Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

    Report Post
    Page 15 of 22 FirstFirst ... 51314151617 ... LastLast
    Results 281 to 300 of 426
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,518
      Rep Power : 46714
      Likes Received
      16434
      Likes Given
      8469

      Default Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Kuanguka kwa CCM – Unabii Utatimia?

      Iko siku ambapo Watanzania wataamka na watakuta kwamba Chama cha Mapinduzi hakishiki tena hatamu za uongozi wa nchi, na badala yake Ikulu na Bunge vimechukuliwa na chama kingine. Siku hiyo ambayo haina jina, itakuwa ni siku ambapo Chama cha Mapinduzi kitaanguka kwa kishindo kikuu na sauti ya kuanguka kwake itasikika kila kona ya Tanzania, na mwangwi wa kuporomoka kwake kurindima katika bara letu la Afrika na mabaki ya mtetemo wa kuvunjikavunjika kwake kusimuliwa kama hadithi za Alfu Leyla wa Uleyla kwa vizazi vijavyo vya Watanzania. Kuanguka kwa Chama cha Mapinduzi kutakuwa ni mwanzo wa msemo, na bila ya shaka kutatungiwa methali.

      Siku hiyo ni siku ambayo kina Malecela, Msuya, Kingunge, Kikwete,Lowassa,Makamba,Karume na magwiji wengine wa Chama hicho waombee wasijeiona. Kwani itakuwa ni siku ya huzuni kwa watawala na furaha kwa watawaliwa! Itakuwa ni siku ambapo “nyota ya jaha” itaangazia Taifa letu na nuru ya “jua la haki” itachomoza na miale yake kumulika kila kona ya Taifa letu. Hiyo ni siku ambapo kama mwali atolewaye nje, kila mtu atatamani kuiona isipokuwa wale ambao huyo mwali ni ishara ya wao kukosa mke na wengine kupata!

      Bila ya shaka unajiuliza iweje nianze kwa kusema maneno hayo. Nilikuwa natafakari maneno ya Mwalimu aliyoyatoa mwanzoni mwa miaka ya 90 mara baada ya vyama vingi kuruhusiwa tena nchini. Baada ya Mwalimu Nyerere kutoa maneno makali ya “Ikulu inanuka Rushwa” watu wengi walianza kujiuliza mapenzi ya Mwalimu kwa chama alichokiasisi na kama anaweza kujitoa kwenye chama hicho. Alipoulizwa kuhusu kujiondoa CCM, mwalimu alijibu “CCM siyo Mama yangu”. Maneno hayo ya Mwalimu yamebakia mawazoni mwangu (na bila shaka ya wengine pia) kama unabii na kama wosia. Hii leo kuna baadhi ya viongozi wa Chama tawala ambao wanasisitiza maneno ya Mwalimu ya “Bila CCM madhubuti Tanzania Itayumba” na kusahau kabisa maneno hayo ya onyo kali kuwa hata kama mtu ana mapenzi kiasi gani na CCM, iko siku anaweza kukiacha na kujitahidi kukivunja! Ni rahisi kukiacha CCM kuliko kumuacha Mama mzazi!

      Siku hiyo ambapo Chama hiki maarufu kitakapojikuta kiko katika kambi ya upinzani ndipo viongozi wake na mashabiki wake watakapotambua kuwa “CCM siyo Mama” na Tanzania itaendelea na inaweza kuwepo bila CCM kuwa madarakani! Hiyo siku iso jina, iko, yaja, na yafanya hima kufika! Kwanini basi CCM itakuja kuanguka kwa mshindo mkuu namna hiyo?

      Ndugu zangu, punda mnyama wa kazi kuna mahali anafikia kikomo! Na akifikia kikomo, punda hendi hata kwa mijeredi mia. Mtu unaweza kumtwisha punda mizigo, lakini akifikia kikomo chake hata umfanye nini punda hanyanyui mguu. Kuna baadhi ya viongozi ambao wanadhani kuwa Watanzania wataendelea kuinama na kukubali kutwishwa mizigo ya kila namna kana kwamba hawasikii maumivu! Ni hawa viongozi ambao huendelea kutuingiza katika mikataba mibovu, wanaendelea kuvumilia ufujaji wa mali ya umma katika maofisi yao, wanaendelea kupuuzia rushwa hadi imezoeleka na kuonekana kama kawaida. Viongozi hawa wanaimba wimbo na pambio ya uongozi bora wakitumbuiza kwa kasida za maneno ya kizalendo. Mawazoni mwao wanaishi wakifikiri kwamba Watanzania wataendelea kuvumilia. Kama punda iko siku hugoma, iko siku Watanzania nao watasema “Sasa inatosha”!

      Siku moja ambayo ipo, Watanzania watajiuliza iweje viongozi wetu wanunue rada Bilioni 40 wakati hospitali yetu ya kijiji yenye kugharibu shilingi milioni moja haina hata bomba la maji! Hiyo siku Watanzania watajiuliza iweje ili kupata elimu nzuri ni lazima wapeleke watoto wao kwenye shule binafsi wakati shule za serikali zilizokuwa zikisifika huko nyuma zikibakia historia? Hawa wana na mabinti wa Tanzania wataamka siku moja na kusema “Imetosha”.

      Chama cha Mapinduzi kitaunguka pia kwa sababu hatimaye Watanzania wataelewa ya kwamba kuendelea kukaa kwa chama hicho madarakani ni kujitakia kutokuendelea na kurudi nyuma kwa maisha yao. Wataelewa kuwa CCM haina lengo hata chembe la kutimiza na zaidi ya kutimiza ahadi zake ambazo imekuwa ikizitoa tangu uhuru. Itadhihirika kuwa CCM iko madarakani ili kuendelea kujikita katika kutawala huku wakifanya mambo machache ya manufaa kwa wananchi huku viongozi wao na watu wachache waliobarikiwa na chama hicho wakiishi katika paradiso ya Bongo.

      CCM itaunguka kwa sababu hata kipofu akigonga ukuta anauzunguka! Kutokuona siyo kikwazo cha kujua kukwama. Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikifanya mambo kana kwamba Watanzania wote ni vipofu na viziwi. Miaka nenda rudi tumewapa imani kuwa labda watabadilika. Wanavutia kwa maneno matamu na nyimbo za shangwe, wanafurahisha kwa rangi nzuri za mavazi yao, na mvuto wa kupepea kwa vibendera vyao vya kijani! Lakini wamekuwa kama makaburi yaliyopakwa chokaa, lakini ndani yake ni mifupa mitupu! Siku hiyo watanzania watakuwa kama kipofu aliyeona mwezi. Watagundua kuwa CCM siyo jua bali ni mwezi mchanga na mwanga ambao watu wamekuwa wakiusifia si mwangaza wa jua, bali mmuliko wa mbalamwezi. Watagundua kuwa wanachotaka kimulike maisha yao na kuanzia maisha ya watoto wao ni chama na viongozi wenye nuru ya jua, ambao mwangaza wao hautegemei kuakisiwa na kitu kingine bali unatoka ndani yao wenyewe! Wataamua kuachana na Chama ambacho miaka nenda rudi kimekuwa kikijificha kati yao mwangaza wa jua na hivyo kuwapa kivuli cha “kupatwa jua”. Watu wamekuwa wakiogopa kuwa huo mwezi ukiondoka kati yao na jua, dunia itafikia mwisho! Kumbe zote hizo ni porojo. Mwezi huzija jua, lakini hatimaye hupisha!

      Chama hicho kitaanguka si kwa sababu hakina watu wenye sura nzuri, na watanashati kwani wamejaa tele, siyo kwa sababu hakina watu waliosoma na kubobea katika nyanja mbalimbali kwani wapo bwelele, bali kwa sababu wale waliodhaminiwa uongozi katika chama hicho na kwa kupitia chama hicho nchi yetu, ni viongozi wasio na maoni, waliolala hadharani, wenye kutetea maslahi ya matumbo yao na ya wanawe, wakihangaika kutwa kucha kufikiri ni jinsi gani watamegeana fedha za walipa kodi. Kwa kutumia vipaji vyao na elimu yao baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wamebuni miradi hewa ya kugereshea umma huku fedha nyingi za miradi hiyo zikiishia vibindoni mwao. Watanzania hatimaye watatambua kuwa wakati wa kuangalia onesho la mazingaombwe umepita, na watataka kitu halisi! CCM haiwezi kubadilika, imelewa ugimbi wa madaraka na kuvimbiwa na mlo wa uchu! Ndiyo! Watanzania watagundua ya kuwa kuwa na CCM au kutokuwa nayo yote ni sawa! Hawana cha kupoteza tena. Kama miaka yote hiyo CCM imeshindwa kuboresha elimu yetu, sekta ya afya na maji, matatizo ya nishati n.k itakuwaje waweze kufanya hivyo miaka arobaini ijayo wakati kizazi kinachoingia madarakani sasa ni cha wana na wajukuu wa viongozi wa chama hicho!? Watanzania watasema “CCM Asante, lakini Kwaheri”!

      Watakishukuru chama hicho kwa kutujengea misingi ya udugu, umoja na mshikamano. Watakishukuru chama hicho kwa kutulindia utaifa wetu na kuhakikisha kuwa tunabakia kuwa huru kisiasa. Watakishukuru Chama hicho kwa kutujengea utambulisho wetu wa “watanzania” na kutufutia hisia ya ukabila na udini. Ndiyo, watakishukuru chama hicho kwa yale machache mazuri ambayo kimefanya kwa muda mrefu, barabara chache za lami, shule, mahospitali, n.k Ndiyo, Watanzania watasema “asante”!!

      Lakini wana hao na mabinti hao wa Kitanzania pia watasema “Kwaheri”! Watakiambia chama hicho kwaheri kwa kushindwa kujenga misingi mizuri ya utawala wa kidemokrasia! Watakiaga chama hicho kwa mamia baada ya kugundua kuwa hakina lengo la dhati la kuwashughulikia wala rushwa wakubwa na viongozi wabadhirifu! Watakiaga chama hicho baada ya kuona kuwa Mikakati yake mingi yenye majina ya ajabu ni sehemu ya mazingaombwe hayo! Wataangalia maisha ya viongozi hao na watoto wao na kuona kuwa wenzao wananeemeka wakati wao wanaganga njaa! Ndiyo! Watakiaga chama hicho kwa sababu, hatimaye watagundua ya kuwa njia pekee ya kukifundisha somo la utawala ni kuwaweka nje ya madaraka na kuwanyima nafasi nyingine ya kura na kula! Ndiyo, CCM itaanguka! Watatambua ya kuwa CCM ni chama cha kisiasa na siyo mama yao mzazi! Watakiaga na kushukuru kwa onesho lao la mazingaombwe, lakini wakati umefika wa kuingia kazini!

      Ni matumaini yangu kuwa maandamano ya wapinzani yanayofanyika jijini Dar hayatakuwa ni ishara tu ya kuchukizwa na matendo ya serikali ya CCM na ufisadi uliokithiri. Ni matumaini yangu kuwa viongozi wa vyama vya upinzani watadhamiria kushirikiana siyo katika kupiga kelele kwa kutumia vipaza sauti hapo Jangwani bali ushirikiano wa kweli utakaofanya waziunganishe nguvu zao na kuunda chama kipya cha siasa chenye itikadi inayoakisi matamanio na matarajio ya Watanzania wengi, na chenye viongozi ambao kwao utumishi wa Taifa lao ndio kitu kinachowasukuma!

      Endapo wapinzani wataishia kuwa waandamanaji, na wapiga kelele lakini wakishindwa kuungana na kutuonesha kuwa wako makini na mafanikio ya nchi yetu, basi CCM itaendelea kupeta kila kukija uchaguzi! Wapinzani wasililie huruma ya CCM ili wabadilishe Katiba au kuwajengea mazingira mazuri ya kushindana nao! Wapinzani wachukua hatima yao mikononi mwao wao wenyewe! Wawaambie Watanzania kuwa lengo lao mwaka 2010 ni kulichukua Bunge la Tanzania kwani limeendelea kuwa kicheko na dhihaka katika utawala wetu wa Demokrasia! Bunge lenye kutoa azimio la kulaani filamu ya mapanki kabla hawajaiona, na likakaa kimya kwenye mikataba ya madini na nishati bila kutoa azimio la kulaani mikataba hiyo, wabunge wa bunge hilo waondolewe kwa kura! Bunge ambalo linatumia siku 60 kuzungumzia maneno ya watu wawili na kushindwa kutumia siku moja kuzungumzia suala la rada, Richmond, IPTL, ATC n.k hilo ni bunge uchwara!! Bunge lenye spika anayeangalia matumizi ya maneno “kukaza” na “kutia” badala ya kuangalia matumizi ya shilingi Bilioni 80 ya vitu tusivyovihitaji Bunge hilo ni karibu ya Bunge la serikali ya nchi ya Wagagagigikoko! Kama kweli wanataka kuwapa Watanzania matumaini viongozi wote wa upinzani ifikapo 2010 wagombee Ubunge wakiwa wamuengana na kuhamasisha Watanzania wawachague wanachama wao! Kama Watanzania watataka Kikwete apewe nafasi nyingine hilo lao, lakini Bunge lisiende CCM!

      Wapinzani wakiweza kunyakuwa wingi katika Bunge la Muungano, basi mwanzo wa CCM kuporomoka utakuwa umefika! Wakiweza kuwashawishi Watanzania baada ya wao kuungana kuwa wanamaanisha wanachosema basi CCM itaanza kutikisika! Watakapochaguliwa Wabunge na wakaanza kusimamia na kupitisha sheria ambazo zina manufaa kwa wananchi watamlazimisha Rais azikubali au atumie uwezo wake wa turufu. Na akifanya hivyo kwenye miswada fulani mara kadhaa avunje Bunge na uchaguzi mpya utafanyika! Huo utakuwa ni mwisho wa Kikwete, huo utakuwa ni mwisho wa CCM!

      Je wapinzani wako tayari kusimama na kuchukua nafasi yao ambayo historia imewatengenezea? Je wako tayari kuitwa majina na kujipanga mstari kuongoza Taifa letu? Je, ndani ya vyama hivyo wapo kweli viongozi ambao Tanzania inaweza kuwaangalia na kuwategemea kuwavusha kutoka katika jangwa la utawala wa CCM.

      Kuna maneno ya Maandiko Matakatifu yanayosema “Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha, geukeni upande wa kaskazini.” (Kumb. 2:3). Ndugu zangu Watanzania, tulivyouzunguka mlima wa CCM sasa imetosha! Tulivyouimbia kwa kuuzoea na kuusifia utawala mbovu wa chama hicho sasa inatosha! Tulivyozoea mazingaombwe na mikataba iliyodumaza uchumi wetu sasa inatosha! Ndiyo CCM inaweza kuwa na watu wachache waadilifu, wamwogopao Mungu, na waipendao nchi yao! Ndiyo inawezekana kuna wale wanaojaribu kuibadilisha toka ndani ili ikidhi mahitaji ya Taifa letu, hata hivyo kuombea watu hawa wapo, inatosha! CCM imefanya mambo mengi mazuri kwa Taifa lakini yakipimwa na yale mabaya kwenye mizani ya Mama Haki, mambo mabaya yanazidi kwa uzito na wingi wake yale mazuri! Kuombea kuwa miaka mitano ijayo mambo yatabadilika inatosha! Tugeuke upande tofauti! Labda tutafika iliko NCHI YA AHADI!

      Kwani kuanguka kwa chama hicho kupo, kunakuja, na kunafanya hima kutufikia. CCM siyo mama yetu! Unabii huo utatimia!!!

      ( nitasahihisha kesho)
      Last edited by Mzee Mwanakijiji; 20th January 2007 at 03:05.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. Miaka 50

    3. #281
      Simoni's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th October 2008
      Posts : 67
      Rep Power : 555
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      CCM kufa? Hapana. Itakachofanya ni kujivua magamba yake kwa sababu CCM ni kizazi cha nyoka. Na vyama vyote vya siasa ni vya uzao huo. Wanaokufa ni viongozi wake basi. JK ataondoka 2015. Baada ya hapo kizazi chake watabakia wachache bungeni. Ikifika 2025 wote watakuwa hawana impact. Wakiwa hai basi watakuwa vikongwe kama walivyo akina Kinguge na Kawawa leo. Nina hakika wewe MM na wengie wetu tunaochangia mada hii ndani ya JF mwaka huo hata meno yatakuwa tunayo ya badnia na wengine watakuwa wametangulia mbele ya haki.Sawa unzungumzia utabiri. Na mimi nakubali. Unajua nyakati hizi zilitabiriwa na Biblia na hata Muhamad (SAW). Si CCM wala si CUF wala CHADEMA ambao viongozi wake ni safi. Hawa wanagombea fursa ya kuendeleza ufisadi. Kwa hiyo jawabu siyo CCM kufa. Imetokea tu hizi ni enzi za ufisadi na hivyo ndivyo ilivyotabiriwa.Leo hii nchini Tanzania tupo enzi za Nuhu. Wapo watu tena wengi sana ambao wamejichimbia katika anasa na ufisadi ambao hata uwaambie vipi roho zao ziliisha kufa. Inatisha kuwa waovu hao wamejaa miongoni mwa viongozi wa serikali na vyama vya siasa, NGOs, makanisani, misikitini, ndani ya familia zetu. Kwa kweli tuko zile enzi ambazo Paulo alimwambia Timotheo katika 2 Timotheo 3 1-9 ambazo ni:• nyakati za taabu. Angalia hali ya uchumi na umasikini miongoni mwa watanzania wengi na utajiri uliokithiri mikononi mwa watu wachache. • Watu wana ubinafsi. Kila mtu anajipigania mwenyewe. Hakuna upendo wa dhati hata kati ya mke na mume wala watoto na wazazi na ndugu hata wa tumbo moja. Kila mtu kivyake vyake tu.• Watu wana tamaa ya fedha mno. Migogoro ya DECI, Upatu na watu kurushana na kutapeliana imkekuwa nim jambo la kawaida.• Watu wana majivuno. Angalia kiburi walicho nacho watanzania wengi?• Watu ni wenye kujiona (dharau). Wanawake kwa waume.• Watu wanamtukana Mungu. Hawamuogopi Mungu ndiyo maana madhambi yamezidi. Angali kashfa za ngono kila uchao. Watu wazima na watoto wadogo. Ushoga, Usagaji n.k Kila guest house inayojengwa inalenga kukidhi shughuli ya ngono.• Watu hawatii wazazi wao• Watu hawana shukrani• Watu ni waovu• Watu hawana upendo moyoni• Watu hawana huruma. Angalia vibaka wanavyouawa. Polisi inavyodhulumu wananchi. Serikali yenyewe inavyodanganya wananchi na kuwaibia haisemeki.• Watu wachongezi (masengenyo, kusingizia)• Watu walafi• Watu wakali• Watu wanachukia chochote kilicho chema. Kilicho haramu kinaonekana halali na kushabikiwa na kushangiliwa na wengi.• Watu ni wahaini• Watu ni wakaidi. Hakuna anayetii utawala wa sheria. Ni nchi isiozingatia sheria• Watu wamejaa kiburi. Watanzania wengi ni wabishi na wajuaji.• Watu wanapenda anasa kuliko Mungu. Angalia miradi mingi ni ya starehe na burudani nchi hii. Kila kijana anataka kuwa msanii. Lugha na hata msamiati unaozungumzwa mpaka na hata viongozi ni wa kihuni.• Wengine wanajifanya wameokoka na kumcha Mungu lakini hawakiri nguvu ya Mungu• Baadhi ya wachungaji badala ya kuwasaidia wanawake ambao huwaendea ili kusaidiwa kwa Neno na kujifunza wanazini nao Haya ni mambo ambayo yaliishatabiriwa na yapo na sisi. Tunachotakiwa ni kufanya kama alivyofanya Nuhu. Kuendelea kumcha Mungu na kuongozwa na Roho wake Mtakatifu ili tusije tukaangamia. Miili yetu tuisalimishe kwa Roho Mtakatifu ili isije ikatuangamiza. Tuepuke kuingia kwenye mojawapo ya kundi hilo.

    4. #282
      Kikojozi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th March 2009
      Posts : 338
      Rep Power : 585
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Tatizo sio CCM. Tatizo ni kushindwa kwetu kuiwajibisha.

      CCM kuondoka sio suluhisho kwani kitakuja chama tawala kingine na kuvurunda kama CCM.

      Suluhisho tujifunze kuwajibisha chama na serikali.

      Nasisitiza: TATIZO SIO CCM
      "A failure is a man who has blundered, but is not able to cash in on the experience." - Elbert Hubbard

    5. #283
      Rwabugiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Posts : 2,737
      Rep Power : 1158
      Likes Received
      67
      Likes Given
      31

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Quote By Kikojozi
      Tatizo sio CCM. Tatizo ni kushindwa kwetu kuiwajibisha.

      CCM kuondoka sio suluhisho kwani kitakuja chama tawala kingine na kuvurunda kama CCM.

      Suluhisho tujifunze kuwajibisha chama na serikali.

      Nasisitiza: TATIZO SIO CCM
      You are kidding!
      ofcourse am sure you know for real TATIZO NI CCM

    6. #284
      Mwawado's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2006
      Location : Tulsa, Oklahoma/MFA-TZ
      Posts : 1,263
      Rep Power : 899
      Likes Received
      113
      Likes Given
      219

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Quote By Kikojozi
      Tatizo sio CCM. Tatizo ni kushindwa kwetu kuiwajibisha.

      CCM kuondoka sio suluhisho kwani kitakuja chama tawala kingine na kuvurunda kama CCM.

      Suluhisho tujifunze kuwajibisha chama na serikali.

      Nasisitiza: TATIZO SIO CCM

      Tatizo ni CCM.......Na sasa hata wale mliowaona wamelala kule Malampaka na Namtumbo wameanza kuona na kujua Ukweli!!Ipo siku isiyokuwa na jina na wala haipo mbali CCM itaanguka anguko la kutoamka!!
      Its not enough to do good if you can do better.

    7. #285
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,518
      Rep Power : 46714
      Likes Received
      16434
      Likes Given
      8469

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Unabii unaelekea kutimia mapema zaidi!
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    8. RukaaJuu Final

    9. #286
      Mopao Josee's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2009
      Posts : 282
      Rep Power : 558
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Lisemwalo lipo....................ila na sisi tubalikeeeeeee tunapigwa mabomu bado tunawakumbatia,tunalazwa kwenye madarasa wakati tuna kwetu BADO hatuoniiii???????? JAMANI mpaka wachukue wake zetu ndo tutareact????? migao ya umeme kwa ujanja wa watu fulani.....TULIANZA NA ARI,NGUVU,KASI MPYA IKASHINDIKANA TUKARIBU MAISHA BORA KWA KILA MTZ,NAYO BILABILA SASA KILIMO KWANZA.duh haah haaa haaaaaa WADANGANYIKA TUNASONGA.

    10. #287
      Sabi Sanda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 298
      Rep Power : 736
      Likes Received
      4
      Likes Given
      2

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Tumuombe Mheshimiwa Rais asigombee Urais Mwaka ujao wa 2010. Pia tubadilishe katiba ya nchi yetu na kuwa na utaratibu kuwa kuanzia mwaka 2010 mtu atakuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi kimoja tu cha miaka mitano tu. Pia itabidi tuweke sheria kuwa kila mwaka wakati wa kipindi cha BUNGE la BAJETI Wabunge wetu wataifanyia tathmini ya utendaji Serikali ya Rais aliyeko madarakani na kutoa uamuzi kama inapasa kuendelea kutuongoza kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja au laa. Uamuzi huu BUNGE letu litaufanya kupitia njia ya kura ambapo utaratibu unaopendekezwa ni kwa hoja kuungwa mkono ya 2/3 ya Wabunge wa Chama tawala na 2/3 ya Wabunge wa Vyama vya Upinzani.

      Naomba kuwasilisha na siku njema kwenu wote.

    11. #288
      kisikichampingo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th October 2009
      Posts : 127
      Rep Power : 512
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Jamani eeeh, naomba kuelimishwa kidigo. Kuna nchi nyingine mbali na Tanzania ambayo Chama Chake kimetawala tangu uhuru wao? Naamini ni chache sana- kama zipo. Kwa maana hii, kuanguka kwa SI SI EM ni dhahiri!

    12. #289
      Chapakazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2009
      Location : Kathmandu
      Posts : 2,910
      Rep Power : 1096
      Likes Received
      256
      Likes Given
      272

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      CCM will definitely go one day! But i dont believe that day is soon! Sababu:

      1. Kuna sehemu nyingi sana nchini hawajui anything beyond CCM.

      2. Watu wengi wamewekeza ndani ya CCM, na hao watu wahatapenda kuona investment yao inaisha. Hawa ndo mafisadi. Msidhani mafisadi ni watu wanaoiba pesa za umma tu, bali hata wafanyabiashara wakubwa waliowekeza CCM wanaopata dili ndogo ndogo ambazo hatujazi-shtukia. Hivyo kuiondoa CCM, sio vita against chama tu, bali ni vita against an elite group of mafisadi ready to pump money and everything else in order to keep CCM in power.

      3. Watanzania wengi hawajui maana ya maisha bora. They think in personal terms badala ya jamii na nchi kwa ujumla. Hii ndo sababu kuu watu wanapokea rushwa katika uchaguzi kwa kusudli wao binafsi kupata mlo. Sio kila mtu lazima awe tajiri, but we can all live a better life. Some of us were never meant to be wealthy, but have enough to live our lives. Bongo kila mtu anataka kuwa millionaire. Wapi na wapi jamani?!
      Change begins with YOU

    13. #290
      Nanu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th May 2009
      Posts : 1,212
      Rep Power : 755
      Likes Received
      38
      Likes Given
      77

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Mambo si rahisi kihivyo. Itachukua miaka mingine 20 CCM kushindwa katika nchi hii. Nadhani, wale wenye maono na kuionea huruma nchi hii, wajitahidi kugombea ubunge ili upinzani angalau wawe karibu na 50% ya wabunge wote ili waweze kudictate miswada ya kupitishwa kwa maslahi ya nchi. Hata kwenye demokrasia komavu zenye uchumi komavu imechukua miaka mingi chama cha upinzani kuchukua madaraka. Zanzibar yawezekana upinzani kuchukua lakini si Tanzania. Na hali hii inabidi hata watawala wa sasa wajue ili yakitokea Zanzibar wasitume jeshi kwenda kuzima kama vile mapinduzi yametokea.
      Peace is meaningless if nothing is right. Do it and Do It Right or Not at All.
      Swallowing His Own Words has never Killed the Politician!

    14. #291
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,625
      Rep Power : 2894
      Likes Received
      3845
      Likes Given
      12250

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Marehemu Karume alikuwa anajigamba kuwa hakutakuwepo uchaguzi Zanzibar kwa miaka hamsini. Miaka sita baadaye alikuwa dead. CCM kama any other empire in history will see its demise in our lifetime. You can quote me on that.

    15. #292
      SYLLOGIST!'s Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th December 2007
      Location : Tanzania
      Posts : 222
      Rep Power : 627
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Manabii ndio nani?
      Reductio ad Absurdum

    16. #293
      Chechenya's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th December 2008
      Posts : 45
      Rep Power : 541
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Mwanakijiji uliyosema au unachotabiria ni kweli. Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri walejee kwa kile kilichotekea SOVIET UNION na chama chao cha kikomunist. Ilikuwa asubuhi na mapema watu walipoamka Boris Yelsini alitangaza kuvunjika kwa dola la KISOVIET. Mali zote za chama zikawa za serikali. Magazeti kama PRAVDA na Komsoskaya yakaambiwa wachukue mitambo yao waondoke kwenye majengo ya umma na wala si ya chama. Majengo yote yaliyokuwa yanatumiwa na chama Yelsin Borisi akayatia makufuli. Wat hawakuamini kilichotokea. Huo ndiyo ukawa mwisho wa Chama tawala katika dola kubwa duniani. Kwa wale wenye kumbukumbu zaidi waziweke hapa ili akina KINGUNGE na wenzake wasome alama za nyakati. Nawasilisha hoja MKUU.

    17. #294
      Sabi Sanda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 298
      Rep Power : 736
      Likes Received
      4
      Likes Given
      2

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Wapinzani mteueni Dr. Slaa kama Mgombea Urais wenu na Mumtangaze Rasmi Kabla ya Januari 2010. Na Maalim Seif Awe Mgombea Mwenza. Pia Tangazeni Kuwa Profesa Ibrahim Nguyuru Haruna Lipumba atakuwa Waziri mkuu akisaidiwa na Zitto Kabwe kama Naibu Waziri Mkuu. Mrema Mpeni Tena Mambo ya Ndani. Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa sasa awe Waziri wa Fedha na Uchumi. Dr Adolf Faustin Kazimoto Mkenda (Nishati na Madini akiwa kama Mbunge wa Kuteuliwa). Na kuanzia Januari Moja 2010 muwe na saa tatu kila siku kwenye Radio zote na TV zote hapa nchini mkiwasiliana na Watanzania wote moja kwa moja. Kazi kwenu na Jumamosi Njema

    18. #295
      Milindi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd March 2009
      Posts : 219
      Rep Power : 564
      Likes Received
      45
      Likes Given
      253

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Hongera mwanakijiji,Kitila na wengine,Dawa ya CCM ni kuungana vyama vya upinzani na kuiondoa CCM madarakani,naomba wana jamii wote tuwe wa kwanza kutia sahihi barua itayoandaliwa na washika dau wakiongozwa na Docebit Kitila kwenda kwa vyama vya upinzani kuwaambia kuwa Watanzania tuntaka chama kimoja cha upinzani chenye nguvu.Tofauti zilizojitokeza Tarime,Busanda na kwa Kabuye zizikwe na vyama viungane kuwang'oa hawa mafisadi madarakani.au walio katika vita ya ufisadi ndani ya chama tawala wajiondoe waanzishe chama kingine kwani utabiri mwingine utakuwa umetimia kuwa wapinzani bora watatoka CCM.Maana tunaona dalili zote za kusambaratika za CCM.
      Wainzani ungana pamoja ondoa ccm madarakani.

    19. #296
      Asked for a BAN's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 11th December 2008
      Posts : 5,550
      Rep Power : 0
      Likes Received
      21
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      CCM na Unabii havina uhusiano!

    20. #297
      Kamuzu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th October 2008
      Location : Vigwaza
      Posts : 716
      Rep Power : 684
      Likes Received
      122
      Likes Given
      48

      Default Re: Jopo La wabunge kuihama CCM

      Mimi siwaamini tu ....... hivi ukilichoma moto chaka walilojificha nyoka wa sumu kali, halafu akatoka simba kuukimbia huo moto kuelekea ulipo, je utampokea ? bila shaka jibu ni hapana. basi wote ni wabaya tu kama waliweza kuishi pamoja bila mkwaruzano mpaka ulipotoea moto ndipo waanze kukimbiana hiyo haibali ubaya wao. na waungue wote pamoja period

    21. #298
      Kamuzu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th October 2008
      Location : Vigwaza
      Posts : 716
      Rep Power : 684
      Likes Received
      122
      Likes Given
      48

      Default Re: CCM mapande

      Quote By Kiungani
      Ni kweli. Nilikaa kwenye mazungumzo ya faragha watu wachache na kiongozi mmoja mkuu wa ki-taifa (PM) wa zamani. Alitoa maoni mengi na moja ni kuwa JMK pamoja na kuwa na nia nzuri na nchi lakini nchi inamshinda na itaendelea kumshinda kutokana na uswahiba wake na wajanja wachache (na akawataja majina watu kama sita hivi). Ajabu ni kuwa mwezi mmoja baadaye huyu huyu bwana akiwa kwenye NEC Butiama, hakusema lo lote la kumsaidia JMK na nchi zaidi ya kusema kuwa kuna haja ya CCM kuwa na mshikamano na mtazamo mmoja. Go figure!
      Unafiki na urafi ndio utawamaliza yetu macho

      ***********
      amani yetu inatumiwa vibaya

    22. #299
      MkuyuMkubwa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th September 2009
      Posts : 50
      Rep Power : 501
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      Hivi CCM ifanye nini ili mjue imeshaanguka? Tanzania hatuna chama tawala. ni makundi tu ya kila mtu na iwake ndo yanatawala hapa. hakuna chama tawala....wengi mnafikiri ili CCM ianguke ni mpaka waondoke madarakani kisheria. hawawezi kuondoka madarakani kwasababu hakuna viongozi wala chama mbadala wa kukabidhiwa hiyo mikoba...JK na wenzake waondoke sasa hivi, wakiache chama gani madarakani? Hakuna.

    23. #300
      Orche's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th July 2009
      Posts : 132
      Rep Power : 529
      Likes Received
      10
      Likes Given
      12

      Default Re: Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

      CCM imeshakuwa ngoma iliyovuma lazima ipasuke tu, aina tiba tene. Maana watanganyika wameshaamka, wameshapata ujasiri wa kusema. Kinachohitajika hapa sasa hivi ni mbadala wa CCM make wapo wengi ndani ya CCM ambao kazi na shughuli zao zote zinategemea CCM na serikali yake hivyo wanaogopa kutoka kulinda chakula cha watoto. Hivyo watakapo ona kuna Chama makini ambacha kinaweza kuwahakikishia shughuli zao wataondoka tu CCM. Upinzani muhimu ujengwa na nguvu ya kiuchumi ya chama!!

    Page 15 of 22 FirstFirst ... 51314151617 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Ajali ya Meli: Unabii wa Justine Kalikawe watimia
      By mamanalia in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 22
      Last Post: 11th September 2011, 21:57
    2. Unabii wangu umetimia!
      By Nyakarungu in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 2
      Last Post: 18th May 2011, 22:56
    3. Yamebaki Masaa Je, Utabiri wa Sheikh Yahaya Utatimia?
      By payuka in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 9
      Last Post: 30th October 2010, 12:01
    4. JK na unabii wa “Ndio Mzee”
      By MawazoMatatu in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 8
      Last Post: 28th July 2010, 09:15

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...