KWANZA KABISA POLE NA SAFARI MUH. LOWASA
Inaonekana kasi mpya imegonga mwamba siamini waziri mkuu ameishiwa na maneno mwana siasa mahiri kama Lowasa au alikuwa amechoka na safari, ameshindwa kujibu swali la waandishi wa habari kuhusu janga la umeme linalo tukabili katika taifa letu imekuwa vichekesho katika vyombo vya habari hapa nchini vikiwemo radio ''eti Lowasa anazidi kuwakatisha mamilion ya watanzania tamaa'' kwa kusema kwamba tatizo la UMEME WAMELIRIDHI kutoka serikali ya awamu ya tatu (mbona Mkapa alikupenda sana )jamani wenzangu mnao lala giza mnakubaliana na kauli hiyo hii ni kauli ya kushindwa kazi .
Ninaamini awamu iliyo pita walikuwa wamesha zaliwa na walikuwa kazini katika wizara nyeti wizari ya MTERA wiazri ya MAJI na KILIMO vyote hivi vinausiana na vimiminiko akulijua hilo au alikuwa anatumia REMOTE kama TV kuendesha wizara yake
Sasa jamani tuangalie jinsi ambavyo tunaweza kuwapa wananchi matumaini ya kila kitu ni kweli JK kazi anaiweza lakini msimuangushe mimi nita mtetea Muh. Kikwete mpaka siku nitakapo ingi kaburini watu wake wana muaribia kama uwezi kujibu maswali usiongee na waandishi wa habari labda ukuonge hivyo lakini wame kutafsiri vibaya.
Pia Muh. Lowasa anavyo penda sherehe atuwezi kusheherekea bila mwanga miaka 45 ya uhuru inakuja hizi sherehe za mabilion kwenye giza kwa nini tusishugulikie maswala ya muhimu sherehe tutazifanya tu tukiwa vizuri. hii ndiyo nchi ya kwanza duniani viongozi na wananchi wao wana fanya sherehe wakati wana matatizo kibao.
Ninakumbuka gazeti la Tanzania Daima la wiki mbili zilizo pita kulikuwa na makala walimuandika mweshimiwa Lowasa ni NEWS EDITOR sasa hili imekuwaje akuliona au hawakukupigia simu?
Muh. Lowasa mimi nina kupa ushauri siyo lazima kujibu kila swali utakalo ulizwa jibu la hili swali lilikuwa rahasi kabisa jibu lake ni ''Tunalishugulikia'' basi umemaliza ninaamini akuna viongozi wanaulizwa maswali magumu kama viongozi wa marekani lakini wanajibu kwa kifupi pili au unachukuwa maswali mengi jibu yale unayo yaweza
Ninaomba nikuambie kuwa waandishi wa habari siyo rafiki zako ,hili unaju ndiyo walio wajenga na ndiyo wata kao wabomoa.
Kwanza kabisa ungeliezea mafanikio ya safari yako kama ulivyo fanya pia umekuja na habari nzuri ya wa Canada kuwekeza katika UMEME basi inatupa sisi matumaini kuwa giza litaisha .
hayo ndiyo maneno yangu kwa maziri husika wewe ni kiongizi mkubwa sana nchini neno lako moja linaweza kuadhiri watu wengi sana.
Bado tuna wapenda kazi mnafanya msikate tamaa haya nimatatizo yanayo tatulika japo kuwa Mmepotea njia rudini njia panda muanza tena mtafika tu. mkiendelea hivi huko katikati mtapotea bado nguvu mnayo.
Jingine Muh. kikwete wananchi wana Kapenda sana sana....... mimi pia nina kupenda sana kama nilivyo eleza mwanzo hata watanzania wakilala gizi wana fikiri Taa zina waka fanyeni haraka msingoje wakakurupushwa.
asanteni

Reply With Quote

Follow Us Here