Show/Hide This

  Topic: Filamu za kitanzania: Mazuri na mabaya

  Report Post
  Page 1 of 5 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 95
  1. #1
   Quemu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th June 2007
   Posts : 1,079
   Rep Power : 924
   Likes Received
   37
   Likes Given
   16

   Default Filamu za kitanzania: Mazuri na mabaya

   Huwa ninapenda kuangalia movie za kibongo.

   Ingawaje tunajitahidi kwenda na wakati, lakini naona kuna makosa kibao ya wazi tunayafanya ambayo yangeweza kuepukika.

   Editing
   Kosa kubwa la kwanza ambalo tunafanya ni kukosa Editors ambao wako serious na kazi zao. Unategemea Editor ndio ambaye angefanya kazi mzuri ya kureview movie , yet bado kuna makosa madogo madogo kibao ambayo yananakera sana kuyaona.

   Mfano – Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)

   1)Sauti - sauti ya hii movie inatoka kama sauti ya mwangwi (echo). Ni kama vile walikuwa wana record kwenye chumba cha mwangwi, halafu baada ya kuchukua sauti za waigizaji wenyewe, wakachukua sauti za ule mwangwi wenyewe. Yaani sauti inatoka kama ya mtu unayeongea naye kwenye simu ambaye amejifungia chumbani au kwenye kopo.

   2)English subtitles - Hapa ndio kuna vituko kweli. Yaani unasoma hizo tafsiri ya English kwenye hii movie mpaka unabaki kushangaa. Ndio najua wengi tunachemsha kwenye English, lakini kama film industry ya Bongo inataka kuwa serious (kujiingiza kwenye soko la nje), basi haitakiwi kuruhusu makosa kama yale. Kuna part moja ndio iliniacha hoi kabisa. Steve na Irene walikuwa restaurant, Zanzibar. Basi Steve akawa anamwambia Irene “tafuna…tafuna…tafuna,” akimsisitizia kuwa atafune chakula anamchomlisha. Sasa kwenye subtitles tafsiri yake ikawa “cat…cat….cat.”……I was like ‘enhe!’ Mwanzo sikujua walikuwa wanajaribu kuandika nini, lakini nikaja kugundua kuwa dhamira yao ilikuwa kuandika “cut…cut…cut,” neno ambalo bado sio tafsiri sahihi ya tafuna.

   Sasa makosa mawili kama haya yalitakiwa yashughulikiwe na editor. Hapa ndipo editor anapo onyesha umahili wake katika fani hii. Udhaifu wa makosa kama haya unaonyesha jinsi gani editors wa kibongo wasivyo serious na kazi zao.

   Wardrobes
   Ukweli ni kwamba waigizaji wana overdress mno. Sasa sijui wanajaribu kuonyesha kuwa wanajua kuvaa sana au vipi? Lakini mara nyingi wanavaa ‘loud clothes’ mno kulingana na scenes/story za movies.

   Mfano - Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)

   Vincent - anavaa very loud suits just kwenda kazini tu. Tena ana match na fancy shoes na hat kabisa. Unakuta kakupigia all white, kuanzia viatu, suruali, koti, kofi, na kakupigia shati moja kali jeusi…. Halafu anaishia kwenda kazini mchana kweupe. I mean, watu upiga hayo mavazi wakiwa wanakwenda kwenye mtoko jioni.

   Steve – huyu yeye anakuvalia jacket moja zito la nguvu kwenye 100 degrees condition. Pia anakupigia miwani moja kubwa sana…Anavaa hivyo vyote only kwenda chuo.

   Miss Uwoya - Huyu ndio alikuwa anafunga kazi kabisa. Well, lazima nikubali kwanza, kuvaa tu anajua. Maana baadhi ya mavazi yake yalikuwa yananifanya niweweseke ile mbaya…lol. Anyway, bibie huyu alikuwa anavaa pamba kali kama zile tulizozizoea kuwaona dada zetu wanugu wakivaa clubs (huku waki drop-it-like-its-hot). Yaani anakupigia capri ya nguvu, huku akimachisha na sleeveless top na fancy cowgirl hat (or whatever it’s called) mchana kweupe…..halafu huyo anaelekea sokoni kwenda kununua nyanya.

   Scenes
   Hawazingatii umuhimu wa mazingira wanayofanyia baadhi ya settings.

   Mfano - Movie ya O’prah (Steve Kanumba, Vincent Kigosi, na Irene Uwoya)

   Vincent supposedly ana ofisi pale kwenye jengo la Millenuim Tower. Sasa unakuta kila anapoenda kupaki pale juu, hakuna hata gari jingine kwenye ile parking. Well, inavyoonekana ile sehemu ya scene walitengeneza either jumamosi or jumapili. Lakini katika hali ya kuongeza ufanisi wa utengenezaji wa fialmu, ningetegemea pengine wangetengeneza scene ya ile sehemu angalu kwa siku mbili tofauti. Yaani, kwa sababu wameazima ofisi ya mtu kutengeneza filamu, basi wangefanya shooting ndani ya hiyo ofisi siku ambayo hakuna wenyeji (jumamosi au jumapili). Halafu wakafanya shooting ya kwenye parking siku ya weekday ambayo kuna magari yamepaki. Hiyo ingeipa movie ufanisi wa reality. I mean, hutegemei parking ya jengo kama lile kuwa empty siku ya kazi.

   All in all, kwa mtazamo wangu, hili hawa wasanii wetu wa filamu waweze kuendelea na kutengeneza filamu zenye angalau standard quality, basi inabidi kuwe na panel ya critics. Ukosoajia utakaotoka kwa panel hii utawasaidia sana wasanii hawa kuzingatia kanuni za uigizaji. Ningependekeza baraza la wasanii Tanzania (kama lipo) liunde hii panel. Njia nyingine ni wadau kuunda a private panel of critics.
   AshaDii and Magembe R. Malima like this.
   We miss 100% of the shots we never take

  2. Mkimbizi's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 23rd August 2008
   Location : Hard disk
   Posts : 222
   Rep Power : 693
   Likes Received
   32
   Likes Given
   36

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Pamoja na salama kuondoka, alikuwa anahusika sana kufanya watu wawe makini kwenye videos za nyimbo. Kwenye movie twahitaji kipindi, mtu wa kukosoaz
   Magembe R. Malima likes this.
   Nimeanza kuchoka kukimbia. Ole wao wale wanaokula rushwa na hela ya wananchi, sababu nikitulia mtaona mtiti wake.

  3. #3
   Quemu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th June 2007
   Posts : 1,079
   Rep Power : 924
   Likes Received
   37
   Likes Given
   16

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Quote By Mkimbizi View Post
   Pamoja na salama kuondoka, alikuwa anahusika sana kufanya watu wawe makini kwenye videos za nyimbo. Kwenye movie twahitaji kipindi, mtu wa kukosoaz
   Sasa huyo Salama yuko wapi siku hizi? Ukosoaji unasaidia sana kwa wale ambao wangependa kuwa serious na kazi zao.

   Ni vizuri watu waanze kuona ukosoaji kama ujengaji, badala ya kuona kama ni chuki na wivu.
   Magembe R. Malima likes this.
   We miss 100% of the shots we never take

  4. Kipanga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th April 2008
   Posts : 684
   Rep Power : 803
   Likes Received
   15
   Likes Given
   0

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Thanks QM kwa observations zako nzuri kuhusu hizi filamu za bongo. Ukweli ni kuwa vijana wengi wa kitanzania wanajitahidi kujiingiza katika kutengeneza filamu ingawa kuna mambo ya msingi yanakosekana katika kuigiza kwao kiasi kwamba hata hizo filamu hupoteza mvuto.

   Film industry inahitaji watu kuwa makini na wanatakiwa kuingia darasani kujifunza si tu kujiridhisha kuwa eti mtu ana kipaji. Nadhani hata suala la kutumia scripts kama lipo litakuwa limeanza hivi karibuni. Hao Directors wa hizo filamu ni watu tu walioamua kujiingiza huko kwenye fani lakini hawana technical know how!

   Lakini kama wasemavyo wahenga mwanzo mgumu, nadhani umefika muda muafaka kwa watu wetu walioko katika film industry wapige hatua zaidi mbele kwa kusomea hiyo fani ili waweze kufanya kazi yenye uhakika kwani ni kwa njia hiyo tu wataweza kufanya kazi ya uhakika itakayowanufaisha na wao wenyewe, otherwise wataishia kujidanganya kuwa wao ni actors, actress, Directors etc kumbe utumbo mtupu!!!
   Magembe R. Malima likes this.
   "All things are created twice. There is a Mental or first creation ,and a physical or second creation to all things"

  5. #5
   Yo Yo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st May 2008
   Posts : 11,195
   Rep Power : 23083
   Likes Received
   1482
   Likes Given
   2625

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Najiuliza kitu kipi kizuri Bongo,jibu hakuna.Ndio maana wakenya wanatuponda.Kama QM angekuwa mkenya ungeona watu jinsi mapovu yengewatoka.Bongo inakera hakuna zuri uozo mtupu.
   Magembe R. Malima likes this.

  6. Sajenti's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th April 2008
   Posts : 3,674
   Rep Power : 1465
   Likes Received
   346
   Likes Given
   95

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Quote By Yo Yo View Post
   Najiuliza kitu kipi kizuri Bongo,jibu hakuna.Ndio maana wakenya wanatuponda.Kama QM angekuwa mkenya ungeona watu jinsi mapovu yengewatoka.Bongo inakera hakuna zuri uozo mtupu.
   ...Yoyo, si kweli kuwa bongo hakuna kitu kizuri alichosema QM ni mtazamo wake kwa jinsi jicho lake lilivyoona hizo filamu. Tnapofanya kitu lazima watu wakubali kukosolewa ndio njia ya kujenga hatimaye kupata kitu kizuri..Hata hao wenye vitu vizuri sidhani kama siku walipoanza kutengeneza tu vilikuwa vizuri, No waliviboresha kadri watu walivyoshauri. Unaweza kuamini mvumbuzi wa gari alipanga liende mbele lakini akajikuta limegoma badala yake likarudi nyuma? Unadhani asingeshauriwa hatimaye kuboresha tungekuwa wapi sasa???

   watanzania lazima tukubali kujifunza na kukubali kukosolewa ndio mchakato wa mafanikio unavyokwenda ndugu!!!
   Magembe R. Malima likes this.
   To get something you never had, you need to do something you never did

  7. #7
   Pasco's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd September 2008
   Posts : 15,484
   Rep Power : 269294190
   Likes Received
   13223
   Likes Given
   60518

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Asante QM kwa observation yako. Nikiwa Bongo last time, niliona
   Programe ya Bongo Movies, Channel Ten, jina la producer alikuwa George Tyson, walikuwa
   Wanafanya review na critic. Tatizo mtangazaji wake sio kwamba hajui kutangaza, bali anaonekana ni mjinga mjinga tuu kama anayeuza sura kwenye screen. Mliopo Bongo kipindi bado kipo?. Kama kinaendelea, wapate mtangazaji serious na utakuwa ni mwanzo mzuri wa kupata serious critic kuziborezaa movies za Bongo.

   Mimi si mpenzi wa movies ila familia wanapenda. Ikitokea niko home wakiangalia, kuna baadhi ya scenes wanajitahidi na baadhi ni zinatia kichefuchefu na kukatisha tamaa kuendelea kuangalia.

   Naudhika sana pale maproducer na actors wanavyomu underestimate mtazamaji kuwa ni mjinga kwa kufanya movie kama mchezo wa kuigiza wa kijinga kijinga, hii inafanya watu serious waachane kabisa na hizi Bongo Movies.

   Nilipokuja kutazama ctedits za baadhi ya hizi movies nikagundua tatizo la msingi, utakuta mtunzi ndio huyo huyo producer, ni yeye starring, ndiyo yeye director, cameraman ndie editor.

   Kwa kifupi hawa wanajitahidi tatizo hawana ujuzi na mambo ya
   Acting zaidi ya kutegemea vipaji tuu vya acting.

   Tangu Mwaka 1971, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- kimekuwa kikitoa wahitimu wa Performing Arts na Film Production. Ndiko aliko Profesa Penina Mlama na Amandina Lihamba najiuliza hawa wahitimu wote hao wameishia wapi?!.

   Kwanye sanaa maonyesho graduate ninayemfahamu akichapa kazi ni Mzee Jangala na Mgunga Mnyamnyenyelwa wa Parapanda. Wengine wote wako wapi?.

   Kuna wakati najisemea kimoyomoyo natamani ningewajua hawa mastaa wetu niwape maoni yangu ili kupunguza michemsho na kuongeza heshima kwa movie zetu.
   .
   Magembe R. Malima likes this.

  8. #8
   Yo Yo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st May 2008
   Posts : 11,195
   Rep Power : 23083
   Likes Received
   1482
   Likes Given
   2625

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Quote By Laligeni View Post
   ...Yoyo, si kweli kuwa bongo hakuna kitu kizuri alichosema QM ni mtazamo wake kwa jinsi jicho lake lilivyoona hizo filamu. Tnapofanya kitu lazima watu wakubali kukosolewa ndio njia ya kujenga hatimaye kupata kitu kizuri..Hata hao wenye vitu vizuri sidhani kama siku walipoanza kutengeneza tu vilikuwa vizuri, No waliviboresha kadri watu walivyoshauri. Unaweza kuamini mvumbuzi wa gari alipanga liende mbele lakini akajikuta limegoma badala yake likarudi nyuma? Unadhani asingeshauriwa hatimaye kuboresha tungekuwa wapi sasa???

   watanzania lazima tukubali kujifunza na kukubali kukosolewa ndio mchakato wa mafanikio unavyokwenda ndugu!!!
   Hakuna kizuri the all sytem is corrupt bongo kuanzia kwa raisi wako mpaka wewe mwenyewe.Ndio maana wakenya wanatupiga madongo.Waigizaji hawa unafikiri ni leo au jana walianza kuambiwa kutengeneza vitu vya uhakika?
   Still mpaka kesho wanatuletea madudu ya kukopi toka Naijeria.
   Magembe R. Malima likes this.

  9. X-PASTER's Avatar
   Moderator Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : Firdaws (Paradise)
   Posts : 11,863
   Rep Power : 38158038
   Likes Received
   1550
   Likes Given
   0

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Kuna haja ya wasanii kujifunza hii sanaa ya uigizaji pale chuo cha sanaa Bagamoyo.

   Bongo Vipaji vipo ila wanakosa muelekeo kwa kutokuwa na elimu ya sanaa.
   Magembe R. Malima likes this.
   'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

   (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)

  10. #10
   n00b's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th April 2008
   Posts : 924
   Rep Power : 28495
   Likes Received
   2071
   Likes Given
   226

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Quick Mover, naomba kwanza nigusie suala la Editors:

   Mpaka sasa Tanzania yetu Director wa Movies za Tanzania anayejulikana rasmi (Professional) ni Severine Kiwango (ambaye kwa sasa ameacha, huyu vyeti anavyo!).

   Nasikitika kukufahamisha kuwa mpaka sasa hatuna Director wa Movies ambaye anaweza kusimama na kukiri mbele za umma kuwa yeye ni professional katika hili. Wengi wao kuhusiana na Sub-Titles huwa wanakuwa na Dictionary mikononi ili kuweza kuandika hizo sub-titles. Wengi wao ni vihiyo (mpaka sasa nakiri ni wote).

   Kazi kubwa ya Director si mtoa hela, ni kutoa commands zote za production. Yani yeye ni Floor Manager katika production ya movie husika.

   Lakini ma-director wa movies zetu hapa Bongo ni wale wenye kutoa pesa ambao huwa wanapenda waandikwe ndio Directors wa movie husika. Huyu hata maana ya Director anakuwa hajui bali anadhani ni ukurugenzi tu.

   Nina mfano, movie ya Fake Pastors, Director wake ni Ray (Vincent Kigosi), Behind Sin (walimaanisha scene!) Director ni Ray pia, na movie nyingi pia ni Director. Kanumba yeye anazo kama Penina, Dar 2 Lagos, Cross My Sin, Point of No Return, The Stolen Will n.k. Just imagine Director mwenyewe ndiye mwigizaji tena ndiye Script Writer. Huyu Steve Kanumba ndiye Super Star wa movies zetu kwa Bongo na kila movie almost yeye ndiye Starring. Wizi mtupu!

   Kwa upande wa Directors naomba niachie hapo kwa kuwatumia wakali wa movies zetu hizi. Wengine ni hivihivi. Naendelea upande mwingine
   Magembe R. Malima likes this.
   I seriously mean it when I say, 'Get a life'

  11. Yo Yo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st May 2008
   Posts : 11,195
   Rep Power : 23083
   Likes Received
   1482
   Likes Given
   2625

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Quote By Pimbi View Post

   Sasa si bora waache kutuchafua macho yetu wafanye shughuli nyingine.Huyo ray anajua kupaka poda tu.
   Magembe R. Malima likes this.

  12. #12
   n00b's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th April 2008
   Posts : 924
   Rep Power : 28495
   Likes Received
   2071
   Likes Given
   226

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Waigizaji wetu:

   Walio wengi si wasanii katika uhalisia. Wema Sepetu, Joketi, Irene Uwoya, Lissa Jensen hawa ni ma-miss. Nadhani wangeendelea na ukanda wao. Kushirikishwa si mbaya lakini inaelekea wanaigeuza kuwa kawaida sasa

   Ngono:
   Bongo msanii hachezi movie (hasa wa kike) bila kutoa rushwa ya ngono. Mabinti wengi wanaonekena kuigiza sababu ya njaa zao na wengine wanaigiza ili kuuza sura wapate mabwana wenye fedha.

   Nina mifano michache:
   Ray (Vincent Kigosi) anaishi na Johari. Huyuhuyu Ray alishawahi kuwa na mahusiano na Mainda (na huyu Mainda alikuwa anatembea na marehemu Max ambaye aliondoka na ngoma), Dotnata, jimama moja la Ilala na wengine lukuki.

   Ray huyu anajifanya hana Baba wakati babake ni mzee Kigosi na anaishi Dodoma. Namshauri akamsalimie babake na amwombe radhi kwa kumkosea heshima. Wewe ni Mgogo na uache kuwadanganya watanzania kuwa wewe ni Mhehe.

   Kanumba alikuwa na mahusiano na wafuatao; Wema Sepetu, Lilian Internet (wa Twanga Pepeta) na wengine lukuki.

   Nora; huyu alipofariki Ngwizukulu akahamia kwa jamaa ambaye baadae mambo yalienda vibaya kwani alijikuta anapigwa picha za uchi na kupata kichaa cha mapenzi. Kwa sasa amejipoza kwa Tito (Carlos).

   Lona; huyu alikuwa anatembea na Kelvin, baadae akahamia kwa Cheni sijui kwa sasa yupo na nani lakini nitamfuatilia.

   Maya; huyu kwa sasa anaishi na Swebe.

   Colleta huyu ana wezere kubwa nasikia alipigwa mtungo na sasa kapata bwana ambaye kaamua kumsomesha.

   Maina; huyu alitembea na Chrisant Mhenga (walifanyia mambo haya machafu pale Tip Top), Cheni, Richie Mtambalike, JB, Tino (Hisani), akaolewa na sasa katemwa kutokana na tabia yake chafu.

   Dida wa Michopsi, huyu kwa sasa yupo Times FM kama mtangazaji wa mipasho. Huyu ameingilia ndoa ya watu na ni mke wa tatu kwa jamaa. Aliingia kwenye maigizo kwa lengo la kupata bwana tu ili mradi apate fweza.

   Cathy (alikuwa Mambo Hayo), huyu kaacha mme wake kaamua kuanza kutembea nje ya ndoa na Dinno.

   Sajuki na Deborah hao sisemi.

   Nimewagusia wachache tu, twende nyanja nyingine
   Magembe R. Malima likes this.
   I seriously mean it when I say, 'Get a life'

  13. #13
   n00b's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th April 2008
   Posts : 924
   Rep Power : 28495
   Likes Received
   2071
   Likes Given
   226

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Kwa upande wa mavazi:

   Wasanii wetu wawe wa kiume au wa kike wana ulimbukeni mbaya sana. Wanaamini kuvaa nguo zinazoonesha maungo yao ndiyo njia ya kuuza picha. Wanausahau utanzania wao na kuiga tabia za ajabu.

   Imagine anayefanya make ups ni Wema Sepetu ama Maya, nao ni waigizaji! Yani basi tu. Kila kitu kinaendeshwa kienyeji ili mradi wamekuja kutushika. Wizi mtupu!

   Location Managers wa movies wetu utakuta ndio haohao waigizaji. Sijui huwa wanapata wapi muda wa kufanya ufuatiliaji. Nawashauri waigizaji waheshimu kazi za wenzao na kuwaacha wafanye kuitangaza sanaa ya Tanzania. Wanatia kichefuchefu! Ukiangalia African Magic ikaja movie ya kitanzania unaona aibu hata kuangalia.

   Wasanii wetu hawana shukrani. Kuna baadhi nimewasaidia sana na hata sijawahi kuona popote wakikiri kuwa nimewasaidia. Sifikirii kamwe kuwasaidia hata chembe. Unamsikia msanii anaongea redioni eti ameanzia mbali na kajitutumua mwenyewe! Wana viburi vya ajabu sana. Waigizaji wa movies zao ni wapenzi wao au ni ndugu zao wa karibu.

   Kwa mwendo huo, wa kutotaka kukosolewa, kutokutoa credit kwa wenye msaada kwa mwigizaji husika hivi sanaa ya maigizo Tanzania itaenda popote? Tamaa kubwa sana, wakenya wakiingia Tanzania katika filamu basi miaka 10 ijayo sanaa hii itakuwa imekufa. Kwanza asilimia 80 ya waigizaji almost ni waathirika, asilimia zaidi ya 80 ya ideas za movies kadhaa huwa ni marudio ya ideas za wengine. Ukiangalia story mwanzo unakuwa ushajua nini kitatokea baadae.

   Filamu inatengenezwa ndani ya wiki moja!
   Magembe R. Malima likes this.
   I seriously mean it when I say, 'Get a life'

  14. Quemu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th June 2007
   Posts : 1,079
   Rep Power : 924
   Likes Received
   37
   Likes Given
   16

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Pasco
   Nilipokuja kutazama ctedits za baadhi ya hizi movies nikagundua tatizo la msingi, utakuta mtunzi ndio huyo huyo producer, ni yeye starring, ndiyo yeye director, cameraman ndie editor.

   Pimbi
   Nina mfano, movie ya Fake Pastors, Director wake ni Ray (Vincent Kigosi), Behind Sin (walimaanisha scene!) Director ni Ray pia, na movie nyingi pia ni Director. Kanumba yeye anazo kama Penina, Dar 2 Lagos, Cross My Sin, Point of No Return, The Stolen Will n.k. Just imagine Director mwenyewe ndiye mwigizaji tena ndiye Script Writer. Huyu Steve Kanumba ndiye Super Star wa movies zetu kwa Bongo na kila movie almost yeye ndiye Starring. Wizi mtupu!
   Basi huu ukweli utakuwa ni ubahili wa hali la juu.

   Kila role ina kazi zake. Haiwezekani hata siku moja Director na Producer kuwa mtu mmoja. Director yeye yuko kwenye mambo ya production. Producer, on the other hand, yuko kwenye management ya movie, i.e uandikaji wa scripts, utafutaji wa waigizaji, na mpaka utoaji na upangaji wa finances za kutengeza movies.

   Quote By Pimbi View Post
   Kazi kubwa ya Director si mtoa hela, ni kutoa commands zote za production. Yani yeye ni Floor Manager katika production ya movie husika.

   Lakini ma-director wa movies zetu hapa Bongo ni wale wenye kutoa pesa ambao huwa wanapenda waandikwe ndio Directors wa movie husika. Huyu hata maana ya Director anakuwa hajui bali anadhani ni ukurugenzi tu.
   Hao watoaji hela kama wanapenda majina yao yaonekana kwenye movie, basi wangechukua title ya Executive Producer. Kwa sababu hii title ndo haswa uniwahusisha wanao finance movies.

   Quote By Pimbi View Post
   Mpaka sasa Tanzania yetu Director wa Movies za Tanzania anayejulikana rasmi (Professional) ni Severine Kiwango (ambaye kwa sasa ameacha, huyu vyeti anavyo!).
   Sasa huyu bwana kwa nini ameacha fani yake?
   Pasco and Magembe R. Malima like this.
   We miss 100% of the shots we never take

  15. Quemu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th June 2007
   Posts : 1,079
   Rep Power : 924
   Likes Received
   37
   Likes Given
   16

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Kwa nini idara ya sanaa isipange mikakati kuhakikisha hizi filamu zinatengenezwa katika misingi inayokubalika?

   Well, suala la mavazi linaweza lisiweze kuthibitiwa vizuri, lakini suala subtitles ni aibu kuliacha liendee. Watu wa sanaa wanaweza kuweka sheria ambayo italazimisha filamu zote kupitia kwao, kwa ajili ya review, kabla hazijapanda sokoni. Kufanya hivi kutasaidia kuondoa matatizo madogo madogo kama ya kiswakinge, na lugha kwa ujumla
   Magembe R. Malima likes this.
   We miss 100% of the shots we never take

  16. PastorPetro's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 25th February 2008
   Location : Boston, MA USA
   Posts : 177
   Rep Power : 705
   Likes Received
   22
   Likes Given
   43

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Tatizo la Bongowood ni watu kutaka pesa za haraka haraka. Quality ya sinema ni mbovu sana na ukweli ni kideo au mcehzo wa kuigiza na siyo filamu. Hazina hadhi ya filamu. Kweli kuna haja ya kusomesha hao wanaojiita madirector na produza Bongo.
   Magembe R. Malima likes this.

  17. Kana-Ka-Nsungu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th October 2007
   Location : 10 Dawning Street
   Posts : 2,290
   Rep Power : 17955033
   Likes Received
   245
   Likes Given
   123

   Default Re: Filamu za Bongo zinahitaji wakosoaji (Critics)

   Nakubaliana na mengi yaliyosemwa na wakosoaji wengi humu lakini ningependa kugusia suala la lugha kwa kuwa nalo linakera.Utakuta title ya filamu imepewa jina katika lugha ya kiingereza lakini movie yenyewe watu wanaongea kiswahili- kiingereza kipo kwenye subtitles tu! kwanini wasanii wetu wanashindwa kufanya utundu na kubuni majina ya kiswahili? Pia nakerwa sana na uvivu wa kufikiri wa hao wanaojiita 'directors', kwa kweli movie nyingi wanazotoa ni za kucopy na kupaste kutoka kwa ndugu zetu wanigeria, wanabadilisha watu na lugha tu!
   Magembe R. Malima likes this.
   If someone knocks you down- its their faulty, but if you stay down its your faulty.

  18. Ilumine's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 27th December 2008
   Location : hapa na pale
   Posts : 196
   Rep Power : 665
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Unhappy Filamu hizi za kibongo vipi?

   Awali ya yote nawashukuru sana wawezeshaji wa mtandao huu.

   Nawapongeza waigizaji, watunzi, waongozaji na wote wanaohusika kuandaa na kutengeneza filamu za kibongo zenye tbs ya juu … LAKINI……

   Filamu hizi zinaelekea kwenye ‘extreme’ nyingine yaani upande wa ‘ngono’ zaidi.

   Ndio, filamu hizi zinatoa mafunzo, lakini, vitu vingine havifai kabisa kuonekana kwa watu. Lazima wakati Fulani kujificha, watoto wasikuone ukitazama filamu hizi. Na pengine yafaa ziwekwe mbali na watoto, kama vile zile dawa zenye sukarisukari zilizoandikwa ‘keep away from children’.

   Ubora wa filamu hizi ni wa hali ya juu, sasa hii isitupelekee kuharibu utamaduni wetu. Nadhani hii itawapunguzia soko kwani, ni usumbufu kukaa na filamu nyumbani ambazo muda wote mzazi anakuwa na hofu watoto wakizitazama. Mbona za ki-Nigeria zipo safi tu. Tunaona watu wakiingia chumbani, basi inaeleweka, sasa sisi watanzania hatuelewi mpaka tuoneshwe kila kinachofanyika! Natoa mfano mmoja tu kwa sasa: Filamu ya ‘The cold Wind’. Tulitazame hili ndugu zanga, na kuchukua hatua kabla mambo haya ‘hayajaota mbawa’

   Asanteni……
   Magembe R. Malima likes this.

  19. Madela Wa- Madilu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th March 2007
   Location : USA
   Posts : 3,139
   Rep Power : 1283939
   Likes Received
   540
   Likes Given
   552

   Default Re: Filamu hizi za kibongo vipi?

   Nadhani tatizo lipo kwenye rating.
   Filamu zote zenye kuonyesha ngono wazi wazi ni lazima ziwekwe kwenye kundi lake.
   Picha yeyote inayoonyesha mwanamke na mwanume wakivua nguo tayari kwa tendo, hata kama tendo lenyewe halifanyiki nilazima ziwekwe kennye kundi la filamu za ngono.

   Hatuwezi kuzuia watu kutengeneza filamu za ngono lakini tunaweza kuwabana kisawa sawa kwa kuwaamuru kuweka Label maalumu ya onyo kama ilivyo kwa wenzetu" ADULT MOVIE"
   Magembe R. Malima likes this.
   MYPEOPLE PERISH FOR LACK OF KNOWLEDGE. HOSEA 4:6

  20. MwalimuZawadi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st September 2007
   Posts : 646
   Rep Power : 824
   Likes Received
   58
   Likes Given
   8

   Default Re: Filamu hizi za kibongo vipi?

   Quote By Madela Wa- Madilu View Post
   Nadhani tatizo lipo kwenye rating.
   Filamu zote zenye kuonyesha ngono wazi wazi ni lazima ziwekwe kwenye kundi lake.
   Picha yeyote inayoonyesha mwanamke na mwanume wakivua nguo tayari kwa tendo, hata kama tendo lenyewe halifanyiki nilazima ziwekwe kennye kundi la filamu za ngono.

   Hatuwezi kuzuia watu kutengeneza filamu za ngono lakini tunaweza kuwabana kisawa sawa kwa kuwaamuru kuweka Label maalumu ya onyo kama ilivyo kwa wenzetu" ADULT MOVIE"
   Sawa mkuu, wataweka hata kiwango 50 years, then what next? Unajua filamu nyingi zinawekewa viwango vya umri ila hakuna anayefuatilia? Tutawaonea tu wasanii wa Tanzania kama hatutaweza kufuata taratibu tunazojiwekea kwa ujumla wake. Mara utasikia BASATA wameifunguia wakati PILAU kibao mtaani. Kisa zinatoka Hollywood. Tuanze kukemea utekelezwaji wa sheria na taratibu zote tulizojiwekea ili twende sawa
   Magembe R. Malima likes this.
   Sent from my Nokia rinGo using JamiiForums

  Page 1 of 5 123 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Haya ni mabaya ya SITTA, niwekee mazuri yake
   By Marytina in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 131
   Last Post: 11th August 2014, 11:39
  2. Idi Amin Dada: Mazuri na Mabaya ya utawala wake
   By Hofstede in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 21
   Last Post: 4th November 2012, 19:07
  3. Mazuri na Mabaya ya Serikali ya Awamu ya Nne!
   By MwanaFalsafa1 in forum Great Thinkers
   Replies: 8
   Last Post: 19th September 2011, 22:08
  4. Filamu nyingi hazina maadili ya Kitanzania
   By MziziMkavu in forum Entertainment
   Replies: 7
   Last Post: 6th September 2011, 19:35
  5. Movie Scene Filamu ya Kitanzania
   By Inkoskaz in forum Jamii Photos
   Replies: 57
   Last Post: 19th November 2010, 17:02

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...