Go Back   JamiiForums.com > Public Forums > Business & Economic Forum

Reply
 
LinkBack Thread Tools Display Modes
  #1 (permalink)  
Old 6th July 2007, 09:54 PM
KadaMpinzani's Avatar
JF Senior Expert Member
 
Join Date: Wed Jan 2007
Location: Chadema Restaurant
Posts: 4,586
Rep Power: 30
KadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to behold
Thanks: 1,654
Thanked 708 Times in 541 Posts
Credits: 101,460
Post Wafadhili wagoma kuipa serikali mabilioni

Wafadhili wagoma kuipa serikali mabilioni
Na Hassan Mghenyi

BAADHI ya wafadhili walioahidi kutunisha bajeti ya serikali mwaka uliopita, wameshindwa kutimiza ahadi zao na hivyo kukwamisha miradi mingi ya maendeleo.


Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyotolewa Juni mwaka huu, inaonyesha kuwa misaada ya wahisani na mikopo nafuu ambayo haijalipwa katika kipindi cha bajeti ya 2006/07 inafikia asilimia 35.


Katika kipindi hicho, bajeti hiyo ya serkali ilitegemea wafadhili kwa asilimia 39. Jumla ya fedha kutoka nje iliyolipwa ni Sh939.7 bilioni kati ya Sh1.439 trilioni zilizoahidiwa.


Katika kipindi hicho, kiasi cha mikopo yenye thamani ya Sh673.8 bilioni kiliidhishwa na wafadhili, na sehemu ya fedha hizo zilitumika kupunguza pengo la bajeti na sehemu iliyobakia ilitumika kulipa deni la ndani.


Wakati hali ikiwa hivyo, serikali katika mwaka huu wa fedha imeongeza utegemezi wa fedha za wafadhili katika bajeti yake kutoka asilimia 39 hadi asilimia 42.


Vile vile serikali imeongeza utegemezi wa fedha za nje katika miradi ya maendeleo kutoka Sh1.092 trilioni mwaka jana hadi Sh1.462 trilioni mwaka 2007/08, sawa na ongezeko la asilimia 33.9.


Kwa mujibu wa ripoti hiyo, deni la taifa limeongezeka hadi dola za Marekani 6,112.4 milioni kufika Mei mwaka huu kutoka dola 6,041.6 milioni Aprili mwaka huu na sababu zinazoelezwa ni kutokana na shughuli za serikali na kupungua kwa thamani ya shilingi.


Kati ya deni hilo, asilimia 75.9 ni la nje na silimia 24.1 ni deni la ndani. Hadi kufika Mei mwaka huu deni la nje liliongezeka hadi kufikia dola za Marekani 4,636.3 milioni kutoka dola 4,597.2 milioni mwezi uliotangulia, ambalo ni ongezeko la asilimia 39.1.


Ripoti hiyo inaeleza kuwa watumiaji wakubwa wa fedha kutoka nje ni serikali kuu ambayo imetumia dola za Marekani 2,684.3 milioni sawa na asilimia 78.1, sekta binafsi dola 583.2 milioini (asilimia17) na mashirika ya umma dola 167.6 milioni (asilimia 4.9)


Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonyesha kuwa deni la ndani nalo limeongezeka hadi kufikia Sh1.857 trilioni mwishoni mwa Mei mwaka huu kutoka Sh1.846 trilioni Aprili 2007 na sababu inayoelelzwa hapo ni amana za serikali ambazo ni asilimia 99.1.


Wadai wakubwa wa deni la ndani ni benki za biashara asilimia 43.2, mifuko ya pensheni asilimia 28 na Benki Kuu asilimia 19.2.


Kuhusu matumizi ya serikali ambayo yamekuwa yakiisumbua serikali kwa muda mrefu, yalifikia Sh3.796 trilioni kwa mwaka wa fedha 2006/07, wakati makusanyo ya kodi za ndani na fedha kutoka nje zilifikia Sh3.377 trilioni hadi Mei 2007, na kusababisha upungufu wa Sh419.7 bilioni.


Katika bajeti yake ya 2006/07, serikali ilikuwa imepanga kutumia jumla ya Sh4.85 trilioni ambapo makusanyo ya kodi za ndani yakiwa Sh2.46 trilioni na fedha kutoka nje Sh2.226 trilioni.


Serikali katika mwaka wake wa fedha mpya (2007/08) inategemea kutumia jumla ya Sh6.067 trilioni, kati yake makusanyo ya kodi za ndani ni Sh3.502 trilioni na fedha za nje ni Sh2.549 trilioni.


Serikali imetenga kutumia Sh3.866 trilioni kwa matumizi ya kawaida na matumizi ya miradi ya maendeleo ni Sh2.201 ambapo kati ya hizo fedha ya nje ni Sh1.462 trilioni.

source: http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=361

maoni yangu binafsi ni kwamba mie naona afadhali sana tena sana kabisa serikali yetu kunyimwa pesa kama mambo yenyewe yataendelea kuwa hivi, wee fikiria mtu kila mwaka anafikiria kukarabati ofisi yake, nyumba yake na mapati kila leo, mambo haya wapi na wapi jamani ? sasa kilichobaki nadhani ni serikali kuanza kupata hasira na inachotakiwa kufanya ni kuisafisha serikali nzima ikiwa pamoja na viongozi wake.
Reply With Quote


  #2 (permalink)  
Old 6th July 2007, 10:15 PM
Icadon's Avatar
JF Senior Expert Member
 
Join Date: Wed Mar 2007
Location: I'm Everywhere you are never there.
Posts: 2,955
Rep Power: 27
Icadon has much to be proud ofIcadon has much to be proud ofIcadon has much to be proud ofIcadon has much to be proud ofIcadon has much to be proud ofIcadon has much to be proud ofIcadon has much to be proud ofIcadon has much to be proud of
Thanks: 319
Thanked 1,287 Times in 799 Posts
Credits: 214,438
Send a message via ICQ to Icadon Send a message via MSN to Icadon Send a message via Yahoo to Icadon
Default

Juzi naona WB wametoa $ 60 Million kwa ajili ya sekta ya Afya...
__________________
This is food for thought, don't let it go to waste and while you are at it feel free to do the dishes.
Reply With Quote
  #3 (permalink)  
Old 6th July 2007, 10:27 PM
JF Senior Expert Member
 
Join Date: Sun Jun 2007
Posts: 1,783
Rep Power: 25
Mzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud of
Thanks: 1,117
Thanked 559 Times in 364 Posts
Credits: 41,528
Default

KadaMpinzani,
Mimi siamini kwenye AID or HAND OUTS ili kutatua matatizo tuliyo nayo- labla on purely humanitarian reasons- ukame, mafuriko n.k. Ndo maana hatuendelei!
Pia hata hizo $ Mil. 60 Icadon ktk Afya- sii zinaiishia kujenga majumba ya kifahari ya wakubwa? Mwananchi wa kawaida haambulii kitu!
Kuna ufafiti ulionyesha kuwa about 50% ya budget huishia hapa katkati- serikli kuu hadi Halimashauri- siyo chini zaidi- haiwafikii walengwa. Hebu angalia Mapungufu ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali yaani bilions of Shs zimepotea au kutumika vibaya- yet hakuna aliyechukuliwa hatua!
Sii heri tu msaada usije ili kweli ya ulaji ieleweke?
Yafaa nini kuendelea kuweka katika pakacha linaloendelea kuvuja?
Reply With Quote
  #4 (permalink)  
Old 6th July 2007, 10:46 PM
KadaMpinzani's Avatar
JF Senior Expert Member
 
Join Date: Wed Jan 2007
Location: Chadema Restaurant
Posts: 4,586
Rep Power: 30
KadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to beholdKadaMpinzani is a splendid one to behold
Thanks: 1,654
Thanked 708 Times in 541 Posts
Credits: 101,460
Default

Mzalendohalisi, ndio maana nikasema nasapoti kabisa serikali kunyimwa pesa. yaani inasikitisha sana kuona wapi hizo pesa zinapoishia.
Reply With Quote
  #5 (permalink)  
Old 6th July 2007, 11:31 PM
Kichuguu's Avatar
JF Senior & Premium Member
 
Join Date: Wed Oct 2006
Location: Popote Porini
Posts: 3,430
Rep Power: 30
Kichuguu has much to be proud ofKichuguu has much to be proud ofKichuguu has much to be proud ofKichuguu has much to be proud ofKichuguu has much to be proud ofKichuguu has much to be proud ofKichuguu has much to be proud ofKichuguu has much to be proud of
Thanks: 1,076
Thanked 2,219 Times in 966 Posts
Credits: 205,647
Default

Je inawezekana kuwa na citizen campaign against foreign donations, loans and handouts? Vitu hivi ndivyo vimelemaza kabisa nchi yetu, na nashangaa kabisa kuwa viongozi wetu wanavionea ufahari. Inabidi watanzania tuamke tivipige vita. Misaada yote isiwe inapitia serikalini, badala yake iende kwa wananchi moja kwa moja kama nguvu ya ziada baada ya serikali kuwa imetimiza wajibu wake kwa raia.


Hebu fikiria wewe kama baba wa familia yako, tuseme una wake wawili na watoto kumi wanoakutegemea lakini eti huwezi kuwahudumia. Sasa kwa vile huna uwezo unaenda kuomba msaada kutoka kwa mtu mwenye uwezo, naye anakuambia kuwa atatoa msaada kwa kuwanunulia watoto wako na wake zako nguo pamoja na mahitaji yao mengine kama matibabu; wewe uwe unanunua chakula tu pamoja na mavazi yako mwenyewe. Je kweli utaona ufahari wowote katika familia yako? Je jamaa huyo akiwanunulia wake zako nguo za ndani zinazowasha mwili wewe utasema nini?

Ni kama mfano huo wa familia, ndiyo maana inabidi serikali yetu pia ione aibu hiyo kwa kuondoa kabisa component ya bajeti inayotegemea misaada na mikopo. Kama msaada utakuja basi tutaupokea na kuongezea juu ya uwezo wetu lakini tusiishi kwa kutegemea misaada na mikopo kabisa. Zamani hizo Azimio la Arusha lilitufundisha hivi: "Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa taifa moja linategema misaada na mikopo ya taifa jingine kwa maendeleo yake."
__________________
Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

Last edited by Kichuguu; 7th July 2007 at 12:39 AM.
Reply With Quote
The Following User Says Thank You to Kichuguu For This Useful Post:
Dua (7th July 2007)
  #6 (permalink)  
Old 6th July 2007, 11:56 PM
JF Senior Expert Member
 
Join Date: Thu Jun 2007
Posts: 264
Rep Power: 22
tz_devil has much to be proud oftz_devil has much to be proud oftz_devil has much to be proud oftz_devil has much to be proud oftz_devil has much to be proud oftz_devil has much to be proud oftz_devil has much to be proud oftz_devil has much to be proud of
Thanks: 199
Thanked 99 Times in 54 Posts
Credits: 7,439
Default

Ninadhani strategic sanctions inaweza ikafanya kazi na wananchi tunaweza kufanya kampeni ya sanctions na ikafaanikiwa. Africa ya Kusini kwa mfano, walifanya wakati wa ubaguzi wa rangi (apartheid) na walifaanikiwa. Misaada inatolewa in the name of mwananchi wa kawaida, lakini haimfikii mlengwa (mwananchi). Kunafaida gani ya msaada ambao haumfikii mlengwa? Let us sanction these people.
Reply With Quote
  #7 (permalink)  
Old 7th July 2007, 12:13 AM
SteveD's Avatar
JF Senior & Premium Member
 
Join Date: Mon Jun 2007
Location: Mapinduzi - Iringa & Nyambiti - Mwanza
Posts: 3,091
Rep Power: 148
SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!SteveD is one of most respected JF members!
Thanks: 3,312
Thanked 1,815 Times in 1,022 Posts
Credits: 355,399
Send a message via ICQ to SteveD Send a message via AIM to SteveD Send a message via MSN to SteveD Send a message via Yahoo to SteveD Send a message via Skype™ to SteveD
Default

Kuna taarifa moja hivi niliisikia kutoka bbc, itabidi niitafute niipate,kwani ilielezea vizuri kweli kuhusu mambo ya kutegemea misaada na madhara yake. mambo ya misaada kusema ukweli yanatia aibu na kama Kichuguu unavyo eleza, misaada wakati unauwezo kweli ni aibu za nguoni. kila kitu tanzani kipo, kinacho hitajika ni ununuzi tu wa haki miliki za kutengenezea mitambo, hati miliki za michoro ya mabara bara, majengo, madaraja n.k., na pia kinacho hitajika ni hela za kununulia vifaa vya kisasa ambazo zinaweza kutokana na kualika wawekezaji au katika makusanyo ya kodi. maisha yetu yanaweza yakaonekana duni kwa miaka mitano hivi tu, lakini baada ya kujiondoa kwenye utegemezi huu wa misaada, maisha yetu yatakuwa bora maradufu hapo punde tu. Tukumbuke nchi nyingi za mashariki ya mbali zimejikomboa zenyewe baada ya kuepuka misaada mingi na masharti yake na sasa ni vivutio vikubwa vya kitalii na maendeleo katika jamii.

SteveD.
__________________
~*~ Happy New Year To You All !! ~*~

Fikra ni kitu kizuri, uzushi unatokana na fikra, fikra za uzushi ni kitu kibaya na ni uzushi, kutotenganisha uzushi na fikra ni kitu kibaya zaidi kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SDD6-07.


Reply With Quote
  #8 (permalink)  
Old 7th July 2007, 12:25 AM
JF Senior Expert Member
 
Join Date: Sun Jun 2007
Posts: 1,783
Rep Power: 25
Mzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud ofMzalendohalisi has much to be proud of
Thanks: 1,117
Thanked 559 Times in 364 Posts
Credits: 41,528
Default

SteveD, Kichuguu na Tz Devil pokeeni 4,
Mnajua Bajeti ya Jirani zetu Kenya 100% ni self financed? Wakati ulo wa Moi in 1990s wafadhili waligoma kumpata tafu Moi- akawaambia waishie! Kwa hiyo mwanzoni ilikuwa shida ila sasa wamesimama! Budget 100% ni kodi yao- ukuja msaada Inshalah- usipokuja- ok.
Yet sisi tumeongeza utegemezi to 39% to 42% mwaka huu.
Je huko ndo kusonga mbele? Na zaidi kuna pesa za Millenium Challenge toka US ambazo zinasubiriwa sana kwa ham- na karibu kila jibu Bungeni in this budget serikali injibu tusubiri pesa hii!
Huku ndo kusonga mbele?
Reply With Quote
  #9 (permalink)  
Old 7th July 2007, 01:06 AM
JF Senior & Premium Member
 
Join Date: Sat May 2006
Location: Songeaonline
Posts: 786
Rep Power: 24
Invincible has much to be proud ofInvincible has much to be proud ofInvincible has much to be proud ofInvincible has much to be proud ofInvincible has much to be proud ofInvincible has much to be proud ofInvincible has much to be proud ofInvincible has much to be proud of
Thanks: 64
Thanked 337 Times in 203 Posts
Credits: 45,864
Default

Madhara makubwa ya misaada/ufadhili ni kukosa uhuru wa kujiamulia mambo.

Ukiona serikali inajisifia kwa kufanikiwa kupata misaada mingi, ujue kuna tatizo la msingi katika fikra za watawala.

Misaada hutumika tu as a bridge kujijengea uwezo wa kujitegemea huko mbele ya safari.

Angalia Tanzania: Mwaka huu utegemezi kwa wafadhili ndio kwanza umeongezeka.

Serikali makini inatakiwa kuwa na mkakati. Kwa mfano: Mwaka 2006/07, utegemezi katika budget ni asilimia 39. Mwaka ujao, mkakati wetu ni kupunguza utegemezi kwa asilimia labda 2, na kufikia 37%. Wakati huo huo kubuni vyanzo mbali mbali vya mapato vya ndani.

Kupunguza utegemezi kutoka nje ndio kuongeza uhuru na usalama wa nchi. Kwa sasa hivi nchi yetu sio huru wala salama kwa asilimia kubwa.


Do we have strategic thinkers in the JK government?
__________________
Tanzania - Dola dhaifu, Viongozi wababe, Wananchi usingizini
Reply With Quote
  #10 (permalink)  
Old 7th July 2007, 01:21 AM
JF Senior & Premium Member
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: T dot
Posts: 4,730
Rep Power: 73
Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!Mkandara is one of most respected JF members!
Thanks: 2,187
Thanked 2,886 Times in 1,391 Posts
Credits: 428,744
Default

Lakini jamani ebu nambieni kitu kimoja!
Inakuwaje wasomi wengi humu wanaweza kuliona hili lakini sio viongozi wetu?... Je hii inatokana na maelezo ya Invincible hapo juu kuwa ni Tatizo la msingi katika fikra za watawala!.

Kusema kweli nashindwa kabisa kuelewa jinsi tunavyofikiria ama wanavyo fikiria viongozi wetu wanapofikia swala hili tena huona siafa kubwa kulitangaza bungeni pale tunaposamehewa!.
Je, kuna uwezekano kweli viongozi wetu wanafikiria kwamba Tanzania inaweza kuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kuendelea mbele kutokana na mikakati ya ukombozi ya IMF na mfuko wa mtu mwingine?

kama alivyosema Kichuguu, hii familia yetu ina wazazi vichaa kabisa hasa pale wanapozidisha hesabu ya wake (mikataba feki) kila wanapopewa msaada. Hivi kweli ni akili hiyo wakati watoto wako wanashinda njaa, mwanamme mwingine anasimama kulea famila yako kisha wewe kwa upuuzi wako unaongeza wake zaidi!.

Sintawalaumu WB hata kidogo ikiwa sisi wenyewe hatujafikia kutambua kuwa umaskini ni kilema badala yake tunatumia kilema hiki kama ndio kitega uchumi cha kusimama msikitini kila Ijumaa!...tukilalamika kuwa ni kazi ya Mungu - Aliyewapa wao ndiye katunyima sisi!
__________________
Exploration of reality
Reply With Quote
The Following User Says Thank You to Mkandara For This Useful Post:
Tabasamu (7th July 2007)
Reply

Bookmarks


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are On
Pingbacks are On
Refbacks are On

Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Hotuba Mbadala TAMISEMI: Slaa ataka Balali ajiuzulu; ambana Lowassa kuhusu Richmond John Mnyika Jukwaa la Siasa 13 16th December 2008 03:21 PM
Bajeti Mbadala 2007/08 John Mnyika Jukwaa la Siasa 30 21st June 2007 10:08 PM
Maendeleo hayawezi kuletwa na ahadi tamu Kitila Mkumbo CLOSED TOPICS 0 17th December 2006 10:35 PM
Neno Maendeleo shy Jukwaa la Siasa 0 15th October 2006 01:55 PM


All times are GMT +3. The time now is 10:05 PM.



Copyright JamiiForums.com