Mkuu naomba nitofautiane nawe, kuwa mwanaume hakumzui mtu asiwe anamshabikia msanii wa kiume. Mbona wana kibao mitaani wanawashangilia na kukubali wacheza mpira wa kiume, wasanii wa kiume wa ulaya na marekani, pia watu wanawashabikia wanasiasa wa kiume na wanafuatilia maisha yao na CV zao, utasema nao wana matatizo ya kijinsia? Pia hakuna ambaye huwa anawahoji 'whether they are straight?' Au kwa kuwa PHD ni mtanzania basi watu wasimshabikie sana? Tujifunze kukubali kuwa binadamu tupo tofauti na kila mtu ana haki ya kushabikia na kupenda msanii/mchezaji/mtu yeyote. Kufanya hivo hakumfanyi mtu awe tofauti na mienendo ya jinsia yake.
Follow Us Here