Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ewura yafafanua bei ya mafuta

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Ewura yafafanua bei ya mafuta

      Ewura yafafanua bei ya mafuta Monday, 27 December 2010 19:57

      Hidaya Omary
      MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya elekezi ya mafuta inayoonyesha kuwa imepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na bei elekezi ya toleo lililopita.

      Taarifa iliyotolewa jana na mamlaka hiyo imeeleza kuwa kushuka kwa bei ya mafuta, kumetokana na kushuka kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia na kupanda kidogo kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

      "Bei za aina zote tatu za mafuta za jumla na rejareja hapa nchini zimeshuka ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 8 mwaka 2010," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

      Taarifa ilieleza "Katika toleo hili bei za rejareja zimeshuka kama ifuatavyo: petroli 0.56%, dizeli (5000 ppm) 2.44%, dizeli (500 ppm) 2.21% na mafuta ya taa 3.19%."

      "Mabadiliko haya ya bei za mafuta hapa nchini yametokana na kushuka kwa bei katika soko la dunia na kupanda kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani, (sarafu ambayo hutumika katika manunuzi ya bidhaa za mafuta kwenye soko la dunia)," imesema taarifa hiyo.

      Taarifa ilifafanua "Bei za jumla kulinganisha matoleo haya mawili zimepanda kama ifuatavyo: Petroli 0.58%, dizeli (5000ppm) 2.53%, dizeli (500 ppm) 2.29% na mafuta ya Taa 3.36%.

      Hata hivyo taarifa hiyo ilisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ili mradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo ambayo ni asilimia asilimia 7.5 ya bei elekezi.


      Katika hatua nyingine adhabu zinazotolewa na Ewura kwa wafanyabiashara wanaozidisha bei ya mafuta, zimefanya wengi kuuza mafuta hayo kwa bei elekezi.

      MKuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Ewura Titus Kaguo, alisema jana kuwa bei halali ya petroli jijini Dar es Salaam Sh 1,666 na kikomo ni 1,791 na bei ya Disel yenye kiwango kikubwa cha salfa ni 1,647 na kikomo ni 1,770 huku bei kikomo kwa diesel yenye salfa chache ni 1,686 na kikomo ni 1813.

      “Pale awali wafanyabiashara walikuwa wakikiuka masharti, lakini baada ya kuona adhabu ni kali kwani wengine waliishia kulipa hadi Sh milioni 80 wameacha kabisa na hakuna kitu kinachoitwa kuongeza bei zaidi ya maelekezo ya mamlaka,” alisema Kaguo.

      Pia alisema pamoja na kuonekana bei zinapanda, kuwepo kwa Ewura kunampa faida mtumiaji kwa asilimia 30 chini zaidi ikilinganishwa kama Ewura isingekuwepo bei zingekuwa za juu zaidi.

      Akizungumzia kupanda kwa bei, alisema hali hiyo inatokana na mabadiliko katika soko la dunia kama itatokea siku bei zikashuka basi, Ewura nayo itashusha kama ilivyofanya mwaka 2009, iliposhusha kutoka 1800 kwa Dar es Salaam hadi 1,100 kwa lita ya mafuta ya petroli na kutengeneza historia ya kushuka kwa bei kwa bei za hapa nchini kwani bidhaa ikipanda haijawahi kushuka,
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ewura yafafanua bei ya mafuta


      MKuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Ewura Titus Kaguo, alisema jana kuwa bei halali ya petroli jijini Dar es Salaam Sh 1,666 na kikomo ni 1,791 na bei ya Disel yenye kiwango kikubwa cha salfa ni 1,647 na kikomo ni 1,770 huku bei kikomo kwa diesel yenye salfa chache ni 1,686 na kikomo ni 1813.
      Hizi bei badi ni juu sana na kamwe nchi hii haitaweza kusonga mbele na mzigo huu wa gharama ya nishati hii..something must give in...................kwa hiyo EWURA waache kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa......................waa ngalie Kenya mbona bei kule zimeshuka maradufu?

      Tofauti iko wapi?
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    4. Miaka 50

    Similar Topics

    1. Wauza mafuta waigomea EWURA
      By nngu007 in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 8
      Last Post: 30th August 2011, 13:32
    2. Ewura yashusha tena bei ya mafuta
      By nngu007 in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 18
      Last Post: 29th August 2011, 18:37
    3. EWURA wametangaza bei mpya za mafuta...
      By only83 in forum Business & Economic Forum
      Replies: 0
      Last Post: 28th August 2011, 22:00
    4. EWURA: Wakagua vituo vya mafuta
      By Hofstede in forum Business & Economic Forum
      Replies: 0
      Last Post: 14th January 2009, 21:26
    5. Ewura mmeshindwa kupunguza bei ya mafuta!!!
      By Pdidy in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 1st November 2008, 07:18

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...