Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Je, wapinzani ni wakombozi?

    Report Post
    Page 8 of 26 FirstFirst ... 67891018 ... LastLast
    Results 141 to 160 of 509
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,518
      Rep Power : 46714
      Likes Received
      16434
      Likes Given
      8471

      Default Je, wapinzani ni wakombozi?

      Kuna baadhi ya watu ambao wanataka tuamini kuwa siku Tanzania ikichukuliwa na wapinzani basi matatizo yote ya Tanzania yatatoweka kama ukungu! Baadhi ya watu hawa, hawaishi kuonesha udhaifu wa chama tawala na serikali yake iliyoko madarakani. Ni watu hawa ambao kwao hakuna jema lolote, na hakuna kitu chochote kizuri ambacho kimewahi kufanywa na serikali iliyoko madarakani. Kwa watu hawa, ili kuweza kuona angalau kitu kizuri basi inabidi utumie darubini!!

      Baadhi ya watu hawa wameonesha uwezo mkubwa wa kuonesha matatizo na udhaifu wa chama tawala ambao hahuitaji darubini kuuona kwano ni dhahiri! Ni rahisi kwao kuonesha mapungufu ya masuala ya mikataba mbalimbali, tuhuma za rushwa n.k! Ni kwa sababu hiyo basi baadhi ya watu hawa pamoja na wapiga debe wengine wa upinzani wamefikia mahali pa kudai kwa ujasiri kuwa CCM na serikali yake havijafanya lolote la maana zaidi ya kutudidimiza kimaisha.

      Ukweli wa mambo ni kuwa hoja zao nyingi ni za msingi na mambo mengine ambayo wanayaonesha ni ya wazi ambayo hata mtu asiye mpinzani anaweza kuyaona! Kwa mtu yeyote anayeipenda nchi yetu hatuna budi kuwashukuru watu hao kwa moyo wao wa kizalendo na kujituma kufichua maovu na ufisadi! Siyo jukumu la watu hao peke yao na vyama vyao kuonesha ubaya, upotofu, na ubovu wa serikali iliyoko madarakani! Si vibaya kabisa kwa wao kwa kutumia mwanga kama wa kurunzi kuangazia umma na kuonesha kuwa baadhi ya viongozi au wafanyakazi wa serikali ni wabadhirifu, wanatumia madaraka yao vibaya, na baadhi yao wamefanya vitendo ambavyo vinapakana kabisa na usaliti kama siyo uhaini dhidi ya jamhuri yetu.

      Viongozi hawa walioko upinzani na wapambe wao wamejitahidi miaka nenda rudi tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi kuiamsha Tanzania ili wananchi waelewe kuwa kuna chaguo jingine na kuna chama mbadala wa CCM. Walijaribu kwa mafanikio makubwa kwenye uchaguzi wa 1995 na kutokana na mvuto wa mmoja wa wapinzani hao aliyewahi kuwa madarakani basi watu waliamua kuachana na CCM na kujiunga na upinzani wakitumaini kuwa hapo "wamefika nyumbani" kwani CCM imewachosha! Lakini katika chaguzi mbili zilizofuata baadaye (2000 na 2005) vyama hivi vimeendelea kufanya vibaya licha ya majina yao na itikadi zao kueleka zaidi!

      Pamoja na kudidimia kwa vyama hivyo kwenye sanduku la kura, viongozi wao bado wanapita kunadi sera zao wakiangazia udhaifu na ubovu wa CCM kuwa ni sababu ya wananchi kuwaamini kuwa wapinzani ndio mbadala wa uhakika wa chama tawala, na hivyo wananchi waanze kuwaamini kwa kuwapa madaraka!

      Swali kubwa na la msingi ambalo kila Mtanzania hana budi kujibu ni kuwa, je wapinzani wakipewa madaraka ya nchi leo hii (siyo kupewa kama hisani bali kutwaa kwa nguvu ya kura) matatizo ya Tanzania yatatoweka ghafla? Je wapinzain wakiwa Ikulu hospitali zetu zote zitakuwa za kisasa, wanafunzi wote watakwenda shule, mishahara italipwa kwa wakati n.k n.k? Je wapinzani wakitwaa madaraka ina maana umasikini wa Tanzania utatoweka ndani ya mwaka mmoja?

      Kama mifano ya wapinzani kuchukua madaraka katika nchi jirani inaonesha lolote, basi mtu yeyote mwenye akili timamu ambaye anadhania kuwa endapo wapinzani watachukua madaraka basi maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa ahuei na yatabadilika kwa ghafla mtu huyo adhanie tena! Ni mabadiliko gani ya kimaisha wananchi wa Kenya wameyapata baada ya NARC kuingia madarakani? Vipi kule malawi baada ya chama cha MDC kuingia madarakani watu wa Bulawayo, Lilongwe, Blantyre, na Karonga maisha yao yamebadilika vipi? Je wapinzani walipochukua madakaraka huko Zambia, maisha ya watu wa Lusaka, Copper Belt, na Capri Mposhi yamebadilika vipi?

      Wapinzani wameendelea kudai kuwa CCM imejaa watu wafisadi wasioipenda nchi yao, wenye kutumia madaraka yao vibaya, je wao wakiingia madarakani na kujaza nafasi zote za utawala kuanzia Rais hadi mwenyekiti wa kijiji watatuhakikishia vipi kuwa hakuna mtu kati mamia ya watumishi hao atakayekula rushwa au kutumia madaraka yake vibaya? Je tuna uhakika gani kuwa vyama vya upinzani vitaweza kumsimamia kila polisi, kila mwalimu, kila meneja, kila Mkurugenzi, kila mwenyekiti wa bodi n.k na kuhakikisha hakuna hata mmoja wao atakayemziba raia kibao hadharani au ambaye atafyatua bunduki yake na kumlipua mpiga debe?

      Kama kweli wapinzani wataahidi kufanya haya yote na kutokosea kabisa, kutoharibu hata mara moja, na wakiahidi kuondoa kero zote na matatizo yote yanayoikabili Tanzania huku viongozi wake wote (Rais hadi mwenyekiti kata wa kijiji cha Mkata) wakiwa waadilifu wasiomezwa na ulafi, wasiolewa madaraka wakitumikia nchi yao kwa mapenzi makubwa, basi Tanzania lazima iwachague wapinzani!! Kwani kwenye vyama vya upinzani hakuna binadamu wote ni Malaika, na wote hawajali matumbo yao wala mifuko yao!! Ni katika vyama hivyo yule Musa Nabii yupo, na ni yeye ndiye atakayetutoa utumwani!! Kama kweli vyama vya upinzani vitafanya mambo hayo yote basi ndugu zangu Watanzania, inawezekana mkombozi yupo katikati yetu na hatujamgundua!!

      Kwa kuelewa hulka za binadamu bila kujali itikadi zao na mitazamo yao kutegemea wapinzani kuwa wakombozi wa Tanzania kwa vile tu ni Watanzania wanaotoka Chadema, TLP, CUF, NCCR, au vyama vingine ni mategemeo ambayo yatapeperuka kama unyasi upeperushwavyo na upepo, ni kama umande unavyopukutika kwenye majani asubuhi inapofika! Manabii wa upinzani wako wapi watutabirie?
      Profesa and Mgibeon like this.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. Miaka 50

    3. #141
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1174
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Asha Abdala
      We Masatu

      Acha kunizulia mambo ati. Tanzania Njema amesema CCM inajisafisha kwa kuondokana na rushwa; mimi nisema katu asilani CCM ni ile ile yenye kukumbatia rushwa. Waanzie wapi kujisafisha ili hali wameingia kwa rushwa? Waanze wapi kujisafisha chamani wakati serikalini wanajichafua kwa rushwa? Waanze wapi kujisafisha chamani wakati chaguzi za chama mwaka huu toka chini zilikuwa na rushwa? Lakini wasema upinzani ujisafishe; lini upinzani umejichafua kwa rushwa kama CCM ili ujisafishe?

      Msinitie vidole vya macho Asha mie. Nataka tu mnieleze nielewe, na mnanijua humu-nikielezwa nikaelewa huwa nakubali kuelewa.

      Hivi Masatu nawewe CCM? Nishawishi basi nami nijiunge. CCM ya Kikwete ina lipi jipya?

      Asha
      Bibie,

      Labda hapa tukubaliane kutokubaliana, mtazamo wangu kuhusu posting ya TN ni kama nilivyoeleza hapo juu, kimsingi nakubaliana na alichosema TN, hata hivyo hayo ni maoni yangu kama mtu binafsi.

      Kwa upande mwingine naheshimu mawazo yako ingawa sikubaliana nayo.

      Suala kama mimi ni CCM au la nadhani hilo langu binafsi na halitakusaidia kama utajua, kwa msingi huo huo swali la ushawishi wangu kwako kujiunga na CCM nitakuwa nimelijibu pia

    4. #142
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,282
      Rep Power : 5568
      Likes Received
      290
      Likes Given
      77

      Default

      Hivi vyama vya upinzani kujisafisha lazima mpaka wasubiri CCM wajisafishe?

      Hayo mambo mawili inatakiwa yaende sambamba. CCM ni chafu na wanakula na kupokea rushwa. Upinzani pia kuna uchafu, wanaongoza vyama kama kampuni zao za mifukoni. Wanatafuna ruzuku badala ya kuzitumia kuendeleza wananchi nk.

    5. #143
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,745
      Rep Power : 1163
      Likes Received
      251
      Likes Given
      2515

      Default

      hivi mchochezi ni mwizi au ni yule raia mwema anaye mwambia mwenzie, kuwa unaibia. mimi naona mwizi ndio mchochezi, so manumba kamata wezi.
      hii ni sawa sawa na wale wezi wa kwenye daladala, anamwibia abiria mwezio, wewe unaona unamtonya jamaa kwamba unaibia, then wezi wana kurudi wewe.

    6. #144
      Asha Abdala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2007
      Location : Zanzibar, Sometimes DSM
      Posts : 1,195
      Rep Power : 862
      Likes Received
      20
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mtanzania
      Hivi vyama vya upinzani kujisafisha lazima mpaka wasubiri CCM wajisafishe?

      Hayo mambo mawili inatakiwa yaende sambamba. CCM ni chafu na wanakula na kupokea rushwa. Upinzani pia kuna uchafu, wanaongoza vyama kama kampuni zao za mifukoni. Wanatafuna ruzuku badala ya kuzitumia kuendeleza wananchi nk.
      We Mtanzania

      CCM wamekiri wenyewe kuwa watu wao wanato rushwa na sasa wanaanza kujisafisha.

      Tupe hoja zinazothibitisha kwamba wapinzani wanaendesha vyama kama kampuni zao na kwamba wanatafuna ruzuku badala ya kutumia kuwaendeleza wananchi(sheria ya vyama vya siasa haisemi kwamba ruzuku ni kwa ajili ya kuwagawia wananchi, inasema ruzuku ni kwa ajili ya kuendesha vyama tu).

      Na katika kutoa hoja zako uchambua chama kwa chama badala ya kusema tu upinzani kwa ujumla kaka.

      Vyama vya upinzani vinavyopokea ruzuku ni hivi hapa na navipanga kwa kadiri ya uwingi wa ruzuku wanazopokea.

      1. CUF

      2. CHADEMA

      3. UDP

      4. TLP

      5. PPT Maendeleo(kwa kuwa na diwani mmoja).

      Sasa jenga hoja yako kwa chama kimoja baada ya kingine. Kile kitakachoonekana kuwa hakina rushwa ama ubadhirifu wa ruzuku hicho ndicho tukiamini na kukipa uongozi badala ya CCM kwa kuwa Masatu amekwepa kunithibitishia ni kwa vipi CCM anayoitetea haina RUSHWA.

      Masatu we wangu, naomba unijibu-ni kweli CCM imebadilika na sasa imeweka pembeni rushwa.

      Aie wewe nijibu basi, usichukie. Hoja hujibiwa kwa hoja.

      Asha

    7. #145
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,030
      Rep Power : 2564
      Likes Received
      788
      Likes Given
      29

      Default

      Mimi najiuliza sana na labda kupata majibu kwamba sasa RA atakuwa kesha kamilisha mpango wake wa kumbana Zitto. Maana kwa CCM hii ni vita kwao kutaka Wadanganyika wasijue lolote . CCM na Polisi watafanya kosa kubwa sana kumkamata Zitto leo kwa hoja tete kama hii. Au kama polisi wameamua kuingia kwenye siasa fine .

    8. RukaaJuu Final

    9. #146
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1174
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default

      Sasa jenga hoja yako kwa chama kimoja baada ya kingine. Kile kitakachoonekana kuwa hakina rushwa ama ubadhirifu wa ruzuku hicho ndicho tukiamini na kukipa uongozi badala ya CCM kwa kuwa Masatu amekwepa kunithibitishia ni kwa vipi CCM anayoitetea haina RUSHWA.

      Masatu we wangu, naomba unijibu-ni kweli CCM imebadilika na sasa imeweka pembeni rushwa.

      Aie wewe nijibu basi, usichukie. Hoja hujibiwa kwa hoja.

      Asha
      Bibie,


      Sina sababu ya kuchukia afterall hii baraza ya kubadilishana mawazo.
      Hakuna mahala niliposema kuwa CCM imeacha rushwa, ukifuatilia kwa makini mjadala toka mwanzo kama ulivyoanzishwa na TN nilichosema ni kuwa kuna some changes (japo kidogo) ktk suala zima la vita dhidi ya rushwa ndani ya CCM.

      Yawezekana ikawa ni danganya toto (kama alivyosema mchangiaji mmoja)hata hivyo hoja yangu ilikuwa ni wapinzani waichukulie hali ya hii kama ni changamoto na kujipanga vizuri.

    10. #147
      Asha Abdala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2007
      Location : Zanzibar, Sometimes DSM
      Posts : 1,195
      Rep Power : 862
      Likes Received
      20
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Masatu
      Bibie,


      Sina sababu ya kuchukia afterall hii baraza ya kubadilishana mawazo.
      Hakuna mahala niliposema kuwa CCM imeacha rushwa, ukifuatilia kwa makini mjadala toka mwanzo kama ulivyoanzishwa na TN nilichosema ni kuwa kuna some changes (japo kidogo) ktk suala zima la vita dhidi ya rushwa ndani ya CCM.

      Yawezekana ikawa ni danganya toto (kama alivyosema mchangiaji mmoja)hata hivyo hoja yangu ilikuwa ni wapinzani waichukulie hali ya hii kama ni changamoto na kujipanga vizuri.

      Wooh, ndio maana nakupenda Masatu

      Hizo 'some changes' ni zipi?

      Kama inawezekana ni danganya toto kama ulivyosema kwa hiyo wapinzani nao wajipange kufanya danganya toto?

      Kwa nini wapinzani wasijipange kusema kwamba CCM inafanya danganya toto?

      Nashukuru kwamba huna hasira.

      Asha

    11. #148
      Asha Abdala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2007
      Location : Zanzibar, Sometimes DSM
      Posts : 1,195
      Rep Power : 862
      Likes Received
      20
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Masatu
      Nadhani TanzaniaNjema ameleta changamoto nzuri sana kwa vyama vya upinzani. Kama nitakuwa nimemuelewa vizuri anachotaka kusema hapa ni kuwa kuna some changes ndani CCM ( Japo ndogo sana) katika suala zima la vita dhidi ya rushwa, kwa mtazamo wake kama wapinzani hawatajipanga vizuri ( na wao kusafisha nyumba zao) CCM itawapiga bao.

      La msingi hapa ni kuifanyia kazi changamoto hii, badala ya kuanza kulaumu CCM kuwa ni danganya toto, dharau kama hizi zaweza kuwa na athari kubwa kwa ustawi wa upinzani.
      Masatu

      Bado niko nawe mpenzi

      Hapa tulikuwa tunajadili kuhusu rushwa ndani ya CCM; umesema hapo juu kuwa wapinzani nao wanapaswa kusafisha nyumba zao. Ni uchafu upi wa rushwa upo kwa kila chama cha upinzani?

      Asha

    12. #149
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1174
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Asha Abdala
      Masatu

      Bado niko nawe mpenzi

      Hapa tulikuwa tunajadili kuhusu rushwa ndani ya CCM; umesema hapo juu kuwa wapinzani nao wanapaswa kusafisha nyumba zao. Ni uchafu upi wa rushwa upo kwa kila chama cha upinzani?

      Asha
      Bibie,

      Nisingependa kugeuza ukumbi huu kuwa ni court chamber kwa cross examination.

      Suala la some changes unless unaishi sayari nyingine na huna habari na yanayoendelea hivi sasa kwenye vyombo vya habari nk.

      Kusafisha nyumba za upinzani kunabeba mambo mengi zaidi ya rushwa, masuala ubadhirifu ktk vyama (huko Chadema kulikuwa na kitimtim mara baada ya uchaguzi) undugunization, kauli za vitisho na za kuhatarisha amani ( Mbowe) nk.

      Kwa ujumla hoja yangu hapa ni kuwa wapinzani wajipange vizuri ku counter hii move ya CCM

      Kama msimamo wako ni kuwa vyama vya upinzani (kwa ujumla wake) ni clean na havina hayo niliyoyasema then bravo sis...

    13. #150
      Kitila Mkumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2006
      Posts : 3,920
      Rep Power : 6964
      Likes Received
      1066
      Likes Given
      35

      Default

      Labda itatusaidia kama tutaweza kuonesha hayo ambayo wapinzani wanatakiwa nao wajisafishe. Kwa mfano, kwa CCM tumesema wazi kuwa kuna rushwa kwa sababu wamekatamatana wao wenyewe wakipeana rushwa kupitia hiyo PCCB yao. Sasa unaposema wapinzania wajisafishe, kwa nini pia usiwe specific kwa kusema kwa hili na lile kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa CCM?

      Haya nimeona pia Mtanzania amesema, pamoja na mambo mengine, kuwa wapinzani "wanatafuna ruzuku badala ya kuendeleza wananchi", sasa this is a serious allegation. je, ni kweli kwamba wapinzani wanatafuna ruzuku, hapa nafikiri anamaanisha kuiba au kutumia hiyo ruzuku kwa manufaa binafsi badala ya kuendeleza hivyo vyama vyao, je ana ushahidi wowote na hili? Au msajili wa vyama ametoa report inayoonesha kuwa viongozi wa upinzani wameiba hela za ruzuku? Halafu unaposema "badala ya kuendeleza wananchi", je, tumejibidisha kujua hasa kazi ya hii pesa ya ruzuku kwa vyama vya siasa ni nini?

      Otherwise, naogopa kwamba tutakuwa tunatoa blanket allegations ambazo lengo linaonekana sio kusaidia sana katika kupambana na ufisadi nchini mwetu bali kuhalalisha kwamba vyama vingine navyo ni vichafu kama CCM, wakati, in the absence of credible evidence, sio kweli!
      A Struggle Without Casualties is No Struggle-Steve Biko

    14. #151
      Rwabugiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Posts : 2,738
      Rep Power : 1158
      Likes Received
      67
      Likes Given
      31

      Default

      Quote By ibambasi
      jamani ebu nipeni tofauti ya UCHOCHEZI na KUHAMASISHA wananchi KUTETEA rasilimali zao,hawa kina manumba wametumwa na nani?

      naona ni yale yale ya kina Nyerere na wakoloni,yaani hizi harakati za kina mbowe zinaleta woga na wasiwasi kwa ccm kama enzi zile za kudai uhuru na ccm sasa wanajiandaa kutumia silaha "YAO" ambayo wanacnhi WOTE huwa tunailipia kodi;POLISI
      Wasi wasi wangu ni kwamba CCM wanataka jifunga goli la pili kwa kutumia polisi! Subirini tuone

      Sidhani kama kuna mtanzania ambaye bado aniona hiyo amani na utulivu wakati kunywa chai mpaka alazwe muhimbili apewe ushauri wa daktari, make bei kilo moja sh. 1500?? kwahiyo chai siku hizi anasa!

    15. #152
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,030
      Rep Power : 2564
      Likes Received
      788
      Likes Given
      29

      Default

      Unajua nilisha sema kwamba Mtanzania ana yale ajenda. Nakuheshimu sana rafiki yangu Mtanzania lakini kuanza kubadilsha mwelekeo wa mada ili kuidhoofisha ndiyo mbinu zenu za ki CCM.Mlishasema Chadema ni mali ya mtu lakini watu wakauliza mlete ushahidi kama kweli si Chama cha Kitaifa hadi leo mko kimya . Baada ya kuona mmefanikiwa kuwayumbisha watu kwamba CUF ni wadini mnahamia sasa Chadema mara ruzuku kwenye vyama mara Chama kampuni nk. Leo CCM kuanzia JK , Mkewe , mwanae na mpwa ama mjomba wake wako kwenye uongozi mkubwa ndani ya CCM , watu wakauliza mkasema wana haki kikatiba , tukisema JK sasa kafanya CCM kuwa kampuni mtasemaje ?

    16. #153
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,030
      Rep Power : 2564
      Likes Received
      788
      Likes Given
      29

      Default

      Ninajua baadhi ya watu toka Usalama na Police HQ na Immigration ni wanachama hapa . Sasa nawashauri wajaribu kuwapa ushauri wakubwa wao juu ya maneno ya amani na utulivu .Wote tuna elewa maana ya maneno haya na faida na hasara zake lakini why watu sasa wanaanza kuongea mambo openly ? Ni bora hata Mbowe anasema lakini kuna ambao hawasemi wanajipanga tu sasa kweli hakuna haja ya kupeana haki sawa kwa wote ?

    17. #154
      Ibambasi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th July 2007
      Location : Iponyamakalai - Isungang'holo
      Posts : 732
      Rep Power : 756
      Likes Received
      124
      Likes Given
      790

      Default

      Quote By Lunyungu
      Ninajua baadhi ya watu toka Usalama na Police HQ na Immigration ni wanachama hapa . Sasa nawashauri wajaribu kuwapa ushauri wakubwa wao juu ya maneno ya amani na utulivu .Wote tuna elewa maana ya maneno haya na faida na hasara zake lakini why watu sasa wanaanza kuongea mambo openly ? Ni bora hata Mbowe anasema lakini kuna ambao hawasemi wanajipanga tu sasa kweli hakuna haja ya kupeana haki sawa kwa wote ?
      ni kweli kabisa,raia wengi hawataki kuongea kwa sababu either wamebanwa sana ila wanasubiri mtu mmoja tu AJITOLEE kuwaongoza,na nadhani huu ndio wasiwasi wa serikali (CCM?)mpaka wameamua kutumia mbinu mmbovu kabisa iliyopitwa na wakati,ETI polisi wachunguze maneno ya UCHOCHEZI.kama manumba anaipenda sana nchi hii kwa nini wasijitolee kuchunguza ufisadi na ubadhirifu wa kutisha huko BoT,Kiwira,etc?fine,kama wameingia siasa watuambie itikadi yao ni ipi...naomba kuwasilisha hoja...

    18. #155
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,282
      Rep Power : 5568
      Likes Received
      290
      Likes Given
      77

      Default

      Lunyungu,

      Hilo ndilo tatizo lenu la kuwa na mawazo kama akina Bush "You are either with us or with the terrorists" Tukiwasema CCM mnashangalilia, tukiongelea CHADEMA au upinzani mnaanza kutupachika majina na kutuvisha uanachama.

      Siku nitakayoamua kuwa mwanachama wa chama cha siasa nitasema wazi na sina cha kuficha.

    19. #156
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 4,035
      Rep Power : 1418
      Likes Received
      610
      Likes Given
      44

      Default

      WANA JF
      Ningeomba mnisaidie, nini maana ya "uchohcezi" kwa tafsiri inayotumiwa hapa. Maana hilo neno linatumika vaguely, what actually entails "uchochezi"?. Ukiwashawishi watu waahce ujinga ni uchochezi? Ukivaa kimini ni uchochezi? maana hasa ya hili neno ni nini? Ukiwaambia watanzania peace and harmony without prosperity is madness, ni uchochezi? Au ndio maneno yaliyopo kwenye katiba yenye lengo la kuwashughulikia watu?

    20. #157
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,030
      Rep Power : 2564
      Likes Received
      788
      Likes Given
      29

      Default

      Wacha tuone tafsiri inaendaje toka kwa hao walio nao jirani .

    21. #158
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1174
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Kitila Mkumbo
      Labda itatusaidia kama tutaweza kuonesha hayo ambayo wapinzani wanatakiwa nao wajisafishe. Kwa mfano, kwa CCM tumesema wazi kuwa kuna rushwa kwa sababu wamekatamatana wao wenyewe wakipeana rushwa kupitia hiyo PCCB yao. Sasa unaposema wapinzania wajisafishe, kwa nini pia usiwe specific kwa kusema kwa hili na lile kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa CCM?

      Haya nimeona pia Mtanzania amesema, pamoja na mambo mengine, kuwa wapinzani "wanatafuna ruzuku badala ya kuendeleza wananchi", sasa this is a serious allegation. je, ni kweli kwamba wapinzani wanatafuna ruzuku, hapa nafikiri anamaanisha kuiba au kutumia hiyo ruzuku kwa manufaa binafsi badala ya kuendeleza hivyo vyama vyao, je ana ushahidi wowote na hili? Au msajili wa vyama ametoa report inayoonesha kuwa viongozi wa upinzani wameiba hela za ruzuku? Halafu unaposema "badala ya kuendeleza wananchi", je, tumejibidisha kujua hasa kazi ya hii pesa ya ruzuku kwa vyama vya siasa ni nini?

      Otherwise, naogopa kwamba tutakuwa tunatoa blanket allegations ambazo lengo linaonekana sio kusaidia sana katika kupambana na ufisadi nchini mwetu bali kuhalalisha kwamba vyama vingine navyo ni vichafu kama CCM, wakati, in the absence of credible evidence, sio kweli!
      Kitila at aleast sasa tunaanza kuongea substance.

      Hoja zako ni nzuri sana, kosa kubwa tunalolifanya hapa ni kufikiri upinzani ni Chadema na Chadema ndio upinzani (haijaandikwa popote bali ni observation yangu tu), niliposema wapinzani (kwa ujumla wao) wasafishe nyumba zao kwanza nilikuwa nalenga pamoja na mambo mengine yafuatayo;

      1. Demokrasia ndani ya vyama, tumeshuhudia Mrema na Cheyo wanavyoendesha vyama na kufukuza viongozi na wanachama kila wanapopingana kimawazo.

      2. Migogoro na uchu wa kugombea madaraka ( same as above)

      3. Matumizi mabaya ya Ruzuku ( mfano Mrema kajinunulia nyumba Sinza na katangaza chama kimemuenzi na kumpa)

      4. Kauli vitisho zenye kuhatarisha amani na utulivu ( Mbowe, CUF, nk)

      5. Kujiimarisha na kuwa na mtandao mzuri wa matawi nchi nzima kwa vyama vyote ( Mfano uchaguzi uliopita kuna majimbo kadhaa wapinzani hawakusimamisha wagombea kwenye ubunge na kwenye Udiwani ndio zaidi)

      6.Harufu ya Udini (CUF)

      7. NK

    22. #159
      Jembajemba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2007
      Posts : 706
      Rep Power : 771
      Likes Received
      8
      Likes Given
      3

      Default

      Quote By ibambasi
      ni kweli kabisa,raia wengi hawataki kuongea kwa sababu either wamebanwa sana ila wanasubiri mtu mmoja tu AJITOLEE kuwaongoza,na nadhani huu ndio wasiwasi wa serikali (CCM?)mpaka wameamua kutumia mbinu mmbovu kabisa iliyopitwa na wakati,ETI polisi wachunguze maneno ya UCHOCHEZI.kama manumba anaipenda sana nchi hii kwa nini wasijitolee kuchunguza ufisadi na ubadhirifu wa kutisha huko BoT,Kiwira,etc?fine,kama wameingia siasa watuambie itikadi yao ni ipi...naomba kuwasilisha hoja...
      Ibambasi, mbona itigadi yao ipo wazi huna haja ya kutafuta tochi.
      .....Being against is not enough. We also need to develop habits of constructive thinking. Edward de Bono


    23. #160
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,282
      Rep Power : 5568
      Likes Received
      290
      Likes Given
      77

      Default

      Kitila,
      Unataka hata nyie CHADEMA mpaka mkamatwe na PCCB ndio mjue au msafishe mapungufu yenu?

      Mengi niliyotaka kuandika naona Masatu kayaandika.

      Pia nafikiri kwa CHADEMA kuna malalamiko kuhusu ugawaji wa nafasi za ubunge kwa wanawake.

      Kulikuwa na suala la viongozi wengi kutoka Kilimanjaro lakini nafikiri hili mmelishughulikia na sasa kamati kuu yenu inawakilisha karibu nchi nzima. Huko ndiko kujisafisha tunakokusema, sio lazima kusubiri PCCB.

    Page 8 of 26 FirstFirst ... 67891018 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Je, wapinzani ni wakombozi?
      By Mzee Mwanakijiji in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 494
      Last Post: 24th July 2011, 12:29
    2. Ukombozi kutoka kwenye Makucha ya Wakombozi Wetu.
      By Kakalende in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 0
      Last Post: 20th April 2008, 12:55
    3. Hawa Wachina Ni Wakombozi Wa Africa Au?
      By Field Marshall ES in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 26
      Last Post: 2nd March 2008, 14:13

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...