JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

  Report Post
  Page 1 of 2 12 LastLast
  Results 1 to 20 of 34
  1. Mlosi Mtulutumbi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th October 2010
   Posts : 685
   Rep Power : 759
   Likes Received
   228
   Likes Given
   247

   Default Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Mjomba wangu daktari, salamu sana,
   Ama baada ya salamu,

   Kwanza nitoe shukrani kubwa kwa kunirudishia majibu ya kina nilipokuuliza swali kwa nini mama na mpenzi wake baba waliamua kuniita mtulutumbi. Nashukuru kwa kunieleza kwa uwazi kuwa mtulutumbi kwa lugha ya watani wetu kule kwenye mapanga shaa humaanisha 'mchawi', mwanzoni nilikereka kidogo lakini sasa naelewa busara zao, kwa maana kama mchawi anavyochukiwa na watu wengi, yawezekana kwa waraka wangu huu kwako watu wengi wakanichukia. Hii ndiyo sababu kubwa ya kufarijika kuitwa 'mtulutumbi' kwa maana watu wengi wasiopenda kufikirisha vichwa vyao kufikiria fikra za mtu aliyefikiria kuandika fikra, basi watanichukia japo najua wewe utanielewa mjomba daktari;

   Kwanza nikupongeze kwa kusitisha mgomo kwa hiari yako, hongera!
   Mgomo uliouanzishwa mwenyewe bila shinikizo, Hongera
   Ukasema unawatetea wananchi ambao hawakuelewa unawatetea kwa nini, hongera!
   ukakutana na 'mtoto wa mkulima' mtani wangu wakati akiwa amekufukuza kazi, hongera!
   Juzi nasikia uliwatuma wajumbe kupata kiyoyozi magogoni, hongera!
   Hongera! Hongera! hongera!

   Hata hivyo, baada ya hongera nyingi nirudi hasa kwenye hoja ya msingi;

   Moja: Kuwatetea wananchi kuhusu huduma bora

   Kwanza,nikusifu kwa jinsi ambavyo umeendelea kutoa huduma pasipo kujali kuwa fani yako inakaribia kuwa kama mganga wa kienyeji, na pengine kuwa chini ya hapo, hili litaliongelea baadaye na naomba unisamehe kukufananisha na 'mganga' wa kienyeji japo naamini wananchi kukuita 'bwana mganga' badala ya 'daktari' inawezekana wanakuona kama mganga wa kienyeji japo sina uhakika kuhusu hilo na mimi si mtaalamu wa kiswahili mjomba. Kama hujui mjomba, Wananchi wengi wa Tanzania "wameshadumaa" akili na hali hii imejengeka toka enzi za hata kabla ya uhuru. Hali hii ambayo inahitaji 'ukombozi wa fikra' kama alivyoeleza Mzee Mwanakijiji katika waraka wake hivi karibuni, ina safari ndefu sana hadi kupata ukombozi huu, na hilo tu ndilo litakaloboresha hali ya ndugu zangu si kisiasa tu bali kiuchumi,kiafya na kadhalika.

   Kama alivyosema mtanzania mmoja katika kitabu chake ambacho naamini hakijasomwa na watanzania wengine kiitwacho Sindano inayovuja, 'Serikali huboresha huduma kwa wananchi kunapokuwa na Service Demand". Service demand aliyoiongelea hapa si ya kusubiri serikali 'ione' uhitaji wa huduma bali 'wananchi' kuwa proactive na kuona kuwa wanahitaji huduma na kwa kuwa serikali ni mwajiriwa wa wananchi, basi 'wananchi wadai' huduma kama haki yao na kazi waliyoituma serikali kufanya. Mfumo huu wa service demand toka kwa wananchi ndiyo wanaoutumia wanaharakati kudai mabadiliko katika mambo kadhaa, mfano miswaada mingi ama mipya ama inayofanyiwa marekebisho au kuwekwa viraka katika nchi zilizoendelea hutokana na 'Pressure' za wanaharakati kutokana na makundi fulani ya kijamii kuona hitaji la huduma na kudai. Hali hii ni tofauti nchini mwetu mjomba, wewe mwenyewe ni shahidi kwani wananchi wamehalalisha umasikini, shida na karaha. Umasikini kwa wananchi umekuwa ni kama binadamu na nguo mjomba, kwamba unapompigania mwananchi anaona kama unataka kumvua nguo..

   Mwananchi huyu huyu mjomba,
   Nani asiyeelewa, haki yake ulidai?
   Ukasema kaelemewa, Huduma kwake hutoi?
   Glovu uletewe, Temeke hadi Moi?
   Vitanda uongezewe, mwanga siwe koroboi?
   Kaposho upewe, hata ukiwa kiomboi?
   Ukamwona Mizengwe, akakuacha hoi?


   Mwananchi wa Tanzania mjomba pengine ulipoteza muda wako kumtetea, au pengine pia nikusifu kwa kuwa umejihakikishia mwenyewe kuwa mwananchi huyu si wa kumkomboa kwani hayuko tayari kukomboka;au hata kukombolewa;
   Anaona kulala chini pale Mwananyamala, Ni haki yake ya msingi;
   Anaona kubebwa kwenye ambulance ya baiskeli kijijini, ni haki yake ya msingi
   Hana bima ya afya, ni haki yake ya msingi
   Anajinunulia dawa kwa kuwa hospitalini hazipo, ni haki yake ya msingi
   Hana uwezo wa kwenda hospitali ya binafsi, ni haki yake ya msingi
   Akuambukize magonjwa au umuambukize wewe kwa kukosa glovu, ni haki yake ya msingi
   Umtibu kama mganga wa kienyeji kwa kuwa huwezi kumfanyia vipimo, ni haki yake ya msingi.
   Analipa kodi katika kiberiti hadi ndala, ni haki yake ya msingi;
   Umuhudumie hata kama una njaa, ni haki yake ya msingi;
   Udaktari ni wito, uongozi wa kisiasa siyo wito, ni haki yake ya msingi;
   Atembee kilomita nyingi kwenda hospitali kwa kuwa mjomba umeng'ang'ania mjini, ni haki yake ya msingi!
   Haki ambayo wataka kumnyang'anya mjomba!

   Je mtu huyu anastahili kutetewa?

   Hapa ndiyo maana nikasema mjomba umepoteza muda wako, japo ni nafasi pia ya kujifunza. Leo ningeweza kuwanukuu wanafalsafa wengi sana lakini nataka suala hili niliongelee kwa lugha nyepesi mjomba wangu daktari...

   Mjomba, unadhani kwa nini mwananchi huyu yuko hivi?

   Kwanza, ni mfumo wa 'ndiyo mzee': Mfumo huu huanzia katika ngazi ya familia, malezi ya familia zetu hutuzuia kuhoji, mila na destruli zetu hutuzuia kuhoji. Wewe unakumbuka nilipohoji katika kikao kimoja pale kijijini kwa nini kila akichinjwa mbuzi au ng'ombe 'wazee' wale nyama laini ya mgongo na paja wakati wanawake wanakula utumbo na vijana wale mbavu? unakumbuka makalipio yaliyonipata? Wakasema mimi 'usomi' umenipotosha, ooh mara mi mlafi ati naingilia 'haki' ya wazee, nisubiri nami nikizeeka ati. Je unakumbuka pia nilipohoji kwa nini wanawake wale chakula jikoni wakati wanaume wanakula kwenye meza unakumbuka fimbo nilizopata toka kwa mzee ukaniokoa wewe? Huo ndiyo mfumo uliojengeka ambao mimi niliupinga mapema. Mila na malezi yetu yanatuandaa tuwe watu wa mapokeo.

   Unakumbuka nilivyomuhoji mchungaji kwanini Yesu alipaa bila mbawa? Unakumbuka nilikaribia kuondolewa kanisani kwa kuwa 'nimepotoka' , kuhojihoji kwangu ndiko kulikonifanya mzee aniite 'mtulutumbi' kwa maana kila niliporudi kijijni nilimchallenge kwa falsafa nilizosoma shule na kimsingi hakujua kuwa kunisomesha ina maana aliniandaa nitofautiane naye na mtu mwingine wa kijijini katika kufikiri, tuyaache hayo, lakini ili watanzania waanze kuhoji hoji, ni lazima tuanzie katika mila na ngazi ya familia, watoto waruhusiwe kuhoji na wapewe majibu ya uhakika.

   Pili, toka enzi za uhuru, kwa kuwa hatukumwaga damu basi watu walimwona Nyerere kama Malaika. Unabisha? Umesahau kanisa katoliki lilipendekeza apewe heshima ya 'Utakatifu'? Sijui walishampa au la lakini ninachoongelea hapa ni kuwa katika mfumo wa kufanya maamuzi, japo walisema ni demokrasia lakini watu wote macho yalikuwa kwa Nyerere. Kama ilivyokuwa kwa mkoloni kuwaamrisha kulima mashamba yao wenyewe bila ujira au kwa ujira mdogo tu kisha mazao yote ya mkoloni na tena wakalipa na kodi na wakaitikia 'Ndiyo mzee' huku wakiimba nyimbo za 'Mungu mbariki mkoloni' sijui kutawaliwa na wakoloni kuliitawala akili yetu mjomba yaani hata sijui kwani mawazo hayo hayo ya ndiyo mzee yakahamishiwa kwa Nyerere na kwa kuwa viongozi wengi wa kisiasa kuanzia mwenyekiti wa kijiji walikuwa wakimwakilisha Nyerere basi kila walichosema kiongozi kasema Nyerere.

   Kama unabisha, post hii tazama
   Nyimbo nitaimbishwa, Nyerere kumsema
   Naweza aibishwa, ati mi si mwema

   Kwa sababu tu, Nyerere ni malaika
   Alitenda mazuri tu, hana alipopotoka
   Basi tumpe sifa tu, apumzike kwa rabuka!


   Hali hii ya 'kutomsema' Nyerere ni ushahidi tosha kuwa msingi uliojengeka ni wa 'hewalaa' pasipo kupewa nafasi ya kuhoji. Hali hii imemjenga mtanzania kuwa mtumwa wa fikra za viongozi. Hali ambao ukihoji tu ati unatishia 'usalama wa taifa' na wala usije kushangaa nami natafutwa kuhojiwa na polisi mjomba. Hii ndiyo maana hata ulipojieleza kuwa umegoma ili upewe mazingira mazuri ya kumuhudumia mtanzania;

   Kiongozi alipoongea, aliaminiwa
   Wewe ulipoongea, Ulilaumiwa
   Kila uliloliongea, ulilaaniwa

   Wakakuita mbinafsi, usiyewajali wenzako
   Waijali yako nafsi, si maadili fani yako
   Ati umeitupa nafasi,umeivunja miiko


   Huyu ndiye mwananchi uliyekuwa unamtetea mjomba!

   Tatu, hadi sasa serikali inaendelea mtindo wa kuwatawala wananchi kifikra
   Nina mifano kadhaa, moja mwaka fulani nilihudhuria kampeni za CCM, katika jimbo hilo ambalo chama cha upinzani kilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda, uelekea mwishoni mwa kampeni CCM ikaleta malori, Kofia, vitenge, chumvi na mgombea aliwanunulia wazee pombe ya kienyeji na ile bendi ya CCM na wanenguaji wake wakakata viuono. Matokeo CCM ilishinda kwa kishindo mjomba
   Nikawa najiuliza; Je Pombe ziliwalewesha wananchi wakawa hawaoni vizuri karatasi ya kupiga kura?
   Je, t-shirt za 'mchina' walizovaa ziliwabana mikono kuilekeza kwa mgombea wa CCM?
   Je, vitenge walivyofunga akina mama viliwabana viunoni na kuwaelekeza kupigia kura CCM?
   Je, chumvi waliyokula kabla ya uchaguzi iliwadumaza akili, wakaona picha ya CCM tu?
   Au ni viuno wa wana TOT viliwachanganya akili? Si unajua tena watanzania kwa mambo yetu yalee....
   Basi sijapata jibu hadi leo!

   Lakini falsafa yangu ni kuwa Watanzania wanaridhika sana na faida au wema wa muda mfupi huku wakisahau madhara yatakayojitokeza baadaye. Hii ndiyo sababu ulipogoma mjomba kila mtu aliyeugua homa alitaka urudi kazini pasipo kujali anaweza kupata tatizo litalohitaji huduma ya muda mrefu kama vile kisukari au hata Hypertension na kama mazingira ya kazi hayajaboreshwa madhara yake ni ya muda mrefu. Yeye alitaka siku hiyo anayoumwa atibiwe basi! Akawa anaangalia wagonjwa waliolazwa sasa pasipo kuangalia ni wangapi watalazwa baadaye iwapo hali ya afya nchini itabaki kuwa hivi hivi kwa miundombinu afya hii hii.

   Nne, mjomba watanzania ni WABINAFSI. Kama hukujua hili basi tambua leo
   Hujifikiria wenyewe, daktari sawa na roboti,
   Huna familia wewe, inayohitaji sapoti
   Huugui wewe,wala hutaki noti


   Huyu Mtanzania huyu mjomba,
   Yeye ahudumiwe, Hata kama una njaa
   Bora tiba apewe, basi asikia rahaa
   Hata posho usipewe, kwake mambo mwaa

   Vipimo usimfanyie, bora dawa andika
   Nafuu ajisikie, arudi kwake Tandika,
   Kwa Lipi akusifie, mshahara wa mashaka?
   Huduma mpatie,ajua huwezi choka!


   Ubinafsi huu mjomba ndiyo uliosababisha kashfa nyingi kama Dowans, Richmond na kadhalika. Ubinafsi huu ukichanganywa na tabia na mila za kutohoji umefanya watanzania wahalalishe GIZA la kila mara. Juzi niliongea nawe nikasikia muungurumo ukanambia majenereta yanashindana kuunguruma kama kwaya za kwenye tamasha la injili. Umeme kwa mfano, unahitajika mahospitalini ili huduma kama za upasuaji na usafishaji wa vyombo vya hospitalini ufanyike. Maji yanahitajika ili huduma za hospitalini ziendelee.

   Mwananchi huyu mbinafsi, uliyekuwa unamtetea, hata haoni madhara ya sekta nyingine katika huduma za afya.

   Yeye anaona ndugu yake akifariki kwa kuwa huwezi kufanya operesheni theatre hakuna umeme, ni haki yake ya msingi
   Kutumia kibatari mjini Dar Es salaam karne ya 21, akapata magonjwa yatokanayo na moshi au akaungua moto. Ni haki yake ya msingi.

   Kuogea makopo wakati kuna bomba bafuni linaleta hewa tu, makopo yaliyojaa fangasi na vimelea vya magonjwa,ni haki yake ya msingi.

   Kupata 'Noise pollution' utokana na miungurumo ya jenereta , ni haki yake ya msingi.

   Kubanana kwenye daladala akapata magonjwa ya kuambikizwa mpaka chawa, ni haki yake ya msingi.

   Ati huyu huyu ndiye uliyekuwa unamtetea

   UMEPOTEZA MUDA WAKO MJOMBA

   Mjomba daktari kama mganga wa kienyeji

   Unakumbuka nimekufananisha na mganga wa kienyeji au babu wa loliondo huko awali?


   Sina lengo la kukukosea heshima hata kidogo. Lakini hebu fikiria, machine ya x ray wilayani kwako ni mbovu toka mwaka juzi; Je, mgonjwa unayehisi kavunjika mbavu utafanyaje kuwa na uhakika? Stethoscope yako siku hizi inapima malaria kama hakuna reagent maabara? Nasikia Ukimwi siku hizi umepamba moto huko, Je, hao akina mama hapo labour ward unawazalishaje kama hakuna glovu? huyo mama mwenye 'Pregnancy induced hypertension' unampa panadol badala ya magnesium sulphate? Je maiti pale mochwali unazitunzaje kama hali ndo hii? Kama jibu ni hapana kwa moja wapo ya maswali haya rahisi basi wewe ni mganga wa kienyeji, tofauti tu ni kuwa huna tunguli. Nakuahidi nitakutafutia mjomba tena lenye bendera ya taifa kwa kuwa naja wewe ni mzalendo kuanzia ngozi hadi moyo.
   Wamama sakafuni, wamelaliana
   ICU huwaoni, hapo amana?
   Utawapa nini, kama dawa huna?


   Mganga wa kienyeji anakuzidi kwani microscope yake ni tunguli, vibuyu vimejaa ukerewe anaweza kuagiza
   Quinine zake ni mitishamba, bado tuna mapori singida anaweza kwenda kuchimba
   Wagonjwa wake wakija,awe bosi au masikini ataingia kwenye kijumba kidogo kikuukuu
   Wewe mabosi wako si wanatibiwa India?
   Ndugu za mabosi wako si wanakuja na vimemo na wewe unawatibu haraka haraka? mabosi hao hao ambao wanakalia nafasi za kusoma huko wizarani....Nafasi za kusoma nje ya nchi zipo lundo waizarani unajua nani anaenda?

   Wewe ni mganga wa kienyeji mjomba, nitakuletea ngozi ya mbuzi hapo hospitalini kwako utibie!

   Tatu, unajua kwa nini hata wataalamu wetu siku hizi wanaishia kufanya tafiti za Prevalence tu?

   Najua hulijui hili mjomba, acha nikutonye, watafiti wengi wa kitanzania wanfanya case studies na prevalence studies!


   Kati ya tafiti kumi utakazo soma za watanzania, 8-9 ni za prevalence na KAP, mara prevalence of HIV, mara knowledge attitudes and practices of....Kiufupi ni tafiti zinazoelezea tatizo bila kutafuta mbinu sahihi za kutatua tatizo.Utasikia prevalence of anemia kwa wato wachanga badala ya a randomized controlled trial of substance x in treatment of anemia. Hali hii ya kufanya tafiti za kuelezea tatizo zimefanya kwanza:

   • Tafiti nyingi za watanzania kutokuwa na tija au kuongeza maarifa mapya
   • Si ajabu kumwona hata profesa anafanya prevalence study badala ya kufanya randomised trial


   Unajua kwanini naongelea haya? Namaanisha hata wasomi wetu hawana mchango stahili kwa taifa letu. Kwani Mponda hana PhD? Kikwete hana PhD (japo ni ya shortcut)? Lucy Nkya hana elimu?. Iwapo wanayo kwa nini unawalaumu leo kuwa hawaongozi vizuri? Kwa nini wameng'ang'ania madaraka hadi leo-Jibu ni lile lile-Nina wasiwasi mkubwa na uwezo wa wasomi wetu kufikiri! Ndiyo maana profesa anafanya prevalence ya HIV, kwa kuwa ama hana uwezo wa kufikiri au hawana uwezo wa kuzifikirisha akili zao kwa uwezo wake. Kisha wanalalamika ati tafiti zao hazitumiki kutengeza sera Tanzania. Hivi waweza kutumia utafiti wa kupima kiwango cha chumvi baharini kutengeneza undeground tunnel kwenda Zanzibar wakati maji chumvi waweza kuyapima hata kwa ulimi?

   Kuna aina mbili za kufikiri mjomba:

   Kwanza ni kufikiri kuhusu jambo fulani kwa uwezo wa kawaida tu "common sense" wa kila binadamu na ukifikiri vizuri kidogo basi hii huitwa busara, yaani uwezo wa kufikiri na kutoa fikra njema kwa uwezo wa kawaida wa kiakili kuliko watu wengine wenye uwezo sawa na wako. Hii ni tafsiri yangu ya busara mjomba.

   Aina ya pili ya kufikiri, ni uwezo wa kuifikirisha akili yako kufikiri kwa kiwango chake stahili. Kiwango chake stahili hapa humaanisha uwezo wa kielimu. Kama mtu ana PhD katika afya ya jamii naamini anaweza kufikirisha akili yake kwa kiwango chake stahili na akapata solution na hawa ndiyo tunaowaita 'mapioneer au wanafalsafa .
   Kwa hiyo kama mtu ana PhD halafu anafanya mambo uliyonisimulia na bado anang'ang'ania madarakani basi huyu hana busara wala haifikirishi akili yake kwa kiwango kinachohitajika kufikiri na hiyo PhD si yake kwani ni sawa na Professor anayefanya tafiti za prevalence au knowledge, attitudes and practices (KAP) ambazo zatakiwa zifanywe na wanafunzi.

   Mjomba, nasikitika kuwa nawe umenaswa katika mtego wa wanasiasa. Japo najua umetumia busara kurudi kazini lakini unarudi kazini ukiwa na vidonda vibichi. Bado faida ya kugoma kwako haiko wazi.
   Kwa maana wakati kima cha chini cha mshahara kwa mfanyakazi katika nchi moja ya majuu niliyotembelea ni dola 8 kwa saa, mjomba wewe unalipwa dola 12 kwa masaa 24 ya calls.

   Hapo hujaweka;
   Gharama ya kumkosa mkeo ambayo unajiweka katika hatari ya kulea watoto wasio wako.
   Gharama ya kung'atwa na mbu mjomba ukaugua Malaria na bado Bima yako ni sawa na ya mwanapollo wa Mererani
   Gharama za kuambikizwa magonjwa unapomhudumia mgonjwa ukiwa na usingizi
   Gharama za msongo mawazo wa kumkosa mkeo usiku.

   Katika vita mjomba, ukiamua kushambulia shambulia hadi ushindi. Kurudi nyuma bila kuwa na mbinu mbadala yenye nguvu zaidi ya awali ni kumpa nafasi adui kukushinda. Kama nilivyosema najua umetumia busara, yaani uwezo wako wa kufikiri kwa akili ya kawaida au common sense. Kwa maana hiyo umefanya jambo jema na la kupongezwa japo umenasa kwenye mtego wa ahadi za Wanasiasa!

   Mjomba wanasiasa wameiharibu nchi yetu! Mchango wa Siasa katika Nchi hii HAUONEKANI mjomba!

   Tanzania ilikuwa mahali pazuri, sawa pamekuwa kama kuzimu
   Japo kuna magari mazuri, ni ya wachache wanaharamu,
   Wao kila siku waishi swari, masikini waishi kama mizimu
   Umasikini kwao si habari, viyoyozi kwao kitu muhimu


   Hivi mjomba nikuulize, hivi kama asilimia 98 ya watu wanaokuzunguka ni mafukara, wewe unajisikiaje?
   Kanisani waenda kufanya nini?
   Kama posho zote Bungeni
   Waongeza mara ishirini?
   Huwaoni masikini?


   Hivi mjomba maisha huchagua kuwa magumu, kwa watu wenye vyeo fulani?

   Kuna wakati mjomba najiuliza maswali mengi, machozi yajaa machoni!
   Naipenda nchi yangu, wala siwezi kuihaini
   Watanzania wenzangu, hata siwezi kuwalaani
   Kila siku moyo wangu, waumia uchunguni
   Hata ndoto zangu, naona tu manyani
   Yasojali wenzangu, yaso na haya usoni
   Yadhurumu ndugu zangu, nyoyo zao za Nyani
   Hakika njomba wangu, Sitafika msibani
   msiba wa adui yangu, fisadi muhaini!


   Mjomba nikuache kwa kashairi haka ka kimombo, naamini bado wakikumbuka toka Medical School mjomba!

   A shoe less leg, a no-mattress bed


   A roofless house, a crop-less farm
   An empty pocket, a numberless check
   A man's slave, a victim of fate
   A nearly dying body, leaving no tales
   Worthless on Earth, a worry-less mind
   Burdens to carry, like a horse's hoof
   An Injustice of mortals, exploit of men
   Death it awaits, a citizen of paradise
   Poor on the Globe, a heaven’s allures
   Mtulutumbi on Earth, a king in heaven!

   Salamu zangu zikufikie mjomba Daktari

   Nisemehe kama kuna makosa ya kisarufi mjomba, muda umenitupa mkono
   Last edited by Mlosi Mtulutumbi; 11th March 2012 at 09:21.


  2. Lasikoki's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th January 2010
   Posts : 642
   Rep Power : 2835
   Likes Received
   113
   Likes Given
   39

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   duh! Am speechless! Huu ujumbe ni mzito sana. Ni ukweli mtupu!

  3. STIDE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st September 2011
   Posts : 995
   Rep Power : 724
   Likes Received
   339
   Likes Given
   114

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Asante sana mkuu!!!
   Nikiifikiria sana Tanzania na watz wake huwa nahisi kurukwa akiri!!
   TUMUOMBE SANA MUNGU ATUTAKASE AKILI!!!!!

  4. Mlingwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th March 2011
   Posts : 382
   Rep Power : 621
   Likes Received
   58
   Likes Given
   225

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Well said Mtulutumbi, hakika umetumia muda wako vyema kutueleza ukweli watanzania, natumai wajomba wamekuelewa.
   ''The difference between people is not that one has more time than the other. The difference is whether they use their time wisely".

  5. AshaDii's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 16th April 2011
   Location : Changeable
   Posts : 16,196
   Rep Power : 33249116
   Likes Received
   17614
   Likes Given
   18766

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Mtulutumbi Asante kwa maneno yako mazito yalojaa hekima, Kiasi kwamba imeniuma sana kua Ni wachache wataupitia na kuwafikia. I wish kila Mtanzania aloguswa na kufuatilia mgomo wote angebahatika kupata huu ujumbe.
   “Never get angry. Never make a threat. Reason with people.”
   - Mario Puzo (The God Father)


  6. zee la weza's Avatar
   Banned Array
   Join Date : 7th February 2012
   Posts : 189
   Rep Power : 0
   Likes Received
   29
   Likes Given
   4

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   asante jembe, ila tuzidi kuwaelimisha akina mama na wazee ili wajitambue na waujue ukweli kuhusu nchi yao. big up mkuu.

  7. ZeMarcopolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th May 2008
   Posts : 13,330
   Rep Power : 141699899
   Likes Received
   5771
   Likes Given
   5446

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Naomba MODs waiweke hii barua ya mjomba sticky ili mjomba akitoka kanisani aikute.
   Natanguliza shukurani.
   "To greed, all nature is insufficient"

  8. everybody's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th October 2010
   Location : Everywhere
   Posts : 337
   Rep Power : 1037
   Likes Received
   101
   Likes Given
   30

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Dah! Kweli wewe mchawi

  9. Juma123's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 23rd January 2012
   Posts : 152
   Rep Power : 531
   Likes Received
   33
   Likes Given
   90

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Ujumbe Mzuri, ila kuchanganya dini umeharibu, Bahati wenzetu Hawana sera ZA kujilipua, vinginevyo kesho tungesikiia maandamano ya ndanda. Tehe tehe tehe

  10. Skype's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Posts : 7,254
   Rep Power : 2201
   Likes Received
   1537
   Likes Given
   996

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Mkuu, umenifikirisha sana beyond my thinking capacity. Nimeshtuka sana kuujua ukweli wa kwa nini watanzania tupo hivi tulivyo. Imeniuma sana.

  11. 4change's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th March 2012
   Posts : 531
   Rep Power : 601
   Likes Received
   100
   Likes Given
   103

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   duh mkuu asante.umenena.salute.
   Inauma sana kwakweli.anyway,solutiön to 'a problem' begins by understanding the presence of that particular problem,going a step further by uncovering its root causes,and formulating plausible/feasible and practical ways/plans of combating it...immediate, short-term,intermediate and long-term plans......napita tu wazee,ngoja ntulize mawazo kidogo maana nchi tunakera,watu wenye akili zao vichwani na kwenye actions zao na sio kwenye vyeti kama kina mponda na wengineo wengi,wanatushangaa sana watanzania.

  12. Mlosi Mtulutumbi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th October 2010
   Posts : 685
   Rep Power : 759
   Likes Received
   228
   Likes Given
   247

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Shukrani sana kwa mlioipitia post hii, tafadhari isambazeni ili watu wengi zaidi wasome. Najua watanzania tunapenda vipost vifupi vifupi hasa vinavyomjadili mtu mmojammoja ambavyo kimsingi havileti tija saana na natambua ni wachache tu wanaopenda kufikirisha akili yao wanaweza kusoma. Ukombozi wa fikra huanzia na kutambua kwa nini unahitaji ukombozi,basi kaka dada, mwanaume , mwanamke isambaze post hii kwa kuwa inawalenga watanzania woote, japo mjomba daktari ametumika kufikisha ujumbe! Asanteni
   Kufanya Jambo Baya ni Dhambi, twafahamu hilo, Ukiwa na nia ya Kutenda au kuamua jema badala yake ukatenda jambo baya kwa Kuogopa kukaripiwa na wafanya Mabaya ni Unafiki na Ufukara wa Fikra!

  13. Mzee Msemakweli's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 12th October 2010
   Posts : 151
   Rep Power : 598
   Likes Received
   30
   Likes Given
   48

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Mkuu wangu maneno yako yanauma sana. Mungu atuokoe ili Wananchi waelewe nini mnadai.

  14. vimon's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 3rd April 2008
   Posts : 161
   Rep Power : 941
   Likes Received
   156
   Likes Given
   18

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Mtulumbi kwa Mara kwanza umenifanya nitoe machozi,yametutokea mengi lakini shukrani ya watanzania ni kututukana niko pembeni na mjomba,tumewasemehe lakini hatutasahau waliotukashifu kwenye huu mgomo.
   invinsible nakuomba uweke sticky
   Challenges are what make life interesting and overcoming them is what makes life meaningful

  15. Nyalotsi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st July 2011
   Posts : 4,591
   Rep Power : 5292208
   Likes Received
   1593
   Likes Given
   1291

   Default

   Quote By ZeMarcopolo View Post
   Naomba MODs waiweke hii barua ya mjomba sticky ili mjomba akitoka kanisani aikute.
   Natanguliza shukurani.
   acha unafiki we ni mmoja ya waliokuwa wanatutukana mtandaoni eti maadili ya udaktari. Tutakutana labour, Mungu atanisamehe kwa staili ntakayokuwa nafanyia kazi. Sie wajinga,wabinafsi,tusio wazalendo, tulogeuka wanasiasa tumekubali. Kuna kazi nyingi nilikuwa nazifanya kwa upendo wa watanganyika wenzangu kumbe mnatuenjoy tu.

  16. vimon's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 3rd April 2008
   Posts : 161
   Rep Power : 941
   Likes Received
   156
   Likes Given
   18

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   Quote By Nyalotsi View Post
   acha unafiki we ni mmoja ya waliokuwa wanatutukana mtandaoni eti maadili ya udaktari. Tutakutana labour, Mungu atanisamehe kwa staili ntakayokuwa nafanyia kazi. Sie wajinga,wabinafsi,tusio wazalendo, tulogeuka wanasiasa tumekubali. Kuna kazi nyingi nilikuwa nazifanya kwa upendo wa watanganyika wenzangu kumbe mnatuenjoy tu.
   Tumsamehe nyalutosi ila walitukwaza sana,mara nyingi wajuwa jinsi gani tunafanya kazi kwa moyo,hivi wanapokuja unakuta hakuna dawa unafanya juu nchini unamwombea za mgojwa mwingine au unabadili regime ilikumuokoa,matusi tuliyoyapata yametujerui na kutufunza kuwa watanzani wanatukejeli.
   nawasamehe kwa sababu wengi walileta sias wakiamini tumetunafanya maigizo na ni maslahi binafsi.
   Hippocratic Oath
   I swear by Apollo, the healer, Asclepius, Hygieia, and Panacea, and I take to witness all the gods, all the goddesses, to keep according to my ability and my judgment, the following Oath and agreement:


   To consider dear to me, as my parents, him who taught me this art; to live in common with him and, if necessary, to share my goods with him; To look upon his children as my own brothers, to teach them this art; and that by my teaching, I will impart a knowledge of this art to my own sons, and to my teacher's sons, and to disciples bound by an indenture and oath according to the medical laws, and no others.
   I will prescribe regimens for the good of my patients according to my ability and my judgment and never do harm to anyone.
   I will not give a lethal drug to anyone if I am asked, nor will I advise such a plan; and similarly I will not give a woman a pessary to cause an abortion.
   But I will preserve the purity of my life and my arts.
   I will not cut for stone, even for patients in whom the disease is manifest; I will leave this operation to be performed by practitioners, specialists in this art.
   In every house where I come I will enter only for the good of my patients, keeping myself far from all intentional ill-doing and all seduction and especially from the pleasures of love with women or with men, be they free or slaves.
   All that may come to my knowledge in the exercise of my profession or in daily commerce with men, which ought not to be spread abroad, I will keep secret and will never reveal.
   If I keep this oath faithfully, may I enjoy my life and practice my art, respected by all humanity and in all times; but if I swerve from it or violate it, may the reverse be my life
   hichi kiapo kinawalinda lakini kina mlinda na daktari. Naomba umsamehe nakuhisi collegue.
   Challenges are what make life interesting and overcoming them is what makes life meaningful

  17. Nyalotsi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st July 2011
   Posts : 4,591
   Rep Power : 5292208
   Likes Received
   1593
   Likes Given
   1291

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   vimon i wont violate any of the oath, lakini kumbuka tunatumia fedha zetu kuwanunulia dawa,kuwasafirisha wanapokosa nauli kwenda kwenye centre za juu ni sie tunaoorganize wapate nauli. Wake zao hawaji na pamba,gloves labour tunachukua jukumu la kuwaombea kwa wagonjwa wengine au kuwanunulia. Tunawanunulia vyakula kwa hela zetu chache tunazopata kwa huruma ili waendelee kuishi tufurahi wote! Watu tunatembea na canula,gloves zetu mfukoni kwa kujua hali za hospitali zetu na kuwasaidia bure! Tunashughulika hata extra time wakati hauko call na haina malipo ili kusaidiana na watanganyika wenzetu. Are all these in hippocratic oath? Tunapina migongo yetu kwa kuinama kuwahudumia, tunapigwa na psychiatric patients bila malipo, leo hii kuichalenge serikali tunaonekana wajinga kiasi hiki kweli? Tunaitwa magaidi, pirates kweli dr? Tukiwaambia hawa watendaji ndo wanaidhinisha matumizi na manunuzi mabovu,tunaambiwa ni kwa sababu ni wabinafsi! Tumesomeshwa bure na kodi za wananchi,hivi wazazi wangu hawalipi hizo kodi? Mimi mwenyewe silipi hiyo kodi? Nani anajua kuwa deni langu bodi ya mikopo ni zaidi ya yule wa bcom? Wanatuambia nchi haina hela,mbona watoto wao wanashusha mahekalu baada ya baba zao kuingia madarakani? Pesa wametoa wapi wanazoruka hewani kila leo,ila za dawa na gloves hakuna? Ndo maana nimesema Mungu anitangulie nifanye majukumu yaliyomo kwenye mkataba na my oath!

  18. Nyalotsi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st July 2011
   Posts : 4,591
   Rep Power : 5292208
   Likes Received
   1593
   Likes Given
   1291

   Default

   Quote By Mzee Msemakweli View Post
   Mkuu wangu maneno yako yanauma sana. Mungu atuokoe ili Wananchi waelewe nini mnadai.
   nani wa kuwapa hiyo elimu? Kama waandishi wa habari walihongwa wakawa watu wa kututafutia wazee wasio na fikra muhimu ili tu watutukane madaktari. Wengine walithubutu hata kututukana wao wenyewe kwa kutojua kuna siri zao watu wanatumia ethics kuzihifadhi, nawashukuru hata waliovunja hizo ethics.

   Hivi kweli tunaitwa WAZANDIKI kwa kusimamia ukweli? Unadhani hao wananchi wataelimishwa na nani kama wanaotoa habari wametumia mgogoro huu wao kujinufaisha? AAAAAAAAAAH KICHWA KINAUUMAAA!

  19. Waberoya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd August 2008
   Location : Busia-Uganda
   Posts : 7,355
   Rep Power : 3102566
   Likes Received
   2461
   Likes Given
   4498

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   best post !!

   100% agree in every your world and concept

   asante kaka
   You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

  20. Jackbauer's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th October 2010
   Location : EAST LONDON
   Posts : 5,868
   Rep Power : 31966
   Likes Received
   1837
   Likes Given
   350

   Default Re: Salaam zangu zikufikie ...mjomba daktari!

   mpwa amesikika


  Page 1 of 2 12 LastLast

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...