Nguruvi3, sitarajii kupata usuli (feedback) kwasababu yapo mambo ya chama yasiyotakiwa kujadiliwa hadharani. Hili la Arusha lina embarrassment kubwa kwahiyo uchangiaji wa wahuisika wa 'pande zote' kama ulivyosema unakinzana na maslahi ya leo au baadaye.
Tulijadili katika kiwango cha mawazo huru na changamoto.
Mgogoro wa Arusha kwa
external risk ulikuwa nazo nyingi kutoka CCM na Serikali. Kumbuka Jiji la mwanza lipomikononi mwa Chadema, Mbeya inaelekea huko, Dar es Salaam ndio hofu ilipo-Chadema imepenyeza katika hot spot na gome ya Iringa imeanguka, Singida tayari kuna uasi.
Mahali Salama kwa CCM ni Mtwara, Lindi, Songea, Tanga, Morogoro, Dodoma.
Kuiachia Arusha ni jambo la mwisho na wangetumia mbinu iwe ya moto,ushirikina au
ulaghai ili kubaki na kiti cha AR.
CCM wanajua kuwa Mwanza na Arusha zikiongozwa na Chadema kwa mafanikio ya Karatu na Tarime itakuwa ugonjwa unaosambaa.
Wanajua rasilimali za AR, umuhimu wake kama makao ya EAC na ushawishi wa AR kwa mikoa jirani.
Chadema walijua hili ndio maana kampeni yao ilivuka hadi mikoani. Kinachoshangaza walikubalije
ulaghai wa CCM kuingia muafaka kwa kutumia madiwani! Walijua lengo ni kuweka Meya wa CCM sio maendeleo ili kuizima Chadema kisiasa,wakakubali mazungumzo.
CCM walipofanikiwa wakatangaza muafaka(jambo jema), halafu wakaanza kampeni za kupaka matope Chadema kuwa ni watu wa vurugu, hawajui wanadai nini, wanakiuka taratibu n.k Pressure ikawepo kutoka katika base ya Chadema iliyokasirishwa sana na muafaka wa kumpa mtu 1 unaibu meya na mwingine mkuu wa kamati kwa gharama kubwa sana ya miasha na ulemavu wa watu.
'External elements' zimekuzwa kwasababu ya internal weakness. Ukitaka kuona udhaifu ni pale kamati kuu inapowasiliana na madiwani moja kwa moja, hatujasikia uongozi wa wilaya au mkoa na ushiriki wake. Maana yake ni kuwa structure haipo sawa. Sijui kama ndio muundo wa Chadema lakini network ya kutoka mwenyekiti Taifa na kuwasiliana na m/kiti wa kata, mhh! naliona tatizo naweza kuwa
panaoic, ila ni tatizo.
Hivyo kukawa na external na interna pressure. Siku zote Chadema ni wazito sana wa ku r
eact kwenye
political issues! pengine huwa wanatafuta umakini, lakini unapokuwa na suala nyeti kama la Arusha ukaliacha siku 14 lijiulize na kujitolea majibu unasababisha
damage kubwa sana.
Hawakufanya
damage control katika kipindi cha wiki mbili wakajikuta wanafanya
crisis management kwa kuunda tume, ambayo kimsingi haikuwa na sababu ya kuwepo!
politically imefanikiwa lakini kimantiki sina uhakika!
Wanachama na wapenzi wamefurahia maamuzi ya CC ya Chadema kwa kuangalia mambo haya;
1. Muafaka haikuwa lengo la maandamano, vifo, ulemavu ili tu mtu awe naibu meya
2. Ilionekana kuwa imewadhalilisha mbele ya umma hasa kwa kejeli za CCM
3. Madiwani wamechukuliwa hatua stahiki kwa utaratibu stahiki na wakati muafaka
4. Chama kimeonyesha njia ya maamuzi magumu hata pale yanapokinzana na masilahi.
Pamoja na
excitement iliyopo, inabidi Chadema walichukue suala la Arusha kwa kujitathmini katika mawasiliano, muundo wa chama, damage control startegy na chochote kilichojiri katika sakata zima.
Msimamo wangu ni kuwa sina tatizo na kile Chadema ilichoamua kusimamia Arusha wala sina tatizo na maamuzi. Tatizo nilionalo ni kuwa handling ya ile issue nzima ikiwa ni pamoja na hukumu kwa baadhi, haikuwa katika viwango
Follow Us Here