JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

  Report Post
  Page 4 of 20 FirstFirst ... 23456 14 ... LastLast
  Results 61 to 80 of 395
  1. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

   Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......

   Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....

   Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuw a lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila, Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyo ngise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....

   Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  2. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Bila kuwasahau wataalam wa Tatunane.....

   Hawa jamaa walikuwa wakiupiga muziki wetu wa asili kwa kutumia ala/vyombo vya kisasa.....Hawa waliutangaza sana muziki wetu nje ya nchi(hasa Denmark na Uholanzi) ambako walikuwa wakifanya maonesho ya mara kwa mara....

   Bendi hii iliundwa na wa wanamuziki kama Omary Naliene(mtaalamu wa kucheza ngoma,kupiga marimba,kuimba na kupuliza filimbi huyu,alikuwa anapuliza filimbi kwa pua), Charles Mhuto(Mpiga drums), Mahdi Tumbo(Mpiga gitaa la solo na muimbaji), Seif Rengwe(Mpuliza trumpet), Teddy Mbaraka(Mpiga gitaa la besi na muimbaji), Omary Abdallah Dulla Mnanga(Mpiga ngoma na muimbaji) na Kipara Yusuph(Mpiga ngoma)

   Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Kulalama,Sangula,Msewe,Wasknai a,Furahia ngoma,Utamaduni,Pili, Naukala,Dunia, Tanzania, Dogoli, Zanzibar, Mangaka, Juma ndala, Kala hasara, Mdundiko, Filimbi, Ludewa na nyingine nyingi ambazo ziliitangaza nchi yetu katika medani ya muziki wa kimataifa....
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  3. Balantanda's Avatar

   Quote By Balantanda View Post

   Click image for larger version. 

Name:	naliene.jpg 
Views:	395 
Size:	12.2 KB 
ID:	32283
   Omary Naliene akipuliza filimbi mbili kwa tundu za pua....

   Click image for larger version. 

Name:	tatunane.jpg 
Views:	466 
Size:	15.4 KB 
ID:	32284
   Kutoka kushoto ni Charles Mhuto,Omary Naliene,Teddy Mbarak na Seif Rengwe...

   Click image for larger version. 

Name:	tatunane3.jpg 
Views:	321 
Size:	56.5 KB 
ID:	32285
   Vijana wa kazi(Tatunane) kabla ya show huko majuu....
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  4. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Quote By King'asti View Post
   i wish ningepata walau audio yake. na wimbo wa kalubandika, huu naweza kuusikiliza kwa repeat mode hata 5 times! sijui nani aliimba ila unanikumbusha nikiwa kinda, naskiliza radio tz,lol
   Wimbo huu uliimbwa na Orch. Marquis Original na baadae kurudiwa na Nguza Vicking(Babu Seya) akiwa kama mwanamuziki wa kujitegema(solo artist)....Mashairi ya wimbo huu yako hivi: ....

   Kama wewe umenipenda kwa nini kunidanganya bwana wee,
   Kujibandika madaraka sio yako bwana wewe,
   Kama wewe umenipenda kwa nini kunidanganya bwana wee,
   Kujibandika madaraka sio yako bwana wewe,

   Nimesikia tetesi kuwa huna lolote hata kazi huna ee,
   Unazurura mchana kutwa ee,kupita kurandaranda mitaani,
   Nimesikia tetesi kuwa huna lolote hata kazi huna ee,
   Unazurura mchana kutwa ee,kupita kurandaranda mitaani,

   Kumbe hukuwa na uwezo wa kunioa ila kuniharibia maisha,
   Heri unaimbie ukweli ulivyo kuliko kunidanganya,

   Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa,
   Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa

   Bridge: (Nguza) Karubandika..........Kumbe wewe tapeli

   Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa,
   Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaaaaaaaaaaaa

   Usinione bweg baba,usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
   Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....
   Usinione bweg baba,usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
   Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

   (Nguza); Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto mie,kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka,pa kulala hana analala kwenye stendi ya basi,pa kulala hana anakesha kwenye kituo cha City,Karubandika yoyo,acha vituko we baba....

   Usinione bweg baba(Karubandika yoo),usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
   Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

   (Nguza); Akiingia kwenye baa kazi yake kuomba bia,akiingia kwenye bia kazi yake kuomba baa,hana hata aibu ee,sigara pia anaomba,hana hata aibu wee na supu pia anabomu,mitaani na kwenye masoko kujitangazia kuwa yeye ni mkurugenzi wa kampuni fulani,kumbe sio hivyo..

   Usinione bweg baba(Karubandika aaa),usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
   Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

   (Nguza); Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto mie,kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka,pa kulala hana analala kwenye stendi ya basi,pa kulala hana anakesha kwenye kituo cha City,Karubandika yoyo,acha vituko we baba....

   Usinione bweg baba(Karubandika aaa),usinione bweg baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
   Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....
   Usinione bweg baba,usinione bwegbaba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
   Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  5. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Quote By King'asti View Post
   thanks balantanda, umenikumbusha mbali sana enzi za utoto. especially huo wimbo wa nikitazama milima ya kwetu. i wish ningepata walau audio yake. na wimbo wa kalubandika, huu naweza kuusikiliza kwa repeat mode hata 5 times! sijui nani aliimba ila unanikumbusha nikiwa kinda, naskiliza radio tz,lol
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  6. Kurunzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st July 2009
   Location : DAR ES SALAAM
   Posts : 3,529
   Rep Power : 1335
   Likes Received
   757
   Likes Given
   303

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Da kiukweli zamani mziki wetu ulikuwa mzuri sana halafu kila mtu aliupenda, nawakumbuka sana sambulumaa band we acha bana, Tucheze wote ngoma ya kwetu.

  7. senator's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th August 2007
   Location : Ziwani
   Posts : 1,936
   Rep Power : 1120
   Likes Received
   49
   Likes Given
   48

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Quote By Nanren View Post
   Dukuduku eeh!!
   "Mara ya kwanza umeniomba tucheze,
   Muziki wa kwetu siwezi kukataa,
   Mara ya pili ukarudia tena,
   Sio kwa kucheza ila kunifinya jicho,...

   Uliza kwanza, kabla ya kufanya upuuzi wako bwana eeh, mimi nimeishaolewa...
   Nimekuja kucheza, nimekuja kufurahisha mwili bwana eeh....

   Dr Balantanda, hebu lete lyrics za huo wimbo bwana..,
   ngoja niendeleze hapo ulipo ishia kwa kumbu kumbu za wana dukuduku

   ..nimekuja kucheza ..nimekuja kufurahisha mwili wangu bwana weee mimi ni muke wa watu
   ..na mume wangu yupo hapa hapaa ..ameniruhusu kucheza muziki wa kwetu
   ..tafadhali bwana duku duku ni wasiwasi wao jamanii eehe mziki wetu unatia fora
   ..wasiwasi wao ..sisi wao baridi kwetu hakuna shida ooho wache wasemee

   bala utafute kwa marefu ingawa najua ulikuwa na ubeti mmoja au mbili then wakawa wanarudia kibwagizo hizo..
   Don't regret what you said, regret what you didn't say when you had the chance....!"

  8. senator's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th August 2007
   Location : Ziwani
   Posts : 1,936
   Rep Power : 1120
   Likes Received
   49
   Likes Given
   48

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Kuna kibao kimoja cha Wana msondo nakikumbuka kwa ubeti mmoja tu Bala kama kipo kwenye maktaba yako kipe mwendelezo

   ..ilikuwa jumamosi ilee... tukiwa msondo ngomaa
   kulia kwangu nilimuona binti shakila mwenye furaha...akilisakata msondooo
   ..nilishindwa kujizuia nikajikuta tupo bega kwa bega
   Nilimuomba tucheze nae bila kupinga alikubali...nikamueleza kuwa nimetokea kumpendaaa
   ..nae akanijibu hapa nimefwata msondo usinifurahishee....wasiliana nami kesho keko machungwaaa ahaa..
   Don't regret what you said, regret what you didn't say when you had the chance....!"

  9. Washawasha's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th August 2006
   Location : jo'burg
   Posts : 8,068
   Rep Power : 54408464
   Likes Received
   1726
   Likes Given
   3089

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   @Bantalanda,ahsante sana kwa thread na ku2kumbusha mbali kwa hizi nyimbo: Mzarau kwao mtumwa

  10. FaizaFoxy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th April 2011
   Posts : 43,190
   Rep Power : 373672701
   Likes Received
   22054
   Likes Given
   16966

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Wakati huo wa u "teen", mimi nilikuwa nikiwajua band iliyokuwa ikipiga pale Splendid, nna uhakika kuna watu wa Dar wazamani watapakumbuka hapo, The Rifters, walikuwa vijana wa Kariakoo, kinaDodger, Salah, Marehem Abdallah Matimbwa, na wengine siwakumbuki, tulikuwa tukienda siku za jumapili saa nane mchana (enzi hizo thubutu tutoke usiku) unaachiwa radhi!

   Baada ya hao nawakumbuka "The Sunburst", enzi za bahari beach, ilikuwa raha sana siku za Jumapili tukienda family nzima anaetaka beach aende anaetaka mziki haya tena...

   Hawa Sunburst ndio hasa walianzisha huu mtindo unapjulikana sasa wa "mduara" kwenye dance za mziki wa kisasa. Nakumbuka walikuwa na nyimbo zao wakiziita za kitoto, kama vile "Ukuti" na mingineo ambayo kuikumbuka m kwa mara moja inakuwa shida.

   Namkumbuka Muimbaji wao James, sijui yuko wapi huyu, nilimuona Kariakoo around 2005, halafu namkumbuka "Drummer boy" John Rocky, huyu yupo na namuona ona sana na baiskeli yake (hajabadilika in spite of age), na niliwahi muona miaka miwili mitatu nyuma akipiga drums pale Moevenpick halafu nikamuona Kempinski. Sijawahi kumuona Drummer boy better than him mpaka hii leo kwa huku kwetu. Namkumbuka pia mpiga wao bass maarufu Bashir, huyu ni mtoto wa yule mzee wa kizanzibari maarufu, gwiji la mziki Marehem Iddi farhan, inasemekana huyu Mzee Farhan watoto zake woote, zaidi ya kumi ni musicians (wakike na wakuime pamoja na mama yao) na inasemekana mpaka wafanyakazi wa nyumbani kwao (house girls na boys) nao pia ni musicians, isitoshe, mpaka majirani zao wengi wamefundishwa mziki na huyo mzee ama wanawe. Huyu Bashiri alikuwa na ndugu zake wanne Audu, Jaffar, Fresh na dada yao Jamila akipiga drums ) nilikuwa nikiwaona wakipiga ala tofauti hapo Sunburst.

   Jamani hizo ni late 60s na 70s.

   Nani anazikumbuka bendi hizi, za watoto wa mjini (in real sense)?
   Last edited by FaizaFoxy; 23rd June 2011 at 10:09.

  11. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Quote By FaizaFoxy View Post

   Faiza nimekukubali..........

   Kweli wewe ni mkongwe aisee.....

   Hao jamaa wa The Sunburst nilichelewa kuwajua aisee.......Ila naambiwa walikuwa ni wazuri sana na ilikuwa ni bendi bora ya mwaka 1973......

   Kingine ninachokijua kuhusu The Sunburst ni wimbo wao wa Banchikicha ambao mpaka sasa hurushwa kwenye vipindi vya zilipendwa vya vituo mbalimbli vy redio nchini.....

   Pia najua kwamba kiongozi wa bendi hii alikuwa ni Kassim Magati
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  12. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Click image for larger version. 

Name:	platforms.jpg 
Views:	219 
Size:	27.4 KB 
ID:	32534
   Click image for larger version. 

Name:	70s2.jpg 
Views:	360 
Size:	9.4 KB 
ID:	32535

   Mnayakumbuka mapigo haya?......

   Picha zote kwa hisani ya John Kitime...
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  13. Ballerina's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd June 2011
   Posts : 392
   Rep Power : 628
   Likes Received
   175
   Likes Given
   381

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Quote By Balantanda View Post
   Kwa leo ngoja nimalize na DDC Mlimani Park Orchestra..........Dah....Hata sijui nianzie wapi hapa maana maelezo yatakuwa marefu kweli,ngoja japo niyafupishe kidogo....

   Historia ya Bendi hii inaanzia mwaka 1978 ambapo takriban wanamuziki wanane waliihama bendi ya Dar International na
   kwenda kuanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park.Baadhi yao ni aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jeff,hawa waliungana na Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka na Abel Barthazar(ambaye ndio hasa muanzilishi wa Mlimani Park)..... Ilijulikan hivyo(Mlimani Park Orchestra) kutokana kuwa na maskani yake pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services.

   Mwaka 1983 waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo walifilisika na na hatimaye bendi hiyo ikachukuliwa na Dar es Salaam Development Corporation (DDC) na hapo ndiyo ikaanza kuvuma kwa jina la DDC Mlimani Park Orchestra ikiwa chini ya wanamuziki galacha na waasisi, Muhidin Maalim Gurumo, Abel Baltazar, Hassan Rehani Bitchuka, ambao walitokea JUWATA Jazz Band huku Cosmas Thobias Chidumule, Michael Enoch ‘King Michael’ na mpiga gitaa la solo mahiri, Joseph Batholemeo Mulenga, wakiwa wametwaliwa kutoka Dar International. ............Mtindo walioutumia tangu enzi hizo ni ule wa Sikinde Ngoma ya ukae.....

   Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana za Sikinde ni pamoja na Sauda/MV Mapenzi(namba 1 na 2),Neema,Usitumie Pesa kama fimbo,Mume wangu Jerry,Clara,Hiba,Matatizo ya nyumbani,Majirani huzima redio,Nidhamu ya kazi,Kassim amefilisika,Talaka ya hasira,Hadija,Barua toka kwa mama,Celina,Editha,Fikiri nisamehe,Pole mkuu mwenzangu,Diana,Pesa,Hata kama,Bubu ataka sema,Mnanionesha njia ya kwetu,Tangazia mataifa yote,Mtoto akililia wembe,Nalala kwa tabu,Duniani kuna mambo,Kiu ya jibu,Dua la kuku,Nawashukuru wazazi,Pata potea,Nelson Mandela,Uzuri wa mtu,mdomo huponza kichwa,Taxi Driver,Tucheze Sikinde,Conjesta na nyimbo niyngine nyingi tamu.....

   Wanamuziki walioipitia bendi hii ni pamoja na King Michael Enock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum,Habib Jeff,Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka,Abel Barthazar,Henry Mkanyia,Fresh Jumbe,Hussein Jumbe,Benno Villa Anthony,Tino Masinge 'Arawa',Hassan Kunyata,Francis(Nassir) Lubua,Maalim Hassan Kinyasi,Abdallah Gama,Max Bushoke,Muharami Said,Kassim Mponda,Julius Mzeru,Said Chipelembe,Ally Jamwaka,Machaku Salum,Ally Yahaya,Shaban Lendi,Joseph Bernard,Juma Hassan Town na wengine wengi....

   Hivi u mwana mziki au?Nimebaki mdomo wazi hapa!Unapata wapi nyimbo hizi?Kama hutajali naomba tuandikie ule wa "nawashukuru wazazi".Pia kuna nyimbo kama Zuwena,bahati mbaya sijui aliimba nani,na ule ;

   mbele yangu kuna simba
   nyuma yangu kuna tembo
   kushoto kwangu kuna chui
   kulia kwangu kuna..............
   sijui nitafanya nini niweze kuokokaaaa,mwenzenu nifanye nini niweze kuokoka jamaaaa

   Huu ulikuwa ukiimba yaani mawazo yangu yananipa picha ya mtu kasimama msituni na hao wanyama wamemzunguka,si unajua mawazo ya kitoto.Nikiupata huu pia nitafurahi sana mkuu.
   "Rise above the muck of the problem and rest in the multitude of possible solutions"

  14. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Salama wakuu?.....

   Leo naombeni tuwaangalie Bima Lee Orchestra....

   Bendi hii ilianzishwa mwnzoni mwa miaka ya 80 na ilikuwa ikimilikiwa na Shirika la Bima la Taifa....Bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo kama Magnet 84 na baadaye Magnet ndele Tingisha(Magnet tingisha)..Bendi hii ilikuwa tishio kweli enzi hizo na ilipata nguvu zaidi mwaka 1984 baada ya kuwapata wanamuziki watano(05) Shaba Dede,Joseph Mulenga na Abdallah Gama(kutoka Mlimani Park orchestra) pamoja na Othman Momba na Jerry Nashon 'Dudumizi'(kutoka Vijana Jazz)....Wanamuziki hawa waliifanya Bima Lee Orchestra iibuke ghafla na kuwa tishio ikitumia mtindo wa Magnet 84....Hapa ndipo walitoka na nyimbo tamu kama Makulata,Neema,Tujemaso na nyinginezo...

   Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana na Bima Lee Orchestra ni pamoja na Makulata,Siri yako,Tujemaso,Frousie,Baba Shani,Samaki baharini,Visa vya Messenja,Ndoa Fungo la Hiyari,Dunia Ni Upepo,Busu Pande Tatu,Uzuri Ni Tabia, Penzi Dawa ya Chuki,Sitaki(visa vyako),Shakaza namba 2,Zenaba,Milionea wa mapenzi na nyinginezo nyingi.....

   Baadhi ya wanamuziki waliowahi kupitia bendi hii na kutamba nayo ni pamoja na Shaban Dede,Joseph Batholomeo Mulenga 'King Spoiler',Jerry Nashon 'Dudumizi',Abdallah Gama,Othman Momba,Rahma Shally,Stamili Uvuruge,Maxmillan(Max) Bushoke,Eddy Sheggy,Belesa Kakere,Suleiman Mwanyiro 'Computer',Roy Bashekanako,Jumbe Batamwanya,Shaban Lendi,Athuman Manicho,Stamili Uvuruge,Boniface Kachale,Lazaro Remmy,Muharami Said,Duncan Ndumbalo na wengine.
   Last edited by Balantanda; 3rd July 2011 at 22:56.
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  15. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Salama wakuu?,habari za siku....

   Kusema ukweli ni hauwezi kuzungumzia maendeleo ya muziki wa Tanzania(hasa muziki wa dansi) bila kuitaja iliyokuwa Redio Tanzania Dar es salaam-RTD(sasa TBC)...Hawa jamaa kwa kiasi kikubwa wamechangia kukua kwa muziki wa Tanzania na kipindi cha nyuma hakukuwa na studio za kutengeneza/kurekodi muziki....Nyimbo za bendi/vikundi vyote zilikuwa zikirekodiwa katika studio za RTD zilizopo Pugu road enzi hizo(sasa hivi Nyerere road)...

   Naomba niiweke makala hii(japo ya siku nyingi) ya Ibrahim Mkamba wa Raia Mwema ambayo inazungumzia umuhimu wa RTD katika kukuza muziki wetu na sanaa/burudani kwa ujumla.....Hakika habari hii inanikumbusha mbali sana;

   Kwa heri RTD, asante kwa muziki.

   CHOCHOTE utakachozungumza leo kuhusu muziki wa kusikiliza wa zamani wa Tanzania ukiwa mtangazaji, mwandishi, mwanamuziki, mpenzi wa muziki au mdau yeyote yule, utakuwa ukizungumzia kazi ya Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).
   Leo tunaiaga rasmi RTD na badala yake tukizikaribisha TBC Taifa, TBC FM na TBC International ya Kiingereza.
   TBC ni kifupi cha Tanzania Broadcasting Corporation ambayo kwa Kiswahili ni Shirika la Utangazaji Tanzania.
   Pamoja na Redio, TBC pia ina Televisheni ya Taifa (TvT) ambayo sasa itakuwa ikiitwa TBC One, baada ya uzinduzi wa leo.
   Ni wazi kuwa mwanamuziki wa zamani akihojiwa popote na kusema "tulirekodi wimbo huu mwaka fulani," akitaja miaka ya nyuma, atakuwa ameizungumzia kazi ya RTD bila hata kusema walirekodi wapi.
   Hata Komandoo Hamza Kalala, Mtaalam wa "Kalbondash", aliposema kwamba nyimbo za Super Matimila za "Almasi" na nyingine zilizorekodiwa pamoja na bendi hiyo mwaka 1981 ndizo za kwanza kwa Kasaloo Kyanga na Skassy Kasambula kuingia studio kurekodi katika maisha yao, studio aliyoizungumzia ilikuwa ya RTD licha ya kutoitaja katika mahojiano hayo na Radio Free Afica (RFA) ya Mwanza.
   "Kalbondash," kama alivyoeleza Kalala katika mahojiano hayo,ni upigaji solo wa mlio mzito kama wa solo la Lwambo Lwanzo Makiadi Franco.
   Kalala alisema alifundishwa upigaji huo na Mosesengo Fan Fan walipokuwa pamoja Super Matimila.
   Kwa ufupi, RTD ndiyo kiwanda kikubwa cha muziki wa miaka ya nyuma na ndiyo imewezesha redio nyingine zilizoanza baada yake kwenye miaka ya 1990 kuwa na nyimbo hizo zinazozitumia kwenye vipindi vyao mbalimbali, hasa vya muziki wa zamani.
   Kwa sababu hiyo, wakati tukiiaga RTD na kuikaribisha TBC Taifa na "ndugu zake", wadau na wapenzi wa muziki hatuna budi kusema asante sana kwa RTD kwa kututengenezea muziki unaotupa raha sana wakati wote.
   Katika kutoa shukrani hizo, ni vizuri tukumbushane kwamba ni redio hiyo iliyosafiri na wanamuziki wetu safari ndefu ndefu.
   Ilikuwa na Cuban Marimba ya Salum Abdallah na ikaendelea kuwa na bendi hiyo ikiwa chini ya Juma Kilaza mpaka ilipotoweka yenyewe baada ya Kilaza kuanzisha bendi ya TK Lumpopo iliyopata huduma ya uhakika ya RTD pia.
   Vile vile, ilikwenda na wanamuziki wa Moro Jazz kokote walikokwenda, mpaka Super Volcano ya Mbaraka Mwinshehe kwa upande mmoja na mpaka kwa Orchestre Lombelombe ya Mombasa na baadaye Kurugenzi ya Arusha za Lazaro Bonzo.
   Ilianza na NUTA Jazz ikaikaribisha JUWATA Jazz na ikaendelea nao hadi OTTU Jazz.
   Redio hiyo pia ilikwenda na Jabali Marijan Rajab tangu STC Jazz, ikapita naye Safari Trippers mpaka Dar International.
   Vile vile iliwasaidia walioibuka kimuziki na kuwainua kuwa wanamuziki wakubwa mno kama TX Moshi William, Mzee wa Dodo Hussein Jumbe, Hemed Maneti na wengi wengine.
   Pamoja na wanamuziki, imeziinua bendi na kuzifanya ziwe kubwa mno na kupendwa sana kama UDA Jazz, Bima, Matimila na nyinginezo.
   Redio hiyo, ilifanikiwa kufanya hayo kutokana na mipango yao ifuatayo:-kwanza,walikuwa hawabagui bendi za kurekodi. Ikienda DDC Mlimani Park ilihudumiwa katika kiwango kilekile ilichohudumiwa bendi ndogo sana ya VB Sound ya Buguruni.
   Pili, ilizitengeneza nyimbo vizuri kwa kuzirekodi kitaalam mno baada ya kufanya marekebisho muhimu ya mashairi kwa kusahihisha lugha na kuondoa lugha zisizofaa kimaadili yetu (hii ni mada mojawapo kati ya zinazokuja wiki za baadaye) na tatu, walizirusha nyimbo zote bila ubaguzi na ndiyo maana, kwetu wasikilizaji, Biashara Jazz, wana Kumbakisa au Dundadunda, Amboni Jazz, Mitonga Jazz, Butiama Jazz na nyingine za ukubwa huo zilikuwa sawa na Marquiz Du Zaire au Urafiki Jazz, wana Chakachua.
   Bendi hizo ndogo zilipata mashabiki zilivyopata bendi kubwa! RTD hawakuwa na ubaguzi kabisa katika kurusha nyimbo, hali iliyofanya mwanamuziki mkali yoyote wa bendi ndogo ainuliwe na ukali wake licha ya udogo wa bendi yake.
   Mtu ajiulize, kama siyo kazi nzuri ya RTD ya kurekodi vizuri na kama siyo kuupiga, bila kujali ukubwa wa bendi yake, wimbo "Rangi ya Chungwa" wa Nyanyembe Jazz leo ungekuwa na umaarufu ilio nao?
   Katika kutokuwa na ubaguzi, redio hiyo haikubagua katika kurusha nyimbo za bendi za Watanzania tupu na za wakongo kama OSS, Marquiz Original, Orchestra Makassy, Kyauri Voice na Fukafuka.
   Hali ilikuwa hivyo tangu enzi ya Super Vea ya Mwanza, Fauvette na Boma Liwanza.
   Vilevile, hawakubagua kurusha nyimbo za bendi za wanachama kama Sola TV, Lola Africa na nyinginezo, za taasisi za umma kama Bimalee, JUWATA Jazz na nyingine na za majeshi kama Polisi Jazz, Usalama ya Moshi, Nyuki Zanzibar, JKT Kimbunga, JKT Kimulimuli, JKT Ruvu, Magereza Jazz, Mwenge Jazz, Mzinga Troup na Uhamiaji Jazz.
   Zaidi ya hayo, hawakuitenga taarab na aina nyingine za muziki.
   Kwa sanaa nyingine, RTD ilirekodi na kutunza ngoma za takriban makabila yote ya Tanzania. Pia walikuwa na kikundi cha maigizo kilichokuwa na waigizaji mahiri sana waliotengeneza michezo mingi ya kuburudisha, kuelimisha, kuhimiza maendeleo na kuiasa jamii dhidi ya imani potofu na dhidi ya ufisadi wa kila aina.
   Miongoni mwa waigizaji wake mahiri walikuwa Marehemu Ibrahim Raha Jongo (Mzee Jongo), Marehemu Ally Ketto (Matuga au Pwaguzi), Marehemu Hamis Tajiri (Meneja Mikupuo) na Marehemu Mama Haambiliki.
   Pamoja nao walikuwapo Rajab Hatia (Pwaguzi), Bartholomew Milulu (Mtaalam wa kuiga lafudhi za makabila mbalimbali), "Hakimu" Said Panda, Mariam Yussuf, Zena Dillip, Nusura Suleiman, Theckla Mjata na wengine.
   Kimsingi, kupitia muziki, RTD, kwa kushirikiana na watunzi mahiri wa muziki, imesaidia sana katika harakati za maendeleo ya nchi yetu tangu tupate uhuru.
   Imefanya hivyo kwa kurekodi nyimbo za maudhui yote kama za sherehe ya uhuru wetu na wito wa Uhuru na Kazi ambao baadaye tuliugeuza na kuwa Uhuru ni Kazi, Muungano wetu, mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Azimio la Arusha, Mwongozo Mpya, Siasa ni Kilimo, Mtu ni Afya, Vijiji vya Ujamaa, Kujitegemea, Kilimo cha kufa na kupona, uzalendo, ukombozi wa Afrika, kulaani ubaguzi na kadhalika.
   Zipo nyimbo nyingi sana za bendi zetu zilizotuhamasisha kuhusu yote hayo. Nyimbo hizo zilikuwa na mashairi yaliyokamilika na midundo ya kuvutia.
   Pamoja na hizo, zilikuwapo nyimbo nzuri sana za mapenzi na za kuonya katika masuala mbalimbali ya kijamii na za kusifu.
   Zote zilirekodiwa kiufundi sana kiasi kwamba baadhi yake ziliporekodiwa kwingine, hazikupendeza kama zile za RTD. Mfano ni wimbo wa "Hiba" wa Sikinde na "Marashi ya Pemba" wa Ndala Kasheba.
   Kwa niaba ya wapenzi wenzangu wa muziki na sanaa, wakati leo tukiiaga RTD na kuikaribisha TBC, nawaomba TBC wafanye yafuatayo:
   Kwanza, waanze utaratibu wa kuingia kwenye ushindani wa kibiashara wa kurekodi nyimbo, hasa za bendi za dansi na muziki wa taarab bila kuacha kuzingatia maadili yetu katika biashara hiyo.
   Pili, wawaendeleze wahandisi wake wa Sauti (Sound Engineers) kwa kuwapa kozi za nje za utaalam wa kisasa wa kurekodi ambao zaidi ni "digital" tofauti na "analogue" waliokuwa wakitumia na kutengeneza muziki mzuri hivyo.
   Jambo la tatu ninalowashauri walifanye ni kurudisha vipindi vya zamani vya muziki wa moja kwa moja kutoka ukumbi wao wa Makoroma (Makoroma Hall), "Mambo Shoo" na baadaye "Klabu Raha Leo".
   Kwa msingi huo, wakati wa sikukuu za Pasaka, Idd na Krismasi, waturudishie "Pasaka shoo", "Idd shoo" na "Krismasi shoo" kukiwa na muziki wa bendi wa moja kwa moja ili tuendelee kujiona kweli tuko kwenye nchi ya amani, iliyojaa shamrashamra.
   Tukiiaga RTD, naomba niseme kuwa tunachoaga ni jina na yale yote ambayo hayakuwa mazuri ndani ya RTD kwani chombo ni kile kile ila sasa kitakuwa TBC.
   Natoa shukrani tena kwa RTD kwa muziki mwingi na mkubwa iliyotutengenezea huku nikiitakia TBC, kwa ujumla wake, mafanikio makubwa baada ya uzinduzi wake wa leo. Happy Birthday TBC!
   Last edited by Balantanda; 20th July 2011 at 17:38.
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  16. Balantanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th July 2008
   Location : Kusadikika
   Posts : 11,429
   Rep Power : 7767
   Likes Received
   3161
   Likes Given
   2228

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Leo naomba tuwakumbuke bendi ya Magereza,Magereza Jazz

   Bendi hii ipo mpaka sasa japo haina makali kama yale ya kipindi kile,hii ni mojawapo ya bendi za majeshi yetu ambazo zilitamba sana enzi zake sambamba na bendi nyingine za majeshi kama Air Jazz, Mwenge Jazz, Polisi Jazz, Uhamiaji Jazz, JKT Kimbunga Stereo, JKT Mafinga,Mzinga Troupe, Ruvu Jazz na nyinginezo.Bendi hii inamilikiwa na jeshi la Magereza Tanzania.Awali ilikuwa ikitumia mtindo wa Super Mnyanyuo(wana super mnyanyuo) na baadae(mwanzoni mwa miaka ya 90) walibadilisha mtindo na kuanza kutumia mtindo wa Mkote ngoma ambapo walianza kujulikana rasmi kama wana mkote ngoma,mtindo ambao wanautumia mpaka sasa.

   Baadhi ya nyimbo za Magereza Jazz zilizotamba enzi hizo ni pamoja na Fatuma mwanangu, Ashura, Edina, Suzana, Nalala nakuota na nyingine nyingi(naomba tukumbushane hapa)

   Baadhi ya wanamuziki waliowahi kupitia bendi hii na kutamba nayo ni pamoja na hayati mzee John Kijiko, Abel Barthazar, Nanah Njige, Billy Mbwana, Ramadhan Mwerevu 'Choma choma', Issa Kamba, Issa Bendera, Wema Abdallah, Happy Siwea, Hamis Muyungwa, Stewart Singano 'Zozo', Gervas Herman, Hassan Kunyata na wengine wengi
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  17. Balantanda's Avatar

   Baadhi ya nyimbo za bendi hii zilizotamba sana ni pamoja na huu hapa chini wa Ashura

   Ashura mimi najuta,
   Mwenzenu kweli najuta sasa,

   Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu [Bwana huyu]
   Nimeamini methali isemwayo [isemwayo]
   Mkataa pema,
   Oooh, pabaya panamwita x2

   Leo hii mwenzenu ,
   Kusema hivi mimi,
   Nilimuacha mume wangu,nilidanganyika,
   Kumuacha mume wangu, kumfuata bwana mwingine,
   Kumbe ni mwizi baba, kumbe ni muongo.

   Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu [Bwana huyu]
   Nimeamini methali isemwayo [isemwayo]
   Mkataa pema,
   Oooh, pabaya panamwita x2   Kibwagizo:

   Nawausia wanawake wenzangu wote eeh,
   Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika x2

   Muachane na mabwana wadanganyifu eeeh,
   Atakupenda wakati una mumeo ooh,
   Ukishaachika wala hana habari nawe
   [Hana habari nawe]

   Atakudanganya kwa curl na relaxer,
   Atakudanyanya kwa khanga za Mombasa,
   Atakudanganya kwa vitende vya Zaire,
   Atakudanganya kwa chips na mayai,
   Na starehe za muda hazina mwisho sikia

   Nawausia wanawake wenzangu wote eeh,
   Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika x2
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  18. Balantanda's Avatar

   Wimbo mwingine wa Magereza Jazz uliotamba sana ni huu wa Edina.

   karibu ndani karibu
   mchumba wangu Edina njooo x 2

   wala usiwe na wasiwasi
   mimi bado sijaoa
   usirudie mlangoni tu, hapa ni kwakoo
   karibuuuuuuuu

   (rudia mwanzo)

   (wote) Kibwagizo
   nakutegemea tuishi vyema kipenzi eh
   nakutegemea tuishi vyema Edina
   kwani silaha ya upendo ni tabia njema ahh mama X 2

   sina bibi wala mke Edina ahh
   wewe ni shada la ua ua
   pokea penzi langu kwa mikono miwili
   Edina chaguo langu mimi

   (wote) kibwagizo

   sina bibi wala mke Edina ahhh
   wewe ni shada la ua la upendo
   pokea penzi langu kwa mikono miwili
   Edina chaguo langu mimi

   (wote) kibwagizo
   "Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane" Regia Mtema.

  19. Yakuonea's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Location : IMEZUILIWA
   Posts : 595
   Rep Power : 661
   Likes Received
   239
   Likes Given
   262

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Mkuu bala tupo pamoja......... I salute you....

  20. ngalikikinakiki's Avatar
   Member Array
   Join Date : 29th March 2011
   Posts : 54
   Rep Power : 554
   Likes Received
   13
   Likes Given
   0

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....

   Kasikilize zilipendwa na kuona picha za wanamuziki wa zamani kwenye blog hii muruwa ya WANAMUZIKIWA TANZANIA. Na pia WANAMUZIKI LEO
   Click image for larger version. 

Name:	ScannedImage-3.jpg 
Views:	218 
Size:	46.3 KB 
ID:	34181

  21. ngalikikinakiki's Avatar
   Member Array
   Join Date : 29th March 2011
   Posts : 54
   Rep Power : 554
   Likes Received
   13
   Likes Given
   0

   Default Re: Tujikumbushe: Bendi zetu za zamani(miaka ya 80 na 90),mitindo yao na wanamuziki wake....  Page 4 of 20 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa RTD
   By Ntambaswala in forum Celebrities Forum
   Replies: 244
   Last Post: 24th October 2013, 16:23
  2. Picha za wanamuziki wa zamani
   By ngalikikinakiki in forum Entertainment
   Replies: 0
   Last Post: 27th August 2011, 09:57
  3. Bendi zetu za Zamani
   By yutong in forum Celebrities Forum
   Replies: 4
   Last Post: 15th July 2011, 22:47
  4. Iko wapi historia ya bendi zetu?
   By vukani in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 4
   Last Post: 14th April 2010, 15:48
  5. Tujikumbushe Marefa wa zamani
   By Ibrah in forum Entertainment
   Replies: 11
   Last Post: 12th April 2010, 18:59

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...