Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Sharobaro the milionea!!

    Report Post
    Results 1 to 11 of 11
    1. #1
      Mawenzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 713
      Rep Power : 582
      Likes Received
      144
      Likes Given
      817

      Default Sharobaro the milionea!!

      Wana JF,

      Hebu tuongelee kidogo kuhusu hawa vijana wanaochipukia ktk utajiri/umaarufu, typical example: Sharobaro.

      Hawa vijana (wake kwa waume) kwa kweli wanahitaji watu wa kuwa kama parents/guardians/mentors/counsellors/advisors ili utajiri na umaarufu usiwaangamize mapema. Wengi wao wanakuwa na elimu ndogo sana na pia hutoka kwenye familia maskini. Kwa hiyo utajiri/umaarufu wa ujanani unawazuzua sana kiasi kwamba tabia zao zinakuwa hatarishi sana kwao.

      Wakipata vijisenti haraka haraka na wakajua kiingereza cha "English Course" basi wanajiona wamemaliza kila kitu!! Wanaparamia na kubadilisha kila kukicha wamama, wanajiremba kupindukia, wanaanza kununua magari ya bei mbaya kabla hata ya kuwa na kibanda!! Na wanapenda kuendesha magari wenyewe tena kwa mbwembwe nyingi ili watu wawaone kuwa wanajua ku-drive! Hawataki kuajiri madereva!!

      Wanakuwa na watu wanaowaita Meneja. Lkn hawa watu inaelekea kazi zao ni kuwasifia, kuwaandalia maonyesho, kuwatongozea, n.k., lakini siyo kuwakanya kwani wanaogopa kuwaudhi na kukosa umeneja!

      Kwa mfano Sharobaro: Inaelekea katoka katika family maskini maana ameishia la saba tu. Hakukuwa na mtu kumwendeleza. Kwa bahati nzuri akaja Dar na kipaji chake kikamwokoa. Lkn bahati mbaya inaelekea alikosa mtu/watu wa ku-monitor tabia yake. Akawa anaishi peke yake. Akawa anafanya apendalo. Mfano mzuri wa hili ni ule uamzi wake wa ghafla kuanza safari ya Tanga saa 11 jioni akiwa peke yake huku akiwa na Sh. 6 million!! Drving kwenye highway, tena usiku, kunahitaji professional drivers, of which he was not!! Kwa nini hakuomba msaada wa kusindikizwa na mmoja wa marafiki zake??

      Hatujui, au sijui, huenda pia alikuwa na kiroba kwenye gari!! Ila linalojulikana ni kuwa alikuwa anatuma na kupokea sms!! Na pia lililo wazi ni kwamba hakufunga mkanda!!

      Sharo alikuwa anajitahidi kuishi kama jina lake lilivyo!

      Tatizo lilopo ni kwamba ukitaka kujitolea kwa nia njema kabisa kuwa kama parent/guardian/mentor/counsellor/advisor watu watasema huyu jamaa anataka kumuibia hela kijana wa watu!!

      Duh! Sasa nini kifanyike ili kuokoa hawa vijana talented? Ikumbukwe kwamba Diamond naye alipata ajali hivi karibuni!!

      Nawasilisha!
      Last edited by Mawenzi; 29th November 2012 at 16:46.
      Nguruvi3, Maswi and Mgaya D.W like this.

    2. Miaka 50

    3. #2
      bornagain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Location : Nyakanazi - Biharamulo
      Posts : 1,615
      Rep Power : 693
      Likes Received
      438
      Likes Given
      320

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Well said mkubwa
      There is a saying in aviation "You haven't crashed until you've crashed. Until then, keep flying the plane".

    4. #3
      mbweta's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 545
      Rep Power : 537
      Likes Received
      55
      Likes Given
      1

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Bdo tunajifunza kutokana na makosa

    5. #4
      Jile79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2009
      Posts : 3,770
      Rep Power : 1267
      Likes Received
      213
      Likes Given
      9

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Umeongea ukweli kabisa. Hata alipofariki kanumba pia kuna watu walitoa ushauri unaofanana na huu wako lkn ukapita km ulivyo. Tatizo watz hatushaulik, hata rais wetu kikwete (japo sikumchagua) hafuati ushauri wa wataalamu walioajiriwa kwa ajili yake kwa kodi za watz.kikwete ni msomi muislamu kutoka bagamoyo. Itakuwa kwa sharo milionea adiyesoma kutoka pale tanga?
      Kwetu Iringa likes this.

    6. #5
      georgeallen's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd June 2011
      Location : Seattle, WA, USA
      Posts : 2,055
      Rep Power : 0
      Likes Received
      516
      Likes Given
      260

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Quote By Mawenzi
      Wana JF,

      Hebu tuongelee kidogo kuhusu hawa vijana wanaochipukia ktk utajiri/umaarufu, typical example: Sharobaro.

      Hawa vijana (wake kwa waume) kwa kweli wanahitaji watu wa kuwa kama parents/guardians/mentors/counsellors/advisors ili utajiri na umaarufu usiwaangamize mapema. Wengi wao wanakuwa na elimu ndogo sana na pia hutoka kwenye familia maskini. Kwa hiyo utajiri/umaarufu wa ujanani unawazuzua sana kiasi kwamba tabia zao zinakuwa hatarishi sana kwao.

      Wakipata vijisenti haraka haraka na wakajua kiingereza cha "English Course" basi wanajiona wamemaliza kila kitu!! Wanaparamia na kubadilisha kila kukicha wamama, wanajiremba kupindukia, wanaanza kununua magari ya bei mbaya kabla hata ya kuwa na kibanda!! Na wanapenda kuendesha magari wenyewe tena kwa mbwembwe nyingi ili watu wawaone kuwa wanajua ku-drive! Hawataki kuajiri madereva!!

      Wanakuwa na watu wanaowaita Meneja. Lkn hawa watu inaelekea kazi zao ni kuwasifia, kuwaandalia maonyesho, kuwatongozea, n.k., lakini siyo kuwakanya kwani wanaogopa kuwaudhi na kukosa umeneja!

      Kwa mfano Sharobaro: Inaelekea katoka katika family maskini maana ameishia la saba tu. Hakukuwa na mtu kumwendeleza. Kwa bahati nzuri akaja Dar na kipaji chake kikamwokoa. Lkn bahati mbaya inaelekea alikosa mtu/watu wa ku-monitor tabia yake. Akawa anaishi peke yake. Akawa anafanya apendalo. Mfano mzuri wa hili ni ule uamzi wake wa ghafla kuanza safari ya Tanga saa 11 jioni akiwa peke yake huku akiwa na Sh. 6 million!! Drving kwenye highway, tena usiku, kunahitaji professional drivers, of which he was not!! Kwa nini hakuomba msaada wa kusindikizwa na mmoja wa marafiki zake??

      Hatujui, au sijui, huenda pia alikuwa na kiroba kwenye gari!! Ila linalojulikana ni kuwa alikuwa anatuma na kupokea sms!! Na pia lililo wazi ni kwamba hakufunga mkanda!!

      Sharo alikuwa anajitahidi kuishi kama jina lake lilivyo!

      Tatizo lilopo ni kwamba ukitaka kujitolea kwa nia njema kabisa kuwa kama parent/guardian/mentor/counsellor/advisor watu watasema huyu jamaa anataka kumuibia hela kijana wa watu!!

      Duh! Sasa nini kifanyike ili kuokoa hawa vijana talented? Ikumbukwe kwamba Diamond naye alipata ajali hivi karibuni!!

      Nawasilisha!
      kwa hiyo wewe umeishia hapo ...huna cha kushauri wala nini?
      hopkingsclark

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,176
      Rep Power : 41581
      Likes Received
      6075
      Likes Given
      1059

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Assumptions nyiiiingi.

      Wengine washaamua kuwa na maisha mafupi na matamu, wewe unafikiri kila mtu anataka kuzeeka.

      Do You.
      Allow others to say their say, but always say your piece, it's only right.

    9. #7
      BONGOLALA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2009
      Posts : 4,876
      Rep Power : 1472
      Likes Received
      1010
      Likes Given
      128

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      nina uhakika kutembea na tsh6m,angekua walau na nyumba ya maana ya kufikia kijijini. unakuta kapanga sinza kodi laki6

    10. #8
      C.T.U's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st June 2011
      Posts : 2,612
      Rep Power : 926
      Likes Received
      715
      Likes Given
      6

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Watanzania kwa kutoa ushauri hawajambo yakwao yanawashinda
      Kiranga and Kwetu Iringa like this.

    11. #9
      Kwetu Iringa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2011
      Posts : 340
      Rep Power : 467
      Likes Received
      54
      Likes Given
      595

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Quote By C.T.U
      Watanzania kwa kutoa ushauri hawajambo yakwao yanawashinda
      Kinyozi hajinyoi kaka!

    12. #10
      joely's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 321
      Rep Power : 498
      Likes Received
      84
      Likes Given
      15

      Default

      Quote By C.T.U
      Watanzania kwa kutoa ushauri hawajambo yakwao yanawashinda
      dah kweli wapuuzi wasioona umakini wa hoja ni wengi

    13. #11
      Thomas Odera's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Location : Karachuonyo - Kisumu
      Posts : 510
      Rep Power : 536
      Likes Received
      61
      Likes Given
      70

      Default Re: Sharobaro the milionea!!

      Ahsante kwa maelezo yako mazuri. Kwa vile watz ni wabishi na hawashauriki wacha vijana wateketea ili wapate maneno ya kuongea kwenye misiba ya watu maarufu

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...