JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: JF Man & Woman Of The Year 2011 Competition

  Report Post
  Results 1 to 2 of 2
  1. Superman's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st April 2007
   Location : On Move
   Posts : 5,593
   Rep Power : 4217542
   Likes Received
   1554
   Likes Given
   1312

   Default JF Man & Woman Of The Year 2011 Competition

   Angalizo: Mods kwa hekima mnaombwa msiiamishe thread hii wala kuichanganya na nyingine yoyote.

   Wanajamii; Wana JF

   Mwaka 2010 tulifanya mchakato wa kumpata JF Man & Woman of The Year 2010. Shindano kama hili pia lilifanyika Mwaka 2009.
   • Washindi wa 2009 "JF SuperLady" au "Celebrity wa JF" alikuwa WoS (Woman of Substance)
   • Washindi wa 2010 "Regia Mtema" (RIP) - Kwa JF Woman of the Year 2010
   • na Nyani Ngabu alifungana na Asprin kama "JF Man of The Year 2010"
   Mchakato wote mpaka mshindi kupatikana unaweza kuupitia hapa:

   http://www.jamiiforums.com/complaint...ar-2010-a.html

   Mwaka huu tunataka kuuboresha mchakato huu na tunapenda kupitia mchakato huu kupata washiriki wengi na kuipa taswira JF kuwa kuna watu wanafakubalika katika hii online community.
   Mwaka huu 2012 tunafanya mchakato wa kuwapata Washindi wa 2011 (lakini michango yao ya sasa inakubalika iingizwe 2011).Tulichelewa kufanya kwa sababu zilizo nje ya uwezo. Categories za Mwaka huu ni:

   • JF WOMAN OF THE YEAR 2011 na pia JF MAN OF THE YEAR 2011 (Overall).

   • Lakini Pia Tutaongeza Category Moja: "JF QUEEN OF MMU" and "JF KING OF MMU"

   Katika mchakato wa awali tutapendekeza majina mbalimbali katika category hizo mbili kulingana na unavyoona anakubalika na mwishoni tutachagua watatu kutoka katika kila category na kisha kuwapambanisha kupitia JF POLLS. Mwaka huu napendekeza tutoe zawadi yenye hadhi fulani kwa washindi ili kutoa changamoto za umakini katika mabandiko haba jamvini. Tutajulishana zawadi hizi tutakapoingia katika mchakato wa Kupiga kura.

   Vigezo vifuatavyo vizingatiwe katika kutoa mapendekezo ya watakaoshindanishwa katika hizi KURA ZA MAONI:

   1. Kama ni category ya WOMAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanamke na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike. Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - JEC (Superman) ya Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

   2. Kama ni category ya MAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanaume na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike.

   Katika 1 na 2: Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya JF (JEC) wa Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

   3. Anayependekezwa lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha kuwa ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na pia post anazobandika. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF.

   4. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.

   5. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.

   6. Kwa Wanaogombea Overall tittle, asibobee kwenye Jukwaa moja tu. Walau awe mchangiaji mzuri wa majukwaa yasiyopungua mawili. Kwa wale wanaopendekezwa MMU basi akubalike katika jumuiya ya MMU

   7. Asiwe mtu wa shari katika majibizano kiasi cha kupelekea Mods kumpa "BAN".

   8. Aonekane wazi katika mabandiko yake anaweza akahisiwa kuwa Kiongozi Mzuri.

   9. Awe Mchangiaji ambaye ni active walau mara moja kwa wiki. Ikiwa zaidi ni vizuri zaidi.

   10. Awe ni mtu asiyeogopa kukemea mabandiko yenye lengo la kutukana, kudhalilisha, kubagua, kuleta mfarakano na kutokuelewana baina ya wanachama wa JF.

   Sasa kila moja yuko huru kutoa mapendekezo yake ya nani wanastahili kuingia katika tatu bora katika kila category.

   Nashauri kuwa mapendekezo ya majina yaambatane na maelezo mafupi.

   Uwanja ni wenu. Karibuni sasa mto mapendekezo au NOMINATIONS.

   Wasalaam

   Signed Seal:

   Superman

   Mwenyekiti - Tume Ya Uchaguzi ya JF (JEC)


   (NB: TANMO Kijana wangu na Msaidizi wangu JEC kuwa Standby)


  2. Superman's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st April 2007
   Location : On Move
   Posts : 5,593
   Rep Power : 4217542
   Likes Received
   1554
   Likes Given
   1312

   Default Re: JF Man & Woman Of The Year 2011 Competition

   Karibuni


  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...