Jamani mwenzenu hivi karibuni nilijikuta nahudhuria sherehe za "miss wherever na Miss Whatever". Nina maana hapa Dar siku hizi kuna mashindano ya Urembo kwenye kila kona hata sijui ni jidudu gani limetuingia (no pun intended). Hivi haiwezekani kuwa Tanzania inaongoza kwa mashindano ya Urembo duniani? Tangu mashindano haya yaanze tena imekuwa ni mashindano kwenye kila namna sasa hivi kuna hadi "miss kitongoji". Nasikia tukiendelea hivi hivi tunaweza kujikuta nyumba yenye watoto wengi wa kike ikajikuta wanaanzisha "miss familia".

But on the other hand, labda wadogo zetu wengi wanahitaji kutambuliwa uzuri wao na hivyo tuwaongezee venues za kushindana na kuwa na "miss wherever" kwenye kila kona. Jinsi gani tunaweza kupunguza haya mashindano ya urembo ambayo kwa kweli yanachukua muda mwingi wa watu na mengine hayana hata kichwa wala miguu?

Asanteni.