Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

    Report Post
    Page 3 of 3 FirstFirst 123
    Results 41 to 53 of 53
    1. #1
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1741
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

      Ndugu wana JF,

      Wakati tunaangalia kulia na kushoto ili kuifanya nchi yetu ipate viongozi yule ambaye kila mtu anamtaka , naona bado natatizwa na hiki kitu kinachoitwa ruzuku!

      Ni kweli ruzuku itolewayo na serikali kwa vyama vya upinzani inaweza ikawa ni chachu ya mabadiliko nchini, lakini pia inaonekana kama ni chanzo cha matapeli wachache kuitumia vibaya, wengine kwa uroho tu, wengine wamekosa ajira na sababu nyingi zifananazo na hizo.

      Napendekeza :

      1. Ruzuku itolewe mwaka mmoja tu kwa vyama vinavyoanza;na kuwe na ufuatiliaji wa hali ya juu, juu ya matumizi ya hizo fedha au

      2. Isitolewe kabisa, kwa sababu:

      (a) Kila chama kizuri chenye sera nzuri kitakachowavutia wananchi ni dhahiri kitapata wanachama wazuri watakaohakikisha wanakitunza chenyewe na watu wake.

      (b) Hali ya sasa hivi hata kama tutasema tunataka demokrasia ni dhahiri utitiri wa vyama hivi, unaleta

      - Uadui kati ya wenyewe kwa wenyewe!

      - Wengine kuona basi CCM iendelee tu maana vyama vingi vimeshajizolea umaarufu, aidha wataleta fujo na mara nyingi wanapigana kwa sababu ya fedha. N hii imeongeza hofu ya watu wengi kuwapigia kura hawa wapinzani.

      - Kudhihirisha kuwa vyama vingi vinataka fedha tu, utavisikia wakati tunakaribia uchaguzi!!

      Tukiwa na vyama ambavyo wananchi ndio wanaokiendesha, tutapata viongozi wanaowajali zaidi wananchi. Tutapata viongozi amabo hatima ya maamuzi yao ni kwa manufaa ya wananchi.

      Kwa jinsi hii tutatengeneza akinaTsavangirai wetu akina Riala Odinga n.k

      Viongozi wengi wa siasa hasa wapinzani , wawajabike wasiwajibike mwisho wa mwezi hela watapata tu.

      Ni heri kupunguza vyama viwe vichache vya kiwananchi zaidi kuliko hali ya sasa. Afadhali hizo hela ziende mahospitalini n.k

      Tukiangalia kwa undani sasa , hali hii ya kupewa ruzuku haitapelea vyama vya upinzani kushinda, sana sana tumeona migogoro ya ruzuku kila siku na watu kufanya ofisi za vyama kama vijiwe.

      Pia kwa vyama vya siasa vikongwe, sijajua wana miradi gani, na wamewaza nini ili kupata income zao!

      Naamini ubunifu wa kuoata hela kwa njia ya halali , ndio ubunifu huo utahitajika pindi watakaposhika nchi.

      Naomba chama, haswa kile kinachoona kiko tayari kujiendesha kwa nguvu ya umma, kiwe cha kwanza kusema hatutaki ruzuku , hizo fedha ziende hospitalini!

      Vyama vikishuka chini, vikawa havina hela na viongozi wake waanze kuishi maisha ya kulingana na fedha za wanachama, wala yasiyo ya kifahari. Hawa vingozi watakuwa viongozi wa kweli.

      Baadhi ya vyama vya siasa tulivyonavyo kamanilivyopata kwenye wikipedia ni:

      • Chama Cha Mapinduzi (Revolutionary State Party)
      • Civic United Front (Chama Cha Wananchi)
      • Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
      • Tanzania Labour Party
      • United Democratic Party
      • Chama cha Haki na Usitawi (CHAUSTA)
      • Democratic Party (DP)
      • Demokrasia Makini (MAKINI)
      • Forum for the Restoration of Democracy (FORD)
      • Jahazi Asilia
      • National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR)
      • National League for Democracy (NLD)
      • National Reconstruction Alliance (NRA)
      • Popular National Party (PONA)
      • Sauti ya Umma (SAU)
      • Tanzania Democratic Alliance (TADEA)
      • Progressive Party of Tanzania-Maendeleo (PPT-Maendeleo)
      • Union for Multiparty Democracy (UMD)
      • United People's Democratic Party (UPDP)

      Naomba tujadili

      wakatabahu

      Waberoya

      Update:

      Msimamo wangu haujabadilika-2011 April

      Msimamo wangu haujabadilika-2012 May
      Last edited by Waberoya; 29th May 2012 at 20:46.
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    2. FemaTV & Radio

    3. #41
      Ben Saanane's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2007
      Posts : 6,702
      Rep Power : 32781
      Likes Received
      4971
      Likes Given
      6451

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      Quote By Waberoya
      Yes my friend! the problem is not helpless, the problem is that people are working up! utapiga miayo, utatandika kitanda, utapifa mswaki,...yaani asubuhi ni kama jana haikuwepo vile. That is excactly what is happening now......

      Let us reasons things for the betterment of our nation
      Tatizo ni Moral Deviation ili kupambana na hizo evil spirits,Let us Redefine our National agenda for the next 50 yrs!Tuna kazi sana.As a nation tuna tatizo Kubwa
      Wametuonyesha Jeuri ya ukaburu,tuwaonyeshe jeuri ya Umkhontho we sizwe kupitia Red Brigade.Tukiwaonyesha woga wetu, itakua silaha imara zaidi kwao kutumaliza-Ben Saanane

    4. #42
      chitambikwa's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Location : KAISHO
      Posts : 3,163
      Rep Power : 1958
      Likes Received
      573
      Likes Given
      424

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      Ruzuku zitatoka lakini kama nchi itaendelea kuwa ya kishenzi kam ilivyo sasa ,pesa haziwezi kupelekwa huko zinakopaswa bali kulipia vipindi kwenye tv eti wamejivua gamba
      IT IS TO THOSE WITHOUT TEETH GOD GIVES MEAT

    5. #43
      MkamaP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2007
      Posts : 4,675
      Rep Power : 1569
      Likes Received
      310
      Likes Given
      93

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      Quote By chitambikwa
      Ruzuku zitatoka lakini kama nchi itaendelea kuwa ya kishenzi kam ilivyo sasa ,pesa haziwezi kupelekwa huko zinakopaswa bali kulipia vipindi kwenye tv eti wamejivua gamba
      Sahizi ndo wanazitumia sana mara nec mara nini kwa mwezi wanapata bilioni kadhaa kufanya upuuzi tu. Ruzuku hiyo kwa vyama inatosha kukodi walimu kufundisha shule za kata wakati tukiangalia suluhisho la mda mrefu.

      Nchi botswana huko gabon wamekuwa wakikodi walimu kutoka nchi mbalimbali na wanafanya vizuri sana sahizi. sie tunapoteza mabilioni eti ruzuku, mabilioni eti mbunge .
      Zifutwe hizi ruzuku kwa vyama na wabunge wapigwe panga nzuri ,hivyo ndo vyanzo vya matatizo yetu.

    6. #44
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,410
      Rep Power : 2881
      Likes Received
      4755
      Likes Given
      2822

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      Waberoya,
      Kuna jambo linakuchangaya. Kuwepo kwa vyama vya siasa lukuki ni haki ya Watanzania, ili kuhakikisha kuwa vyama hivyo si miradi ndiyo maana ruzuku inatolewa kwa chama chenye wabunge. Kwahiyo sio kila chama cha siasa kinapata ruzuku kama ulivyoelewa wewe.

      Uwepo wa taasisi za kisiasa ni muhimu. Tumeona hivi karibuni nchi kama za Libya, Tunisia na Misri zinavyohangaika kuwa na taasisi mbadala za kisiasa baada ya mabadiliko na hatuwezi kusema hapa kwetu hili haliwezi kutokea.
      Ni kutokana na kuimarika kwa vyama vaya kisiasa tunaona serikali inatoka usingizini ingawa bado wala ruzuku wakubwa CCM wamebaki kupiga makofi na kusema ndiyoooo, kuwazomea akina Zitto, Lema n.k, lakini kazi yao tunaiona. Jambo la muhimu ni uwazi wa matumizi ya ruzuku au kupunguza ili iwiane na hali halisi ya maisha yetu.

      Kuhusu pesa kuna maeneo mengi ya kuangalia kama idadi ya wabunge. Inakuwaje tunakuwa na mkuu wa wilaya mmoja ambaye ndani ya eneo lake ana wabunge wawili au watatu. Kwanini nchi masikini kama yetu iwe na WABUNGE 320! zaidi ya 100 hawakupigiwa kura.
      Inakuwaje ofisi za bunge ziwe Dodoma na shughuli zote zifanyaike Dar es Salaam. Inakuwaje mbunge akiwa Dodoma ambapo ni ofisi yake alipwe per diem! halafu uwepo mpango wa kuwajengea nyumba.
      Inakuwaje kuwepo na bajeti ya halmashauri na mfuko wa mbunge jimboni, ili hali yeye ni mjumbe ndani ya halmashauri.
      Wabunge wa kuteuliwa wanamwakilisha nani na wapi? wabunge wa kuteuliwa na rais wanakazi gani bungeni?
      Kwanini kuwe na ofisi ya bunge Dodoma na nyingine Dar.
      Kwanini mapato halisi ya mbunge yanakuwa siri ili hali mapato ya wafanyakazi wengine yapo wazi, kuna nini kinafichwa?
      Kwanini mbunge akopeshwe pesa za gari ili hali aliweza kufanya kampeni kwa msuururu wa magari jimbo zima? Na kwani mbunge anyerudi bungeni akopeshwe gari tena wakati analo la awali.

      Nadhani haya ni mambo ya kujiuliza huko tuendako,ili kufanya siasa iwe kazi ya kutoa huduma na si biashara ambayo mtaji wake ni demeokrasi.

    7. #45
      MkamaP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2007
      Posts : 4,675
      Rep Power : 1569
      Likes Received
      310
      Likes Given
      93

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      Quote By Nguruvi3

      Umeongea vizuri, lakini binafsi sielewi kwakweli watanzania nini tunakitaka. Huwezi sema unatetea ufisadi na ukafumbia pesa zinazotafunwa na wabunge pamoja na ruzuku.

    8. Study Abroad

    9. #46
      Uswe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,775
      Rep Power : 792
      Likes Received
      435
      Likes Given
      437

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      Quote By Nguruvi3
      Waberoya,
      Kuna jambo linakuchangaya. Kuwepo kwa vyama vya siasa lukuki ni haki ya Watanzania, ili kuhakikisha kuwa vyama hivyo si miradi ndiyo maana ruzuku inatolewa kwa chama chenye wabunge. Kwahiyo sio kila chama cha siasa kinapata ruzuku kama ulivyoelewa wewe.

      Inakuwaje kuwepo na bajeti ya halmashauri na mfuko wa mbunge jimboni, ili hali yeye ni mjumbe ndani ya halmashauri.
      Wabunge wa kuteuliwa wanamwakilisha nani na wapi? wabunge wa kuteuliwa na rais wanakazi gani bungeni?
      Kwanini kuwe na ofisi ya bunge Dodoma na nyingine Dar.

      Kwanini mapato halisi ya mbunge yanakuwa siri ili hali mapato ya wafanyakazi wengine yapo wazi, kuna nini kinafichwa?
      Kwanini mbunge akopeshwe pesa za gari ili hali aliweza kufanya kampeni kwa msuururu wa magari jimbo zima? Na kwani mbunge anyerudi bungeni akopeshwe gari tena wakati analo la awali.

      Nadhani haya ni mambo ya kujiuliza huko tuendako,ili kufanya siasa iwe kazi ya kutoa huduma na si biashara ambayo mtaji wake ni demeokrasi.
      RUZUKU Hapana, Pinga Ruzuku kwa vyama vya siasa, Pinga Ruzuku! Wawe na sera nzuri, wananchi wataovutiwa na sera zao watawachangia, sipendezewi hata kidogo na tabia ya CCM kukumbatia mafisadi lakini sina namna ya kukataa kodi yangu isiende CCM kupitia ruzuku.

      Ni kweli marupurupu na posho za wabunge ni nyingi na hazina tija! kinachouma zaidi, zile ni kodi zetu
      mbona sioni umeme, maji wala barabara, 30% PAYE na Kodi nyingine katika bidhaa, zinaenda wapi?

    10. #47
      Uswe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,775
      Rep Power : 792
      Likes Received
      435
      Likes Given
      437

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      tuendelee kujadili

      CCM inapata zaidi ya 800 milioni kila mwezi, CDM zaidi ya 200 milioni kila mwezi, CUF zaidi ya 117 milioni kila mwezi

      haya mabilioni yanayoungua kila mwezi yanatakiwa yakanunue dawa, yajenge barabara, yakanunue vifaa hospitalini

      VYAMA VYA SIASA VISIPEWE RUZUKU!
      Last edited by Uswe; 27th May 2012 at 06:53.
      Waberoya likes this.
      mbona sioni umeme, maji wala barabara, 30% PAYE na Kodi nyingine katika bidhaa, zinaenda wapi?

    11. #48
      Uswe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,775
      Rep Power : 792
      Likes Received
      435
      Likes Given
      437

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

      RUZUKU Hapana, Pinga Ruzuku kwa vyama vya siasa, Pinga Ruzuku! Wawe na sera nzuri, wananchi wataovutiwa na sera zao watawachangia, sipendezewi hata kidogo na tabia ya CCM kukumbatia mafisadi lakini sina namna ya kukataa kodi yangu isiende CCM kupitia ruzuku, hawa Jamaa wanachukua zaidi mil 800 kwa mwezi!!!
      Waberoya likes this.
      mbona sioni umeme, maji wala barabara, 30% PAYE na Kodi nyingine katika bidhaa, zinaenda wapi?

    12. #49
      chama's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th August 2010
      Posts : 4,849
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1157
      Likes Given
      908

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya upinzani iondolewe!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      amesema vyama vya upinzani tu; CCM iendelee kuenjoy ruzuku yake ya bilioni 2 na ushee kwa mwezi. So, kina Zitto naona kwa mpango huu mmekwisha! LOL
      Ni hatari sana kwa mwandishi wa habari kupindisha maneno; Mwanakijiji unajua kalamu ni hatari kuliko AK47? Hebu rudia kuisoma tena habari nzima na onyesha wapi Waberoya CCM iendelee kupewa ruzuku. Ama huu ni mwanzo wa Chadema kujiingiza kwenye siasa za ulaghai? Kumbuka wewe ni kiongozi halafu ni mwandishi.

      Chama
      Gongo la Mboto DSM

    13. #50
      Uswe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,775
      Rep Power : 792
      Likes Received
      435
      Likes Given
      437

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya upinzani iondolewe!

      Quote By chama
      Ni hatari sana kwa mwandishi wa habari kupindisha maneno; Mwanakijiji unajua kalamu ni hatari kuliko AK47? Hebu rudia kuisoma tena habari nzima na onyesha wapi Waberoya CCM iendelee kupewa ruzuku. Ama huu ni mwanzo wa Chadema kujiingiza kwenye siasa za ulaghai? Kumbuka wewe ni kiongozi halafu ni mwandishi.

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      how i wish tungeacha kujadili mtu/watu

      Kila mwezi CCM wanakunja zaidi ya 800M, CHADEMA zaidi ya 200M na CUF zaidi ya 117M, haya ni makosa, hizi pesa zinatakiwa zikanunue madawa na vifaa hospitalini, zinatakiwa zikalipe walimu, zinatakiwa zikalipe madaktari, zinatakiwa zikajenge vyoo shule za msingi, hapa tumeplan vibaya!!
      Waberoya likes this.
      mbona sioni umeme, maji wala barabara, 30% PAYE na Kodi nyingine katika bidhaa, zinaenda wapi?

    14. #51
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1741
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

      Sijawahi kubadilika kuhusu hii hoja, kama vyama vina wanachama basi wanachama wake ndio wakitunze chama na viongozi wao na si kodi zetu!!

      zaidi ya billioni moja kwenda kwa wanasiasa na kulisha matumbo yao si haki!! is unfair

      tuna priorities nyingi mno na kibaya sisi ni maskini tunaongoza kidunia!!

      Please unga mkono hili: RUZUKU KWA VYAMA VYA SIASA ZIKOMESHWE!
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    15. #52
      Uswe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,775
      Rep Power : 792
      Likes Received
      435
      Likes Given
      437

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

      Quote By Waberoya
      Sijawahi kubadilika kuhusu hii hoja, kama vyama vina wanachama basi wanachama wake ndio wakitunze chama na viongozi wao na si kodi zetu!!

      zaidi ya billioni moja kwenda kwa wanasiasa na kulisha matumbo yao si haki!! is unfair

      tuna priorities nyingi mno na kibaya sisi ni maskini tunaongoza kidunia!!

      Please unga mkono hili: RUZUKU KWA VYAMA VYA SIASA ZIKOMESHWE!

      zaidi ya billioni moja kwenda kwa wanasiasa na kulisha matumbo yao si haki!! is unfair = well said, naomba mods mu-sticky huu uzi, don't let this movement die, RUZUKU KWA VYAMA VYA SIASA HAPANA!
      Waberoya likes this.
      mbona sioni umeme, maji wala barabara, 30% PAYE na Kodi nyingine katika bidhaa, zinaenda wapi?

    16. #53
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1741
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

      Ruzuku kwa vyama vya siasa hapana!
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    17. Miaka 50
    Page 3 of 3 FirstFirst 123

    Similar Topics

    1. Replies: 18
      Last Post: 5th May 2013, 14:20
    2. Replies: 2
      Last Post: 19th April 2011, 20:35
    3. Replies: 0
      Last Post: 7th April 2009, 14:52

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...