijawahi kuona taifa liliondelea kwa serikali yake kumiliki viwanda na mashirika, ila nimeona mataifa yakiendelea kwa kukusanya kodi tu! na kusimamia sheria!

      William.

    10. #67
      W. J. Malecela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th March 2009
      Posts : 4,511
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2029
      Likes Given
      1819

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By kimondo
      Prof. Shivji aliwahi kupewa u RDD (Regional Development Director) katika Mkoa wa Rukwa enzi za Mwalimu, akachemka.
      - Sawa sawa nilikuwa sijaiona hii, thanks great thinker!

      William.

    11. #68
      W. J. Malecela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th March 2009
      Posts : 4,511
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2029
      Likes Given
      1819

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By Mimibaba
      Bahati mbaya si rahisi sasa kumdanganya mtwana anaeguswa na athari za maamuzi ya kipuuzi na hasa anapojua haki zake.

      1. Mwinyi was a disaster

      2. Mkapa was a calamity

      3. JK is both a disaster, a calamity and a liability

      4. CCM is the devil himself engineering all the above

      My uncle Willy you a right product of the above
      - Sure I live with that!

      William.

    12. #69
      engmtolera's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2010
      Posts : 3,605
      Rep Power : 1330
      Likes Received
      779
      Likes Given
      655

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By W. J. Malecela
      - Katika dunia hii sijawahi kuona taifa liliondelea kwa serikali yake kumiliki viwanda na mashirika, ila nimeona mataifa yakiendelea kwa kukusanya kodi tu! na kusimamia sheria!

      William.
      nakupa mfano mdogo sana

      china
      serikali inamiliki china mobile,china unicom,usafirishaji wa reli,barabara na majini,viwanda(baadhi inamili kwa 100% na baadhi imeshare na wawekezaji)

      nimekupa mfano mdogo sana
      W. J. Malecela likes this.
      "The person who says it cannot be done should not interrupt the person doing it."

    13. #70
      W. J. Malecela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th March 2009
      Posts : 4,511
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2029
      Likes Given
      1819

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By engmtolera
      nakupa mfano mdogo sana

      china
      serikali inamiliki china mobile,china unicom,usafirishaji wa reli,barabara na majini,viwanda(baadhi inamili kwa 100% na baadhi imeshare na wawekezaji)

      nimekupa mfano mdogo sana
      - Mkuu nimewahi kuishi Shanghai, China wana utawala unaoheshimu Sheria hakuna mahali wanamiliki 100% anything katika hayo mashirika machache ambayo Serikali yao imeamua kwamba ni lazima yawe chini ya serikali, infact hata US shirika la post na amtrack Train, bado yapo chini ya serikali na ni baada a mabunge ya nchi zao kuamua kwamba hayo mashirika machache walioyaacha under serikali yakipewa private wananchi watateseka sana,

      - Otherwise sio hata 1% ya mashirika yote ya mataifa yao, hiyo inakubalika ninaamini hata sisi bado tuna umiliki mkubwa kwenye posta yetu, hilo wala sio ishu mkuu!

      William.

    14. #71
      engmtolera's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2010
      Posts : 3,605
      Rep Power : 1330
      Likes Received
      779
      Likes Given
      655

      Default Re: Ubinafsishaji: Why Mkapa was 1000% Right!

      Quote By W. J. Malecela
      - Mkuu nimewahi kuishi Shanghai, China wana utawala unaoheshimu Sheria hakuna mahali wanamiliki 100% anything katika hayo mashirika machache ambayo Serikali yao imeamua kwamba ni lazima yawe chini ya serikali, infact hata US shirika la post na amtrack Train, bado yapo chini ya serikali na ni baada a mabunge ya nchi zao kuamua kwamba hayo mashirika machache walioyaacha under serikali yakipewa private wananchi watateseka sana,

      - Otherwise sio hata 1% ya mashirika yote ya mataifa yao, hiyo inakubalika ninaamini hata sisi bado tuna umiliki mkubwa kwenye posta yetu, hilo wala sio ishu mkuu!

      William.
      haya rudi tanzania,tunajivunia kwa kiwanda kipi,migodi wanamiliki wawekezaji(china pale inner mongolia ambako ndiko kwenye upatikanaji wa madini -serikali inamiliki 100%)

      usafirishaji wa abiria (daladala) serikali inamiliki 100% ingawaje na wawekazaji wapo) UDA tumeuza,

      faida ya ubinafsishaji tanzania haipo ,zaidi ya kusaidia wajanja wachache
      Zakumi likes this.
      "The person who says it cannot be done should not interrupt the person doing it."

    15. #72
      Mwakalinga Y. R's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 22nd October 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 2,169
      Rep Power : 972
      Likes Received
      924
      Likes Given
      2278

      Default Re: Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?

      Mkapa alibugi mambo mengi sana.Alitumia kivuli cha so called utandawazi kwenye Mkt Economy kufanya uchafu alioufanya kipindi cha utawala wake.Alidanganya uma kuwa alichokuwa anakifanya ni matakwa ya utandawazi.Utandawazi aliokuwa anaushabikia Mkapa ni ufisadi na uporaji rasilimali kwa nchi na kuwapa wageni.

      Ukipitia kabrasaha kutoka IMF kuhusu ubinafsishaji vipo vipengele, wazi vinaeleza kuhusu vitu ambavyo serikali inaweza kuacha kubinafsisha. Hii ni kwa ustawi wa nchi kuweza kuwa na nguvu/sauti kwenye uchumi . Pia ni njia ya kulinda rasilimali za nchi-Mfano Bank ya taifa,Ports ,Railwayz.Pia imeelezea wazi kuhusu rasilimali kama madini kuwa serikali inaweza ingia ubia kulinda maslahi ya wananchi kutokuporwa rasilimali zao moja kwa moja.

      Suala la kustaajabu Mkapa na genge lake la wezi wakadanganya uma kwa manufaa yao. Wakati huo huo baadhi ya wasomi walikuwa wanatumiwa kuwapumbaza wananchi kuwa mashirika ya fedha duniani IMF na WB ndio yanatoa muongozo huo unaotunyonya(wakimsafisha Mkapa)

    16. BAK
      #73
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,537
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8278
      Likes Given
      8280

      Default Re: Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?

      ....Duh enzi hizo!!!! kaka Mbu naye alikuwa anachangia kwenye siasa...siku hizi yuko kwenye football na MMU kwingine hachezi kabisa
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    17. FemaTV & Radio
    Page 4 of 4 FirstFirst ... 234

    Similar Topics

    1. Hawara wa zamani wa Ryan Giggs ajutia...
      By Rutashubanyuma in forum Celebrities Forum
      Replies: 2
      Last Post: 23rd December 2011, 07:31
    2. Ajutia kugawa namba ya simu
      By kilimasera in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 36
      Last Post: 18th January 2011, 03:15
    3. Mkapa vs kikwete
      By pcman in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 23
      Last Post: 23rd September 2010, 00:55
    4. Kikwete Vs. Mkapa
      By Mzee Mwanakijiji in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 9
      Last Post: 21st January 2008, 14:47

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...