Kulikuwa na "mabingwa wa salamu" ambao walikuwa hawakosekani aidha kutuma salamu au kutumiwa salamu kwenye vipindi mbalimbali vya radio. Unayakumbuka majina yao?
Kulikuwa na "mabingwa wa salamu" ambao walikuwa hawakosekani aidha kutuma salamu au kutumiwa salamu kwenye vipindi mbalimbali vya radio. Unayakumbuka majina yao?
[email protected]
Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji
Dah namkumbuka Sita wa Sita toka Mwanza nafikiri.
Alafu kuna Mwilo Bare mzee wa Naaaaaaaaaaaaaaaam huko huko kanda ya ziwa.
Zakaria Ndemfoo wa Babati
Kuna S. Tingisha sijui wa wapi huyu jamani.
husein makabureta!!!
A baby is something you carry inside you for nine months, in your arms for three years and in your heart till the day you die
Juhudi Mr.Luvanda kamanda wa wakinga.
Lowena Msonda
Sabuni jina la mwanzo limenitoka nasikia huyu ni USWT sasa alikuwa mwalimu mkuu shule ya Mzimuni:o
If u can't stand for something , u will fall for anything !
Chesko mzee wa matunda..jina hilo kupitia salam za radio one!
Thomas Mushi Kimboka
Issa Hasan Majeshi aka kamanda wa salamu
Kangomba H Kangomba.
.
.
.
Walikuwa wananifurahisha wale akina sijui nani Mwanyika akiwa "Safarini Uingereza" yaani bila kuweka hicho kipengele cha safarini bado hainogi.. Watu walikua wabunifu.
He who wants to keep his garden tidy doesn't reserve a plot for weeds
Namkumbuka Wajadi Fundi, ila sina hakika kama alikuwa anaishi Ikwiri au Utete Rufiji. Zimekuwa siku nyingi!!!
Hapa MM utakuwa umetukumbusha mbali kweli Huyo WAJADI FUNDI WAJADI alikuwa nae moto kwenye salaam..dah wapo wengi kweli naona hii thread itakuwa balaaa inakumbusha mbaaali kweli wakati hakuna option ya kusikiliza radio nyingine zaidi ya RTD na external service yao!!..nakakumbuka hadi kale kamziki kao ka salamu...afu kulikuwa na kipindi maalum cha mabingwa wa salam..kadi ngapi wametuma ..afu zawadi zenyewe flana au pesa kiduchu enzi hizo
Don't regret what you said, regret what you didn't say when you had the chance....!"
Duu, umenikumbusha mbali,
Enzi hizo miaka ya mwanzo ya 90, nilikuwa na rafiki wa karibu, mtangazaji RTD, alinihadithia mambo mengi.
Siku hizo mshahara wa Mtangazaji RTD akianza kazi ilikuwa ni Shilingi,
3,660.65.
Kikombe cha chai ya maziwa canteen yao pale Pugu Rd. ilikuwa Sh. 20, chapati, 20, andazi 10, mayai mawili ya kukaanga 40. Kipande cha kuku wa kukaanga ni sh.60.
Hao mabingwa wa salamu, walikuwa kila ukisoma kadi yake, kuna mahali unapita, anakupiga na Sh. 100. ukimaliza kipindi cha salaam, ukishuka canteen, hiyo 100, unapata chai, chapati 2 na mayai mawili ya kukaanga, kipande cha kuku na soda juu.
Jioni ukipita maeneo fulani, sio vi offer vinafululuza, akina dada ndio usiseme, enzi hizo redio yenyewe ilikuwa moja.
Hawa mabingwa wa salamu, ndio walikuwa wakiongoza kumwaga hizo 100, wakifuatiwa na wanamuziki wanaotaka nyimbo zao zipigwe, hawa walikata fungu kubwa zaidi,
Enzi hizo, Mghanii wetu akiwa 'Mzee Athumani Khalfani' akilipwa Sh.100 kughani kipindi cha nusu saa.
Jameni watu wametoka mbali!. Wee acha tuu!.
Mungu awarehemu watangazaji wote waliotangulia, na walibakia mpaka sasa, wapewe pongezi nyingi, na hata wazuri waliochipukia na wanaoendelea kuchipukia pia pongezi, ukiondoa wale wachache wana vamia fani.
mimi nasema wadau hao jamaa walikuwa wanatembeleana tu kwa kufahamiana kwa salamu,mimi namkumbuka baba dulla one.Nasikia kipindi hiko mtuma salamu anatoka tanga anakwenda kumsalimia mwenzake wa mwanza na akifika anapokelewa na anakirimiwa enzi hizo utu na ubinadamu ulikuwepo sio sasa mtu anapata ajali unamsachi kabla ya kumpa huduma.
zamani watanzania walikuwa wanapendana,wanajaliana katika raha na shida na ilikuwa ukimsalimia mtu kupitia redio pekee ya taifa,RTD huyo alietumiwa salamu anajisikia na kama watu walisikia jina lake watamtafuta na kumwambia na nikumfata alipo maana simu ya kiganjani ilikuwa bado kipindi hiko .Wewe angalia watu walivyokuwa wastaarabu unaweza ukatuma barua kwa mzee wako labda huko Rombo mkuu kwa kumpa mtu anaesafiri na bus na akipita maeneo hayo anaidondosha huku bus linakwenda itapodondokea inaokotwa na lazima ifike kwa mlengwa salama ,jaribu sasa uone.
Pasco,
Kumbe kununua waandishi wa habari kumeanza siku nyingi? Loohh
Ni vizuri kufahamu hilo maana wengine tunafikiri hii kitu imeanza na ufisadi.
Nguruwe pita leo sina Mkuki(By Malila wa JF).
Thobias Mnyani wa uhuru na msimbazi. Rashid nguruwe wa korogwe.Bingwa wa salam tanzania alikuwa Zakaria Ndemfoo,radio zote za kiswahili kuanzia germany,south africa nk lazima utamsikia- Aliwahi kusema asiposikia jina lake redioni hupungua nusu kilo
Follow Us Here