Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mawazo yenu pls

    Report Post
    Results 1 to 9 of 9
    1. #1
      Chinga boy's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 190
      Rep Power : 398
      Likes Received
      33
      Likes Given
      0

      Default Mawazo yenu pls

      Heshima kwenu wanajamvi,nipo ktk harakati za kujiari na kuachana na ajira na lengo langu ni kununua coaster kwa ajili ya daladala na kwa kuwa sina capital ya kutosha lengo langu niombe mkopo benk kutumia nyumba yangu.so wadau mnanishauri vipi kwa hili.natangulisha shukrani zangu

    2. Miaka 50

    3. #2
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,659
      Rep Power : 717
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: Mawazo yenu pls

      Nakushauri fanya utafiti wa kutosha kuhusu hio biashara ya Daladala kabla hujapoteza nyumba,
      Baba Mtu likes this.

    4. #3
      Don David's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th January 2012
      Location : Arusha
      Posts : 173
      Rep Power : 406
      Likes Received
      25
      Likes Given
      80

      Default Re: Mawazo yenu pls

      Aisee kama utaiendesha na kuitunza we mwenyewe chukua lakini kama utanunua ya kumpa dereva acha kabisa utapoteza nyumba yako bro..

    5. #4
      Mudamali's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 51
      Rep Power : 360
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Hongera ndugu kwa kuwa na mtaji wa kutosha.
      Ni hivi; Jaribu kuwekeza kwenye vitu visivyohamishika (Immobile properties)

      Kawaida ukitaka kununua gari, kama una mtaji wa magar mawili unashauriwa kununua gari 1; ukiwa na wa magar manne unatakiwa kununua magari mawili n.k. kwani hii ni biashara isiyo nauhakika muda wote, ko inahtaji mtaji mkubwa.
      Fikiria umenunua gari baada ya wik 1 likapata ajal na likaharibika itakuwaje?
      kwa kuanzia biashara ya magari sio nzuri jaribu bussiness nyingine.

    6. UKI
      #5
      UKI's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Location : Mali
      Posts : 682
      Rep Power : 486
      Likes Received
      149
      Likes Given
      176

      Default Re: Mawazo yenu pls

      Kwanza nakupa hongera kwa kuamua kujiajiri mwenyewe mkuu please nakuomba hilo la kuomba mkopo uliangalie kwa jicho lako mara mbili maana najua mkopo una manufaa zaidi na ni njia mojawapo ya kumsaidia mfanyabiashara kwa kumuongezea mtaji kabla hujafanya maamuzi yako ya kuitoa nyumba yako kwa kupata mkopo ingatia haya.

      1. umeamua kuomba mkopo ka ajili ya kununua coaster je unakipato kingine cha kuendesha familia kuhusu matumizi madogo madogo ya kila siku hapo nyumbani?

      Hili kosa hufanyika na watu wengi sana maana ukiamua kuomba mkopo wa hela jaribu kuitumia kwa makusudio ya huo mkopo maana vijana wengi huwa wakiomba mkopo mara utasikia katoa hela kidogo hapo kalipia sijui ada, kanunua mchele, na vitu vidogo vidogo asikuambie mtu ukitumia hata sh 2000 hapo umepunguza makusudio ya mkopo huo so ni vizuri ujitathimini kwanza uhakikishe kuhusu matumizi madogo madogo unayo angalau ya kukutosheleza ndani ya miezi nane au zaidi bila kugusa hata senti moja ya hiyo biashara yako. maana utakapoanza biashara yako ujue kuna return ambayo utakuwa unarudisha kil mwezi na inategemea utaomba kwa muda gani, hili ni muhimu sana

      2. Pili uko tayari kuwa bandigu? hili lina maana sana unaweza kufikiri nakufundisha tabia mbaya ila ukweli kabisa tupo katika jamii ya kitanzania na tumelelewa hivyo nasema hivyo kwa sababu tunapoona mtu amenunua coaster au anakitu flani cha gharama tayari masikio yetu na fikra zetu tunafikiri ameshatajirika na wala hatujuia katoa wapi hiyo hela so unachotakiwa ndugu yangu funika masikio na macho ya watu maana watu watakuja kulilia matatizo ya shida zao usifikiri watakuja kukuomba mahela mengi hapana watakuja hata sh 1000, mara 5000 mwisho michango mara jirani anaumwa sisemi usiwe eti mkimya kabisa naomba uangalie pale kwenye ulazimu tu na uwe serious maana siku ukianguka hakuna atakayekusaidia zaidi ya kukucheka wakishangilia nyumba yako inapigwa mnada.

      3. tatu je hiyo biashara ya daladala nani anakuwa dreva ni wewe au unaajiri mtu? mapendekezo nafikiri hujafikia hatua ya majukumu mengine mengi maana umesema ndio unataka kuanza hiyo biashara ninapendekeza wewe mwenye uwe driver maana wakati wa mwanzo ni muhimu sana ili kupata uzoefu angalau mwaka mzima ili ukija kumuajiri mtu hawezi kukudanganya maana utakuwa umepata uzoefu wa kutosha.

      4. mwisho kabisa je mkopo huo na hiyo biashara inalingala na kiasi ambacho utakuwa unarudisha kwa mwezi hili ni muhimu sana ili usije ukawa unapigiwa na credit officer unazikimbia simu jaribu kufanya uchunguzi wako kwanza
      nakutakia biashara njema na mafanikio katika hilo.

      Asante
      NTINGINYA likes this.

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 3,978
      Rep Power : 1218
      Likes Received
      247
      Likes Given
      41

      Default

      Kama unatamani kulala kwenye gari basi fanya unachotaka kufanya

    9. #7
      amazon's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 55
      Rep Power : 363
      Likes Received
      13
      Likes Given
      24

      Default Re: Mawazo yenu pls

      Hiyo Coaster unayotaka kununua ni mpya au used??.. Nina experience ya hiyo biashara. Nilinunua daladala used, kidogo nipate presha.. Jamani ni Biashara ngumu sana..Ilibidi niliuze baada ya miezi sita tena kwa bei ya hasara.. Ushauri wangu ni kwamba uwe makini na hiyo biashara na inahitaji supervision kubwa sana..Kila la heri.

    10. #8
      elmagnifico's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th July 2011
      Location : Brussels
      Posts : 1,933
      Rep Power : 2544
      Likes Received
      539
      Likes Given
      36

      Default Re: Mawazo yenu pls

      ndugu yangu hiyo biashara inategemea sana na upepo. Mimi ndugu yangu aliwahi poteza nyumba hivi hivi kisa alichukua mkopo akanunua gari ya abiria kwa ajili ya kufanyia biashara yaliyo mkuta hatakuja kusahau.
      Sikutishi lakini biashara ya magari inahitaji uzoefu na uangalizi wa hali ya juu yani unaweza pata hasara kwa mara moja ukapoteza kila kitu.

    11. #9
      Jestina's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Posts : 3,631
      Rep Power : 1449
      Likes Received
      845
      Likes Given
      351

      Default Re: Mawazo yenu pls

      mkuu usiache kazi yako,biashara ya daladala ni wachache sana wanaimudu,wengi ni presha tu...tusije kukupoteza bure hapa jamvini...

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...