JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

  Report Post
  Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast
  Results 61 to 80 of 85
  1. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Napendekeza nadharia tete (Hypotheses) zifuatazo, lengo kuu ikiwa ni kutupa sote nafasi ya kuzipima nadharia hizi tete, kwa kutumia uzoefu wetu na uelewa wetu juu ya utamaduni wa CCM, hasa kwa kuzingatia matukio na mazingira ya nyakati hizi. Matokeo ya zoezi hili la kupima nadharia tete hizi yatatoa majibu ya aina mbili: Aidha majibu - KWELI, hivyo kufanya nadharia hizi tete kusimama, au majibu - SIO KWELI, hivyo kuziangusha hizi nadharia tete. Nadharia tete zipo nne kama ifuatavyo:

   I. Ingawa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM halazimiki atoke miongoni mwa wajumbe wa NEC na pia suala hili halipo kikatiba, Chama Cha Mapinduzi hakina utamaduni wa kuteua wagombea wake wa Urais ambao sio miongoni mwa wajumbe wa NEC.

   II. Ili mwana CCM awe na nafasi nzuri ya kuteuliwa kubeba bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, inamlazimu mwanachama huyu, agombee na ashinde uchaguzi wa wajumbe wa NEC kwenye uchaguzi wa ndani wa CCM mwaka huu wa 2012. Kwa kufanya hivyo, mwana CCM huyo atakuwa ni mjumbe wa NEC-CCM ifikapo mwaka wa uchaguzi mkuu, 2015, hivyo kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuteuliwa kubeba bendera ya CCM mwaka 2015.

   III. Wanachama wa CCM wenye malengo ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015, ambao kwa sasa wanashikilia nafasi mbili kwa pamoja – yani ubunge na ujumbe wa NEC, chini ya mabadiliko ya katiba ya CCM ya hivi karibuni, itawalazimu aidha waachie nafasi zao za ubunge na kubakia wajumbe wa NEC, au waendelee na Ubunge na waachane na ujumbe wa NEC, huku wakisubiri Baraka za Mwenyekiti wa CCM Taifa za kuwateua kuwa wajumbe wa NEC, kupitia zile nafasi kumi, miezi michache kabla ya mchakato wa kutafuta mgombea Urais kupitia CCM, ili mwanachama huyo awe katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda katika kinyang’anyiro hicho May, 2015.

   IV. Kwa maana hii, Mchezo wote wa kinyang’anyiro cha Urais kupitia CCM mwaka 2015, umebadilika kutokana na mabadiliko ya katiba ya CCM, hivyo tutarajie majina mapya kutawala mbio hizi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa CCM Novemba mwaka huu wa 2012, majina ambayo wengi hatukuyatarajia.
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  2. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
   Kwani haya mabadiliko tayari yamekuwa rasmi kabla ya Katiba yenyewe kufanyiwa mabadiliko na Mkutano Mkuu?
   Ndio hapo sasa. Kwani Nape anavyozungumza ni kama kinachosubiriwa ni formality tu, na yeye hajazungumza lolote kuhusu Mkutano Mkuu wa CCM, bali NEC. Iwapo mabadiliko haya yatahitaji kupata baraka za mkutano mkuu, je ina maana kwamba Mkutano Mkuu wa October 2012, utakuwa na agenda ya mabadiliko ya katiba ya CCM, nje ya shughuli yake ya kwenda kuteua wajumbe wa NEC kule dodoma?

   Kwa kweli CCM bado ina kazi kubwa mbeleni.
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  3. Bulesi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th May 2008
   Posts : 5,818
   Rep Power : 32129378
   Likes Received
   1241
   Likes Given
   190

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Mchambuzi View Post
   Upo sahihi. Na tukumbuke kwamba wabunge walioingia NEC kupitia Bunge ni watu kama Sitta, Mwakyembe na wengine wachache. Hawa walichagua kugombea kupitia bunge tofauti na wenzao ambao walitumia njia nyingine kama zile za kugombea mikoani na pia vile vile kupitia kura za mkutano mkuu wa CCM taifa. Kwa mtazamo wangu, mtu kama Sitta ataendelea kuwa mbunge na Mjumbe wa NEC kwani sioni akipigiwa kura za hapana na wabunge iwapo atawania nafasi hiyo mwaka huu.
   I can see Lowassa using this avenue to become a NEC member very successfully because the number of MPS is manageable and he knows their weakness!! Hivyo basi kama mabadiliko haya yalikuwa kumuengua asiingie Nec basi they will have to go back to the drawing board.!

  4. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Bulesi View Post
   I can see Lowassa using this avenue to become a NEC member very successfully because the number of MPS is manageable and he knows their weakness!! Hivyo basi kama mabadiliko haya yalikuwa kumuengua asiingie Nec basi they will have to go back to the drawing board.!
   Hilo linawezekana kwani nafasi kumi za NEC kupitia bunge ni nyingi kwa mtu aliyejipanga. Lakini tujiandae kuona mpambano ambao haujawahi kutokea kwa sababu miaka ya nyuma, viongozi wengi walikuwa hawajishughulishi na NEC kupitia nafasi hizi.
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  5. Mtazamaji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th February 2008
   Location : global village
   Posts : 5,978
   Rep Power : 1894
   Likes Received
   1350
   Likes Given
   2657

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Ngoja niwe mtabiri wa Nyota ya CCM na future yake

   Inawezekana JK anataka kufanya mabadiliko akilini mwake nia ikiwa ni labda moja au yote kati ya haya
   • Kupunguza nguvu ya makundi na mgawanyiko ndani ya CCM .
   • Anataka kuwa Mgombea wa CCM awe Underdog not from top layer kama ulivyosema ( eg Asha Rose Migiro, )
   • Kutumia mbinu zilizotumika kumdiss sitta bungeni Indirectly. Anaweza kuwa anataka kukwepa tatizo na kupenda sasa mgombea atoke Zanzibar. Bungeni iltumiika zamu ya wanawake. Hapa kuna tatizo linaweza kufunikwa kwa style ya sasa tuwape nafasi upende mwingine wa mmuungano ....... Bila shinikizo au msukumo fulani naturally hilo la Zanzibar haliwezi kutokea 2015

   Faida na hasara

   kuweka "underdog" kunaweza imarisha umoja wa chama unaolega lega lakini hatakuwa na uthubutu , ubavu wala uwezo hata wa kufanya japo sanaaa kama alizofanya Kikwete za "kuwambia" kina Mramba na Yona wacheze "filamu" ya ufisadi mahakamani.

   So kama JK alivyokuwa mwepesi wa Kusema mwacheni MKapa apumzike, Huyo anayetafutwa sasa kwenye mfumo huu mpya ni yule ambaye sijui niseme ni best-worst zaidi ya JK .(If your view JK is better basi anayetafutwa atakuwa worst na IF JK wa worse to you huyu atakuwa "worsset "lol kuchapia kunaruhusiwa ......

   Sabbau hataweza either kuwakomoa au kuwafikisha kihalali mahakamani baadhi ya vigogo na hata kuwa a uwezo hata wa kufanya sanaa kama za kina Yona na mramba alizofanya JK.

   So kichama inaweza kuwa ni move nzuri ya kujivua gamba lakini kiungozi wa serikali........... mhhhh

   Mtazamaji
   Mchambuzi likes this.

  6. Nguruvi3's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st June 2010
   Location : Kidabashi-Dongobeshi
   Posts : 8,373
   Rep Power : 367131656
   Likes Received
   14072
   Likes Given
   8384

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Mchambuzi,
   Kuna kipengele kimoja kinachoathiri nadharia zote 4 kama ulivyoziweka. Sina uhakika kama nitakuwa nimekielewa vema, nisahihishwe kama nitakuwa nimeelewa kinyume.

   Kuna wajumbe 10 wa NEC wa kuteuliwa na mwenyekiti.
   Nadharia I : Mgombea anaweza kuteuliwa na mwenyekiti akijua kuwa ni mgombea mtarajiwa.
   Hili litaendeleza utamaduni wa mgombea kutoka NEC

   II:Mwenyekiti anaweza kumshawishi asigombee wilayani ili ampe nafasi kati ya zile 10. Hili litakuwa ni mkakati wa kulinda heshima ya mtarajiwa endapo itatokea vinginevyo huko wilayani.
   Haitaleta maana mtu aliyeshindwa Wilayani, kuteuliwa katika 10 na halafu awe mgombea

   III: Ni kama I na II

   IV: Kwa vile I,II,III vinawezekana, basi uwezekano wa kupata jina jipya nje ya NEC au wasiozoeleka ni mdogo.

   Na mwisho niulize, kwanini mwenyekiti apewe nafasi 10 sawa na nafasi za jumuiya kama UVCCM. Hapa Demokrasia inafanyaje kazi.
   Last edited by Nguruvi3; 16th February 2012 at 18:17.
   Tanzania kwanza, Tanganyika Kabla-Mchambuzi(JF)

   No Tangayika, no stable Tanzania

  7. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Nguruvi3 View Post
   Kuna wajumbe 10 wa NEC wa kuteuliwa na mwenyekiti. Nadharia I : Mgombea anaweza kuteuliwa na mwenyekiti akijua kuwa ni mgombea mtarajiwa. Hili litaendeleza utamaduni wa mgombea kutoka NEC.
   Nakubaliana na wewe. Ni vigumu sana kwa CCM kumpitisha mgombea ambae hatokani na wajumbe wa NEC. Ingawa Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano inasema kwamba moja ya vigezo vya kumpata mgombea urais ni kwamba ni lazima awe na sifa zinazolingana na zile za mbunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi, historia inatuonyesha kwamba uzoefu wa uongozi ndani ya Chama huwa ni kigezo kikubwa na kinaangalia mbali zaidi ya 'ubunge au ujumbe wa baraza la wawakilishi'. Kigezo kikubwa huwa ni Uzoefu wa Chama kupitia nafasi ya NEC.

   Katika vinyang'anyiro kwa kutafuta mgombea Urais, wagombea wote wanaopita hadi ngazi za mwisho kabisa huwa wanatokana na wajumbe wa NEC. Kwa mfano, moja ya hoja zilizomwangusha Professor Mwandosya ambazo zilikuwa zinajengwa na makundi yote yaliyokuwa yanashindana katika uchaguzi wa mwaka 2005 ilikuwa ni hoja kwamba Mwandosya hana uzoefu wa kutosha ndani ya Chama, ingawa tayari alikuwa ni Mbunge kwa muda. Ndio maana licha ya kushika nafasi ya tatu, Mwandosya alipata kama 6% ya kura zote, kwani wajumbe wa mkutano mkuu waliaminishwa kwamba hana uzoefu ndani ya CCM, na kweli wengi walikuwa hawamjui. Salim akipata zaidi ya 30% na Kikwete akinyakua karibia 60%.

   II:Mwenyekiti anaweza kumshawishi asigombee wilayani ili ampe nafasi kati ya zile 10. Hili litakuwa ni mkakati wa kulinda heshima ya mtarajiwa endapo itatokea vinginevyo huko wilayani. Haitaleta maana mtu aliyeshindwa Wilayani, kuteuliwa katika 10 na halafu awe mgombea.
   Pia, nakubaliana na wewe kwa hili. Iwapo nadharia ya kwanza ina mashiko, kitachofuata lazima iwe hiki unachokisema, kwani ikitokea Mwenyekiti akawa na jina lake analotaka lipite mwaka 2015, ni muhimu ufanyike mpango mahsusi wa kumwingiza mtu huyo kwenye NEC, hasa kupitia zile nafasi kumi ambazo mwenyekiti ana uwezo wa kuzitumia. Vinginevyo iwapo mtu huyo tayari atakuwa anajulikana leo hii yeye ni nani kwa jina, ni rahisi sana kwa wengine wenye nia na 2015 kufanya kila hila ili asipite huko wilayani au popote pale atakapogombea ujumbe wa NEC, kwani mtu huyo akianguka NEC ni pigo kubwa kwa mkakati wa 2015,kwani hoja itajengwa kwamba hakubaliki ndan ya Chama n.k. Hivyo njia pekee ya kumjenga na kumjengea heshima ni kwa kumteua kupitia zile nafasi kumi alizonazo mwenyekiti wa CCM taifa.

   IV: Kwa vile I,II,III vinawezekana, basi uwezekano wa kupata jina jipya nje ya NEC au wasiozoeleka ni mdogo.
   Hapa kidogo mtazamo wangu ni tofauti na wako. Kwa mtazamo wangu, kama I, II na III vina mashiko, basi kuna uwezekano mkubwa sana kwamba mgombea atakaeteuliwa 2015 atakuwa mtu ambae wengi hawakumtarajia, lakini lazima atatokana na wajumbe wa NEC walioteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa mwaka 2012.

   Na mwisho niulize, kwanini mwenyekiti apewe nafasi 10 sawa na nafasi za jumuiya kama UVCCM. Hapa Demokrasia inafanyaje kazi?
   Sababu kubwa ya Mwenyekiti kupewa nafasi kumi, kwa mtazamo wangu huwa ni kwa nia njema kwamba pengine chama kinaweza kubaini kwamba kuna mtu kwenye jamii ambae ni muhimu sana na anayeweza kuwa mtaji wa CCM lakini kwa vile hakugombea NEC, basi hawezi kuingia katika vikao muhimu vya maamuzi, au kuteuliwa kushika nafasi muhimu ndani ya chama n.k. Hivyo Mwenyekiti hupewa nafasi hizi kumi kikatiba ili kutimiza lengo hilo. Lakini in practice, mimi sioni kama utaratibu huu huwa unatumika kama ilivyokusudiwa, na badala yake huwa unatumika zaidi kulipana fadhila. Ni kama zile nafasi kumi za ubunge ambazo Rais anazo, ni mara chache sana wateule wote kumi wakawa ni kwa manufaa ya serikali na chama chake, zaidi huwa ni kulipana fadhila au kubebana kisiasa, kama njia ya kusaidia kuishi/kupata posho/kutokuwa idle n.k. Lengo ni zuri in theory lakini in practice sidhani teuzi zote huwa ni kwa manufaa ya serikali/chama (CCM).
   Last edited by Mchambuzi; 19th February 2012 at 03:19.
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  8. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Pasco View Post
   Nadhani ujumbe wa nec utakuwa sio dili tena!. Na kwenye katiba mpya tutapendekeza mawaziri wasiwe wabunge ili tuweke professionals na wabunge wabaki ni watumishi wa watu only!. Rushwa ya uongozi itapungua"
   Mkuu Pasco,

   Matukio ya sasa huko dodoma yanafufua hoja nyingi katika mjadala huu; Hili la wagombea nafasi za uongozi kuzidi watu elfu mbili, na pia hili la wasomi kufurika kwa wingi kuwania nafasi hizo ndani ya Chama, lakini vile vile hizi tetesi za majina kadhaa kukatwa, je ujumbe wa NEC bado sio dili tena?
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  9. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
   Kwani haya mabadiliko tayari yamekuwa rasmi kabla ya Katiba yenyewe kufanyiwa mabadiliko na Mkutano Mkuu?
   Hili ni swali la siku nyingi lakini sasa ndio naona umuhimu wake; mabadiliko haya yameishia huko huko NEC na Kamati kuu na ni utaratibu huu mpya ndio unatumika sasa katika kupata wajumbe wa NEC huko dodoma hivi tunavyozungumza; ulitabiri vyema kuhusu mabadiliko ya kuongeza nguvu za wanachama vis-a-vis yakusaidia house keeping;
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  10. Bongolander's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th July 2007
   Location : Tandale
   Posts : 5,256
   Rep Power : 1781
   Likes Received
   1705
   Likes Given
   246

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Mchambuzi View Post
   Mkuu Pasco,

   Matukio ya sasa huko dodoma yanafufua hoja nyingi katika mjadala huu; Hili la wagombea nafasi za uongozi kuzidi watu elfu mbili, na pia hili la wasomi kufurika kwa wingi kuwania nafasi hizo ndani ya Chama, lakini vile vile hizi tetesi za majina kadhaa kukatwa, je ujumbe wa NEC bado sio dili tena?
   I am just curious about Philip Mangula. Looks like Rostam is not in play now, labda anaweza kuwa mjumbe.

   Mchambuzi nashindwa kufahamu hasa vyombo vya chama ni vipi vye nguvy zaidi na vinafanya maamuzi yake kwa njia gani.

   Kama unaweza kunisaidia ningependa kujua NEC ya CCM ni nini na nani members, CC ya CCM ni nini na members wake ni wapi, na zina tofauti gani. Na kwanini rais "hawezi" kutoka nje ya hapo.

   Lakini uchaguzi uliopita naona ilikuwa very clear kuwa pamoja na sarakasi zote ndani ya CCM, rais wa Tanzania si lazima atokane na NEC ya CCM. Bila uchakachuzi nadhani Slaa angekuwa rais.
   Mchambuzi likes this.

  11. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Bongolander,

   I am just curious about Philip Mangula. Looks like Rostam is not in play now, labda anaweza kuwa mjumbe.
   Kwa mtazamo wangu, Mangula would never serve CCM from Lumumba katika nyakazi hizi hata akiitwa kesho kwani CCM Lumumba imekuwa Taasisi ya Fitina, Majungu na Madili (Ulaji), na katika haya yote, Mzee Mangula hatoshi;

   Mchambuzi nashindwa kufahamu hasa vyombo vya chama ni vipi vye nguvy zaidi na vinafanya maamuzi yake kwa njia gani.

   Kama unaweza kunisaidia ningependa kujua NEC ya CCM ni nini na nani members, CC ya CCM ni nini na members wake ni wapi, na zina tofauti gani. Na kwanini rais "hawezi" kutoka nje ya hapo.

   Lakini uchaguzi uliopita naona ilikuwa very clear kuwa pamoja na sarakasi zote ndani ya CCM, rais wa Tanzania si lazima atokane na NEC ya CCM. Bila uchakachuzi nadhani Slaa angekuwa rais.
   Mkuu Bongolander, ili tuweze kuelewa umungu wa NEC, pengine tujaribu kuchimba zaidi dudu hili linaloitwa CCM ili tuelewe kwa mapana zaidi nguvu ya NEC; CCM bado inashika hatamu ingawa hivi sasa hii dhana inaonekana imepitwa na wakati ndani ya mfumo wa vyama vingi; Lakini in practice, bado Chama kinashika hatamu. Nianze na maneno ya Msekwa ambayo kwa kiasi kikubwa bado ni relevant katika siasa za leo. Msekwa anasema haya katika kitabu chake: Msekwa, P (1977): Towards Party Supreme:

   *************
   “Halmashauri kuu ya TANU imekuwa siku zote ni kiungo muhimu cha uunganishi. Vyombo vikuu vya chama ni Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu…Lakini Halmashauri Kuu ndio yenye nguvu za Chama. Pale katiba ya Chama ilipofanywa kuwa sehemu ya katiba ya nchi, Chama hapo kikawa kimejijengea uhalali wa kikatiba. Moja katika nguzo kuu katika utawala wa kisiasa ni kuwa na chama kikubwa ama kiwe kimehodhi au la; kwa sababu muendesho wa siasa za kisasa hautakuwa rahisi pale patapokosekana jamii iliyoungwa pamoja katika mfumo wa chama. Lakini pamoja na na nafasi kubwa inayochukua chama katika maendesho ya kisiasa na kiserikali, mara nyingi huwa panakosekana nguvu za kisheria, hadhi na dhamana ya chama, ikiwa ni pamoja na wale walio madarakani. Katika hili, basi kwa kuifanya TANU kuwa na uhai wa kikatiba, Katiba ya Muda ya 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweweka historia kwa kuanzisha dhana mpya, hasa katika mtizamo wa kisheria”

   Pius Msekwa, 1977.
   **************
   Pamoja na kwamba nchi ilipata katiba yake ya kwanza ya kudumu miaka 12 baade i.e. 1977 baada ya kuwa na katiba ya muda ya 1965, suala la CCM kushika hatamu (hivyo umungu wa wajumbe wa NEC), halikubadilika na badala yake, CCM ndio ikajikita zaidi katika anga za umungu, kwani sasa katiba ya CCM (ASP+TANU) 1977 ikawa merged na katiba ya nchi (1977), huku katiba ya CCM ikiwa supreme to katiba ya Nchi, hence umungu wa wajumbe wa NEC. Kwa mfano, rejea jinsi gani Jumbe, Maalim Seif, Ahmed Rashid Mohamed (Mbunge wa sasa CUF), walipofukuzwa uanachama wa chama cha siasa (CCM) kwa mujibu wa Katiba ya Chama na kupoteza nyadhifa zao za ubunge n.k, na Katiba ya nchi haikuweza kuwaokoa; Lakini tazama leo sakata la kina kafulila na Ahmed Rashid Mohamed, wote wametimuliwa uanachama CUF na NCCR lakini kwa vile katiba ya nchi haisema hatima ya mbunge ni nini pale anapovuliwa uanachama, kesi zao zitaendelea kupigwa tarehe mpaka katiba mpya itakapozaliwa, hoping kwamba pengine italitazama hili; ndio maana hata leo, ukimfukuza mtu kama Sitta, Mwakyembe kwenye chama kama vile kamati ya Msekwa, Mwinyi na Kinana ilivyokuwa inashinikizwa ije na mapendekezo hayo, kwa wakati ule, wote hawa wangeendelea tu kuwa wabunge kwani katiba ya nchi imepwaya katika hilo kwa sababu ilitungwa kuitumikia CCM and nothing else;

   Vile vile tutazame hotuba ya Mwalimu mwaka 1974 iliyotoka kwenye gazeti la Daily News ambayo pia inazungumzia mambo ambayo leo hii bado ni relevant when it comes to CCM na utawala wa nchi:

   “…kwa kuwa chini ya katiba ya chama kimoja, TANU imeshika hatamu. Inaweza kutoa maagizo ya sera za jumla kwa serikali sera ambazo zinatakiwa zitekelezwe kwa ajili ya Maendeleo ya nchi, na kinaweza kuwa na nguvu kutoa maagizo maalum juu ya mambo ambayo yanahitajika yapewe kipaumbele katika jambo lolote la uhai wa taifa. Zaidi ya hayo, itaweza kuitisha Baraza la Mawaziri, Waziri ye yote au mtendaji ye yote wa serikali, kujieleza juu ya shughuli zao au kutofanikiwa kwao katika utendaji wao”

   Natumaini sasa upo kwenye nafasi nzuri ya kuelewa “WHY THE NEC RUSH” (nimeiba dhana ya GOLD RUSH).
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  12. #71
   Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,294
   Rep Power : 17073796
   Likes Received
   14255
   Likes Given
   2650

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Nitaenda mbali zaidi na kusema uwaziri pia. Na mpaka sasa, kwa mtu kuwa rais hata kama hupo kwenye NEC na ukubwa wa CCM/ serikalini, utafanyiwa fast tracking.

   Nakumbuka circa 1984 tulipoletewa Ally Hassan Mwinyi kama "rais wa muda wa Zanzibar" kulikuwa na uncle mmoja wa Usalama wa Taifa alikuwa anatuambia "huyo ndo rais wenu ajaye".

   Ukweli ni kwamba CCM ni chama cha top down, ukweli mwingine ni kwamba kwa mazingira yetu ya leo, kupanda CCM mpaka uwe juu ni lazima ufanye uchafu. Kutoka hapo tunapata ukweli mwingine kwamba kiongozi safi - ambaye yuko lakini hajulikani na wala hawezi kupanda ngazi katika CCM- hawezi kupatikana kutoka CCM.
   Mchambuzi, andate and Nyakipambo like this.
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  13. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Kiranga View Post
   Nitaenda mbali zaidi na kusema uwaziri pia. Na mpaka sasa, kwa mtu kuwa rais hata kama hupo kwenye NEC na ukubwa wa CCM/ serikalini, utafanyiwa fast tracking.

   Nakumbuka circa 1984 tulipoletewa Ally Hassan Mwinyi kama "rais wa muda wa Zanzibar" kulikuwa na uncle mmoja wa Usalama wa Taifa alikuwa anatuambia "huyo ndo rais wenu ajaye".

   Ukweli ni kwamba CCM ni chama cha top down, ukweli mwingine ni kwamba kwa mazingira yetu ya leo, kupanda CCM mpaka uwe juu ni lazima ufanye uchafu. Kutoka hapo tunapata ukweli mwingine kwamba kiongozi safi - ambaye yuko lakini hajulikani na wala hawezi kupanda ngazi katika CCM- hawezi kupatikana kutoka CCM.
   Mkuu kiranga,
   Nimevutiwa sana na mtazamo wako huo nilio highlight kijani; Mimi nimekuwa na mtazamo kwamba mgombea wa CCM 2015 hawezi kuwa mtu ambae atakuwa mgeni masikioni mwetu kwa sababu kuu moja - CCM haina muda wa kutosha lakini vile vile resources za kutosha kumtembeza mtu mpya nchi nzima ajulikane kwa wananchi huku wakishawishiwa ndiye chaguo bora; Hata Mwalimu pamoja na nguvu zake zote mwaka 1995 alilazimika kumtembeza Mkapa nchi nzima lakini aliambuliwa ushindi mdogo sana tofauti na ilivyotarajiwa, na moja ya sababu kubwa ilikuwa ni ugeni wa mgombea katika medani za siasa in the eyes of watanzania walio wengi. Kwa 2015, kuleta jina jipya itakuwa ni taabu sana na inaweza ndio ikawa final seal ya kifurishi cha CCM kuelekea benchi la upinzani;

   kama utakubaliana na mtazamo wangu huu, kauli yako kwamba:

   ...Kutoka hapo tunapata ukweli mwingine kwamba kiongozi safi - ambaye yuko lakini hajulikani na wala hawezi kupanda ngazi katika CCM- hawezi kupatikana kutoka CCM
   Je ina maana kwamba katika majina haya yanayotajwa tajwa hakuna atakayeweza kufika pale juu na akabakia kuwa msafi na tayari kupambana na mgombea wa Chadema?
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  14. #73
   Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,294
   Rep Power : 17073796
   Likes Received
   14255
   Likes Given
   2650

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Mchambuzi View Post
   Mkuu kiranga,
   Nimevutiwa sana na mtazamo wako huo nilio highlight kijani; Mimi nimekuwa na mtazamo kwamba mgombea wa CCM 2015 hawezi kuwa mtu ambae atakuwa mgeni masikioni mwetu kwa sababu kuu moja - CCM haina muda wa kutosha lakini vile vile resources za kutosha kumtembeza mtu mpya nchi nzima ajulikane kwa wananchi huku wakishawishiwa ndiye chaguo bora; Hata Mwalimu pamoja na nguvu zake zote mwaka 1995 alilazimika kumtembeza Mkapa nchi nzima lakini aliambuliwa ushindi mdogo sana tofauti na ilivyotarajiwa, na moja ya sababu kubwa ilikuwa ni ugeni wa mgombea katika medani za siasa in the eyes of watanzania walio wengi. Kwa 2015, kuleta jina jipya itakuwa ni taabu sana na inaweza ndio ikawa final seal ya kifurishi cha CCM kuelekea benchi la upinzani;

   kama utakubaliana na mtazamo wangu huu, kauli yako kwamba:   Je ina maana kwamba katika majina haya yanayotajwa tajwa hakuna atakayeweza kufika pale juu na akabakia kuwa msafi na tayari kupambana na mgombea wa Chadema?
   Majina yote yanayotajwa tajwa yako juu tayari.

   Kuna mtu ambaye anatajwa tajwa ambaye hajapata ujumbe wa NEC au uwaziri?
   Mchambuzi likes this.
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  15. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Kiranga View Post
   Majina yote yanayotajwa tajwa yako juu tayari.

   Kuna mtu ambaye anatajwa tajwa ambaye hajapata ujumbe wa NEC au uwaziri?
   Naposema JUU maana yangu ni kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM May 2015;
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  16. #75
   Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,294
   Rep Power : 17073796
   Likes Received
   14255
   Likes Given
   2650

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Mchambuzi View Post
   Naposema JUU maana yangu ni kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM May 2015;
   Ndiyo na mimi nimekuuliza kuna mgombea yeyote anayeongelewa CCM seriously ambaye hajawahi kuwa na uwaziri au ujumbe wa NEC?

   Ambaye anaweza kusema mie sijachafuliwa na siasa za kupanda ngazi CCM?
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  17. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Kiranga View Post
   Ndiyo na mimi nimekuuliza kuna mgombea yeyote anayeongelewa CCM seriously ambaye hajawahi kuwa na uwaziri au ujumbe wa NEC?

   Ambaye anaweza kusema mie sijachafuliwa na siasa za kupanda ngazi CCM?
   Inawezekana basi sielewi vizuri una maanisha nini hasa unaposema:

   "...Kutoka hapo tunapata ukweli mwingine kwamba kiongozi safi - ambaye yuko lakini hajulikani na wala hawezi kupanda ngazi katika CCM- hawezi kupatikana kutoka CCM."
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  18. #77
   Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,294
   Rep Power : 17073796
   Likes Received
   14255
   Likes Given
   2650

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Mchambuzi View Post
   Inawezekana basi sielewi vizuri una maanisha nini hasa unaposema:

   "...Kutoka hapo tunapata ukweli mwingine kwamba kiongozi safi - ambaye yuko lakini hajulikani na wala hawezi kupanda ngazi katika CCM- hawezi kupatikana kutoka CCM."
   Namaanisha kwamba inawezekana kukawa na mwenyekiti wa CCM wa kijiji ambaye ni safi kabisa ana nia nzuri, ana uwezo mzuri lakini hawezi kupendekezwa kwa sababu hajulikani (na kama ulivyosema pengine justification ni fair kabisa kwamba kama hajulikani kumnadi itakuwa kazi kubwa sana)

   Lakini ukweli unarudi pale pale kwamba, ukikubali kwamba kupanda ngazi CCM kunahusiana moja kwa moja na kuchafuka - huwezi kupata ubunge bila rushwa kwa mfano- basi utakubali kwamba muundo wa sasa wa CCM wa kwamba kuna umwritten rule kwamba mgombea ni lazima acheze sana kwenye NEC na uwaziri huko, inamaanisha kwamba mgombea yeyote atakayeletwa na CCM atakuwa mchafu.

   Ndo maana nashangaa sana watu wanasema "Lowassa this" "Membe that" wakati wote baba yao mmoja mama yao mmoja na wote wamepanda ngazi kwa kutumia siasa za CCM ambazo zimejaa uchafu.

   Ndo maana nasema kiongozi mzuri anayefaa hatumjui kitaifa, tunaowajua kitaifa wachafu na hawafai.

   And to a certain extent this phenomenon is transcending beyond CCM.

   Scary thought indeed.
   Mchambuzi likes this.
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  19. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Kiranga View Post
   Namaanisha kwamba inawezekana kukawa na mwenyekiti wa CCM wa kijiji ambaye ni safi kabisa ana nia nzuri, ana uwezo mzuri lakini hawezi kupendekezwa kwa sababu hajulikani (na kama ulivyosema pengine justification ni fair kabisa kwamba kama hajulikani kumnadi itakuwa kazi kubwa sana)

   Lakini ukweli unarudi pale pale kwamba, ukikubali kwamba kupanda ngazi CCM kunahusiana moja kwa moja na kuchafuka - huwezi kupata ubunge bila rushwa kwa mfano- basi utakubali kwamba muundo wa sasa wa CCM wa kwamba kuna umwritten rule kwamba mgombea ni lazima acheze sana kwenye NEC na uwaziri huko, inamaanisha kwamba mgombea yeyote atakayeletwa na CCM atakuwa mchafu.

   Ndo maana nashangaa sana watu wanasema "Lowassa this" "Membe that" wakati wote baba yao mmoja mama yao mmoja na wote wamepanda ngazi kwa kutumia siasa za CCM ambazo zimejaa uchafu.

   Ndo maana nasema kiongozi mzuri anayefaa hatumjui kitaifa, tunaowajua kitaifa wachafu na hawafai.

   And to a certain extent this phenomenon is transcending beyond CCM.

   Scary thought indeed.
   This is a very insightful analysis; Sasa nimekupata vizuri; Nakubaliana na wewe kwamba wengi ya wanaotajwa tajwa sasa kwamba ni potential for CCM 2015, lakini muhimu zaidi yeyote atakae penya May 2015, huyo atakuwa tayari atakuwa amesha chafuka;
   Kiranga likes this.
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  20. Bongolander's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th July 2007
   Location : Tandale
   Posts : 5,256
   Rep Power : 1781
   Likes Received
   1705
   Likes Given
   246

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Kiranga View Post
   Namaanisha kwamba inawezekana kukawa na mwenyekiti wa CCM wa kijiji ambaye ni safi kabisa ana nia nzuri, ana uwezo mzuri lakini hawezi kupendekezwa kwa sababu hajulikani (na kama ulivyosema pengine justification ni fair kabisa kwamba kama hajulikani kumnadi itakuwa kazi kubwa sana)

   Lakini ukweli unarudi pale pale kwamba, ukikubali kwamba kupanda ngazi CCM kunahusiana moja kwa moja na kuchafuka - huwezi kupata ubunge bila rushwa kwa mfano- basi utakubali kwamba muundo wa sasa wa CCM wa kwamba kuna umwritten rule kwamba mgombea ni lazima acheze sana kwenye NEC na uwaziri huko, inamaanisha kwamba mgombea yeyote atakayeletwa na CCM atakuwa mchafu.

   Ndo maana nashangaa sana watu wanasema "Lowassa this" "Membe that" wakati wote baba yao mmoja mama yao mmoja na wote wamepanda ngazi kwa kutumia siasa za CCM ambazo zimejaa uchafu.

   Ndo maana nasema kiongozi mzuri anayefaa hatumjui kitaifa, tunaowajua kitaifa wachafu na hawafai.

   And to a certain extent this phenomenon is transcending beyond CCM.

   Scary thought indeed.
   Wasafi na wanaofaa wametulia kimya. Wachafu na wasiofaa, hasa wale wanaoogopa mabadiliko kutokana na yanayoweza kuwakuta kutokana na madhambi waliyofanya, wanahangaika sana kuutafuta urais na uongozi.

   Kufikia May 2015 kutokana na kasi kuwa kubwa na wengine kutokuwa na sifa bila kujali uchafu wao, ili wawe mbele tutasikia baadhi wamekufa katika mazingira ya ajabu, tutasikia wengine wana magonjwa ya ajabu na wengine watastaafu siasa bila hata kujua sababu hasa ni nini.

   Lakini kutokana na kuwa security establishment ya Tanzania imekematwa na CCM na bado ina sera ya kuilinda CCM at the expense of national peace, security na prosperity, yoyote atakayetwaa kuteuliwa na CCM, bado ana fursa ya kuwa kiongozi. Unless mazingira ya kuchakachua kura yawe tofauti na yale ya mwaka 2010.
   Mchambuzi likes this.

  21. Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2007
   Location : Tanzania
   Posts : 4,492
   Rep Power : 20330751
   Likes Received
   8000
   Likes Given
   6962

   Default Re: Nadharia Tete: Bila Ujumbe NEC, Urais Haiwezekani

   Quote By Bongolander View Post
   Wasafi na wanaofaa wametulia kimya. Wachafu na wasiofaa, hasa wale wanaoogopa mabadiliko kutokana na yanayoweza kuwakuta kutokana na madhambi waliyofanya, wanahangaika sana kuutafuta urais na uongozi.

   Kufikia May 2015 kutokana na kasi kuwa kubwa na wengine kutokuwa na sifa bila kujali uchafu wao, ili wawe mbele tutasikia baadhi wamekufa katika mazingira ya ajabu, tutasikia wengine wana magonjwa ya ajabu na wengine watastaafu siasa bila hata kujua sababu hasa ni nini.

   Lakini kutokana na kuwa security establishment ya Tanzania imekematwa na CCM na bado ina sera ya kuilinda CCM at the expense of national peace, security na prosperity, yoyote atakayetwaa kuteuliwa na CCM, bado ana fursa ya kuwa kiongozi. Unless mazingira ya kuchakachua kura yawe tofauti na yale ya mwaka 2010.
   ...muhimu pia ile kanuni ya mshindi ni mshindi ambayo sioni jitihada za kuibadilisha, CCM 50.1%, Chadema 49.9%, Rais ni mgombea wa CCM;
   "In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."

   J.K Nyerere, 1965.

  Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...