najua kwenye siasa watu wanaweza kurushiana maneno. Lakini kwa vyovyote vile lugha inayotumiwa na lucinde haiwezi kukubalika kwenye jamii yoyote iliyostaarabika. Na mbaya zaidi mikutano mingi ya ccm inahudhuriwa na watoto. Lakini cha ajabu viongozi wa juu wa ccm (taifa) wanaonekana kukubaliana na matusi haya vinginevyo wangekuwa tayari wamemkalisha chini lucinde.
Mtu kama lucinde anaonekana kuongelea ngono all the time! Mbele ya watoto! Ustaarabu gani huu?
Maadam wakubwa zake kwa maana ya uongozi wa juu wa ccm umeshindwa kuona matumizi ya lugha yanayopingana kabisa na mila, tamaduni na heshma wa watu wa wameru basi ni jukumu la wazee na vijana wa meru kuchukuwa hatua.
Napendekeza wazee wa kimeru au vijana wa kimeru waitishe mkutano na waandishi wa habari ili kutoa onyo kwa lucinde kwa kutumia lugha inayoharibu kabisa taswira ya watu wa arumeru. Lucinde anataka ulimwengu uamini kuwa watu wa arumeru wanataka kusikiliza matusi na sio sera?
Follow Us Here