TMF|JamiiForums Blog
  • Member Login:
http://www.jamiiforums.com/zain.jpg

+ Reply to Topic
Results 1 to 5 of 5
  1. #1
    JF Premium Member Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri is a jewel in the rough Mshiiri's Avatar
    Join Date
    Mon Jun 2008
    Location
    Sillicon Valley - USA
    Posts
    824
    Thanks : 12
    Thanked 33 Times in 17 Posts
    Rep Power
    64

    Default Insurance covers, scam or deal?

    Nimejaribu kutafuta sana maana nzima ya insurance na siipati kabisa. Sijawahi ona au kusikia jamii fulani hapa Tanzania au mtu fulani kapata kanufaika na bima hizi za mali. Labda tuwaulize ndugu zetu wanaounguliwa na ma-godown pengine wanajua means! Au pengine ni mimi sina elimu ya kutosha ya bima za mali na vyombo kama magari. Bima za afya na mifuko ya jamii kama NSSF ana PPF wao wako clear sana na utendaji wao na hii nawapa pongezi katika kukwamua Tanzania na lindi la umaskini. Kwa mdau anayejua kuhusu hizi insuarence za magari na mali anifahamishe au anijuze tafadhali. Kwa sababu mimi sioni why pay for insurance ambayo kulipana mpaka upigwe danadana na uishie kukata tamaa wakati polisi wanakubonyeza ulipe na kama umelipa katika ajali hawafanyi lolote na kama hujalipa moto utauona. Huu si wizi kweli? Watu wanapata ajali katika basi lakini huishia kusikojulikana wala hawa mabwana bima hawaonekani hata wakisema katika eneo la tukio. Hivi si wizi huu kweli?
    "Absence of evidence is not evidence of absence" - No win-win situation:D

  2. #2
    Senior Member REOLASTON will become famous soon enough REOLASTON will become famous soon enough REOLASTON will become famous soon enough REOLASTON will become famous soon enough REOLASTON will become famous soon enough REOLASTON will become famous soon enough REOLASTON will become famous soon enough REOLASTON will become famous soon enough
    Join Date
    Tue Feb 2009
    Posts
    71
    Thanks : 0
    Thanked 1 Time in 1 Post
    Rep Power
    22

    Default Re: Insurance covers, scam or deal?

    Tatizo ni kwamba watanzania walio wengi hatujui maana ya bima na ndio maana makampuni ya bima hapa nchini yanafaidika sana kwa hilo.

  3. #3
    JF Premium Member Power to the People will become famous soon enough Power to the People will become famous soon enough Power to the People will become famous soon enough Power to the People will become famous soon enough Power to the People will become famous soon enough Power to the People will become famous soon enough Power to the People will become famous soon enough Power to the People will become famous soon enough
    Join Date
    Wed Jul 2007
    Posts
    258
    Thanks : 13
    Thanked 13 Times in 6 Posts
    Rep Power
    24

    Default Re: Insurance covers, scam or deal?

    Insuarance companies za huku kwetu are here to rip us off. hata ukiwa una genuine claim mpaka uipata ni mbinde kwa kweli. Mi nimeshuhudia kijana mmoja aliyepata ajali akiwa kazini kwa bahati nzuri kampuni alikokuwa anafanya kazi had insured its employees. sasa claim ikapelekwa kijana na maumivu yake it took him 8 months kama sio zaidi ndio akapewa hiyo compansation. sasa you wonder kwa nini nikate bima ya kitu chochote kama usumbufu ni wa aina hii. na huu ni mfano mmoja ambao nimeushuhudia bado kuna ile unasikia huku na kule watu wakilalamika.

  4. #4
    JF Senior Expert Member Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali will become famous soon enough Ngambo Ngali's Avatar
    Join Date
    Fri Apr 2009
    Posts
    1,127
    Thanks : 396
    Thanked 584 Times in 341 Posts
    Rep Power
    24

    Default Re: Insurance covers, scam or deal?

    Unaweza kuigawa kwa sehemu mbili anayekata bima na mhanga. Mara nyingi watu waliokata bima wakienda kudai ni kasheshe letehiki kile etc ukishtuka miaka mitatu nxt barua inakuja we cant consider your claim sababu imepitwa na muda. Wakati mwingine unapeleka madai unaambiwa hee hukutoa taarifa ya ajali kwa kampuni ya bima katika muda unaotakiwa hivyo hustahili kulipwa. So ukipelekwa mapema unazungushwa mpaka muda wa kudai unakwisha ukichelewa ndo basi kabisa.

    Upande wa pili, waathirika ndo usiseme hawajui kama wana haki, fikiria katika daladala ni wangapi wanakuwa na tiketi valid. Wachache sana wakati huo ni ushahidi kuwa tarehe ya ajali ulikuwa kwenye basi. Watanzania wangapi wanajua kuwa wakiwa kwenye basi wanastahili kulipwa kukiwa na ajali, Wachache sana. Ikitokea ajali fomu lazima ijazwe na mwenye gari, ajali imetokea Mbeya mwenye basi yuko tanga huyu mtu anaweza kuafford kusafiri all the way kupata signature ili ipelekwe bima? Jee mwenye basi atafaidika nini endapo ataisaini ile fomu, kwani asiposaini hakuna wa kumlazimisha. Anyway factors ni nyingi unaweza andika mpaka kesho really it is a big problem for sure.

  5. #5
    Member Nameless- will become famous soon enough Nameless- will become famous soon enough Nameless- will become famous soon enough Nameless- will become famous soon enough Nameless- will become famous soon enough Nameless- will become famous soon enough Nameless- will become famous soon enough Nameless- will become famous soon enough
    Join Date
    Thu May 2009
    Posts
    34
    Thanks : 0
    Thanked 5 Times in 2 Posts
    Rep Power
    0

    Default Re: Insurance covers, scam or deal?

    Quote Originally Posted by REOLASTON View Post
    Tatizo ni kwamba watanzania walio wengi hatujui maana ya bima na ndio maana makampuni ya bima hapa nchini yanafaidika sana kwa hilo.
    Hii ni kweli. Hata kwa wachache wanaojua maana ya bima na kuzinunua, wengi wao hawajali kusoma ile mikataba. Kwa hiyo anapopata janga ndo anaanza kuhangaika, ninachojua kila janga lina sera/mkataba wake na taratibu zake za kudai bima endapo limetokea hilo janga husika.

    Kuna uzembe na kuzungushwa ktk kudai bima lakini kuchelewa kwingine ni kujaribu kujiridhisha kwamba hakuna udanganyifu, kuna mtu anakata bima kampuni tofauti na anapeleka madai kote kote, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za bima, pia kuna anayeunguliwa na gari kikweliii na yupo anayenyofoa spare kibao kisha akawasha kiberiti, bima haiwezi kulipa tu kwa vile umedai, lazima uchunguzi ufanyike.

    Wengine hawatofautishi bima na polisi, mfano unapotakiwa kupeleka taarifa za polisi, labda ajali/tukio au ukaguzi wa gari, wakati mwingine inachukua muda kuipata, hiyo nayo mtu anaona ni usumbufu wa bima, lakini siyo. Mara nyingi ukifanikiwa kupeleka nyaraka wanazozitaka, haichelewi kihivyo.

    Ushauri wangu ni kwamba tusomage sera/mkataba, na pia pale pale unaponunua bima, tupate kujua taratibu za madai.


 

Topic Information

Users Browsing this Topic

There are currently 1 users browsing this thread. (0 members and 1 guests)

     

Tags for this Topic

Bookmarks

Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts