Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

    Report Post
    Page 1 of 4 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 62
    1. #1
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default UPDATES - Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Ndugu Wana-Jamii

      Ni matumaini yangu mnaendelea vyema na shughuli za kila siku, pamoja na changamoto mbalimbali zinazotukabili. Kwa wale tunaofahamiana kwa kukutana ua namna yeyote ile; MALILA, LAT, KANYAGIO, THE FINEST, na wengine ambao nisingeweza kuwataja wote, habari za siku nyingi…..!!!; kwa muda mrefu sikupatikana sana katika jukwaa hili kama MGOMBEZI, hii ilitokana na harakati zangu za kuhamia hapa mjini Dodoma.

      Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi kila wakati ni vyema kuangalia au kutafuta jinsi ambavyo mitandao hii inaweza kutumika katika kuleta maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa jumla; kama inavyotumika JAMII FORUM. Kupitia mtandao wa FACEBOOK ambao vijana wetu wengi wamejikita huko niliamua kuanzisha kundi (Group) linaloitwa WAJASIRIAMALI KWELI, kwa lengo la kushirikishana elimu ya ujasiriamali na kupeana mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika kuanzisha shughuli za uzalishaji mali. Kwa wale wanaotembelea Facebook watakuwa wanaelewa kwamba kwenye FACEBOOK kuna option ya kuunda kundi na kujitengenezea Page. Nimeona ni vyema kuleta mawazo haya pia kwa “Great Thinkers”, ambapo naamini nitapata michango ya kutosha.

      WAJASIRIAMAILI KWELI: Log In | Facebook

      Dhana ya UJASIRIAMALI katika jamii yetu inaelekea kupoteza mwelekeo au uhalisia. Naamini utaungana nami kwamba mtazamo wa wengi juu ya MJASIRIAMALI, ni pamoja na kununua bidhaa za kichina na kupita nazo mtaani kuuza au hata kama amepanga mahali kuuza. Kwa hiyo basi dhana ya UJASIRIAMALI ni kununua na kuuza (trading), jambo ambalo ninaona kama tunapoteza mwelekeo.

      Hiki ni kikundi cha wajasiriamali wakionyesha bidhaa zao; lakini bidhaa nyingi zilizopo ni kutoka china.

      MAANA YA UJASIRIAMALI:

      Neno ujasiriamali linatokana na maneno mawili ambayo ni UJASIRI na MALI. Hivyo maana ya ujasiriamali ni kuwa na: -

      • Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
      • Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
      • Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.


      Kwa hiyo mjasiriamali:


      • ni mtu ambaye ana sifa na uwezo wa kutambua mapema fursa za kutengeneza faida na mwenye kuunganisha nguzo kuu za uzalishaji mali (nguvu kazi, mtaji na rasilimali);
      • ni mwanzilishi wa wazo na mwenye maono ya mbali ya jinsi ya kufanya biashara, uwezo wa kupanga, kuratibu na kutekeleza wazo lake na kufikia mafanikio;
      • pia ni mwenye kujiamini, kujituma kwa muda mrefu, kukubali makosa na kujisahihisha, mbunifu na mwenye kuwa tayari kutumia vizuri uwezo na maarifa ya watu wengine


      Tunaweza kusema hizi ndizo NGUZO kuu tatu (3) za MJASIRIAMALI:


      1. Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
      2. Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
      3. Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.


      Hivyo basi mtazamo wa WAJASIRIAMALI KWELI ni kujenga uwezo wa kutekeleza nguzo hizi miongoni mwetu, hasa kwa vijana ambao tunawategemea katika shughuli za uzalishaji mali; kama tusemavyo “VIJANA NDIO TAIFA LA KESHO”. Tutajengana kwa kupeana elimu ya ujasirimali na mbinu mbalimbali katika kushinda vikwazo mbalimbali.

      Msemo tunaotumia…, - “TIMIZA NDOTO ZAKO KWA KUCHANGIWA MTAJI” Je una maana gani?

      MTAJI NI NINI?

      Mtaji ni uwezo unaoweza kutumika katika kuzalisha mali au kuongeza kipato. Kuna usemi unasema “MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE”, kwamba nguzu za mtu zaweza kutumika katika uzalishaji au kuongeza kipato. Katika kuanzisha biashara uwezo huu unaweza kutokana na nguvu alizonazo mtu; kwa maana ya uwezo binafsi juu ya kile anachotaka kufanya, pamoja na rasilimali atakazohitaji.

      DHANA YA KUCHANGIWA MTAJI:

      Watu wengi wamekuwa na mawazo mazuri katika kuanzisha biashara lakini kikwazo kikubwa ni MTAJI. Katika kutekeleza nguzo namba tatu (3) ya Mjasiriamali; “Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara”. Nimeamua kutumia dhana ya kuchangiana katika kutekeleza wazo la mtu binafsi katika kuanzisha biashara.

      Jamii yetu imekuwa na utamaduni wa kuchangiana katika kutimiza lengo la mtu binafsi; hii imekuwa ikitumika katika kufanikisha sherehe mbalimbali za ndugu au jamaa au rafiki zikiwemo za kuzaliwa, ubatizo, kipaimara, maulidi, harusi n.k. Kwamba mtu anakusanya watu wachache ni kuwaeleza haja ya kufanikisha jambo lake na kuwataka ndugu au jamaa au marafiki kumchangia kwa hali na mali katika kufanikisha jambo hilo.

      Hivyo basi kutokana na utamaduni huu ambao tumekuwa tukitumia katika kufanikisha sherehe na shughuli nyingine za kijamii, tunaweza kutumia sasa utamaduni huu katika kutekeleza malengo ya mtu binafsi ambaye anataka kuanzisha shughulli za uzalisha mali au biashara kwa kumchangia mtaji.

      Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi muungano huu tunaweza kuutumia vyema katika kuangalia mahitaji ya wengine katika kutimiza ndoto zao.

      Mchango tunaoweza kumpatia mtu ni pamoja na mawazo yetu katika kuboresha wazo husika na rasilimali zinazohitajika.

      MRADI WA MAJARIBIO (PILOT PROJECT):

      Nikiwa kama mwezeshaji wa kujitegemea, nimeamua kutekeleza wazo langu kwa vitendo kwa kuliwakilisha kwenye jamii kwa lengo la kuomba michango yao, kupitia “NIWEZESHE CAMPAIGN”.

      KILIMO CHA MAPAPAI – STAN’S PAPAYA

      Kumekuwa na uhitaji mkubwa wa mapapai katika mji wa Dodoma na hata sehemu nyinginezo za nchi kutokana na utafiti mdogo niliyofanya, Bei ya papai katika maeneo mengi ya nchi inakadiriwa kuwa Tsh. 1000 – 3000, hapa Dodoma ni kati ya Tsh 2000 – 3000. Nikiwa kama mjasiriamali nimeona vyema kutumia uhitaji huu kama fursa ya biashara kwa kuanza kilimo cha mapapai ili kwa sehemu niweze kuchangia uzalishaji wa bidhaa hii, ambapo itasaidia pia kupunguza bei katika soko. Dhamira yangu ni papai kumfikia mlaji kwa bei kati ya Tsh. 500 – 1000. Vile vile nimehamasika kuanzisha kampeni ya matumizi ya mapapai, ikiwa ni pamoja kulitumia kama tunda na bidhaa nyinginezo zitokanazo na papai. Unaweza kutembelea page yangu kupitia mtandao wa FACEBOOK ambapo utapata dondoo za matumizi ya papai na mengineyo. Stan's PaPaYa | Facebook


      Ili niweze kuanzisha mradi huu nahitaji kiasi cha fedha Tsh. 5,920,000, ambapo mchango wangu binafsi zitakuwa gharama za uendeshaji zitakazo gharimu kiasi cha Tsh. 950,000/=. Hivyo basi mchango wa fedha ninao hitaji kutoka kwa jamii ni kwa ajili ya gharama za uanzishaji (start-up fund), ambazo ni Tsh. 4,970,000/=. Natafuta watu 1000 kutoka katika jamii watakaoweza kunichangia Ts.4970/= kila mmoja.

      Nawatafuta watu hawa kupitia mitandao ya kijamii (JAMII FORUM na FACEBOOK) pamoja na jamaa inayonizunguka.
      Unaweza kuwakilisha Mchango wako kupitia:

      TIGO PESA - 0714 460528 or M - PESA - 0757 941044

      (Mwisho ya kupokea michango tarehe 30/06/2012)

      Taarifa za kupokelewa kwa michango na utekelezaji wa mradi hatua kwa hatua zitawakilishwa kupitia:

      JAMII FORUM - Business & Economic Forum, Katika post hii
      FACEBOOK - Stan,s PaPaYa Stan's PaPaYa | Facebook
      WAJASIRIAMALI KWELI Log In | Facebook

      NB: Ikiwa upo ndani ya Mji wa Dodoma, unaweza kutoa order ya Mapapai na kufanya malipo ya awali. Kiwango cha chini ni mapapai kumi (10) na kila papai utalipia Tsh.500/=

      Naomba kuwasilisha..............!!!, Natanguliza Shukrani.......!!!

      MAHITAJI YA MRADI:


      A: UWEKEZAJI

      I: RASILIMALI

      MAHITAJI MAELEZO KIASI BEI JUMLA
      Ununuzi wa Shamba Heka 1 1,000,0000/= 1,000,000/=
      Ujenzi wa Nyumba ya Wafanyakazi Nyumba 1 700,000/= 700,000/=
      VIFAA VYA UMWAGILIAJI – Umwagiliaji kwa njia ya matone (Drip irrigation systems)
      Bomba – ¾ inch (pvc) Mita 1500 1000/= 1,500,000/=
      Tank la Maji 1000 Lita 1 160,000/= 160,000/=
      Pump ya kusukuma maji 1 300,000/= 300,000/=
      Bomba la kuvuta maji Mita 5 10,000/= 50,000/=
      Bomba la kupeleka kwenye Tank Mita 20 3,000/= 60,000/=
      Ujenzi wa Mnara wa Tank 1 300,000/= 300,000/=
      JUMLA 4,070,000/=

      NB: KILIMO CHA UMWAGILIAJI:
      Kilimo cha umwagiliagi kwa njia ya matone (Drip Irrigation System), ambapo mabomba (mipira) itapita kataka kila shina la mche na kudondosha matone ya maji yanapohitajika.



      II: UPANDAJI

      MAHITAJI MAELEZO KIASI BEI JUMLA
      Maandalizi ya Shamba Heka 1 100,000/= 100,000/=
      Mbole – Samadi ya Ng’ombe Tani 10 10,000/= 100,000/=
      Manunuzi ya Mbegu 1000 500/= 500,000/=
      Upandaji wa Mbegu 1000 200/= 200,000/=
      JUMLA 900,000/=

      III: UENDESHAJI

      NB: Kutokana na mbegu itakayotumika Mche wa papai utachukua Miezi sita (6) mpaka kuanza uzalishaji.

      MAHITAJI MAELEZO KIASI BEI JUMLA
      Mfanyakazi (miezi 7) Miezi 7 100,000/= 700,000/=
      Gharama Nyinginezo 250,000/= 250,000/=
      JUMLA 950,000/=

      JUMLA YA MTAJI = Tsh. 5,920,000/=

      B: JINSI YA KUPATA MTAJI:

      Mtaji nategemea kupata kwa kuchangiwa na wana-jamii kama ifuatavyo:

      MCHANGO BINAFSI – Gharama za Uendeshaji 950,000/=
      MCHANGO WA WANA-JAMII – Rasilimali + Upandaji 4,970,000/=
      JUMLA 5,920,000/=

      Hivyo Basi Wana-Jamii = 1000
      Kila mmoja anaweza kunichangia = Tsh. 4,970/=

      ****************************** *****UPDATES****************************** *****

      A: HATUA ZA UTEKELEZAJI:

      31/May/2012 - Upatikanaji wa eneo/shamba huko Michese, bado halijalipiwa.



      B: MICHANGO KUTOKA KWA JAMII:

      S/NO ID AMOUNT DATE
      1 Bakari Kawiza 5,000 29-May-12
      2 Fadhili Chitanda 5,000 29-May-12
      3 Amkawewe 5,000 4-Jun-12
      4 Kaunga 10,000 4-Jun-12
      5 Rose Lusinde 10,000 5-Jun-12
      6 Malila 10,000 7-Jun-12
      7 Miundombinu 20,000 9-Jun-12
      8 Mary Msemwa 6,000 10-Jun-12
      9 Leonard Kisenha 5,000 11-Jun-12
      10 Kibanga Ampiga Mkoloni 20,000 11-Jun-12
      11 Kitokota 10,000 13-Jun-12
      12 Asrams 5,000 17-Jun-12
      13 Jalala 10,000 20-Jun-12
      14 Muhinda 10,000 20-Jun-12
      Total contributions as today:
      131,000
      Total Amount Requested: 4,970,000
      Balance:
      -4,839,000
      Last edited by Mgombezi; 25th June 2012 at 12:09.
      Ebenezer

    2. Miaka 50

    3. #2
      Ruhazwe JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2011
      Posts : 3,172
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      776
      Likes Given
      721

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      dah!.....mkubwa!kwa sasa nikupe pongezi za kuwa na mawazo mazuri sana,ntarudi tena ila chukua saluti!
      Mgombezi likes this.

    4. #3
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Nakushukuru Mkuu, Ruhazwe Jr; nategemea mchango wako.
      Ebenezer

    5. #4
      KISWAHILI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 26th April 2012
      Posts : 83
      Rep Power : 373
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Umejipanga!!

    6. #5
      asrams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th September 2011
      Posts : 601
      Rep Power : 510
      Likes Received
      106
      Likes Given
      64

      Default

      Hongera sana kaka, inshaAllah utafanikisha lengo lako. Je kuna nafasi ya kununua hisa??


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
      Last edited by asrams; 3rd June 2012 at 22:44.

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By asrams
      Hongera sana kaka, inshaAllah utafanikisha lengo lako. Je kuna nafasi ya kununua hisa??


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
      Nashukuru kaka, wakati utakapofika basi nitaweza kutangaza kuuza hisa; kwa sasa niwezeshe.....!!!.
      Ebenezer

    9. #7
      asrams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th September 2011
      Posts : 601
      Rep Power : 510
      Likes Received
      106
      Likes Given
      64

      Default

      Quote By Mgombezi
      Nashukuru kaka, wakati utakapofika basi nitaweza kutangaza kuuza hisa; kwa sasa niwezeshe.....!!!.
      Bila shaka kaka. Nipo nje ya nchi lakini ntakuwezesha kabla ya tar.15 inshaAllah


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
      Mgombezi likes this.

    10. #8
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By asrams
      Bila shaka kaka. Nipo nje ya nchi lakini ntakuwezesha kabla ya tar.15 inshaAllah


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
      Nashukuru kaka....., karibu nyumbani...!!!
      Ebenezer

    11. #9
      Bujibuji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2009
      Location : NYUMBANI PANONO
      Posts : 13,886
      Rep Power : 11203
      Likes Received
      7055
      Likes Given
      5279

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      JF is food for thought. Nimejifunza mengi sana kwenye uzi wako, sijui nikupe zawadi gani ya kukufaa.
      Wastaafu na wale wote wanaokaribia kustaafu, pia wale wasio na ajira wewe ni mwalimu wao mzuri.
      Mgombezi likes this.
      KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J. K. NYERERE

    12. REX
      #10
      REX's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th March 2012
      Location : KCMC-MOSHI
      Posts : 182
      Rep Power : 397
      Likes Received
      24
      Likes Given
      2

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Kaka hongera sana,naamin kwa mwenye uwezo wa kuelewa amekuelewa.big up bro!
      Mgombezi likes this.

    13. #11
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Bujibuji
      JF is food for thought. Nimejifunza mengi sana kwenye uzi wako, sijui nikupe zawadi gani ya kukufaa.
      Wastaafu na wale wote wanaokaribia kustaafu, pia wale wasio na ajira wewe ni mwalimu wao mzuri.
      Mkuu Bujibuji, Nashukuru; bali mchango wako wa NIWEZESHE itakuwa zawadi kubwa na utakuwa umechengia wengi kujifunza.
      Ebenezer

    14. LAT
      #12
      LAT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Posts : 4,526
      Rep Power : 1498
      Likes Received
      1156
      Likes Given
      1659

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      dah ... very exciting project ..... think of processing pawpaw/papaya beverage (smooth juice or hard liqueur)

      utatoka mkuu

      anyways ..... count me in on your charity fundraising list ..... !
      Mkeshahoi likes this.

    15. len
      #13
      len's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 87
      Rep Power : 450
      Likes Received
      15
      Likes Given
      29

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Hongera sana Mgombezi kwa mawazo yako mazuri sana, wewe kweli ni mjasiriamali. Tarajia mchango wangu wakati wowote na ninaamini utakuwa ukitupatia feedback ya maendeleo ya mradi.
      If God be for us who can be against us?

    16. #14
      muhinda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th December 2011
      Posts : 218
      Rep Power : 419
      Likes Received
      92
      Likes Given
      178

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Nafurahi sana kuchangia mambo ya aina hii, sio harusi.
      count me in.
      Ila mkuu tuna uhakika gani kama kweli upo serious au unakusanya pesa ya kula ulabu tu?

    17. #15
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By LAT
      dah ... very exciting project ..... think of processing pawpaw/papaya beverage (smooth juice or hard liqueur)

      utatoka mkuu

      anyways ..... count me in on your charity fundraising list ..... !
      Nakushukuru Mkuu LAT, kwa mchango wako wa mawazo katika kuboresha wazo hili; nitafanyia kazi ushauri wako. Nategemea kupokea kutoka kwako, Niwezeshe.....!!!
      Ebenezer

    18. #16
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By len
      Hongera sana Mgombezi kwa mawazo yako mazuri sana, wewe kweli ni mjasiriamali. Tarajia mchango wangu wakati wowote na ninaamini utakuwa ukitupatia feedback ya maendeleo ya mradi.
      Nashukuru Mkuu LEN; nitakuwa nawakilisha taarifa za kupokea michango na hatua za utekelezaji hapa jamvini.
      len likes this.
      Ebenezer

    19. #17
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By muhinda
      Nafurahi sana kuchangia mambo ya aina hii, sio harusi.
      count me in.
      Ila mkuu tuna uhakika gani kama kweli upo serious au unakusanya pesa ya kula ulabu tu?
      Nashukuru Mkuu MUHINDA, hii ni moja kati ya changamoto tuliyonayo katika jamii yetu; kwani kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakitafuta michango ya fedha kwa matumizi yasiyo sahihi. Nakuahidi mchango wako kutekeleza lengo husika na utapokea taarifa.
      Malila likes this.
      Ebenezer

    20. #18
      Malila's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2007
      Posts : 2,605
      Rep Power : 10971
      Likes Received
      831
      Likes Given
      447

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Mgombezi
      Nashukuru Mkuu MUHINDA, hii ni moja kati ya changamoto tuliyonayo katika jamii yetu; kwani kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakitafuta michango ya fedha kwa matumizi yasiyo sahihi. Nakuahidi mchango wako kutekeleza lengo husika na utapokea taarifa.
      Asante kwa kunikumbuka, huku Dar mimi nakimbizana na jamii farm ya siku zile pale Lunch Time. Tumefikia pazuri kwa sasa, na june hii tunatia wanyama wa kwanza. tuombee na sisi tunakuombea, nitafutie mbegu ya papai fupi.
      Mkeshahoi and Mgombezi like this.
      Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe.

    21. #19
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Malila
      Asante kwa kunikumbuka, huku Dar mimi nakimbizana na jamii farm ya siku zile pale Lunch Time. Tumefikia pazuri kwa sasa, na june hii tunatia wanyama wa kwanza. tuombee na sisi tunakuombea, nitafutie mbegu ya papai fupi.
      Nashukuru Mkuu Malila; Kwa kweli ninawakumbuka sana kwa changamoto tunazoendelea kupeana, napata update za KILIMOTZ; Pongezi za pekee kwako kwa kazi njema unayoendelea nayo,nawatakia kila la kheri kwa hatua mliyofikia, nitaungana nanyi baada ya kupata utulivu kidogo hapa makao mapya. Baada ya kuotesha mbegu ninazotarajia, nitakupa matokeo yake na baada ya hapo nitaweza nitakushauri njia sahihi. Nategemea mchango wako, Niwezeshe......!!!
      Ebenezer

    22. #20
      Chasha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2011
      Posts : 2,455
      Rep Power : 953
      Likes Received
      1209
      Likes Given
      237

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Mkuu muleta maada kwanza kabis nikupongeze sana make hizi ndo moja ya investment ambazo zinaweza watoa WATANZANIA, kama kuna uwekezaji wenye tija moja wapo ni huu wa kwako, na kinacho takiwa ni kuwa na VISION nzuri, Na ni bora na wengine tukawa tunajifunza kutoka kwa jamaa hapa, mleta maada hata akipresent hii proposal yake mahali fulani watu wanaweza kumuelewa,

      - Ni bora watanzania tuachane kabisa na Biashara za uchuuzi ambazo hazina tija kabisa na tujikite kwenye project za aina hii na zinginezo ambazo zinatija kwa Taifa,

      - Na vitu kama hivi ndo vinatakiwa kupewa kipa umbele badala ya jamii kuwekeza kwenye Anasa, kama Harusi zisizo kuwa na Tija kwa Taifa, na kiwango anacho omba mlete thread ni kidogo sana ambacho hata Ndugu, jamaa na marafiki wangeweza kuchangia lakini Ndugu, Jamaa na marafiki hawawezi changia kwa sababu hakuna ulaji kwao, hapo mleta thread angetangaza kuoa zingeisha patikana

      -ok mkuu nitafanya process nitakutumia, ingawa kwa sasa niko mbali kidogo, ila nitakutumia mchango
      ,

    Page 1 of 4 123 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...