Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

    Report Post
    Page 15 of 27 FirstFirst ... 5131415161725 ... LastLast
    Results 281 to 300 of 521
    1. #1
      Guantanamo Bay's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th February 2009
      Posts : 29
      Rep Power : 529
      Likes Received
      6
      Likes Given
      1

      Default Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Jamani naomba niulize kwa wana JF ambao ni wataalamu wa ujenzi.

      Naomba wanipatie bajeti ya kujenga nyumba ya kawaida yenye vyumba 5, sebule, kitchen, dinning na sitting room ina cost kwa makisio shilingi ngapi?

      Naomba nielimishwe,

      Asanteni.

    2. FemaTV & Radio

    3. #281
      Laigwanan76's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st November 2010
      Posts : 503
      Rep Power : 531
      Likes Received
      98
      Likes Given
      61

      Default Re: Gharama za Kujenga Nyumba Tanzania

      Quote By Gama
      Hii estimate ni sahihi??!. Stucture yangu ni 10x11=110sqm. X500,000=55000000. This isn't realistick in a tz context. Mimi nimejenga kwa 15mil tu. Kama hizo ndo estimate mnazofanya kwenye miradi ya serikali ndo maana hatuendelei.
      Mmh milion15 tu......labda banda la kuku

    4. #282
      Shark's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 25th January 2010
      Posts : 4,573
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1305
      Likes Given
      245

      Default

      Quote By rmashauri
      Mkuu kama sikosei Kibada imepimwa, kwahiyo inabidi upate kibali cha kujenga toka manispaa ya Temeke. Mojawapo ya vitu vinavyohitajika huko ni michoro ya nyumba yako (both Architectural and structural drawings). Sasa katika michoro hiyo maswali yako kuhusu nguzo zikaeje yatakuwa yamejibiwa. Matofali unaweza kulaza ground floor na first floor ukasimamisha. Tofali inabidi ununue zile za kutengenezwa na mashine (vibrated) ni imara zaidi kuliko za kufyatua wewe mwenyewe. Kuhusu kokoto tembelea maduka ya vifaa vya ujenzi huko Kibada baadhi yao wanafanya hiyo biashara. Kama mfuko wako umekaa vizuri tumia kokoto nyeusi ambazo zitakufanya uwe na nyumba imara zaidi (Ukizitaka ni PM nitakupa namba ya jamaa aliyetuuzia kwa bei nzuri kuliko sehemu zingine, Tani 18 @Tshs. 680,000 sometimes chini ya hapo kutegemea bei ya dizeli).
      Ahsante sana kaka,
      Kibada imepimwa mkuu,
      Na hizo zote Architectural and structural drawings ninazo, may be sijazipitia kwa undani kuona kama zime-specify kulaza au kusimamisha tofali.
      Nitakucheki basi about kokoto,
      Then nitaku-PM for more clarification na msaada zaido

    5. #283
      MGAWARIZIKI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th December 2010
      Posts : 306
      Rep Power : 488
      Likes Received
      45
      Likes Given
      12

      Default Re: Gharama za Kujenga Nyumba.

      Nakushauri jenga nyumba yenye vyumba 3 vya kulala, sebule, jiko inatosha sana ukipata mgeni mwenye jinsia ya kike atalala na watoto wa kike na mwenye jinsia ya kiume atalala na watoto wa kiume huna haja ya kujenga vyumba vingi gharama itakuwa kubwa

    6. #284
      rmashauri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Location : Ng'wanza Sukuma
      Posts : 2,860
      Rep Power : 1200
      Likes Received
      350
      Likes Given
      681

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By Shark
      Ahsante sana kaka,
      Kibada imepimwa mkuu,
      Na hizo zote Architectural and structural drawings ninazo, may be sijazipitia kwa undani kuona kama zime-specify kulaza au kusimamisha tofali.
      Nitakucheki basi about kokoto,
      Then nitaku-PM for more clarification na msaada zaido
      Mara zote kuwa intouch na mhandisi aliyekutengenezea hizo structural drawings maana ndo zinaonyesha jengo linatakiwa liweje.
      karibu sana mkuu.
      Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote (Mithali 14:34)

    7. #285
      Mtanganyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2007
      Location : US
      Posts : 1,357
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      106
      Likes Given
      20

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Wakubwa, nimekuwa nikifuatilia swala zima la unjenzi humu, na sasa umefika muda wangu wa kujenga kasehemu ka kulala. Pesa zangu ni za kudundurisa hivyo najenga kwa speed ya kinyonga, tunapiga zege tunapumzika, tunasimamisha tofali mpaka dirishani tunapumzika... slow motion... Hivyo nina maswali yangu kadhaa.

      Nina kiwanja Tegeta Mivumoni, Kimepimwa, Ukubwa wa kiwanja ni sqrm 600, ukubwa wa nyumba ni sqrm 450 (225 ground flow, 225 top flow) ina four bedrooms, mbili ziko up stairs mbili zipo down stairs, ina two living rooms, dining room, kitchen, pray room and four and half bathrooms. Plan yangu kuijenga ni 24 month project. Kwa sasa nina focus kwenye msingi, hivyo nataka kujua jee gharama zangu za msingi zitakuwaje?

      Maana Kokoto niandae tani ngapi? Mchanga Tani Ngapi? Nondo Tani Ngapi? Cement Tani Ngapi? Mbao za zege kiasi gani? water Membrane Sheet Ngapi? Tofali za aina gani na ngapi? Kisha ufundi shillingi ngapi?

      Nakubaliana na hesabu za Lakini tano kwa sqrm, lakini nadhani analysis yake hainipi full picture. So, nimeamua kuhire contractor lakini nitamlipa kwenye labor hour and I will control material. and if necessary I will hire consultant every now then. Lakini kwa sasa nataka kujua gharama hizo hapo juu.
      If a free society cannot help the many who are poor, it cannot save the few who are rich.

    8. Miaka 50

    9. #286
      Horseshoe Arch's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2009
      Location : Block A
      Posts : 1,285
      Rep Power : 760
      Likes Received
      161
      Likes Given
      39

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Mtanganyika km una mchoro sioni sababu ya kutomshirikisha mkadiriaji...maswali yako hapa yatajibiwa kwa mazoea tu...kwa mfano depth ya foundation yako haiko wazi,aina ya foundation kwa maana ya strip,pad,raft au pile & beam,...uzito utakatarajiwa kukaa juu ya msingi huo n.k...kwanini usichukue hatua kumwona mshauri badala ya kufanya kazi kwa mazoea? Maana mwishowe hutakua umesave sana sana utaingia gharama zinazoweza kuepukika!
      We are what we think. With our thoughts we make the world.

    10. #287
      Mtanganyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2007
      Location : US
      Posts : 1,357
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      106
      Likes Given
      20

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By Horseshoe Arch
      Mtanganyika km una mchoro sioni sababu ya kutomshirikisha mkadiriaji...maswali yako hapa yatajibiwa kwa mazoea tu...kwa mfano depth ya foundation yako haiko wazi,aina ya foundation kwa maana ya strip,pad,raft au pile & beam,...uzito utakatarajiwa kukaa juu ya msingi huo n.k...kwanini usichukue hatua kumwona mshauri badala ya kufanya kazi kwa mazoea? Maana mwishowe hutakua umesave sana sana utaingia gharama zinazoweza kuepukika!
      Horseshoe, nataka kwanza kupata estimate kutoka kwa watu kabla sijamuona mkandarasi. Concrete Slab ni kama ifuatavyo, Pile and Beam is my plan kwa sasa, urefu wa nguzo kwenda chini ni one meter, nina nguzo 23 zote zinabidi ziungwe na nondo across then zege limwagwe. I just need rough number kisha nikae chini nifanye my own analysis kabla sijaenda kukaa na building economist
      If a free society cannot help the many who are poor, it cannot save the few who are rich.

    11. #288
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,606
      Rep Power : 15261
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2866

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By Mtanganyika
      Wakubwa, nimekuwa nikifuatilia swala zima la unjenzi humu, na sasa umefika muda wangu wa kujenga kasehemu ka kulala. Pesa zangu ni za kudundurisa hivyo najenga kwa speed ya kinyonga, tunapiga zege tunapumzika, tunasimamisha tofali mpaka dirishani tunapumzika... slow motion... Hivyo nina maswali yangu kadhaa.

      Nina kiwanja Tegeta Mivumoni, Kimepimwa, Ukubwa wa kiwanja ni sqrm 600, ukubwa wa nyumba ni sqrm 450 (225 ground flow, 225 top flow) ina four bedrooms, mbili ziko up stairs mbili zipo down stairs, ina two living rooms, dining room, kitchen, pray room and four and half bathrooms. Plan yangu kuijenga ni 24 month project. Kwa sasa nina focus kwenye msingi, hivyo nataka kujua jee gharama zangu za msingi zitakuwaje?

      Maana Kokoto niandae tani ngapi? Mchanga Tani Ngapi? Nondo Tani Ngapi? Cement Tani Ngapi? Mbao za zege kiasi gani? water Membrane Sheet Ngapi? Tofali za aina gani na ngapi? Kisha ufundi shillingi ngapi?

      Nakubaliana na hesabu za Lakini tano kwa sqrm, lakini nadhani analysis yake hainipi full picture. So, nimeamua kuhire contractor lakini nitamlipa kwenye labor hour and I will control material. and if necessary I will hire consultant every now then. Lakini kwa sasa nataka kujua gharama hizo hapo juu.
      Mimi naweza kukujibu kama ifuatavyo:
      Ujenzi wa nyumba yako umekuwa si wa kama sisi waswahili bali wa kitaalamu. Kwa kuwa nyumba yako ni two floors na ina ramani tayari, kwa kawaida wachoraji wazuri wa ramani hufanya makadirio ya ujenzi, ingawa gharama hupanda kila wakati, hata hivyo katika makadirio ya mchoro huo wamekuorodheshea idadi ya vifaa vitakavyotumika kwa kila stage kuanzia msingi hadi kufikia second floor. Kujua bei yake nenda kenye maduka ya vifaa vya ujenzi kujua bei ya kila kifaa zidisha kwa idadi inayotakiwa utajua bei yake.

      Kwa mfumo wa nyumba yako unatakiwa kufuata makadirio ya ramani ya mchoraji, pia ujue kwa kuwa inabeba uzito mkubwa kutokana na kuwa na second floor unatakiwa kuwa makini sana katika kufuata ushauri wa wataalamu wa fani hiyo, vinginevyo ukifanya njia ya mkato majuto ni mjukuu.

      Njia nyepesi tunazoshauri mara nyingi hapa ni kwa ajili ya nyumba za kawaida ambazo ni single floor ambazo hazibebi uzito wa pekee isipokuwa paa na ceiling board. Kama ingekuwa nyumba ya aina hiyo tungekusaidia lakini kwa hiyo ushauri wangu tumia tu makadirio ya mchora ramani ndio msingi mzuri wa kujua gharama yake. Kumbuka utahitaji mbao nyingi pamoja na magome mengi kutokana na complications nyingi za ujenzi wa ghorofa pamoja na mbao kadhaa za uandaaji wa mtembele wa wabeba nzege kwa ajili ya second floor. Hayo tu nakushauri. Thanks.

    12. #289
      Ellie's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd September 2011
      Posts : 122
      Rep Power : 414
      Likes Received
      14
      Likes Given
      55

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Mkuu nitafite am a quantity surveyor, I can work that out, nipate mchoro Nita quantify, +255712833135

    13. #290
      Mtanganyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2007
      Location : US
      Posts : 1,357
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      106
      Likes Given
      20

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By Candid Scope
      Mimi naweza kukujibu kama ifuatavyo:
      Ujenzi wa nyumba yako umekuwa si wa kama sisi waswahili bali wa kitaalamu. Kwa kuwa nyumba yako ni two floors na ina ramani tayari, kwa kawaida wachoraji wazuri wa ramani hufanya makadirio ya ujenzi, ingawa gharama hupanda kila wakati, hata hivyo katika makadirio ya mchoro huo wamekuorodheshea idadi ya vifaa vitakavyotumika kwa kila stage kuanzia msingi hadi kufikia second floor. Kujua bei yake nenda kenye maduka ya vifaa vya ujenzi kujua bei ya kila kifaa zidisha kwa idadi inayotakiwa utajua bei yake.

      Kwa mfumo wa nyumba yako unatakiwa kufuata makadirio ya ramani ya mchoraji, pia ujue kwa kuwa inabeba uzito mkubwa kutokana na kuwa na second floor unatakiwa kuwa makini sana katika kufuata ushauri wa wataalamu wa fani hiyo, vinginevyo ukifanya njia ya mkato majuto ni mjukuu.

      Njia nyepesi tunazoshauri mara nyingi hapa ni kwa ajili ya nyumba za kawaida ambazo ni single floor ambazo hazibebi uzito wa pekee isipokuwa paa na ceiling board. Kama ingekuwa nyumba ya aina hiyo tungekusaidia lakini kwa hiyo ushauri wangu tumia tu makadirio ya mchora ramani ndio msingi mzuri wa kujua gharama yake. Kumbuka utahitaji mbao nyingi pamoja na magome mengi kutokana na complications nyingi za ujenzi wa ghorofa pamoja na mbao kadhaa za uandaaji wa mtembele wa wabeba nzege kwa ajili ya second floor. Hayo tu nakushauri. Thanks.

      Asante sana mkuu, nitajitahidi... sema mchoraji ni friend wangu tangu pale Azania na alishakimbilia ughaibuni hivyo ameniorodheshea vitu lakini bei zetu za madafu hazijui.
      If a free society cannot help the many who are poor, it cannot save the few who are rich.

    14. #291
      CAMARADERIE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2011
      Location : 1 Luthuli Street
      Posts : 4,163
      Rep Power : 2719
      Likes Received
      1587
      Likes Given
      1145

      Default Re: Gharama za Kujenga Nyumba.

      Quote By MGAWARIZIKI
      Nakushauri jenga nyumba yenye vyumba 3 vya kulala, sebule, jiko inatosha sana ukipata mgeni mwenye jinsia ya kike atalala na watoto wa kike na mwenye jinsia ya kiume atalala na watoto wa kiume huna haja ya kujenga vyumba vingi gharama itakuwa kubwa
      Hapo pekundu A VERY BIG NO...........
      A compliment is something like a kiss through a veil

    15. #292
      rmashauri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Location : Ng'wanza Sukuma
      Posts : 2,860
      Rep Power : 1200
      Likes Received
      350
      Likes Given
      681

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By Mtanganyika
      Wakubwa, nimekuwa nikifuatilia swala zima la unjenzi humu, na sasa umefika muda wangu wa kujenga kasehemu ka kulala. Pesa zangu ni za kudundurisa hivyo najenga kwa speed ya kinyonga, tunapiga zege tunapumzika, tunasimamisha tofali mpaka dirishani tunapumzika... slow motion... Hivyo nina maswali yangu kadhaa.

      Nina kiwanja Tegeta Mivumoni, Kimepimwa, Ukubwa wa kiwanja ni sqrm 600, ukubwa wa nyumba ni sqrm 450 (225 ground flow, 225 top flow) ina four bedrooms, mbili ziko up stairs mbili zipo down stairs, ina two living rooms, dining room, kitchen, pray room and four and half bathrooms. Plan yangu kuijenga ni 24 month project. Kwa sasa nina focus kwenye msingi, hivyo nataka kujua jee gharama zangu za msingi zitakuwaje?

      Maana Kokoto niandae tani ngapi? Mchanga Tani Ngapi? Nondo Tani Ngapi? Cement Tani Ngapi? Mbao za zege kiasi gani? water Membrane Sheet Ngapi? Tofali za aina gani na ngapi? Kisha ufundi shillingi ngapi?

      Nakubaliana na hesabu za Lakini tano kwa sqrm, lakini nadhani analysis yake hainipi full picture. So, nimeamua kuhire contractor lakini nitamlipa kwenye labor hour and I will control material. and if necessary I will hire consultant every now then. Lakini kwa sasa nataka kujua gharama hizo hapo juu.
      Mkuu nakupa matumizi ya nyumba ambayo ground floor ina ni square meter 210. Gharama za msingi ilikuwa kama ifuatavyo:-

      1. Nondo 8 mm = 79 pcs, 12mm = 70 pcs, 16 mm = 53 pcs (tani moja).

      2. Mchanga = Lori 8 za Tani 18

      3. Kokoto = Lori 12 za Tani 18

      4. Tofali (za chipping i.e zenye kokoto ndani) = 2000

      5. Mbao za zenge (record haikuwekwa vizuri ila ziligharimu 2.2 milioni in August 2011)

      6. Damp Proof Membrane sheet 46

      7. Simenti = mifuko 347

      8. Mawe (for hard core) (ulitumika mchanga badala ya mawe, lori 25 za Tani 18).

      9. Ufundi = 6 milioni (walitumika mafundi wa mitaani).

      Pamoja na vikorombwezo vya hapa na pale around Tshs. 35.5 mil zimetumika kujenga msingi tu.

      Nakutakia kila la kheri mkuu katika project hiyo.
      Last edited by rmashauri; 18th January 2012 at 08:20. Reason: spelling
      Mazingira and Duduwasha like this.
      Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote (Mithali 14:34)

    16. #293
      Mtanganyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2007
      Location : US
      Posts : 1,357
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      106
      Likes Given
      20

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By rmashauri
      Mkuu nakupa matumizi ya nyumba ambayo ground floor ina ni square meter 210. Gharama za msingi ilikuwa kama ifuatavyo:-

      1. Nondo 8 mm = 79 pcs, 12mm = 70 pcs, 16 mm = 53 pcs (tani moja).

      2. Mchanga = Lori 8 za Tani 18

      3. Kokoto = Lori 12 za Tani 18

      4. Tofali (za chipping i.e zenye kokoto ndani) = 2000

      5. Mbao za zenge (record haikuwekwa vizuri ila ziligharimu 2.2 milioni in August 2011)

      6. Damp Proof Membrane sheet 46

      7. Simenti = mifuko 347

      8. Mawe (for hard core) (ulitumika machnga badala ya mawe, lori 25 za Tani 18.

      9. Ufundi = 6 milioni (walitumika mafundi wa mitaani).

      Pamoja na vikorombwezo vya hapa na pale around Tshs. 35.5 mil zimetumika kujenga msingi tu.

      Nakutakia kila la kheri mkuu katika project hiyo.
      Mkuu asante sana, Nashukuru hapa nina pakuanzia.....
      rmashauri likes this.
      If a free society cannot help the many who are poor, it cannot save the few who are rich.

    17. #294
      Duduwasha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 2,620
      Rep Power : 6248
      Likes Received
      523
      Likes Given
      418

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Nataka kujenga Nyumba yenye paa la Zege ili miaka ijayo niuze juu au baadae niongeze kujenga ghorofa moja tu hapo gharama zinakuwaje Wataalam

    18. #295
      rmashauri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Location : Ng'wanza Sukuma
      Posts : 2,860
      Rep Power : 1200
      Likes Received
      350
      Likes Given
      681

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By Mtanganyika
      Mkuu asante sana, Nashukuru hapa nina pakuanzia.....
      Karibu mkuu
      Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote (Mithali 14:34)

    19. #296
      bagamoyo1's Avatar
      Member Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 48
      Rep Power : 381
      Likes Received
      12
      Likes Given
      1

      Default Re: Gharama za Kujenga Nyumba.

      Quote By Bantugbro
      Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

      Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

      Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?
      alichoseam manyusi ni sawa ila ulichoandika hapa sio sio sahihi , kitaaluma huwezi kujenga vyumba vitano kwenye jengo la 50 m2 au kwa kiswahili mita 50 za mraba kama sijakosea kila kila kitu kina kiwango chake ukitaka kujenga vhumba 5 unatakiwa kuwa na jengo lisilopunua 100-120m2 kama hueliwi ni mita 10 kwa 10 , hivi sasa bongo hutaweza kujenga nyumba yenye kiwango kwa vhini ya sh 500,000 kwa m2

    20. #297
      Mtanganyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2007
      Location : US
      Posts : 1,357
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      106
      Likes Given
      20

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Wakubwa nimeongea na mmoja wa marafiki zangu, yeye ni architecture na amefanya kazi na tanroad kwa muda. Nimempeleka kwenye site na amashauri yafuatayo. Ameshauri kupiga Beam chini ambazo zitaunganisha na column, kisha tutajaza mawe mwisho tufunge mkanda.

      Nimesikia wengi hapa wanasema ni muhimu kupiga concrete slab chini. Jee lipi ni lipi?
      If a free society cannot help the many who are poor, it cannot save the few who are rich.

    21. SMU
      #298
      SMU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th February 2008
      Location : Mavurunza
      Posts : 4,531
      Rep Power : 3810
      Likes Received
      1311
      Likes Given
      1916

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By Mtanganyika
      Wakubwa nimeongea na mmoja wa marafiki zangu, yeye ni architecture na amefanya kazi na tanroad kwa muda. Nimempeleka kwenye site na amashauri yafuatayo. Ameshauri kupiga Beam chini ambazo zitaunganisha na column, kisha tutajaza mawe mwisho tufunge mkanda.

      Nimesikia wengi hapa wanasema ni muhimu kupiga concrete slab chini. Jee lipi ni lipi?
      Hapa inategemea unaposema "chini" unazungumzia kitu gani hasa (msingi au jamvi?). Kwa hiyo unaposema "kupiga Beam chini" inaweza kuwa ndio huo huo msingi ambao wengine wanaweza kuuita "slab". Au pengine kwa kusema slab walikuwa wanamaanisha 'jamvi'. Kwa hiyo ili kupata majibu mazuri pengine ungesema ni chini ipi unayoizungumzia - level ya msingi au jamvi?
      "Rather than love, than money, than fame, give me truth" ----Thoreau

    22. #299
      Mtanganyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2007
      Location : US
      Posts : 1,357
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      106
      Likes Given
      20

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Quote By SMU
      Hapa inategemea unaposema "chini" unazungumzia kitu gani hasa (msingi au jamvi?). Kwa hiyo unaposema "kupiga Beam chini" inaweza kuwa ndio huo huo msingi ambao wengine wanaweza kuuita "slab". Au pengine kwa kusema slab walikuwa wanamaanisha 'jamvi'. Kwa hiyo ili kupata majibu mazuri pengine ungesema ni chini ipi unayoizungumzia - level ya msingi au jamvi?

      SMU asante sana kwa response mkuu. Ninapozungumzia level ya msingi. Engineer wangu amesema kwamba kwa nyumba ya ghorofa moja kinacho itajika kwa msingi ni kuweka nguzo, nyumba ina nguzo 23, kuziunga nguzo kwa nguzo na Concrete Beam. Kisha kupandisha tofali la msingi. Then kujaza mawe na kuweka kifusi. then tunapiga jamvi la 3 inch. Amesema Nondo tani mbili za Mil 12 zinatosha au tani moja na nusu za Mil 16. Kama zikitumia Mil 12 then zinafungwa sita kwenye beam na column kama ni 16 zinafungwa 4.

      Swali langu jee huu mkeka wa chini hauitaji kulaza nondo kama ule wa juu? Kutoka na ujuzi wangu mdogo wa engineer, kama akifanya kama nilivyozungumzia hapo juu. Kisha tukalaza tofali na sababu nina nguzo nyingi jee hii haitotosha kusupport slab ya juu? Sababu nimesoma watu wanaeleza nondo tani tatu au zaidi kwenye msingi? Jee hizi zote zilitumika katika nyanja gani?

      Ujenzi sio mchezo nimekubali.
      If a free society cannot help the many who are poor, it cannot save the few who are rich.

    23. #300
      majuto's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th December 2009
      Posts : 15
      Rep Power : 481
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Gharama za kujenga nyumba Tanzania

      Garama ya Milioni 500, tuangalie living standard ya mtanzania, income then mention hiyo bei; Watanzania Wezi kabisa, Nenda Nairobi angalia majumba yaliyojengwa, then waulize construction cost, almost 1/4 ya bei ya Tanzania; Pili Nyumba ya milioni 500 ni approx.= $340,000.00 Ingia kwenye Internet tafuta hiyo nyumba kwa nchi yoyote duniani, amabo vipato vyao still ni kubwa kuliko Tanzania, angalia structure utakayo ona, ni gorofa nzuri tena inayo basement, garage lenye automatic door, hao watu waambie wakujengee kama hiyo na bei ipungue. Tusidanganyane, garama za nyumba inakadiriwa kulingana na pale unapo jenga, ata ukitaka kuuza nyumba ya vyumba vitatu manzese the same nyumba Osterbay cost more. Mambo kama haya ndo maana tuko nyuma east Africa and we can not compete. ujenzi wa nyumba ya kawaida iwe $330000, hiyo nyumba ya $33000 hata in west only few people can afford it. Ukienda Texas hiyo nyumba ni $150,000 tu - Je tutafika???

    Page 15 of 27 FirstFirst ... 5131415161725 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Usiogope kujenga nyumba Tanzania kwa kuogopa gharama
      By janejean in forum Matangazo madogo
      Replies: 84
      Last Post: 7th November 2012, 16:37
    2. Naweza kujenga nyumba kwa TZS Milioni 20...?
      By Jestina in forum Business & Economic Forum
      Replies: 156
      Last Post: 2nd November 2012, 13:28
    3. Kwanini Wakerewe wengi hawapendi kujenga nyumba Ukerewe?
      By patience96 in forum JF Chit-Chat
      Replies: 43
      Last Post: 26th October 2012, 19:06
    4. Kwa Wanaume tu: Tunapoamua Kujenga Nyumba Ndogo
      By Kaizer in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 327
      Last Post: 2nd September 2012, 14:47
    5. Replies: 23
      Last Post: 28th July 2009, 16:55

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...