Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dk Stephen Ulimboka Jembe na Nguzo ya MADAKTARI Nchini

    Report Post
    Page 4 of 8 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 141
    1. #1
      Chief Lugina's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st July 2011
      Posts : 177
      Rep Power : 439
      Likes Received
      53
      Likes Given
      57

      Default Dk Stephen Ulimboka Jembe na Nguzo ya MADAKTARI Nchini


      Madaktari wakiwa wameshika mikono huku waiimba nyimbo za kuashiria umoja katika mgomo wao unaoendelea jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix

      Geofrey Nyang’oro
      SAKATA la madaktari nchini linazidi kuchukua sura mpya baada ya wataalamu hao kukataa hoja za ujumbe wa Serikali ulioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, Hawa Ghasia huku wakigoma kusikiliza kauli yoyote kutoka kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda

      Wakati mawaziri hao wakikumbwa ana tafrani hiyo tayari wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na ile ya Mkoa wa Dodoma wametishia kusitisha utoaji huduma ifikapo Jumatatu kama masuala yao hayajapatiwa ufumbuzi.

      Vigogo wa Serikali waliofika kukutana na madaktari hao jana ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na naibu wake, Dk Lucy Nkya, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Blandina Nyoni, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa.
      Tukio hilo lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Star Light, Jijini Dar es Salaam ambako madaktari hao walikusanyika na baadaye kupewa taarifa kuwa kuna ujumbe wa Serikali utafika kwa majadiliano. Madaktari hao waliwatimua ujumbe huo baada ya kuusikiliza juu ya wito wao wa kuwataka wasitishe mgomo ili wafungue ukurasa wa majadiliano, wakajibiwa kuwa kwa sasa ni wakati wa kutekeleza kwa vitendo na siyo ahadi.

      Ujumbe huo wa Serikali uliwasili ukumbini hapo majira ya mchana na kukaribishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Stephen Ulimboka ambaye baada ya kuwawekea viti pembeni mwa jukwaa kuu, aliwatambulisha kwa washiriki. “Ugeni tuliokuwa tunasubiri umefika, si rahisi sisi wote kuwafahamu ni vema wangejitambulisha wao kwa majina kisha tuendelee na utaratibu tuliojiwekea,” alisema Dk Ulimboka.

      Mara baada ya kauli hiyo, wageni hao walianza kujitambulisha. Wa kwanza alikuwa Waziri Ghasia aliyewasalimia madaktari hao na kujitambulisha kisha kueleza kuwa aliongoza ujumbe huo kuwasilisha taarifa ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Dalili mbaya kwa ujumbe huo, zilianza kujitokeza walipoitika kwa nguvu salamu ya Waziri Ghasia huku wakiwanyamazia Waziri wa Afya na maofisa waandamizi wa wizara hiyo.

      Baada ya tukio hilo kumalizika, Dk Ulimboka alitoa taratibu za mkutano kuwa ni kusoma taarifa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa Waziri Mkuu. “Sisi hapa tutawakabidhi taarifa iliyoandaliwa na madaktari ambayo ni maalumu kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baada ya kuwasomea, tutawakabidhi kisha tusubiri majibu ya taarifa yetu tukiwa hapahapa,” alisema Dk Ulimboka.

      Dk Ulimboka alisoma taarifa hiyo mbele ya wageni hao ambayo ilitaja madai yao kadhaa ikiwemo kumtaka Waziri Ghasia kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa katika wizara hiyo, Waziri Mponda na naibu wake Dk Nkya, Katibu Nyoni na Mganga Mkuu, Dk Mtasiwa.

      Mara baada ya kusoma taarifa hiyo alikabidhi barua hiyo kwa Waziri Ghasia huku akisisitiza kuwa wataendelea na mgomo hadi watakapopatiwa majibu ya hoja zao.

      “Tunaomba taarifa hiyo imfikie haraka Waziri Mkuu, ijadiliwe kwa haraka na kutoa majibu yatakayotupatia ufumbuzi ili nasi turudi kazini tukaokoe maisha ya Watanzania,” alisema Dk Ulimboka ambaye kwa kauli yake iliashiria kufunga mjadala.

      Baada ya kauli hiyo, Waziri Ghasia alisimama na kueleza kuwa wao walifika wakiwa na ujumbe toka kwa Waziri Mkuu hivyo ni vema wangekubaliwa wauwasilishe ambapo alimtaja Waziri wa Afya Dk Mponda kuwa angeusoma.
      Dk Ulimboka alijibu hoja hiyo akisema “Madaktari hatuna tatizo na ujumbe toka kwa waziri Mkuu Mizengo Pinda ila ujumbe kutolewa na Waziri wa Afya Dk Hadji Mponda hatukubali kwasababu hatuna imani naye labda kama kweli ni taarifa, ungesoma wewe,” alisema Dk Ulimboka na kukaa chini.

      Waziri Ghasia alikubaliana na hoja hiyo na katika kuwasilisha taarifa hiyo, alisema alisononeshwa kusoma majibu yanayohusu madai ya madaktari hao kwa niaba ya waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Afya wakati yeye (Dk Mponda) akiwepo.

      Ghasia alisema wizara imetafakari kwa kina suala la madaktari waliokuwa kwenye mafunzo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili na kuwarudisha kwenye kituo hicho cha kazi huku ikiahadi kuwalipa stahili zao.
      “Wazira imetafakari kwa kina na imeamua kuwarejesha madaktari wote waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili na wanatakiwa kuripoti katika vituo hivyo vya kazi kuanzia Jumatatu,” alisema Ghasia.

      Kuhusu madai mengine, alisema Serikali itaendelea na majadiliano ya pamoja huku akiwaomba warejee kazini.
      “Sisi tuwaombe tu kwamba madai yenu yote Serikali inayafanyia kazi. Suala la nyumba tayari tumeshapata fedha kutoka Global Fund kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za madaktari ili waweze kukaa karibu na vituo vyao vya kazi,” alisema Ghasia. Akijibu ombi la kuwataka warejee kazini, Dk Ulimboka alisema hilo litategemea majibu ya taarifa walioiwasilisha kwa Waziri Mkuu, ambapo alisisitiza kuwa wao wataendelea na mikutano katika ukumbi huo.

      “Sisi tutaendelea na mikutano kujadili taarifa yenu na pia tungeshauri taarifa hii mtuletee kwa maandishi, lakini pia tunasubiri majibu ya taarifa yetu tuliyoiwasilisha kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambayo tumeitoa kwa maandishi,” alisema Dk Ulimboka. Dk Uliomboa aliwataka wawakilishi hao wa Serikali kutambua kuwa ujumbe haukuwa wa kushawishiana kurudi kazini bali ni wa kupeana taarifa.

      Kauli hiyo iliashiria kwamba hoja ya ujumbe huo haina uzito wa kuwashawishi kuacha mgomo huku wakikataa hoja zao sasa kujadiliwa na wizara badala yake walisisitiza Waziri Mkuu kushughulikia suala hilo. Walimtaka Waziri Mkuu, kutoa majibu ya madai yao kwa wakati ili asiwafanye kufikia hatua ya kusitisha huduma katika vitengo vya dhararu.

      “Mgomo huu unaendelea nchi nzima hadi majibu ya madai yetu tuliyowasilisha kwa Waziri Mkuu yamepatiwa majibu.
      Tunashauri kazi hiyo ifanywe haraka vinginevyo tusije tukashawishika kusitisha huduma kwenye vitengo vya dharura,” alisema Ulimboka.

      Tishio la mgomo zaidi
      Wakati huo huo, Chama cha Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kimesema kuwa wauguzi wataendelea kutoa huduma kwa kusuasua hadi Jumatatu na kama suala hilo litakuwa halijapatiwa ufumbuzi, watasitisha huduma na kufunga hospitali.

      “Sisi tutaendelea kutoa huduma katika mazingira ya shida hivi mpaka Jumatatu tu,” alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Paul Magesa.
      Believe those who are seeking the truth. Doubt those who find it.

    2. FemaTV & Radio

    3. #61
      gwino's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 19th November 2010
      Posts : 243
      Rep Power : 479
      Likes Received
      25
      Likes Given
      10

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By kingxvi
      jamaa anapenda sifa za kijinga sana toka zamani namjua vizuri
      na bado, utaendelea kumjua vizuri

    4. #62
      Ndyali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2011
      Posts : 549
      Rep Power : 487
      Likes Received
      140
      Likes Given
      3

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By FaizaFoxy
      Cha kushangaza ndio hicho, anaogopa nini kama kweli yupo kwenye haki?

      Tukiwaambia hawa ni wachochezi, hamkubali.
      Hata Magamba kwa magamba hawainiani, kuna tetesi kuwa FF ndiye mwenye roho mbaya ya kuwatilia sumu magamba wenzie Unachekesha!!
      only83 likes this.

    5. #63
      Zak Malang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2008
      Posts : 4,835
      Rep Power : 1922
      Likes Received
      187
      Likes Given
      2

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Kama kawaida yao utawala wa magamba, wakishindwa nguvu ya hoja, basi hukimbilia nguvu za dola! Duh tutafika?
      Being prolific doesnt mean you are an accomplished person

    6. #64
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      jeshi la ulimboka karibu linashindwa yetu macho

    7. #65
      Somoche's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th October 2010
      Posts : 1,861
      Rep Power : 813
      Likes Received
      345
      Likes Given
      338

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Ilitakiwa kada nyingine tumuunge mkono ili serikali hii chovu iamke sasa tatizo kada zingne wanafiki tu...

    8. Miaka 50

    9. #66
      MwanaFalsafa1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Posts : 5,446
      Rep Power : 9879
      Likes Received
      609
      Likes Given
      445

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By Kimbunga
      Mkuu mimi si shujaa ndio maana najificha. Shujaa yuko mafichoni kwani anaendesha vita ya msituni?
      Kwani yeye kajiita shujaa mkuu?

    10. FJM
      #67
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,170
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5318
      Likes Given
      4585

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By MAMA POROJO
      kakimbia presha ya pinda anasingizia usalama ili asionekane muoga
      Nilifikiri hoja ni mgomo, whether kuna mtu mmoja mmoja anaonekana au la hilo linabadilisha nini kwenye mgomo? TBC1 wamefanya kazi kubwa sana ya kuficha ukweli, lakini kama umeangalia ITV Muhimbili hali si hali. Ambulance zinaondoka na wagonjwa. hakuna hata mtu wa kuwapokea. Dr Ulimboka awe shimoni au awe Kempenski lakini ukweli ubaki pale pale, mgomo huu umeanika udhaifu mkubwa mno kwa serikali yetu kutatua mgogoro sehemu za kazi.

    11. #68
      Mshiiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2008
      Location : Sillicon Valley - USA
      Posts : 1,351
      Rep Power : 1233
      Likes Received
      58
      Likes Given
      17

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Acha unafiki wakutane naye wa nini ikiwa kama kila madai tyao yako kwa maandishi???? Huku kutafutana sababu tu. Think outside the box meeeeen.


      Quote By Kimbunga
      Wamefanya makosa. Jana wameambiwa wakakutane na PM wao wakajificha. Kama una nia nzuri ya majadiliano kwa nini ujifiche?
      “You will not be punished for your anger; you will be punished by your anger.”

    12. #69
      PATALI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th December 2011
      Posts : 88
      Rep Power : 393
      Likes Received
      35
      Likes Given
      0

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By FaizaFoxy
      Cha kushangaza ndio hicho, anaogopa nini kama kweli yupo kwenye haki?

      Tukiwaambia hawa ni wachochezi, hamkubali.
      Kuna anakufahamu..kaniambia ulivokuwa mdogo ulibakwa na babako ndo mana akili si nzuri!

    13. #70
      Zak Malang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2008
      Posts : 4,835
      Rep Power : 1922
      Likes Received
      187
      Likes Given
      2

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By Marksman
      Kama kawaida yao utawala wa magamba, wakishindwa nguvu ya hoja, basi hukimbilia nguvu za dola! Duh tutafika?
      Ni moja ya dalili ya utawala huu kufikia ukingoni. Mwenye mtazamo tofauti na ajitokeze hapa!

    14. #71
      Zak Malang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2008
      Posts : 4,835
      Rep Power : 1922
      Likes Received
      187
      Likes Given
      2

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By FaizaFoxy
      Cha kushangaza ndio hicho, anaogopa nini kama kweli yupo kwenye haki?

      Tukiwaambia hawa ni wachochezi, hamkubali.

      Tangu lini serikali ya magamba inakuwa kwenye haki? wabunge posho juu sawa, madaktari mishahara juu hapana! sina muda wa kukutolea orodha ndefu ya ukiukwaji wa haki wa utawala wa magamba!
      Uwezo Tunao likes this.

    15. #72
      Sigma's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 26th February 2011
      Location : The 2nd House on the Left
      Posts : 4,258
      Rep Power : 0
      Likes Received
      915
      Likes Given
      613

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By MAMA POROJO
      kamanda ulimboka vita ya msituni imepitwa na wakati toka mafichoni
      Yuko nyumbani,
      umewahi kuona msitu sinza?


    16. #73
      Kigarama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2007
      Location : Manzese kwa Mfuga Mbwa
      Posts : 2,359
      Rep Power : 16278
      Likes Received
      974
      Likes Given
      703

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By Kimbunga
      Shujaa anajificha tena? Huko mafichoni ana silaha gani na analindwa na nani?
      Osama alijificha kwa miaka mingapi jee athari zake kwa nchi za magaribi zikoje. Leo osama hayupo falsafa na itikadi yake pia haipo? Kujificha kwangu mimi si uoga bali ni mbinu sahihi ya mapambano kwenye nchi kama yetu ambayo vibaraka ni wengi kuliko wazalendo wa kweli.

      NA ATAKAYEMSALITI Dr. ULIMBOKA NI LAZIMA ASULUBIWE!!

      Freestyler likes this.
      UKIDHANI WEWE SI MWENDAWAZIMU PIMA KWANZA UHUSIANO WAKO NA MACHIZI!!

    17. #74
      Chakaza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2007
      Location : everywhere
      Posts : 3,540
      Rep Power : 1474
      Likes Received
      881
      Likes Given
      522

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Sasa ndio nimeanza kuona umuhimu wa ICC kule The Hague, CCM endeleeni kutafuta njia za ku eliminate watu kimyakimya kuna siku tutawaona watu wamevaa headphone kusikiliza mashtaka yao.
      Hatutajua chochote iwapo hatutahoji na kudadisi

    18. #75
      LE GAGNANT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2011
      Posts : 1,228
      Rep Power : 709
      Likes Received
      222
      Likes Given
      184

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By katatuu
      hana mpango.kama hawezi kujitokeza kisa anatafutwa basi asitishe mgomo.sasa watakutana vipi wakati hawajitokezi hadharani.mikakati yao wataiendeshaje.ama kweli kunguru mwuoga hukimbiza bawa lake.yeye nilitegemea atakuwa mstari wa mbel
      e kwa lolote.madak
      anatumia"guerrilla warfare", hawezi jitokeza mojakwa moja kama kuna hatari ya kushikwa. Hata bw mashaal wa hamas yuko mafichoni syria na struggle zinaendelea.
      SI VYOTE VING'AAVYO NI DHAHABU

    19. #76
      Losambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2011
      Location : Katikati
      Posts : 2,346
      Rep Power : 850
      Likes Received
      688
      Likes Given
      296

      Default

      Quote By MAMA POROJO
      kamanda ulimboka vita ya msituni imepitwa na wakati toka mafichoni
      Hata mtoto hukaa miezi tisa tumboni na ndipo hutoka. Wakati bado.

    20. #77
      Maneno Anania's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th January 2012
      Posts : 51
      Rep Power : 381
      Likes Received
      5
      Likes Given
      1

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Sina hakika kama usalama wa Taifa wameshindwa kumkamata! Wakihitaji kufanya hivyo najua wanaweza.

    21. #78
      1800's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 1,656
      Rep Power : 891
      Likes Received
      415
      Likes Given
      21

      Default

      Quote By MTM
      fichuka basi na wewe useme jina lako... mambaff
      Jinga ilo mkuu,hachana nalo!eti linasema shujaha anajificha!nyambafu kabisa,ulimboka alishajiweka wazi toka mwanzo na kaikosesha usingz serikali!watanzania wafunguke sasa!

    22. #79
      JOB SEEKER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st August 2011
      Posts : 138
      Rep Power : 422
      Likes Received
      32
      Likes Given
      8

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By Ndyali
      Mkuu MTM, umenipa jioni njema, comment za hili lijamaa ni za kukurupuka uharo wa kipindupindu.
      heshima kidogo mzee jogoo hafi kwa utitiri

    23. #80
      Ndyali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2011
      Posts : 549
      Rep Power : 487
      Likes Received
      140
      Likes Given
      3

      Default Re: Dr ulimboka aongea kutokea mafichoni...adai anatafutwa na wana usalama.

      Quote By MAMA POROJO
      kamanda ulimboka vita ya msituni imepitwa na wakati toka mafichoni
      Tangulia wewe kutumia ID halisi ushughulikiwe, unacheleweshea ukombozi kutoka kwa mkoloni mwenye magamba.

    Page 4 of 8 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...