Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

    Report Post
    Page 3 of 4 FirstFirst 1234 LastLast
    Results 41 to 60 of 62
    1. #1
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default UPDATES - Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Ndugu Wana-Jamii

      Ni matumaini yangu mnaendelea vyema na shughuli za kila siku, pamoja na changamoto mbalimbali zinazotukabili. Kwa wale tunaofahamiana kwa kukutana ua namna yeyote ile; MALILA, LAT, KANYAGIO, THE FINEST, na wengine ambao nisingeweza kuwataja wote, habari za siku nyingi…..!!!; kwa muda mrefu sikupatikana sana katika jukwaa hili kama MGOMBEZI, hii ilitokana na harakati zangu za kuhamia hapa mjini Dodoma.

      Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi kila wakati ni vyema kuangalia au kutafuta jinsi ambavyo mitandao hii inaweza kutumika katika kuleta maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa jumla; kama inavyotumika JAMII FORUM. Kupitia mtandao wa FACEBOOK ambao vijana wetu wengi wamejikita huko niliamua kuanzisha kundi (Group) linaloitwa WAJASIRIAMALI KWELI, kwa lengo la kushirikishana elimu ya ujasiriamali na kupeana mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika kuanzisha shughuli za uzalishaji mali. Kwa wale wanaotembelea Facebook watakuwa wanaelewa kwamba kwenye FACEBOOK kuna option ya kuunda kundi na kujitengenezea Page. Nimeona ni vyema kuleta mawazo haya pia kwa “Great Thinkers”, ambapo naamini nitapata michango ya kutosha.

      WAJASIRIAMAILI KWELI: Log In | Facebook

      Dhana ya UJASIRIAMALI katika jamii yetu inaelekea kupoteza mwelekeo au uhalisia. Naamini utaungana nami kwamba mtazamo wa wengi juu ya MJASIRIAMALI, ni pamoja na kununua bidhaa za kichina na kupita nazo mtaani kuuza au hata kama amepanga mahali kuuza. Kwa hiyo basi dhana ya UJASIRIAMALI ni kununua na kuuza (trading), jambo ambalo ninaona kama tunapoteza mwelekeo.

      Hiki ni kikundi cha wajasiriamali wakionyesha bidhaa zao; lakini bidhaa nyingi zilizopo ni kutoka china.

      MAANA YA UJASIRIAMALI:

      Neno ujasiriamali linatokana na maneno mawili ambayo ni UJASIRI na MALI. Hivyo maana ya ujasiriamali ni kuwa na: -

      • Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
      • Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
      • Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.


      Kwa hiyo mjasiriamali:


      • ni mtu ambaye ana sifa na uwezo wa kutambua mapema fursa za kutengeneza faida na mwenye kuunganisha nguzo kuu za uzalishaji mali (nguvu kazi, mtaji na rasilimali);
      • ni mwanzilishi wa wazo na mwenye maono ya mbali ya jinsi ya kufanya biashara, uwezo wa kupanga, kuratibu na kutekeleza wazo lake na kufikia mafanikio;
      • pia ni mwenye kujiamini, kujituma kwa muda mrefu, kukubali makosa na kujisahihisha, mbunifu na mwenye kuwa tayari kutumia vizuri uwezo na maarifa ya watu wengine


      Tunaweza kusema hizi ndizo NGUZO kuu tatu (3) za MJASIRIAMALI:


      1. Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
      2. Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
      3. Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.


      Hivyo basi mtazamo wa WAJASIRIAMALI KWELI ni kujenga uwezo wa kutekeleza nguzo hizi miongoni mwetu, hasa kwa vijana ambao tunawategemea katika shughuli za uzalishaji mali; kama tusemavyo “VIJANA NDIO TAIFA LA KESHO”. Tutajengana kwa kupeana elimu ya ujasirimali na mbinu mbalimbali katika kushinda vikwazo mbalimbali.

      Msemo tunaotumia…, - “TIMIZA NDOTO ZAKO KWA KUCHANGIWA MTAJI” Je una maana gani?

      MTAJI NI NINI?

      Mtaji ni uwezo unaoweza kutumika katika kuzalisha mali au kuongeza kipato. Kuna usemi unasema “MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE”, kwamba nguzu za mtu zaweza kutumika katika uzalishaji au kuongeza kipato. Katika kuanzisha biashara uwezo huu unaweza kutokana na nguvu alizonazo mtu; kwa maana ya uwezo binafsi juu ya kile anachotaka kufanya, pamoja na rasilimali atakazohitaji.

      DHANA YA KUCHANGIWA MTAJI:

      Watu wengi wamekuwa na mawazo mazuri katika kuanzisha biashara lakini kikwazo kikubwa ni MTAJI. Katika kutekeleza nguzo namba tatu (3) ya Mjasiriamali; “Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara”. Nimeamua kutumia dhana ya kuchangiana katika kutekeleza wazo la mtu binafsi katika kuanzisha biashara.

      Jamii yetu imekuwa na utamaduni wa kuchangiana katika kutimiza lengo la mtu binafsi; hii imekuwa ikitumika katika kufanikisha sherehe mbalimbali za ndugu au jamaa au rafiki zikiwemo za kuzaliwa, ubatizo, kipaimara, maulidi, harusi n.k. Kwamba mtu anakusanya watu wachache ni kuwaeleza haja ya kufanikisha jambo lake na kuwataka ndugu au jamaa au marafiki kumchangia kwa hali na mali katika kufanikisha jambo hilo.

      Hivyo basi kutokana na utamaduni huu ambao tumekuwa tukitumia katika kufanikisha sherehe na shughuli nyingine za kijamii, tunaweza kutumia sasa utamaduni huu katika kutekeleza malengo ya mtu binafsi ambaye anataka kuanzisha shughulli za uzalisha mali au biashara kwa kumchangia mtaji.

      Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi muungano huu tunaweza kuutumia vyema katika kuangalia mahitaji ya wengine katika kutimiza ndoto zao.

      Mchango tunaoweza kumpatia mtu ni pamoja na mawazo yetu katika kuboresha wazo husika na rasilimali zinazohitajika.

      MRADI WA MAJARIBIO (PILOT PROJECT):

      Nikiwa kama mwezeshaji wa kujitegemea, nimeamua kutekeleza wazo langu kwa vitendo kwa kuliwakilisha kwenye jamii kwa lengo la kuomba michango yao, kupitia “NIWEZESHE CAMPAIGN”.

      KILIMO CHA MAPAPAI – STAN’S PAPAYA

      Kumekuwa na uhitaji mkubwa wa mapapai katika mji wa Dodoma na hata sehemu nyinginezo za nchi kutokana na utafiti mdogo niliyofanya, Bei ya papai katika maeneo mengi ya nchi inakadiriwa kuwa Tsh. 1000 – 3000, hapa Dodoma ni kati ya Tsh 2000 – 3000. Nikiwa kama mjasiriamali nimeona vyema kutumia uhitaji huu kama fursa ya biashara kwa kuanza kilimo cha mapapai ili kwa sehemu niweze kuchangia uzalishaji wa bidhaa hii, ambapo itasaidia pia kupunguza bei katika soko. Dhamira yangu ni papai kumfikia mlaji kwa bei kati ya Tsh. 500 – 1000. Vile vile nimehamasika kuanzisha kampeni ya matumizi ya mapapai, ikiwa ni pamoja kulitumia kama tunda na bidhaa nyinginezo zitokanazo na papai. Unaweza kutembelea page yangu kupitia mtandao wa FACEBOOK ambapo utapata dondoo za matumizi ya papai na mengineyo. Stan's PaPaYa | Facebook


      Ili niweze kuanzisha mradi huu nahitaji kiasi cha fedha Tsh. 5,920,000, ambapo mchango wangu binafsi zitakuwa gharama za uendeshaji zitakazo gharimu kiasi cha Tsh. 950,000/=. Hivyo basi mchango wa fedha ninao hitaji kutoka kwa jamii ni kwa ajili ya gharama za uanzishaji (start-up fund), ambazo ni Tsh. 4,970,000/=. Natafuta watu 1000 kutoka katika jamii watakaoweza kunichangia Ts.4970/= kila mmoja.

      Nawatafuta watu hawa kupitia mitandao ya kijamii (JAMII FORUM na FACEBOOK) pamoja na jamaa inayonizunguka.
      Unaweza kuwakilisha Mchango wako kupitia:

      TIGO PESA - 0714 460528 or M - PESA - 0757 941044

      (Mwisho ya kupokea michango tarehe 30/06/2012)

      Taarifa za kupokelewa kwa michango na utekelezaji wa mradi hatua kwa hatua zitawakilishwa kupitia:

      JAMII FORUM - Business & Economic Forum, Katika post hii
      FACEBOOK - Stan,s PaPaYa Stan's PaPaYa | Facebook
      WAJASIRIAMALI KWELI Log In | Facebook

      NB: Ikiwa upo ndani ya Mji wa Dodoma, unaweza kutoa order ya Mapapai na kufanya malipo ya awali. Kiwango cha chini ni mapapai kumi (10) na kila papai utalipia Tsh.500/=

      Naomba kuwasilisha..............!!!, Natanguliza Shukrani.......!!!

      MAHITAJI YA MRADI:


      A: UWEKEZAJI

      I: RASILIMALI

      MAHITAJI MAELEZO KIASI BEI JUMLA
      Ununuzi wa Shamba Heka 1 1,000,0000/= 1,000,000/=
      Ujenzi wa Nyumba ya Wafanyakazi Nyumba 1 700,000/= 700,000/=
      VIFAA VYA UMWAGILIAJI – Umwagiliaji kwa njia ya matone (Drip irrigation systems)
      Bomba – ¾ inch (pvc) Mita 1500 1000/= 1,500,000/=
      Tank la Maji 1000 Lita 1 160,000/= 160,000/=
      Pump ya kusukuma maji 1 300,000/= 300,000/=
      Bomba la kuvuta maji Mita 5 10,000/= 50,000/=
      Bomba la kupeleka kwenye Tank Mita 20 3,000/= 60,000/=
      Ujenzi wa Mnara wa Tank 1 300,000/= 300,000/=
      JUMLA 4,070,000/=

      NB: KILIMO CHA UMWAGILIAJI:
      Kilimo cha umwagiliagi kwa njia ya matone (Drip Irrigation System), ambapo mabomba (mipira) itapita kataka kila shina la mche na kudondosha matone ya maji yanapohitajika.



      II: UPANDAJI

      MAHITAJI MAELEZO KIASI BEI JUMLA
      Maandalizi ya Shamba Heka 1 100,000/= 100,000/=
      Mbole – Samadi ya Ng’ombe Tani 10 10,000/= 100,000/=
      Manunuzi ya Mbegu 1000 500/= 500,000/=
      Upandaji wa Mbegu 1000 200/= 200,000/=
      JUMLA 900,000/=

      III: UENDESHAJI

      NB: Kutokana na mbegu itakayotumika Mche wa papai utachukua Miezi sita (6) mpaka kuanza uzalishaji.

      MAHITAJI MAELEZO KIASI BEI JUMLA
      Mfanyakazi (miezi 7) Miezi 7 100,000/= 700,000/=
      Gharama Nyinginezo 250,000/= 250,000/=
      JUMLA 950,000/=

      JUMLA YA MTAJI = Tsh. 5,920,000/=

      B: JINSI YA KUPATA MTAJI:

      Mtaji nategemea kupata kwa kuchangiwa na wana-jamii kama ifuatavyo:

      MCHANGO BINAFSI – Gharama za Uendeshaji 950,000/=
      MCHANGO WA WANA-JAMII – Rasilimali + Upandaji 4,970,000/=
      JUMLA 5,920,000/=

      Hivyo Basi Wana-Jamii = 1000
      Kila mmoja anaweza kunichangia = Tsh. 4,970/=

      ****************************** *****UPDATES****************************** *****

      A: HATUA ZA UTEKELEZAJI:

      31/May/2012 - Upatikanaji wa eneo/shamba huko Michese, bado halijalipiwa.



      B: MICHANGO KUTOKA KWA JAMII:

      S/NO ID AMOUNT DATE
      1 Bakari Kawiza 5,000 29-May-12
      2 Fadhili Chitanda 5,000 29-May-12
      3 Amkawewe 5,000 4-Jun-12
      4 Kaunga 10,000 4-Jun-12
      5 Rose Lusinde 10,000 5-Jun-12
      6 Malila 10,000 7-Jun-12
      7 Miundombinu 20,000 9-Jun-12
      8 Mary Msemwa 6,000 10-Jun-12
      9 Leonard Kisenha 5,000 11-Jun-12
      10 Kibanga Ampiga Mkoloni 20,000 11-Jun-12
      11 Kitokota 10,000 13-Jun-12
      12 Asrams 5,000 17-Jun-12
      13 Jalala 10,000 20-Jun-12
      14 Muhinda 10,000 20-Jun-12
      Total contributions as today:
      131,000
      Total Amount Requested: 4,970,000
      Balance:
      -4,839,000
      Last edited by Mgombezi; 25th June 2012 at 12:09.
      Ebenezer

    2. FemaTV & Radio

    3. #41
      Kitokota's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th June 2012
      Posts : 10
      Rep Power : 352
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: UPDATES - Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Nimeipenda. Nzuri sana hangaika dunia hii inahitaji juhudi binafsi. Nitachangia kesho mchana.

      John Kennedy wa USA aliwahi sema "Don't ask what the USA has done for you,but rather ask yourself what have you done for USA"
      Last edited by Kitokota; 10th June 2012 at 21:41. Reason: some word missing
      Mgombezi likes this.

    4. #42
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: UPDATES - Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Kitokota
      Nimeipenda. Nzuri sana hangaika dunia hii inahitaji juhudi binafsi. Nitachangia kesho mchana.

      John Kennedy wa USA aliwahi sema "Don't ask what the USA has done for you,but rather ask yourself what have you done for USA"
      Natanguliza shukrani Mkuu KITOKOTA.....!!!
      Ebenezer

    5. #43
      Kibanga Ampiga Mkoloni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th August 2007
      Location : Here! here!
      Posts : 4,763
      Rep Power : 1627
      Likes Received
      1185
      Likes Given
      1701

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Kaka yangu nishakukaribisha(Facebook) uje kuchukua hope itatosha!
      Mgombezi likes this.
      For the Holy Quran says in Sura 42, verse 41: 'All those who fight when oppressed incur no guilt, but Allah shall punish the oppressor, Come the day.

    6. #44
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Kibanga Ampiga MKoloni
      Kaka yangu nishakukaribisha(Facebook) uje kuchukua hope itatosha!
      Nashukuru KIBANGA AMPIGA MKOLONI, naamini utakuwa umesoma kwa makini maelezo ya awali na utakuwa umeelewa dhamira yangu. Ningependa kufahamu, umenialika katika kundi gani la kuweza kupata hope?, japokuwa na mchango wako wa NIWEZESHE nauhitaji pia.
      Ebenezer

    7. #45
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Kibanga Ampiga MKoloni
      Kaka yangu nishakukaribisha(Facebook) uje kuchukua hope itatosha!
      Samahani kaka, mwanzo nilisoma ujumbe huu na kutengeneza tafsiri tofauti; Nashukuru kwa mchango wako wa Tsh. 20,000/=
      Ebenezer

    8. Miaka 50

    9. #46
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Nimepokea kiasi cha Tsh 96,000/= kutoka kwa wachangiaji 10; bado ninahitaji kiasi cha Tsh 4,874,000/= ili niweze kuanza mradi huu. Nimekuwa nikitafuta watu 1000 kutoka kwenye jamii watakaoweza kunichangia Tsh 4970/= kila mmoja ili niweze kupata Tsh 4,970,000/= ninazohitaji katika kuanzisha mradi huu. Kutoka na michango ya watu 10 niliyopokea ni sawa na watu 19 kama kila mmoja angetoa kiasi cha Tsh. 4970/=, hivyo basi ninahitaji watu 981 kunichangia kiasi cha Tsh 4970. Nawashukuru wale wote walioguswa na hitaji hili na kunichangia, hasa wale waliotoa kwa kiwango cha juu na kuweza kufidia watu 9 zaidi. Bado ninahitaji mchango wako....NIWEZESHE....!!!
      Ebenezer

    10. #47
      asrams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th September 2011
      Posts : 601
      Rep Power : 510
      Likes Received
      106
      Likes Given
      64

      Default

      Kaka mie mchango wangu ntatoa mwisho mwa wiki hii,


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD

    11. #48
      Kitokota's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th June 2012
      Posts : 10
      Rep Power : 352
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Juzi nilikuahidi kuwa nitakurushia cho chote ingawaje siioni message yangu. Hapana shaka ahadi ni deni, pokea mchango wangu. Elfu kumi tu.Asante.
      Mgombezi likes this.

    12. #49
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Kitokota
      Juzi nilikuahidi kuwa nitakurushia cho chote ingawaje siioni message yangu. Hapana shaka ahadi ni deni, pokea mchango wangu. Elfu kumi tu.Asante.
      Nashukuru Mkuu KITOKOTA, nimepokea mchango wako.
      Ebenezer

    13. #50
      Jalala's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th April 2010
      Posts : 40
      Rep Power : 470
      Likes Received
      8
      Likes Given
      9

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Nimekutumia mchango wangu elfu kumi utakuwa umeipata EM
      Mgombezi likes this.

    14. #51
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Jalala
      Nimekutumia mchango wangu elfu kumi utakuwa umeipata EM
      Nashukuru JALALA kwa mchango wako, nimepata.
      Ebenezer

    15. #52
      asrams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th September 2011
      Posts : 601
      Rep Power : 510
      Likes Received
      106
      Likes Given
      64

      Default

      Kaka nishatuma mchango wangu, na muwakilishi wangu kanambia umempigia, je ni kweli ? Mwisho wa mwezi ntatoa nyingine inshaAllah tukiwa hai na panapo uzima


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
      Mgombezi and Kitope like this.

    16. #53
      Kitope's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th October 2011
      Posts : 158
      Rep Power : 415
      Likes Received
      22
      Likes Given
      30

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Tupo pamoja mkuu, ila tu labda ungesogeza deadline ili kwa wale wenye nia ya kukuchangia na kwa sasa wanasubiri mwisho wa mwezi waweze kukuunga mkono wakati unapofika wa mishiko. kisha Baada ya hapo ni ushauri wangu kuwa uwezekano ni mkubwa kuwa pesa zitakuwa hazijakamilika,

      Lakini kile ambacho utakuwa umejaaliwa kukikusanya mpaka wakati huo wewe anza tu mchakato wa mambo madogo madogo. na kadri unavyowahakikishia wana Jf hatua ulizofikia na kuwathibitishia lazima watajitokeza wafadhili zaidi na hata hao waliokwisha toa huenda wakaingiwa moyo wa kutoa zaidi.
      Kila La kheri.
      Mkulima mwenzio,
      Kitope
      Mgombezi likes this.

    17. #54
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By Kitope
      Tupo pamoja mkuu, ila tu labda ungesogeza deadline ili kwa wale wenye nia ya kukuchangia na kwa sasa wanasubiri mwisho wa mwezi waweze kukuunga mkono wakati unapofika wa mishiko. kisha Baada ya hapo ni ushauri wangu kuwa uwezekano ni mkubwa kuwa pesa zitakuwa hazijakamilika, lakini kile ambacho utakuwa umejaaliwa kukikusanya mpaka wakati huo wewe anza tu mchakato wa mambo madogo madogo. na kadri unavyowahakikishia wana Jf hatua ulizofikia na kuwathibitishia lazima watajitokeza wafadhili zaidi na hata hao waliokwisha toa huenda wakaingiwa moyo wa kutoa zaidi.
      Kila La kheri.
      Mkulima mwenzio,
      Kitope
      Nashukuru KITOPE kwa ushauri wako, nimeupokea vyema; kweli niliweka malengo ya kuendesha kampeni hii ndani ya mwezi mmoja yaani mwezi huu JUNE. Umuhimu wa kuongeza deadline unaonekana kwani mpaka sasa nimefikia lengo kwa asilimia 2.6%. Naamini wengi watajitokeza kunichangia katika kipindi hiki cha mwisho wa mwezi na kuniwezesha kupata kiasi cha Tsh. 2,000,0000; na kuniwezesha kuanza hatua za utekelezaji katika mwezi ujao wa JULY 2012.
      Ebenezer

    18. #55
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Quote By asrams
      Kaka nishatuma mchango wangu, na muwakilishi wangu kanambia umempigia, je ni kweli ? Mwisho wa mwezi ntatoa nyingine inshaAllah tukiwa hai na panapo uzima


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
      Nashukuru Mkuu ASRASMA, nimepokea mchango wako; natanguliza shukrani kwa ahadi yako.
      Ebenezer

    19. #56
      asrams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th September 2011
      Posts : 601
      Rep Power : 510
      Likes Received
      106
      Likes Given
      64

      Default

      Quote By Mgombezi
      Nashukuru Mkuu ASRASMA, nimepokea mchango wako; natanguliza shukrani kwa ahadi yako.
      Hakuna tabu kaka


      Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD

    20. #57
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Ifikapo JAN-2013, Niwezeshe kutimiza ndoto yangu kwa kunichangia kiasi cha Tsh 4970 tu, nahitaji wachangiaji 974 ili kukamilisha kiasi ninachohitaji ili kufanikisha kuanza kwa mradi huu.
      Ebenezer

    21. #58
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Muhimu kufanya upembuzi yakinifu katika kutafuta eneo la shamba ; hivyo basi kwa sasa nimepata maeneo mawili (2) tofauti ambapo nitatakiwa kufanya maamuzi wakati wa kununua; nimepeta shamba katika kijiji cha Michese na Nala hapa Dodoma. Niwezeshe Kutimiza ndoto yangu kwa mchango wako.

      Shamba lililopo katika kijiji cha MICHESE ambo lina takribani heka 3 na nusu



      Shamba lililopo katika kijiji cha MICHESE ambo lina takribani heka 2



      Ebenezer

    22. #59
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      UPDATES: 28 June 2012 - MALIPO YA AWALI KWA AJILI YA SHAMBA LILILOPO KATIKA KIJIJI CHA NALA:

      Shamba nililopata katika kijiji cha Nala lina ukubwa wa heka mbili (2) na litagharimu kiasi cha Tsh. 1,500,000/=. Leo nimelipa malipo ya awali kiasi cha Tsh. 700,000/=, bado Tsh. 800,000/=. Malipo haya ya awali yametokana na mchango binafsi wa Tsh. 100,000/= kutokana na michango niliyopokea kutoka kwa jamii na kiasi cha Tsh. 600,000/= ni mchango binafsi.



      Mkono wa Kulia; Mimi, Kutoka kushoto; Mzee Mosha akiandaa makubaliano ya kuuza shamba na kupokea malipo ya awali. Walioketi kwenye matofali; aliyevaa shati jeupe na kuwekewa mkono begani na bwana aliyesimama huyu ndiye mwenye shamba, Mzee Cheni na wengine ni viongozi wa Mtaa wa Nala.



      Kulia; Bwana Mwinyi akipokea malipo ya awali kwa niaba ya mwenye Shamba Mzee Cheni (Hayupo katika picha hii)

      NB: Katika mchanganuo wa mradi gharama za shamba nilikadiria kiasi cha Tsh.1,000,000/= kwa heka, lakini hapa nimepata heka 2 kwa Tsh. 1,500,000/=; niliamua kuchukua heka mbili kutokana na maoni ya wadau niliokuwa nakutana nao, kwani walishauri ni vyema kuchukua heka zaidi ya moja ili kuwe na eneo la ziada kidogo.

      Nawashukuru wale wote waliotoa michango yao mpaka sasa na kuniwezesha kuchukua hatua za awali za utekelezaji, lakini bado naomba mchango wako ili niweze kutimiza ndoto hii.

      Msaada: Kwa anayefahamu jinsi ya kukuza picha niomba anielekeze au kufanya hivyo; ningependa picha hizi kuonekana vyema.
      Ebenezer

    23. #60
      muhinda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th December 2011
      Posts : 215
      Rep Power : 419
      Likes Received
      92
      Likes Given
      176

      Default Re: Niwezeshe Kutimiza Ndoto Yangu

      Mkuu Mgombezi,
      naona jina langu kwenye list ya waliochangia umelikosea.
      Ni Muhinda sio Milinda.
      nakutakia kila la kheri.
      Mgombezi likes this.

    Page 3 of 4 FirstFirst 1234 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...