Nalilia mtoto
Nakulilia Mola wangu weee,
Nakuwaza Mola wangu wee,
Yalonipata makubwa naona balaa,
Wala hamu sina x2
Wenzangu wana watoto,
Mimi sina hata wa dawa eeeh,
Niwatumapo wana wa wenzangu,
Mama zao hunisimanga x2
Nalia nasikitika bahati sina,
Kwa waganga wa kila namna nimefika ni bure tuuuu,
Hospitali za kila namna nimekenda ni bure tuuuu,
Mola nimemuomba na sadaka nimetoa ni bure tuuuu,
Mola, Mola, Molaaa eeeh,
Mola eeeh nataka mtoto,
Mola Mola, Molaa eeh,
Mola eeh, nalilia mtoto
Mtoto angelikuwa ni nguo ningenunua,
Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,
Hata angelikuwa kilema au mbaya kama Remmy ni mtoto tu!
Mola Mola, Mola eeeh....
Follow Us Here