Utapeli tigopesa sasa unatisha!
Jamani nina ndg yangu amelizwa laki sita asubuhi ya leo. Mteja kaja na pesa cash awekewe ktk akaunti yake. Akamkabidhi wakala na wakala naye akamrushia electronic money. Alipotaka kufanya transaction ya mteja mwingine (baada ya yule kuondoka) ndipo akagundua zile laki sita alizopewa hazimo ndani ya pochi yake. Kwenda tigo, jamaa alishachukua zile alizoingiziwa kwenye akaunti yake!
Eti imekaaje hii jamani mbona inatisha? mnaofanya biashara hii vipi experience zetu jamani? watu wa tigopesa mnalionaje hili?
Last edited by mito; 9th July 2012 at 16:53.
Haki ya mtu haipotei, inacheleweshwa tu!
Follow Us Here