hii ndiyo message niliyopata baada ya kuapply mkopo wa vyombo vya usafiri kwa wafanyakazi wa serikali.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
hii ndiyo message niliyopata baada ya kuapply mkopo wa vyombo vya usafiri kwa wafanyakazi wa serikali.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Unamaanisha mikopo ya magari?
Wa2 wengine wanapenda kuwalisha sumu wenzao tu, hiyo meseji uliyopata ni ni ipi?
Labda hamna sifa! au mpo kenye list, ninavyofahamu wote walioomba awamu ya kwanza walishapewa fedha na tayari watumishi wameomba kwa awamu ya pili ndo wanasubiri. Naamini waraka uliuelewa vizuri usilaumu wasiohusika. Km wewe ni mtumishi wa serikali naamini utakuwa unaelewa namna taratibu za fedha zinavyochukua muda c km taasisi za fedha zinazotoa ndani ya saa 24, kuwa na subri mkuu na fuatilia kwa wakuu wako kwa ufafanuzi zaidi.
Maneno ya mfa maji wewe una mikopo lukiki bado unataka kukopa, ndo maana huna sifa, jifanyie tathmini mkuu acha kulalamika.
Mkuu hii habari siyo kweli. Mbona mie nimepata. Ila mikopo yenyewe siyo mizuri kwani gari wanazokopesha ni mpya tu hivyo makato yake wengi hawawezi kulipa. Wangekopesha hata magari yaliyotumika. Nadhani mkuu kipato chako inaonesha hukopesheki. Kwani mie nimekopeshwa MITSUBISH HARD TOP 2500 CC kwa 51,705,120.00
Mafurahia watu wanaojitahidi kueleza ukweli, sa huyu jamaa keshamwaga sumu humu inywewe af ye anakaa pembeni, kumbe anajua hana vigezo, af sheriamya kununua 'used' nafkiri anajua serikali haiimind,
Mkuu Mpigauzi nimependa ulivyochangia hoja kwa umahiri mkubwa, mimi pia ni mtumishi wa serikali kipato changu hakizidi milioni moja na nusu na wala hakipungui milioni moja kwa mwezi. Naomba ni-pm jinsi ya ku-apply hiyo mikopo/hatua za kupitia.
Maana kwenye idara yetu huo waraka tunausikia tu lakini wakubwa bado wameukalia, je nianzie wapi hapa hapa ua hazina moja kwa moja?
Jingalao, wewe unafahamu kabisa unadaiwa NMB, SACCOS na Bayport. Ni ngumu tu hata mtu wa kawaida kukukopesha siyo tu kutokukopesheka bali haukatiki!
Kwanza mikopo hii inatolewa kwa wafanya kazi wa serikali tu, wizara na idara za serikali na siyo Halmashauri.
Kila idara/kitengo kinakuwa kinapata mgao kulingana na bajeti iliyotolewa kwa mwezi husika, mkuu wa kitengo atatoa taarifa kwa watumishi ili wajaze fomu za maombi kwa kulingana na mgao, mikopo hiyo inatolewa kwa makundi kadhaa mf. mkopo wa samani, matengenezo ya gari/pikipiki, kununua gari lililotumika au gari jipya n.k
Sifa ya mwombaji ni lazima asiwe na mkopo unaoendelea au km upo akiomba kukopeshwa salio la mshahara(basic salary/take home balance) isiwe chini ya 1/3 ya mshahara wako basic.
Ahsante kwa ufafanuzi kamanda nimekupata.Je kuna wakati maombi yanakua pending kwa muda mrefu sana.au tunapigwa juu kwa juu na wakubwa.zetu.maana ukiwa mikoani hata kuambiwa zipo hawsemi
Follow Us Here