JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

  Report Post
  Results 1 to 10 of 10
  1. HKigwangalla's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th February 2008
   Location : Dar es salaam, Tanzania
   Posts : 716
   Rep Power : 851
   Likes Received
   916
   Likes Given
   226

   Default Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Tafakuri Tunduizi:

   Vijana wa kitanzania wana ndoto za kuishi maisha mazuri. wanahangaika kujenga nyumba zao mbali na mji, wengine itawachukua lifetime kukamilisha ujenzi wa nyumba zao na mara nyingi ili kukwepa adha ya kupanga watajikuta wanaishi kwenye nyumba ambazo hazijakamilika. Kiinua mgongo chao kinatunzwa kwenye mifuko ya jamii na mwisho watakuja kupewa wakiwa wamezeeka na wakiwa wametumiki...a nchi yao, ujana wao wakiwa wameishi maisha magumu sana. Kwa nini iwe hivyo?

   Mimi nadhani wana-deserve better from their hard work. Serikali ijenge nyumba nyingi, nzuri na iwakopeshe wafanyakazi wanaowekeza kiinua mgongo chao kwenye mifuko ya jamii.

   Hii itawafanya wajenga nchi wetu wafanye kazi kwa bidii na waishi maisha mazuri leo na siyo jasho lao lifaidishe kizazi kingine kijacho kesho. Hii itawafanya waongeze morali kwenye kazi na pia wawe more committed kwenye kazi maana alama za usaliti wa viongozi hazitoonekana wazi zaidi na kila mtanzania ataona serikali inamuangalia kila mtu.

   Zoezi liwe endelevu na kila mmoja wetu mwisho wa siku aje kupata nyumba hizi bora. Maeneo yatabaki wazi kwa kiasi kikubwa na yatatumika kwa kazi nyingine za uzalishaji na siyo ujenzi huu kama wa leo wa vinyumba scattered kila mahali. Mpango huu utakuwa umelenga mbali na hivyo miundombinu ya viwanda, treni za abiria, mabasi ya kasi, maji na umeme itakuwa kwenye mpango na hivyo utekelezaji wake utakwenda kwa awamu kadri tunavyoendelea!
   Dr. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA
   Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi...!


  2. Saint Ivuga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2008
   Posts : 25,340
   Rep Power : 88801448
   Likes Received
   7583
   Likes Given
   13009

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Hili wazo ni zuri na linatekelezeka kirahisi, tatizo hao watekelezaji ndio hawapo na sijui watafufuka lini..na tuna hadi chuo cha ardhi /mipango miji hawa sijaona kazi zao bado kwani kwenye miji mikubwa wote tunashuhudia jinsi watu wanavyijenga kiholela holela
   JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.

  3. zumbemkuu's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 11th September 2010
   Location : street dweller
   Posts : 8,633
   Rep Power : 355221031
   Likes Received
   4045
   Likes Given
   13803

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   hapa nimekukubali mkuu, wazo zuri sana.
   ''Overcome the devils with a thing called love'' bob marley

  4. #4
   Jadi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd August 2011
   Posts : 1,015
   Rep Power : 729
   Likes Received
   264
   Likes Given
   8

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   nakubaliana nawe HK kabisa,hawa kina Dau et al wanajilimbikizia pesa yetu,hata kama leo michango yetu inapelekwa wakati shilingi ina nafuu kwa dola,itafika siku sh haina maana lakini wao watatupa hela ileile,inauma sana

  5. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,951
   Rep Power : 77628742
   Likes Received
   14701
   Likes Given
   2693

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Serikali si inajitoa katika biashara na hata imeuza nyumba? Kwa nini unataka serikali ijiingize tena katika biashara ya nyumba?

   Kwa nini usichangie kitu cha kuleta mabadiliko ktika sekta binafsi?
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..


  6. zumbemkuu's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 11th September 2010
   Location : street dweller
   Posts : 8,633
   Rep Power : 355221031
   Likes Received
   4045
   Likes Given
   13803

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Quote By Saint Ivuga View Post
   Tatizo viongozi wetu wanaongea sana lakini utekelezaji ni sifuri.
   wanakuwa na sera na mawazo ya upande wa kuume, matendo yao upande wa kushoto.
   ''Overcome the devils with a thing called love'' bob marley

  7. #7
   Keil's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd July 2007
   Posts : 2,359
   Rep Power : 1216
   Likes Received
   768
   Likes Given
   292

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Vijana/Watanzania wanaochangia kwenye mifuko ya jamii ni wachache sana ukilinganisha na idadi ya watanzania wote. SO, hili pendekezo lako lina walakini, bado haliwezi kuwa suluhisho la slums au uwepo wa nyumba za mbavu za mbwa.

   Pili, michango kwenye mifuko ya jamii ni mdogo sana kwa kuwa mishahara ya wafanyakazi wengi ni midogo. So, project unayoipendekeza ni wachache ambao wanaweza ku-qualify kupewa hiyo mikopo kwa kuwa kiwango ambacho watakuja kulipwa kama kiinua mgongo pindi watakapostaafu hakilingani na thamani ya nyumba zitakazojengwa. Chukulia mshahara wa mfanyakazi anayepokea shilingi laki 2 au 3 (majority ya wafanyakazi wa serikali), hata akifanya kazi miaka 40, bado hawezi kulipa nyumba ya shilingi milioni 100 kutokana na mchango wake kwenye mfuko wa jamii.

   Whoever atakayekubali kujenga nyumba kwa ajili ya kuwakopesha wananchi, anaangalia kwanza uwezekano wa mkopeshwaji kama ana uwezo wa kulipa hiyo nyumba na kigezo ni mshahara wake na mafao yake ya uzeeni, kwamba certain part ya deni itakatwa kwenye mshahara na kama mpaka wakati wa kustaafu hajamaliza kulipa deni then mafao yake yatakatwa ili kukamilisha malipo.

   Hiyo ni biashara na watakao-qualify ni wachache sana ukilinganisha na idadi ya wafanyakazi wenye ajira.

   Je, wamachinga ambao ni jeshi la vijana wanaofanya kazi za ubangaizaji, watakopeshwa na nani?

   Sidhani kama hili pendekezo linaweza kuwa suluhisho la uwepo wa slums au nyumba za mbavu za mbwa. Wapo ambao hawawezi ku-afford kiwanja, so mahali popote akiona panawezekana kujenga kibanda, anajiwekea kibanda cha mbavu za mbwa kulingana na hela aliyo nayo. Kwa kuwa akisema afuate taratibu za kupata kiwanja, anaweza kukuta vihela vyake vinaishia kwenye ununuzi wa kiwanja na utapeli mwingine wa Idara ya Ardhi na halmashauri ya mji/jiji/manispaa.

   Ili idea yako iweze kuwa na mashiko wa upande wafanyakazi, mahali pa kuanzia, boresheni mishahara ya wafanyakazi, serikali ikifuta posho zote na zikaingizwa kwenye mishahara, mishahara itaongezeka na pia michango ya mifuko ya jamii nayo itaongezeka na hivyo kuwafanya wafanyakazi wengi wa-qualify kupata hizo nyumba za mikopo.

   Pia boresheni mazingira kwa vijana wanaotaka kujiajiri wenyewe, kuna urasimu mwingi sana kwenye ku-formalize biashara na wengi wanaona ni usumbufu na hivyo wanaishia kufanya informal business na hawawezi ku-access mikopo kutoka kwenye mabenki. Kuna opportunities nyingi sana za kujiajiri, lakini serikali yetu na wabunge wetu mna kasumba moja tu ya kuona watu kutoka nje ndo wanaweza. Matokeo yake leo tuna wamachinga kutoka China na wana vibali vya kuwaruhusu kufanya bishahara hiyo!

  8. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,951
   Rep Power : 77628742
   Likes Received
   14701
   Likes Given
   2693

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Unataka habari za kukopesha wananchi katika nchi ambayo haina hata credit bureaus/ ranking system.

   Matokeo yake unaenda kuomba mkopo wa kujenga nyumba, unaambiwa hupewi mkopo mpaka utoe hati ya nyumba yako kama collateral.

   Ebo, sasa mie sina nyumba, nakuja kukopa nijenge nyumba, mnataka niwape title deed!
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  9. #9
   FJM's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Posts : 8,099
   Rep Power : 82810706
   Likes Received
   6092
   Likes Given
   4766

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Quote By Jadi View Post
   nakubaliana nawe HK kabisa,hawa kina Dau et al wanajilimbikizia pesa yetu,hata kama leo michango yetu inapelekwa wakati shilingi ina nafuu kwa dola,itafika siku sh haina maana lakini wao watatupa hela ileile,inauma sana
   Naomba niwe tofauti kidogo kwenye pension. Ni vizuri tuelewe tofauti kati ya pension na social welfare kwa maana ya un-employment benefits. Pension ni malipo ya uzeeni, wakati ambapo kwa hali ya kibinadamu mtu unakuwa hauna tena nguvu ya kuweza kuchacharika na kazi kama wakati ya ujana. Kila nchi ina umri wa 'uzee' lakini kwa vyovyote vile mzee hawezi kuwa mtu mwenye miaka 30, 35, au hata 45! Hata hivyo unaweza kuwa kwenye kundi la uzee (kwa maana ya malipo ya uzee) kama unapatwa na matatizo kazini ambayo yatasababisha wewe kutuweza kuendelea kufanya kazi e.g ajali etc.

   Kwa upande wa Un-emploment benefitsm haya ni malipo kwa watu ambao wako kwenye umri wa kufanya kazi, wana uwezo wa kufanya kazi lakini kwa sababu mbalimbali hawako kwenye ajira i.e kupunguzwa, uhaba wa ajira etc. Kwa kawaida wenye kutoa hizi un-employment benefits ni 'state' kwa maana ya dola/serikali na sio shirika moja moja.

   Dau na NSSF yake, PPF, PSPF, LAPF na mashirika mengine ya pension ni mashirika ya PENSION na sio un-employment benefits. Pension FUNDS zinaendeshwa kwa kanuni na masharti ya ki-pension. Zinachukua kiasi cha hela kwa wanachama na kuwekeza ili wapate faida na kuwalipa pindi pale umri wa uzee unapofikia au wanashindwa kufanya kazi kutokana na umri/magonjwa. Kama itatokea kwamba mwanachama (mfanyakazi) anakuwa nje ya ajira (mfano kapunguzwa) wakati umri wake bado ni chini ya category ya uzee hilo lilitakiwa liwe shauri la 'state'. Na hapa ndio linakuja tatizo la nchi zetu ambazo hazina kitu kinazhoitwa un-employement benefits.

   Hapo kwenye red; malipo ya pension hutolewa kwa formula baada ya 'actuary' kufanya evaluation. Huwezi kuchukuwa michango ya watu (future ya watu tena wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi itakuwa imepungua) na kufanyia shughuli ambazo hauna uhakika nazo 100% kwamba zitakuwa na faida.

   Pamoja na yote hayo ninao wasiwasi kiasi na 'boldness' ya NSSF kwenye suala zima la uwekezaji. Sababu kubwa hata Kingwangala anajata NSSF ni kutokana na ukweli kwamba hawa mabwana (NSSF) wamekuwa mstari wa mbele kumwaga hela kwenye miradi mingi. Nasema boldness wameji-expose sana kwenye miradi mingi, huku baadhi ikiwa na risks au ina shinikizo kubwa la kisiasa.

   Nirudie Pension ni future ya watu hivyo unapowekeza hela kwa harufu ya kisiasa iko hatari ya kupata hasara maana hukufanya business decision' Na unapopata hasara maana yake mfuko (pension funds) mfuko unapungukiwa na uwezo wake kutoa au kuongeza kiwango cha pension kwa mwanachama. Hiki ndicho kinanipa shida. NSSF na wengine wanaweza kujitetea likini tumekuwa tunasoma matumizi mabaya ya resources, mikopo ambayo haijarudi. Nani analipa? Kwa vyoyote ni mwanachama.

  10. HKigwangalla's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th February 2008
   Location : Dar es salaam, Tanzania
   Posts : 716
   Rep Power : 851
   Likes Received
   916
   Likes Given
   226

   Default Re: Majawabu ya Kigwangalla: Tuijenge Upya Miji Yetu!

   Hili wazo ambalo mimi naona ni wazo litakalotoa majawabu ya kero za nyumba, ya mipango miji na pia suluhisho la kuongeza motisha na commitment miongoni mwa wachapa kazi wetu, ni wazo la mbolea sana.

   Mifuko ya jamii imekuwa ikitumiwa kwa njia tofauti katika nchi tofauti. Kuna baadhi wamegawa contributions katika makundi tofauti tofauti, kunakuwa kuna kundi la:

   1. retirement-related benefits
   2. investment and insurance related benefits
   3. healthcare and education related benefits.

   Utakuta kwenye nchi zinazotumia mifuko hii kuwanufaisha wananchi wake wachangiaji, kunakuwa na viwango vya juu sana vya michango ambayo sasa inagawanwa kwenye hizo account tatu tofauti. Nchi nyingine zinawakata kidogo sana wachangiaji na michango mikubwa inatokana na serikali ama waajiri, ambayo ni ya lazima. nchi nyingine zinatoa protection za bure kwa wananchi wake walio katika makundi ama hali maalum. Nchi nyingine michango hii ni ya hiari.

   Sasa kwa Tanzania, model ninayoona inatufaa ni kama hii ya kuwa na michango mikubwa na kuruhusu tupate bima za maisha, za afya, mikopo ya kujisomesha, ya kusomesha watoto wetu, tupate bima ya afya, na pia turuhusiwe kutumia kiasi fulani cha michango yetu kuwekeza kwenye hisa (Tbills, Tbonds, Unit trust, Gold etc). Kuwa na hizi benefits haimaanishi kwamba eti tunaondoa malipo ya uzeeni ama ya wakati wa hali maalum, sema tunaboresha tu sasa, kwa faida yetu wenyewe.

   Na mpango wa nyumba si kuwa eti utakuwa wa watu wachache, tunaweza ku-explore vizuri zaidi ni jinsi gani kila mtu anaweza kufaidika na nyumba hizi, na kwa kuwa shirika la nyumba litakuwa linafanya kazi kwa faida, litatunisha mtaji wake kwa haraka kutokana na michango hii litaweza kujenga nyumba za hadhi tofauti tofauti na watu wakanunua kwa gharama tofauti tofauti. Watu wasio na ajira rasmi wanaweza kuhamasishwa na kuelimishwa kuingia kwenye mifuko hii, na kwanza hata wao watahamasika wenyewe tu wakijua wenzao wanavyofaidika!

   Naomba kuwasilisha,
   HK.
   Dr. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA
   Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi...!


  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...