Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
Nimeshangazwa sana kusikia Mh. S. SItta
akisema Sioi hakuwa chagua la wanaccm maana kapandikizwa
kwa mizengwe.
Akiongea kwa masikitiko kwa ccm kuzidi kudhoofika na kutokukubalika
kwa wananchi amamuomba mwenyekiti wa chama kusafisha chama ili nyota
ya chama ianze kung'ara. Hii ni kwa mjibu wa sitta baada ya kuongea na waandishi wa HAbari
Mytake:
Naona chama kinazidi kuparaganyika na sitta anazeeka vibaya
maana unafiki wake ndo unamponza
re: Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
Huu sasa ndio unafiki wa kisiasa.
Kwan huyo SIO hakupitishwa na NEC ambayo yeye ni MJUMBE? Je alichukua hatua gani?
Mbona Jack Masamaki (mgombea udiwani kata kirumba-CCM) ambaye alikuwa chaguo la CCM, na ambaye yeye SITTA alimpigia kampeni ameshindwa pia?
Huyu mzee akubali kushindwa tu, HUU NI WAKATI WA CDM
re: Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
ki-pschologia hapo sitta anajaribu kujustify failure,kwa taarifa yake hata yeye sio chaguo la wananchi,mimi nawashangaa watu wa urambo wametuleteeje bungeni sitta tumewakosea nini
re: Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
Sitta anatakiwa aamue moja, ama abaki CCM au awe nje ya CCM. Serikali ya ccm ndiyo inamlisha, inampa makazi na vikwerombwezo vyote, hawezi kufaidi mafao ya CCM na serikali yake wakati huo huo anaituhumu! Huku ni kujikosha.
Hadithi za kusema 'mimi ni mpinga ufisadi' ni hadaa. He is either with CCM or against them. period.
Kuhusu Sioi, CC ya CCM ilimpitisha huyu kijana, sasa Sitta analeta porojo gani? Au hiyo CC iliyoongozwa na Kikwete ilikuwa ni cc ya Dovutwa? Kama yeye Sitta alishindwa kumpigia debe 'mteule' wake wakati wa kura za maoni ni jambo jingine lakini hawezi kujitokeza leo na kuharamisha maamuzi ya CC ya CCM. Huo ni usaliti kwa chama chake maana yeye (Sitta) ni miongoni mwa viongozi wa juu wa CCM.
Hakuwa chaguo la wana ccm!!!alafu anamuomba mwenyekiti gani asafishe chama wakati ni jk aliongoza vikao mara mbili na kumpitisha sioi? Tulieni mnyolewe
Mkuu si unajua kifo cha mfa maji ndo kama hivyo kutapatapa sana tu
re: Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
Huyu Mzee anababaika,haeleweki wala haaminiki na hajui asimame wapi manake tamu anaipenda na chungu anaipenda, mbona hakuyaeleza haya mwanzoni tena baada ya kurudia uchaguzi wao wa ndani?..
re: Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
By Kachanchabuseta
Nimeshangazwa sana kusikia Mh. S. SItta
akisema Sioi hakuwa chagua la wanaccm maana kapandikizwa
kwa mizengwe.
Akiongea kwa masikitiko kwa ccm kuzidi kudhoofika na kutokukubalika
kwa wananchi amamuomba mwenyekiti wa chama kusafisha chama ili nyota
ya chama ianze kung'ara. Hii ni kwa mjibu wa sitta baada ya kuongea na waandishi wa HAbari
Mytake:
Naona chama kinazidi kuparaganyika na sitta anazeeka vibaya
maana unafiki wake ndo unamponza
re: Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
huyu mzee ni mnafiki yani unafiki wake umepitiliza. Yeye na mwenzake mwakyembe mwanzoni nilikuwa nawaona watu wa maana sana lakini siku zinavyozidi kwenda wanazidi nichefua.
Huyu sitta anatafta umaarufu lengo likiwa uraisi 2015 apitishwe na chama cha magamba kuwa mgombea jambo ambalo kwa upande wangu naona ni ndoto sidhan kama ana nguvu sana katika chama cha magamba.
Kama hakuwa chaguo lao mbona hakusema mapema amesubiri uchaguzi uishe kama si mnafiki ni nini?
re: Samwel Sitta: Siyoi Sumari hakuwa Chaguo la wanaCCM
Chadema sasa waandae mikakati mizuri ya kukubalika katika ukanda wa Pwani kama Majimbo yote ya Mkoa wa pwani, baadhi ya Majimbo ya Dar es salaam( Temeke& Kigamboni) Majimbo ya Mtwara na Lindi na kukijenga chama katika visiwa vya Unguja na Pemba kufanya hivyo itakuwa ni kukipa mkono wa kwaheri CCM na CUF
Follow Us Here