manyaunyau anatisha. pale mwananyamala alifukuza mchawi mchana kutoka pale kwa bi zakalia ndani kwa ndani hadi kwa mtogole watu kibao wanamfuata akanyosha hadi manzese huku ameshikilia paka mdomoni na vijana wake wakipiga ngoma, akanyonya hadi mabibo ndani kwa ndani hiyo mi nikaunga tela, tukaibukia external tukapita makuburi tukatelemka tukapanda tukaibukia kimanga, akadaka paka mwingine kanyonya damu, tukaenda hadi tabata visiwani hadi tabata bima hiyo ishafika saa 12 jioni....
"If I have seen further it is by standing on the shoulders of Giants" (Newton, 1675)
Hii ya kunywa damu mbichi ya paka ndio inayoogopesha watanzania walio wengi wa uswahilini, kwa sisi tuliozoea ma-discovery channel na ma-animal planet hiyo ni issue ya kawaida sana wale wazungu sio tu wanakunywa damu bali hata nyama wanaila laivu,sio sumu ukinywa hiyo damu ni mazoea tuu, sasa dubu alipoona mtu ananyonya damu ya paka akaacha kila kitu na kujoin msafara!
Hata Sokoine alipofariki 1984 tulisikia mengi. Wakadai kageuzwa msukule. Mganga mmoja akadai ana uwezo wa kumrudisha lakini eti aliomba ruhusa kwa Nyerere akakataliwa! Tukasikia uvumi kuwa Sokoine kaonekana Kariakoo wakati alishazikwa Monduli-Juu! Uvumi tu. Na huyu Manyaunyau ni walewale. Lakini ana ujasiri wa ajabu sana, hebu fikiria anavyomkata paka shingo na kunyonya damu yake! Hiyo tu inatosha kuwabadili watu akili maana wanaamini haiwezekani mtu anywe damu ya paka bure tu! Loh, tunayo kazi!
Hivi na akili zako timamu bado na wewe unaingizwa kwenye kundi la wajinga na kuamini kuna binadamu mwenye uwezo wa kumchinja paka kwa meno?
Hivi haujui kwamba mbwa kuna wakati anazidiwa na paka na anakimbia? paka kamwe hawezi kuchinjwa kwa meno na binadamu, paka ni sawa na chui tofauti yao ni maumbo tu, unachokiona kwa Manyaunyau ile ni midoli inatengenezwa South Africa na ndani yake kunakuwa na tomato source
Kwa mtu ambaye amesoma Dar es salaam enzi zetu mashuleni walikuwa wanakuja watu wa Mazingaombwe (magician ) na hicho ndicho anachokifanya Manyaunyau ni kiini macho tu hakuna la zaidi wala hakuna jipya.
Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.
Follow Us Here