| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
#11
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Dhana kuu ya fikra zangu, iko katika namna tunavyoweza kutumia rasilimali yetu ya uwanja mpya wa michezo uliopo jijini Dar es Salaam kwa manufaa ya kuendeleza utalii nchini.
Hapana shaka katika ukanda huu waAfrika Mashariki, uwanja huu ni mkubwa na unastahili kutumika kwa hadhi inayostahili kuvuta utalii. Kwa maana hiyo tulicho nacho ni mali. Naamini tukioanisha suala la michuano ya kombe la dunia kufanyika nchini Afrika Kusini, zipo timu za soka zitakazofika nchini kufanya mazoezi na watakapokuwa humu watabaini vivutio vilivyopo. Cha muhimu kwa wadau wa michezo wa kigeni watakapofika nchini kufanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya kombe la dunia ambayo iko usoni, tunahitaji kuwekeza mikakati yetu humo humo nasi tufaidike. Kama ilivyokuwa katika mkutano wa Sullivan uliofanyika mjini Arusha mwaka huu, nasi tulitakiwa kuelekeza mikakati kwa wageni hawa wanaofika kufanya mazoezi nchini, kuhakikisha tunapata faida ya kujitangaza katika utalii. Sasa hivi si haba. Nilifurahi nilipomsikia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipotamka Bungeni kwamba juhudi za kujitangaza zimechukua sura ya mafanikio. Mfano mojawapo aliyoutoa ni kwamba, nchini Marekani vivutio vya kitalii vimetangazwa katika televisheni maarufu ya CNN na matokeo yake yanaonekana, kwamba kuna watalii wengi wanaomiminika kutoka huko. Nionavyo, hiyo ndio namna hata kwa wageni watakaofika kufanya mazoezi katika viwanja vyetu kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia, mambo ya namna hiyo tutayashuhudia na utalii wetu ukawa na manufaa kwetu sote. Inastahili sasa hivi wadau wakakuna ubongo juu ya aina gani mikakati wanayopaswa kuweka na aina yote ya fursa zilizoko kutumika na hatimaye hatua iliyopigwa ionekane. Hebu tuthubutu ili tuweze.
__________________
Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki,na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 02:57 PM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||